Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

 
Yericko Nyerere. Tunasubiri jibu lako Bwana tuwajue hao viongozi wa uhaini waliosamehewa na JKN.
 
kichwakigumu, Do santos, ndiyo maana serikali imeyapuuza madai yenu kwa sababu hizihizi mnazoziona humu ndani. Mnataka tuamini tu. Tukitaka uthibisho mnasema tukaandike paper/kitabu. Dunia itajaa wasomi mbumbumbu kama watu wataruhusiwa kuandika papers halafu wasitetee hizo papers zao. Jiulizeni wenyewe.
Serikali imewapuuza kwa sababu hizi ni tungo na hisia tu zisizokuwa na ushahidi wowote.
 
kichwakigumu, Do santos, ndiyo maana serikali imeyapuuza madai yenu kwa sababu hizihizi mnazoziona humu ndani. Mnataka tuamini tu. Tukitaka uthibisho mnasema tukaandike paper/kitabu. Dunia itajaa wasomi mbumbumbu kama watu wataruhusiwa kuandika papers halafu wasitetee hizo papers zao. Jiulizeni wenyewe.
Serikali imewapuuza kwa sababu hizi ni tungo na hisia tu zisizokuwa na ushahidi wowote.
 

Si hivyo Bwana Sweke.

Serikali tuliwapa ushahidi katika ''Mwembechai Killings...'' kitabu cha Prof. Njozi.

Mkapa alisema tutoe ushahidi wa kisayansi.

Tulipotoa kitabu kikapigwa marufuku.

Lakini kitabu cha kutoa majibu kwetu cha Dr. Mbogoni kimo mtaani ''The Crescent
and the Cross.''

Hata hivyo baada ya hicho kitabu pamekuwa na mawasilano mengi na serikali.

Tatizo ni serikali ina hofu kukubali ukweli kuta taifa linanyemelewa na tatizo kubwa.

Nakuona unaandika kwa kibri.
Unatoa majibu ya kibri.

Majibu kama hayo yamesababisha vita kwingi duniani.

Jifunze kujibu kiungwana.
Majuto huwa mjukuu.

Laiti tungelijua...
 

serikali inayowajali wananchi wake na usalama,pia na amani ya nchi itapuuzia vipi watu wachochezi kama ndugu moh' said na maandiko yake pasi na kumchukulia hatua??mbona sasa mna kisebu sebu??mara mchonganishi,mara moh' said mfitini,anaharibu amani ya nchi,mara ni mhaini,kama mna uthibitisho na mnaitakia mema nchi hii kwanini sasa msipleke huyu mtu kortini na ushahid wa uhaini wake mnao??na hali huyu mtu mnamfaham hadi anapoish hajifichi??
Na hiyo serikali kama ingeona hayo yalisemwa na ndugu moh' said ni uzandiki,uongo na uchochezi kwanin isingemchukulia hatua?serikali haijapuuzia la hasha,ila imekosa hoja na namna pekee ya kuepusha lawama ni kupiga kimya,lakini ukweli unazid kusambaa..

Victory won...!!
 
Mjinga ni kama bubu au kiziwi. Akianza kukupiga asipoona machozi au damu hakuachii hata kidogo. Tafakari.
 
Nami nasubiri lile jibu langu kati Wakurya na Waarabu mkuu.
Kwa kuwa tunaizunguzmia Tanzania nachukulia Zanzibar na Huko Mara. Utaona kwa kina kabisa na fuatilia matukio ya watu kuuwana, kukatana visu na hata kukeketa. pata taarifa za mwaka za Matukio ya polisi.
 

Ndugu zangu marafiki hawa wawili Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere hivi ndivyo walivyoagana. Soma hapo chini:

Kabla hajafariki dunia Abdulwahid alifanya mazungumzo na Nyerere. Mazungumzo haya baina ya Abdulwahid na Nyerere yalifanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 1968 wakati mashekhe na Waislam mashuhuri wanasombwa na kutupwa gerezani.

Abdulwahid na Nyerere walikuwa wametoka mbali. Watu hawa walikuwa marafiki wa zamani. Huenda kama isingelikuwa kwa msaada wa Abdulwahid historia ya TANU na ya Nyerere mwenyewe zingechukua mkondo tofauti.

Mazungumzo haya yalikuwa muhimu kwa Abdulwahid kwa sababu kwa kiasi fulani alihisi anahusika na yale yaliyokuwa yakiwasibu Waislam, wale kutoka Dar es Salaam.

Taarifa za Waislam kukamatwa usiku na kuwekwa kizuizini zilikuwa zikimfikia karibu kila siku. Abdulwahid hakuweza kujifanya kuwa haathiriki na matokeo yale.

Baadhi ya watu ambao Nyerere alikuwa anawatupa gerezani walikuwa watu ambao yeye Abdulwahid binafsi walimuunga mkono wakati anaanza siasa na watu ambao aliwashawishi wamuunge mkono Nyerere wakati wa kuunda TANU.

Abdulwahid alimwambia Nyerere huenda yeye akawa hana hisia wala uhusiano wowote na watu ambao yeye anatia saihihi wakamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini kwake yeye hao ni jamaa zake anaokutananao ama msikitini au mitaani. Yeye kama mtu anayeishi miongoni mwa Waislam na zile familia zao alikuwa anaelewa majonzi yao.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba watu wale wanajua kuwa yeye, Abdulwahid ndiye aliyesamsaidia Nyerere wakati akiwa mgeni mjini Dar es Salaam, watu wakamjua na kumkubali na hivyo kuja kuweza kufika hapo alipofika.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kuwa ndugu na jamaa za wafungwa wale wanamjia wakimbembeleza amsihi Nyerere awatoe ndugu zao jela. Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba kule kuwatia watu kizuizini ni uonevu kwa sababu wale watu hawana uwezo wa kupindua serikali yake.

Kwa sauti ya masikitiko Abdulwahid alimaliza maelezo yake kwa kumwambia Nyerere, ''Naondoka hapa nikiwa nataka kuamini kuwa wewe Julius Nyerere, leo hujatugeuka.''

Kwa maneno hayo Abdulwahid aliaga na kuondoka.

Alichosikia Nyerere kuhusu Abdulwahid baada ya maneno yale ilikuwa taarifa ya kifo chake jioni moja Jumamosi tarehe 12 Oktoba, 1968.

Mkewe Mama Maria Nyerere, alizimia aliposikia habari zile za msiba. Alikuwa Abdulwahid ndiye aliyewapokea yeye na mume wake mara ya kwanza walipokuja Dar es Salaam.
 
Kuna threads tatu humu za Mzee Mohamed Said, Mag3 na hii ya Yericko Nyerere. Zimesheheni kila kitu. Ni zaidi ya kitabu cha mzee huyu mfia dini.
 
Last edited by a moderator:
Mjinga ni kama bubu au kiziwi. Akianza kukupiga asipoona machozi au damu hakuachii hata kidogo. Tafakari.

Unawakosea sana Viziwi na Bubu kuwaweka kwenye kundi la wajinga. Mjinga ni mtu yeyote asiyefahamu kitu au jambo fulani, ----, Jura, Galagula, Bozi, Mpumbavu, Juha.

Hakuna uhusiano kati ya ujinga na Kiziwi na Bubu.
 

Nadhani hamkumwelewa Mkapa. Alitaka ushahidi wa kisayansi nyinyi mkampelekea tungo na hisia. Tena huyu aliwaonea huruma na kuwapa yale majengo ya Tanesco kule Morogoro ili mfanye chuo chenu. Sijaona hata sehemu moja mlipomshukuru.
Halafu...nilishakuuliza hili...hivi wenzetu kweli huwa mnahimizana sana kusoma hii elimu dunia? Maana ni Bilali tu na Mufti Simba niliyowasikia wakisema waislam mnatakiwa kuchangamkia fursa ya elimu siyo kulalamika tu.
 
Duu! Kweli wee mzee ni mfia Dini. Lakini huna jinsi maana dunia mzima inaendeshwa na kuongozwa na mfumo kristo.

Kashindwa Osama bin Laden utaweza wewe? Yaani naona umepagawa na hizi dini tulizoletewa na wajanja.
 

WC

Nimekuelewa vizuri soma hapa chini utaelewa zaidi:

Baada ya kurejea kutoka Tabora, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, Elias Kassenge na Bhoke Munanka walifuatana na Nyerere kwenye ziara ya Jimbo la Mashariki kuwaeleza watu umuhimu na maana halisi ya uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Nyerere aliwafafanulia watu kile ambacho Waafrika wangepoteza endapo TANU ingesusia uchaguzi. Lakini Sheikh Takadir alikuwa akishiriki katika mikutano ile kimwili tu; moyo na fikra zake havikuwa pale.

Alikuwa na wasiwasi jinsi matukio yalivyokuwa yakitokea katika TANU na namna siasa ilivyokuwa ikichukua mwelekeo mpya. Sheikh Takadir alikuwa anautazama kwa hofu uongozi wa Wakristo katika TANU ambao ulikuwa ukielekea kuchukua uongozi baada kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria.

Kwa sababu ya yale masharti magumu ya uchaguzi, TANU ilibidi itazame nje ya uongozi wake ili kupata wagombea uchaguzi wenye sifa zilizohitajika kugombea uchaguzi dhidi ya UTP. TANU iliwachagua Julius Nyerere, Chief Abdallah Said Fundikira, John Ketto, Nesmo Eliufoo, John Mwakangale, Lawi Sijaona, Paul Bomani na George Kahama kusimama kama wagombea wa TANU.

Baadhi ya hawa walikuwa watu ambao hawakuinukia katika TANU au harakati za siasa. Sheikh Takadir alihofu kuwa hawa Wakristo walioelimishwa na wamisionari na ukuzingatia kuwa walikuwa watu wapya katika harakati, mara watakaposhika madaraka watafanya juhudi kudumisha hali ile ile ya ukoloni, wakiwa hawana dhima ya kuongoza harakati kufikia lengo lake lake lililokusudiwa.

Sheikh Takadir alikuwa kiongozi wa kwanza katika TANU kuwatanabaisha Waislam kuhusu hatari hii mpya iliyokuwa ikiwabili.

Sheikh Haidar Mwinyimvua, mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU na mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU katika mwaka 1958 na aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sheikh Suleiman Takadir, anakumbuka jinsi Sheikh Takadir ghafla alipotoa dukuduku lake kwa Nyerere, dukuduku ambalo lilionekana lilikuwa halina sababu:

''Ilikuwa katika ofisi ya zamani ya TANU tukisubiri kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Ghafla tu Sheikh Takadir alisimama wima akishikilia fimbo yake ya kutembea akimuelekezea Nyerere huku akisema, ëHuyu mtu katu hatakuja kutujali sisi atakuja kuwajali ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta.''

Sheikh Takadir alirudia maneno haya mara mbili. Sisi sote katika kile chumba cha mkutano tulipigwa na butwaa kutokana na maneno yale. Nilimwona Nyerere akilia. Nyerere alitugeukia sisi na kutuuliza, ''Je, Sheikh Suleiman amesema maneno yale kwa niaba yenu?''

Tulijibu kwa pamoja kuwa hatukuwa na habari kuhusu shauri lile; na mkutano ukavunjika hapo hapo.
 

bilali na mufti simba ni miongoni mwa waathirika wa mpango huu tunaoujadili kwa sasaa,put them into segregated schools,feed them with inferior education then rule them under the umbrellar of your institution(bakwata)
kwani ni nani asiejua wale wapo hapo kwa kucheza dance waliyoalikwa kuicheza pasi na kuitambua??wamerogwa kutoka na ujinga wao na umaskini wao,waerevu tunatambua hilo,na jamii yote sasa inajua hilo.
 
Mwalimu alipata uhamisho wa kikazi kutoka Tabora kuja Pugu sekondari ya sasa. Pale alipokelewa na kupewa nyumba ya kuishi kabla hajaanza kuwatafuta wanaTAA wenzake wa hapa Dar.

Mwalimu alikuwa anapambana na UDINI uliokuwa ukifukuta miaka ya sitini hapa. Baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha na harakati hizi za kidini walikuwemo masheikh pia. Asingewaacha.

Abdulwahid alishindwa na Mwalimu kwenye kinyang'anyiro cha URAIS wa kwanza wa TANU. Abdu hakumpenda tena Mwalimu tangu wakati huo kwani kushindwa kule hakukutarajia kwa namna alivyokuwa amejikita ndani ya TAA ya Dar.

Yaliyobaki yote ni historia tukufu ya nchi yetu. Serikali yetu haina na haitakuwa na DINI.
 
Kuna threads tatu humu za Mzee Mohamed Said, Mag3 na hii ya Yericko Nyerere. Zimesheheni kila kitu. Ni zaidi ya kitabu cha mzee huyu mfia dini.

Unaamini kabisa kuwa thread inaweza ikashinda kitabu?

Kitabu kina bibliografia.
Kitabu kina rekea na wapi zimetoka.

Kitabu kinapitiwa na wataalamu wa somo hilo kabla publisher hajakichapa.
Leo kitabu kifananishwe na thread.

Tena kitabu ambacho kimo katika Cambridge Journal of African History.
Hivi kweli nyie ndugu zangu mnajua mnachosema?

Na mbona una hamaki?
Hii lugha ya kunishambulia ya nini kaka?

Mbona mie siwashambulii nyie binafsi naweka hoja tu zijieleze?
Tulia ndugu yangu tujadiliane kistaarabu.
 


wanaonyesha wazi wazi ishara ya kushindwa,wanalia na kutoa machozi huku wanaficha nyuso zao tusiyashuhudie machozi hayo,wanajipa tabu bure kuupokea ukweli huu,lakini kumbuka kuambiwa ukweli siku zote kunauma,kunahitaji moyo wa kijasiri sana ili kuweza kuupokea ukweli huo.
Lugha zao za kejeli na jazba hazitasaidia malumbano haya ya hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…