Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Maneno yako hapo kwenye blue yanakinzana na ya Mohamed Said. Mzee wetu tumetoka naye mbali sana tangu zile nyuzi za makala zake za miaka 50 ya uhuru lakini hatupati ufafanuzi na uthibitisho kwenye mambo mengi anayomtuhumu Nyerere badala yake anatupa mabandiko ya vitabu na papers zake.
Mimi kwenye suala la elimu kwa kweli ningependa kupata ufafanuzi zaidi maana mtu akikunyima elimu kwa makusudi ni kwamba amekufanyia dhulma kubwa sana.
Mohamed Said ameendika tangia nchi hii inapata uhuru mpaka pale Kighoma Malima aliteuliwa kuwa waziri wa elimu, wizara hiyo ilikuwa inaongozwa na wakristu tu. Anasema ilifikia mpaka wakati padre/mchunguji aliongoza wizara hiyo. Teuzi hizo za wakristu zilikuwa na lengo la kuwakandamiza waislam kielimu na kuwapendelea wakristu na ndiyo maana (kwa mtazamo wa MS) Kighoma Malima alipoingia wizarani akakutana na madudu mengi.
Kuna siku nimemuuliza hivi hawa mawaziri wote waislam(Juma Kapuya,Maghembe, Shukuru Kawambwa) waliotumikia hiyo wizara ya elimu baada ya Malima hawayaoni hayo madudu tena wakati huu vitu vipo wazi zaidi? Hakunipa jibu la maana. Yeye Mohamedi said anajua dhulma hiyo kushinda waziri muislam anayetumikia wizara hiyo.

Ni huyuhuyu Shukuru Kawambwa aliyeacha kazi zake na kwenda kupokea maandamano yenu(wanafunzi waislam) Kidongo chekundu kuhusiana na ile issue ya wanafunzi wa ndanda. Na aliwaahidi atalishughulikia lile tatizo. Lakini nadhani ni naibu waziri wa elimu wakati huo Kassim Majaliwa(Muislam) ndiye aliyeivalia njuga issue ile na mwisho wake wote tunajua kilichokuja julikana.
Ni huyuhuyu Shukuru Kawambwa aliyetoa ufafanuzi mzuri tu kwenye vyombo vya habari kuhusu majibu ya Islamic Knowledge yaliyokosewa.
Sasa inashindikana vipi kwa huyu muislam kuona dhulma wanayofanyiwa waislam kwenye wizara yake? Anatumikia Kanisa?
Si mnaswali naye misikitini huyu?
Jamani tuwe wakweli. Leo hii ukifeliswa ni rahisi sana kujua umeonewa au la kwa sababu mitihani huwa inabaki pale wizarani kwa muda kuruhusu watu ku appeal na hivyo mitihani yao kuangaliwa upya. Mkuu muulize mohamed said anajua nini kuhusu jinsi mtihani invyosahihiswa mpaka kufikia kutolewa matokeo.

Binafsi kama angeniletea cases za wanafunzi kadhaa za waislam walioonewa na baada ya kuappeal wakapata matokeo mazuri zaidi, ningemuelewa. Au aniletee cases kadhaa za wanafunzi wa kiislam waliofaulu lakini hawakuchaguliwa kuendelea na masomo nitamuelewa.
Lakini asituambie tuamini tu.

SWEKE,NDIO KUSEMA HUJUI KAMA WALE MAWAZIRI WAPO PALE KWA PROTOKALI YA KISIASA TUH?HUJUI WATENDAJI WA HAYO MADUDU NI MFANO WA WATU WENYE NYADHIFA KAMA ZA KINA NDALICHAKO NAKADHALIKA??

HAITOSHI KWAKO WEWE KUJA KUELEZEA UWEPO WA MAWAZIRI WA KIISLAM KATIKA KIPINDI CHA MWINYI,MKA PA AMA KIKWETE ILI UWEZE KUFUKIA FUKIA MASHIMO YA HOJA ZILE ZILIZOTOLEWA KUHUSU DHULMA TAJWA,NA DHULMA FAFANULIWA AMBAZO UNA KIRI KIUNAFIKI YA KWAMBA HUZION,,

LAZIMA UTAMBUE YA KWAMBA BAADA YA MALIMA KUJA ALIOWAKUTA WANAFANYA HUJMA HIZO SIO WANASIASA KAMA YEYE MOJA KWA MOJA,BALI KUNA WATENDAJI MAHUSUSI WALIOKAWA WANAFNYA VITENDO HIVYO AMA KWA KUAGIZWA AU KWA HULKA ZAO ILI KUWEKA KIZAZI CHAO KWA MANUFAA YA BAADAE AMBAYO BILA SHAKA LEO HII MATUNDA YAO MNAYAENZI,SI NDIYO??EEEH,NI KWELI KABISA,SISI WAISLAM HATUTAKI KUSOMA,SAWA,,SISI WAISLAM TUMEZOEA SANA KULALAMIKA LALAMIKA,,SAWA PIA,,

SISI WAISLAM NI WATU WA HOVYO NA WENYE MATATIZO DUNIA NZIMA NI KWELI KABISA,LAKINI KWANIN TUNAPOZUNGUMZA BAADHI YA MAMBO YENYE UHALISIA HAYAJIBIWI BALI ZINAKUJA HOJA ZA KUTUSEMA KWANZA PASI NA KUZIJIBU HOJA HIZO?
YALE YA JUZI YA JOYCE NDALICHAKO NA MATOKEO YA ISLAMIC KNOWLEDGE NI MFANO TUH WA PICHA LILIVYO,NADHAN SASA UNAWEZA PATA PICHA KIDOGO
 
Yericko Nyerere. Tunasubiri jibu lako Bwana tuwajue hao viongozi wa uhaini waliosamehewa na JKN.
 
kichwakigumu, Do santos, ndiyo maana serikali imeyapuuza madai yenu kwa sababu hizihizi mnazoziona humu ndani. Mnataka tuamini tu. Tukitaka uthibisho mnasema tukaandike paper/kitabu. Dunia itajaa wasomi mbumbumbu kama watu wataruhusiwa kuandika papers halafu wasitetee hizo papers zao. Jiulizeni wenyewe.
Serikali imewapuuza kwa sababu hizi ni tungo na hisia tu zisizokuwa na ushahidi wowote.
 
kichwakigumu, Do santos, ndiyo maana serikali imeyapuuza madai yenu kwa sababu hizihizi mnazoziona humu ndani. Mnataka tuamini tu. Tukitaka uthibisho mnasema tukaandike paper/kitabu. Dunia itajaa wasomi mbumbu kama watu wataruhusiwa kuandika papers halafu wasitetee hizo papers zao. Jiulizeni wenyewe.
Serikali imewapuuza kwa sababu hizi ni tungo na hisia tu zisizokuwa na ushahidi wowote.

Si hivyo Bwana Sweke.

Serikali tuliwapa ushahidi katika ''Mwembechai Killings...'' kitabu cha Prof. Njozi.

Mkapa alisema tutoe ushahidi wa kisayansi.

Tulipotoa kitabu kikapigwa marufuku.

Lakini kitabu cha kutoa majibu kwetu cha Dr. Mbogoni kimo mtaani ''The Crescent
and the Cross.''

Hata hivyo baada ya hicho kitabu pamekuwa na mawasilano mengi na serikali.

Tatizo ni serikali ina hofu kukubali ukweli kuta taifa linanyemelewa na tatizo kubwa.

Nakuona unaandika kwa kibri.
Unatoa majibu ya kibri.

Majibu kama hayo yamesababisha vita kwingi duniani.

Jifunze kujibu kiungwana.
Majuto huwa mjukuu.

Laiti tungelijua...
 
kichwakigumu, do santos, ndiyo maana serikali imeyapuuza madai yenu kwa sababu hizihizi mnazoziona humu ndani. Mnataka tuamini tu. Tukitaka uthibisho mnasema tukaandike paper/kitabu. Dunia itajaa wasomi mbumbu kama watu wataruhusiwa kuandika papers halafu wasitetee hizo papers zao. Jiulizeni wenyewe.
Serikali imewapuuza kwa sababu hizi ni tungo na hisia tu zisizokuwa na ushahidi wowote.

serikali inayowajali wananchi wake na usalama,pia na amani ya nchi itapuuzia vipi watu wachochezi kama ndugu moh' said na maandiko yake pasi na kumchukulia hatua??mbona sasa mna kisebu sebu??mara mchonganishi,mara moh' said mfitini,anaharibu amani ya nchi,mara ni mhaini,kama mna uthibitisho na mnaitakia mema nchi hii kwanini sasa msipleke huyu mtu kortini na ushahid wa uhaini wake mnao??na hali huyu mtu mnamfaham hadi anapoish hajifichi??
Na hiyo serikali kama ingeona hayo yalisemwa na ndugu moh' said ni uzandiki,uongo na uchochezi kwanin isingemchukulia hatua?serikali haijapuuzia la hasha,ila imekosa hoja na namna pekee ya kuepusha lawama ni kupiga kimya,lakini ukweli unazid kusambaa..

Victory won...!!
 
Watu wenye elimu ndogo wanakusumbua wewe msomi uoni kama wewe ndiyo utakuwa na matatizo. Hivi duniani kuna msomi anaye muogopa mjinga. Waislam wana elimu ndogo kama unavyosema dawa yao kuwapuuza tu mkuu unatokwa na povu la nini wakati nyie ni wasomi mmekwenda shule.
Mjinga ni kama bubu au kiziwi. Akianza kukupiga asipoona machozi au damu hakuachii hata kidogo. Tafakari.
 
Nami nasubiri lile jibu langu kati Wakurya na Waarabu mkuu.
Kwa kuwa tunaizunguzmia Tanzania nachukulia Zanzibar na Huko Mara. Utaona kwa kina kabisa na fuatilia matukio ya watu kuuwana, kukatana visu na hata kukeketa. pata taarifa za mwaka za Matukio ya polisi.
 
kinachonistaajabisha ni kuwa imepita miaka 15, na hakuna kitabu au hata journal article inayopingana na yote yaliyotajwa na mzee wetu Mohamed Said. Hili tu pekee halitoshi kusema kuwa kinachosemwa ni kweli?

Au labda niulize, research huwa inachukua muda gani? labda wenzetu mpaka leo wanafanza hiyo research

Kaka Do Santo, tupo pamoja kumsahihisha huyu kijana

Ndugu zangu marafiki hawa wawili Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere hivi ndivyo walivyoagana. Soma hapo chini:

Kabla hajafariki dunia Abdulwahid alifanya mazungumzo na Nyerere. Mazungumzo haya baina ya Abdulwahid na Nyerere yalifanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 1968 wakati mashekhe na Waislam mashuhuri wanasombwa na kutupwa gerezani.

Abdulwahid na Nyerere walikuwa wametoka mbali. Watu hawa walikuwa marafiki wa zamani. Huenda kama isingelikuwa kwa msaada wa Abdulwahid historia ya TANU na ya Nyerere mwenyewe zingechukua mkondo tofauti.

Mazungumzo haya yalikuwa muhimu kwa Abdulwahid kwa sababu kwa kiasi fulani alihisi anahusika na yale yaliyokuwa yakiwasibu Waislam, wale kutoka Dar es Salaam.

Taarifa za Waislam kukamatwa usiku na kuwekwa kizuizini zilikuwa zikimfikia karibu kila siku. Abdulwahid hakuweza kujifanya kuwa haathiriki na matokeo yale.

Baadhi ya watu ambao Nyerere alikuwa anawatupa gerezani walikuwa watu ambao yeye Abdulwahid binafsi walimuunga mkono wakati anaanza siasa na watu ambao aliwashawishi wamuunge mkono Nyerere wakati wa kuunda TANU.

Abdulwahid alimwambia Nyerere huenda yeye akawa hana hisia wala uhusiano wowote na watu ambao yeye anatia saihihi wakamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini kwake yeye hao ni jamaa zake anaokutananao ama msikitini au mitaani. Yeye kama mtu anayeishi miongoni mwa Waislam na zile familia zao alikuwa anaelewa majonzi yao.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba watu wale wanajua kuwa yeye, Abdulwahid ndiye aliyesamsaidia Nyerere wakati akiwa mgeni mjini Dar es Salaam, watu wakamjua na kumkubali na hivyo kuja kuweza kufika hapo alipofika.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kuwa ndugu na jamaa za wafungwa wale wanamjia wakimbembeleza amsihi Nyerere awatoe ndugu zao jela. Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba kule kuwatia watu kizuizini ni uonevu kwa sababu wale watu hawana uwezo wa kupindua serikali yake.

Kwa sauti ya masikitiko Abdulwahid alimaliza maelezo yake kwa kumwambia Nyerere, ''Naondoka hapa nikiwa nataka kuamini kuwa wewe Julius Nyerere, leo hujatugeuka.''

Kwa maneno hayo Abdulwahid aliaga na kuondoka.

Alichosikia Nyerere kuhusu Abdulwahid baada ya maneno yale ilikuwa taarifa ya kifo chake jioni moja Jumamosi tarehe 12 Oktoba, 1968.

Mkewe Mama Maria Nyerere, alizimia aliposikia habari zile za msiba. Alikuwa Abdulwahid ndiye aliyewapokea yeye na mume wake mara ya kwanza walipokuja Dar es Salaam.
 
Kuna threads tatu humu za Mzee Mohamed Said, Mag3 na hii ya Yericko Nyerere. Zimesheheni kila kitu. Ni zaidi ya kitabu cha mzee huyu mfia dini.
 
Last edited by a moderator:
Mjinga ni kama bubu au kiziwi. Akianza kukupiga asipoona machozi au damu hakuachii hata kidogo. Tafakari.

Unawakosea sana Viziwi na Bubu kuwaweka kwenye kundi la wajinga. Mjinga ni mtu yeyote asiyefahamu kitu au jambo fulani, ----, Jura, Galagula, Bozi, Mpumbavu, Juha.

Hakuna uhusiano kati ya ujinga na Kiziwi na Bubu.
 
Si hivyo Bwana Sweke.

Serikali tuliwapa ushahidi katika ''Mwembechai Killings...'' kitabu cha Prof. Njozi.

Mkapa alisema tutoe ushahidi wa kisayansi.

Tulipotoa kitabu kikapigwa marufuku.

Lakini kitabu cha kutoa majibu kwetu cha Dr. Mbogoni kimo mtaani ''The Crescent
and the Cross.''

Hata hivyo baada ya hicho kitabu pamekuwa na mawasilano mengi na serikali.

Tatizo ni serikali ina hofu kukubali ukweli kuta taifa linanyemelewa na tatizo kubwa.

Nakuona unaandika kwa kibri.
Untoa majibu ya kibri.

Majibu kama hayo yamesababisha vita kwingi duniani.

Jifunze kujibu kiungwana.
Majuto huwa mjukuu.

Laiti tungelijua...

Nadhani hamkumwelewa Mkapa. Alitaka ushahidi wa kisayansi nyinyi mkampelekea tungo na hisia. Tena huyu aliwaonea huruma na kuwapa yale majengo ya Tanesco kule Morogoro ili mfanye chuo chenu. Sijaona hata sehemu moja mlipomshukuru.
Halafu...nilishakuuliza hili...hivi wenzetu kweli huwa mnahimizana sana kusoma hii elimu dunia? Maana ni Bilali tu na Mufti Simba niliyowasikia wakisema waislam mnatakiwa kuchangamkia fursa ya elimu siyo kulalamika tu.
 
DINI yenu inavumilia kwa taabu sana maoni huru. Salman aliandika "fiction" tu ambayo haina tofauti sana na yule mtoto wa Mbagala aliyekojolea Quran. Adhabu yake afe! DINI yenu hamtaki Mtume Mohamad( S.A.W) aguswe au kama kuna makosa alifanya yasemwe!

Simlinganishi Mwalimu na Mtume wenu, lakini haya uliomsingizia ya kukandamiza Uislam huku misikiti ikiongezeka na Waislam wanaongezeka, tuyaiteje haya.

Yesu katukanwa sana tena sio kwa maandishi tu bali hata filamu kabisa. Tembea hata leo hii mitaa yote ya hapa Dar ukimtukana Yesu, hakuna atakayejali. Jaribu hivo kwa upande mwingine uone. Hautavuka hata nyumba ya tatu!
Duu! Kweli wee mzee ni mfia Dini. Lakini huna jinsi maana dunia mzima inaendeshwa na kuongozwa na mfumo kristo.

Kashindwa Osama bin Laden utaweza wewe? Yaani naona umepagawa na hizi dini tulizoletewa na wajanja.
 
Utayakwepa vipi makanisa huku ukidai kwamba tumo ndani ya MfumoKristo? Historia ulioiandika umeihusisha na DINI. Tunachojaribu bila mafanikio kukusihi ukiondoe kwenye historia yako hii ni DINI yako. Wazee wako hawa hawakusahaulika kwa sababu ya imani yao kama ambavyo hawakutumwa na dini yao "kupigania" uhuru wa nchi hii.

WC

Nimekuelewa vizuri soma hapa chini utaelewa zaidi:

Baada ya kurejea kutoka Tabora, Sheikh Suleiman Takadir, Bibi Titi Mohamed, Elias Kassenge na Bhoke Munanka walifuatana na Nyerere kwenye ziara ya Jimbo la Mashariki kuwaeleza watu umuhimu na maana halisi ya uchaguzi uliokuwa mbele yao.

Nyerere aliwafafanulia watu kile ambacho Waafrika wangepoteza endapo TANU ingesusia uchaguzi. Lakini Sheikh Takadir alikuwa akishiriki katika mikutano ile kimwili tu; moyo na fikra zake havikuwa pale.

Alikuwa na wasiwasi jinsi matukio yalivyokuwa yakitokea katika TANU na namna siasa ilivyokuwa ikichukua mwelekeo mpya. Sheikh Takadir alikuwa anautazama kwa hofu uongozi wa Wakristo katika TANU ambao ulikuwa ukielekea kuchukua uongozi baada kuingia katika Baraza la Kutunga Sheria.

Kwa sababu ya yale masharti magumu ya uchaguzi, TANU ilibidi itazame nje ya uongozi wake ili kupata wagombea uchaguzi wenye sifa zilizohitajika kugombea uchaguzi dhidi ya UTP. TANU iliwachagua Julius Nyerere, Chief Abdallah Said Fundikira, John Ketto, Nesmo Eliufoo, John Mwakangale, Lawi Sijaona, Paul Bomani na George Kahama kusimama kama wagombea wa TANU.

Baadhi ya hawa walikuwa watu ambao hawakuinukia katika TANU au harakati za siasa. Sheikh Takadir alihofu kuwa hawa Wakristo walioelimishwa na wamisionari na ukuzingatia kuwa walikuwa watu wapya katika harakati, mara watakaposhika madaraka watafanya juhudi kudumisha hali ile ile ya ukoloni, wakiwa hawana dhima ya kuongoza harakati kufikia lengo lake lake lililokusudiwa.

Sheikh Takadir alikuwa kiongozi wa kwanza katika TANU kuwatanabaisha Waislam kuhusu hatari hii mpya iliyokuwa ikiwabili.

Sheikh Haidar Mwinyimvua, mjumbe wa Baraza la Wazee wa TANU na mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU katika mwaka 1958 na aliyekuwa rafiki mkubwa wa Sheikh Suleiman Takadir, anakumbuka jinsi Sheikh Takadir ghafla alipotoa dukuduku lake kwa Nyerere, dukuduku ambalo lilionekana lilikuwa halina sababu:

''Ilikuwa katika ofisi ya zamani ya TANU tukisubiri kufanya mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Ghafla tu Sheikh Takadir alisimama wima akishikilia fimbo yake ya kutembea akimuelekezea Nyerere huku akisema, ëHuyu mtu katu hatakuja kutujali sisi atakuja kuwajali ndugu zake. Usipoziba ufa utajenga ukuta.''

Sheikh Takadir alirudia maneno haya mara mbili. Sisi sote katika kile chumba cha mkutano tulipigwa na butwaa kutokana na maneno yale. Nilimwona Nyerere akilia. Nyerere alitugeukia sisi na kutuuliza, ''Je, Sheikh Suleiman amesema maneno yale kwa niaba yenu?''

Tulijibu kwa pamoja kuwa hatukuwa na habari kuhusu shauri lile; na mkutano ukavunjika hapo hapo.
 
nadhani hamkumwelewa mkapa. Alitaka ushahidi wa kisayansi nyinyi mkampelekea tungo na hisia. Tena huyu aliwaonea huruma na kuwapa yale majengo ya tanesco kule morogoro ili mfanye chuo chenu. Sijaona hata sehemu moja mlipomshukuru.
Halafu...nilishakuuliza hili...hivi wenzetu kweli huwa mnahimizana sana kusoma hii elimu dunia? Maana ni bilali tu na mufti simba niliyowasikia wakisema waislam mnatakiwa kuchangamkia fursa ya elimu siyo kulalamika tu.

bilali na mufti simba ni miongoni mwa waathirika wa mpango huu tunaoujadili kwa sasaa,put them into segregated schools,feed them with inferior education then rule them under the umbrellar of your institution(bakwata)
kwani ni nani asiejua wale wapo hapo kwa kucheza dance waliyoalikwa kuicheza pasi na kuitambua??wamerogwa kutoka na ujinga wao na umaskini wao,waerevu tunatambua hilo,na jamii yote sasa inajua hilo.
 
Ndugu zangu marafiki hawa wawili Abdulwahid Sykes na Julius Nyerere hivi ndivyo walivyoagana. Soma hapo chini:

Kabla hajafariki dunia Abdulwahid alifanya mazungumzo na Nyerere. Mazungumzo haya baina ya Abdulwahid na Nyerere yalifanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 1968 wakati mashekhe na Waislam mashuhuri wanasombwa na kutupwa gerezani.

Abdulwahid na Nyerere walikuwa wametoka mbali. Watu hawa walikuwa marafiki wa zamani. Huenda kama isingelikuwa kwa msaada wa Abdulwahid historia ya TANU na ya Nyerere mwenyewe zingechukua mkondo tofauti.

Mazungumzo haya yalikuwa muhimu kwa Abdulwahid kwa sababu kwa kiasi fulani alihisi anahusika na yale yaliyokuwa yakiwasibu Waislam, wale kutoka Dar es Salaam.

Taarifa za Waislam kukamatwa usiku na kuwekwa kizuizini zilikuwa zikimfikia karibu kila siku. Abdulwahid hakuweza kujifanya kuwa haathiriki na matokeo yale.

Baadhi ya watu ambao Nyerere alikuwa anawatupa gerezani walikuwa watu ambao yeye Abdulwahid binafsi walimuunga mkono wakati anaanza siasa na watu ambao aliwashawishi wamuunge mkono Nyerere wakati wa kuunda TANU.

Abdulwahid alimwambia Nyerere huenda yeye akawa hana hisia wala uhusiano wowote na watu ambao yeye anatia saihihi wakamatwe na kutupwa gerezani.

Lakini kwake yeye hao ni jamaa zake anaokutananao ama msikitini au mitaani. Yeye kama mtu anayeishi miongoni mwa Waislam na zile familia zao alikuwa anaelewa majonzi yao.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba watu wale wanajua kuwa yeye, Abdulwahid ndiye aliyesamsaidia Nyerere wakati akiwa mgeni mjini Dar es Salaam, watu wakamjua na kumkubali na hivyo kuja kuweza kufika hapo alipofika.

Abdulwahid alimwambia Nyerere kuwa ndugu na jamaa za wafungwa wale wanamjia wakimbembeleza amsihi Nyerere awatoe ndugu zao jela. Abdulwahid alimwambia Nyerere kwamba kule kuwatia watu kizuizini ni uonevu kwa sababu wale watu hawana uwezo wa kupindua serikali yake.

Kwa sauti ya masikitiko Abdulwahid alimaliza maelezo yake kwa kumwambia Nyerere, ''Naondoka hapa nikiwa nataka kuamini kuwa wewe Julius Nyerere, leo hujatugeuka.''

Kwa maneno hayo Abdulwahid aliaga na kuondoka.

Alichosikia Nyerere kuhusu Abdulwahid baada ya maneno yale ilikuwa taarifa ya kifo chake jioni moja Jumamosi tarehe 12 Oktoba, 1968.

Mkewe Mama Maria Nyerere, alizimia aliposikia habari zile za msiba. Alikuwa Abdulwahid ndiye aliyewapokea yeye na mume wake mara ya kwanza walipokuja Dar es Salaam.
Mwalimu alipata uhamisho wa kikazi kutoka Tabora kuja Pugu sekondari ya sasa. Pale alipokelewa na kupewa nyumba ya kuishi kabla hajaanza kuwatafuta wanaTAA wenzake wa hapa Dar.

Mwalimu alikuwa anapambana na UDINI uliokuwa ukifukuta miaka ya sitini hapa. Baadhi ya watu waliokuwa wakijihusisha na harakati hizi za kidini walikuwemo masheikh pia. Asingewaacha.

Abdulwahid alishindwa na Mwalimu kwenye kinyang'anyiro cha URAIS wa kwanza wa TANU. Abdu hakumpenda tena Mwalimu tangu wakati huo kwani kushindwa kule hakukutarajia kwa namna alivyokuwa amejikita ndani ya TAA ya Dar.

Yaliyobaki yote ni historia tukufu ya nchi yetu. Serikali yetu haina na haitakuwa na DINI.
 
Kuna threads tatu humu za Mzee Mohamed Said, Mag3 na hii ya Yericko Nyerere. Zimesheheni kila kitu. Ni zaidi ya kitabu cha mzee huyu mfia dini.

Unaamini kabisa kuwa thread inaweza ikashinda kitabu?

Kitabu kina bibliografia.
Kitabu kina rekea na wapi zimetoka.

Kitabu kinapitiwa na wataalamu wa somo hilo kabla publisher hajakichapa.
Leo kitabu kifananishwe na thread.

Tena kitabu ambacho kimo katika Cambridge Journal of African History.
Hivi kweli nyie ndugu zangu mnajua mnachosema?

Na mbona una hamaki?
Hii lugha ya kunishambulia ya nini kaka?

Mbona mie siwashambulii nyie binafsi naweka hoja tu zijieleze?
Tulia ndugu yangu tujadiliane kistaarabu.
 
unaamini kabisa kuwa thread inaweza ikashinda kitabu?

Kitabu kina bibliografia.
Kitabu kina rekea na wapi zimetoka.

Kitabu kinapitiwa na wataalamu wa somo hilo kabla publisher hajakichapa.
Leo kitabu kifananishwe na thread.

Tena kitabu ambacho kimo katika cambridge journal of african history.
Hivi kweli nyie ndugu zangu mnajua mnachosema?

Na mbona una hamaki?
Hii lugha ya kunishambulia ya nini kaka?

Mbona mie siwashambulii nyie binafsi naweka hoja tu zijieleze?
Tulia ndugu yangu tujadiliane kistaarabu.

wanaonyesha wazi wazi ishara ya kushindwa,wanalia na kutoa machozi huku wanaficha nyuso zao tusiyashuhudie machozi hayo,wanajipa tabu bure kuupokea ukweli huu,lakini kumbuka kuambiwa ukweli siku zote kunauma,kunahitaji moyo wa kijasiri sana ili kuweza kuupokea ukweli huo.
Lugha zao za kejeli na jazba hazitasaidia malumbano haya ya hoja.
 
Back
Top Bottom