Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Tuendelee..
Nithibitishie uchochez wa Moh Said..
Bi maana bado sijashawishika hadi sasa,na Yericko kabakia kuwa chakubimbi wa hoja za watu tuh,hadi sasa kagoma kuchukuwa pesa kwenda TBC kutuchukulia ile Audio speech..
Hii inaleta walakini sana..
 
Last edited by a moderator:
gombesugu umeandika maneno meeeengi ila na wewe pia kama wenzako uonyesha chuki yako kwa Mwanakijiji mara oh unampinga mwandishi mwenzako(na hili ndo kubwa linalowakera kumhusu)...,mmekuja na accusations nzito nzito(sasa sijui kukosoa siku hizi ndo accusation nzito nzito)....mara umerukia ya Rostam Aziz hata sijui umeyatoa kwenye page gani kwenye huu mnakasha...mara unajivunia u-Tanga wako...mambo chungu nzima na inaoneka "umefunguka" kweli ya moyoni,umeshindwa kuona hata point zake hapo juu

Unasema kwamba watu wanang'ang'ania vimakosa viduchu hivi kwenye historia kuna "vimakosa viduchu"?!

Inavyoonekana ulimpania sana Mwanakijiji

Na wewe kama Mwl Mzee Mohamed umekuja na maneno ya andikeni na nyie

Unataka mjadala mwingine mpya ambao mtashiriki nyie tu kwasababu kukosolewa hamkupendi sasa mnataka mlishane wenyewe kwa wenyewe

Mimi sijauona huo Udini wa Mwanakijiji unaousema hapa
 
Last edited by a moderator:
Ami,

..hebu punguza udini ndugu yangu.
JokaKuu! .Msiwe mnasingizia udini kila waislamu wanapodai keki yao ya uhuru.

Nionavyo mimi wafanyabiashara wa asili yoyote ile wanakula jasho lao.Keki hasa iko kwenye maofisi ya serikali.Hawa ndio wanaokula keki kutokana na unga unaopelekwa na wafanyabiashara.Ilibidi kwenye hizi ajira rasmi basi kusiwe na ubaguzi ili kila mtu ale sehemu yake ya keki.
Kumbuka hata wazee wetu walipopigania uhuru hawakupigania ili waje wawe wafanyabiashara bali waingie serikalini kuongoza wafanyabiashara,wavuvi,wafugaji na wakulima.
Wafanyabiashara watu wa mfumo wakiwapangia janga basi wa kuwaokoa ni Mwenyezi Mungu tu.Hii inathibitisha ni watu wadogo mno katika taifa kuliko waajiriwa wa serikalini.Muajiriwa wa kawaida tu wa TRA akiamua kumfilisi Bakhresa basi hata mwezi haufiki atafunga kila kitu.

..kuhusu Maalim Seif na kikao cha masuala ya ZNZ, hivi unataka kusema kwenye serikali ya ZNZ Muislamu ni Maalim Seif peke yake, wengine wote ni Wakristo??.
Maalim Seif peke yake ndiye watu wa mfumo wanayemhofia na si kwa kuwa ni muislamu pekee bali uislamu wake haufichi kwa kiwango fulani.
..Kitwana Kondo ninavyokumbuka alishindwa na Frank Magoba. Huyu alisimamishwa na chama cha CUF. Je, unakituhumu chama cha CUF, Maalim Seif akiwa Katibu Mkuu, kushiriki mpango wa kumhujumu Muislamu mwenzake Kitwana Kondo??..
Kwenye siasa mfumokristo unajali zaidi kuliko kwenye wafanyabiashara.Mfumo unapenya bila kizuizi kwenye vyama vyote.Hivyo Seif anaweza asijue Frank Magoba aliingiaje na kutokaje.Magoba asingeweza kumwangusha Kitwana Kondo kwenye jimbo alilo na ushawishi nalo na hakuwa na rekodi mbaya katika jimbo lake.

..Prof.Lipumba anakosa uraisi kwasababu chama chake hakina nguvu huku Tanganyika, siyo kwasababu ya dini yake. .
Hadithi ya Lipumba ni kama ya Seif.Na chama cha Lipumba hakina sababu ya kukosa nguvu isipokuwa mfumokristo ndio unaokipiga vita.
Huu mfumo unaingilia masuala yote ambako waislamu wapo.Hata mahakama hazifanyi kazi yake hasa inapokuwa watuhumiwa ni waislamu.Sio kama tunavyodanganywa.

Taarifa nilizonazo ni kuwa sheikh Ponda mwishowe atafungwa na si kwa kuwa ana kosa bali mfumo tu unataka kuonesha jeuri yake na unapata kiburi kumuachia akarudi msikitini kwake.
 
Tuendelee..
Nithibitishie uchochez wa Moh Said..
Bi maana bado sijashawishika hadi sasa,na Yericko kabakia kuwa chakubimbi wa hoja za watu tuh,hadi sasa kagoma kuchukuwa pesa kwenda TBC kutuchukulia ile Audio speech..
Hii inaleta walakini sana..

THE BIG SHOW,

..uchochezi wa Mohamed Said ni pale anaposema hatua za kuwekwa kizuizini baadhi ya mashekhe ilitokana na chuki za kidini, na siyo masuala ya siasa.

..sasa sisi wengine tume-argue tena na tena kwamba walioswekwa ndani hawakuwa mashekhe tu, au waumini wa dini ya Kiislamu.

..wananchi waliotiwa msukusuko na Mwalimu Nyerere walikuwa wa imani mbalimbali siyo Waislamu peke yao. Mfano mdogo ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi, ambao Mohamed Said anataja Waislamu peke yao, tena wale wenye nasaba naye, huku akiacha wengine wa imani tofauti.

..Jumuiya na vyama vya wafanyakazi zilivunjwa na kuundwa JUWATA, lakini Mohamed Said anazungumzia jumuiya ya Waislamu peke yake.

..Utaratibu wa MACHIFU ulifutwa, lakini Mohamed Said halalamiki kuhusu hilo. Sababu ni nini? Kuna maeneo yamerudi nyuma baada ya Machifu kuondolewa maana wale viongozi wa Tanu waliochukua nafasi zao walikuwa ndiyo watega kazi wakubwa waliokuwa wakikwaruzana na Machifu.

..Vyama vya Ushirika navyo vilivunjwa, shule na hospitali za makanisa zilitaifishwa, etc etc , kwanini kwa miaka 15 sasa Mohamed Said hazungumzi kuhusu maamuzi yote hayo niliyoyaorodhesha anazungumza mambo ya uchonganishi tu kati ya Waislamu na Wakristo??

..matokeo ya uchochezi huu wa Mohamed Said, ndiyo unaona sasa tuna vijana kama Ami ambao kila jambo wanaliangalia kwa kurunzi la Uislamu vs Ukristo. Hivi huoni kwamba mwisho wa yote haya ni mbaya? What do u need kuelewa kwamba mafarakano ya kidini hayana mshindi??

cc: gombesugu, Jasusi, Nguruvi3, Wimana, Son of Alaska
 
Last edited by a moderator:


Nakufuatilia JokaKuu,nakufuatilia vyema sana..
Labda nikuulize kitu kimoja,wewe una pata taabu kwa hoja za Moh Said kueleza hao wazee waliwekwa kizuizin kutokana na chuki za kidini kwa kupinga ushahid uliotolewa au kwa kuchukua ufananisho wa watu wengine ambao waliwekwa kizuizin pia??
Usikute hao waliwekwa kizuizin kwa sababu zao ambazo walistahiki kuwekwa nazo,sasa unataka Moh Said asizungumze anayoyafaham eti kwa kuchelea wengine ambao waliwekwa kizuizin kwa sababu zao??
 
Last edited by a moderator:
Ami,

..hapana, harakati za uhuru zilikuwa na nia ya kujenga Tanganyika mpya ambayo haitakuwa na ubaguzi wa aina yoyote, katika nyanja zote.

..kudai kwamba watu walikuwa wanagombea nafasi za kazi serikalini ni kuleta utani wakati wenzako tunajadili mambo mazito.

..mimi sina tatizo na wafanyabiashara kula jasho lao. lakini natatizwa ni hali ambapo WAZAWA wa nchi hii hawaonekani ktk umiliki wa biashara kubwa kubwa, ambazo ndiyo mhimili wa uchumi wa nchi hii. sasa hivi ni miaka 52 toka tupate uhuru, kwanini biashara zote kubwa bado zimo mikononi mwa jamii zilezile zilizokuwa zikihodhi shughuli hizo wakati wa mkoloni??

..Kuhusu Kitwana Kondo vs Frank Magoba, what exactly r u trying to say?? Kwamba mfumo Kristo uliiba kura kwa niaba ya CUF? Hebu funguka zaidi tuweze kukuelewa.

..Tukirudi kwenye suala la Shekhe Ponda, aliyeuza kiwanja na aliyenunua hicho kiwanja wote ni Waislamu. Kitu gani kinashindikana kwa Waislamu kuamua suala hilo wao wenyewe?? Hata hapo napo mtadai "mfumo Kristo" ndiyo kikwazo??
 
Last edited by a moderator:
THE BIG SHOW,

..msingi wa hoja za Mohamed Said una walakini.

..ushahidi alioutoa haukidhi conclusions zake.

..zaidi, kuna wakati Mohamed anaficha taarifa mbalimbali ili kuhalalisha conclusions zake.
 
Last edited by a moderator:
THE BIG SHOW,

..msingi wa hoja za Mohamed Said una walakini.

..ushahidi alioutoa haukidhi conclusions zake.

..zaidi, kuna wakati Mohamed anaficha taarifa mbalimbali ili kuhalalisha conclusions zake.


Kabla hujakiona kibanzi kwenye jicho la Moh Said,hebu kwanza toa boriti kwenye jicho lako Jokakuu..
Moh Said is a peaceful musliman..
Huo ndio ukweli wenyewe..
 
Kabla hujakiona kibanzi kwenye jicho la Moh Said,hebu kwanza toa boriti kwenye jicho lako Jokakuu..
Moh Said is a peaceful musliman..
Huo ndio ukweli wenyewe..
THE BIG SHOW,

..Mohamed Said ana chuki binafsi na Mwalimu Nyerere.

..ndugu zake walitiwa kizuizini wakati wa utawala wa Mwalimu.

..mtu kama huyo anapoandika kitabu kuhusu zama hizo unategemea nini?

..binafsi sina shida na yeye kuandika vitabu, lakini wakati anafanya hivyo angepaswa kueleza hiyo background yake.
 
Last edited by a moderator:
Gombesugu.
Mkuu nimekusoma uko vizuri yaani umefanya siku yangu yaleo imalizike kwa furaha, umeandika kwa hisia sana na kwa utulivu sana ambae hatakuelewa atakuwa ni kiburi chake dah pongezi nyingi kwako nimepata elimu kubwa kutoka kwakolakini najua kuna watu huku matusi na kejeli ndio sera zao hawata acha kutukana lakini ukweli utabaki kuwa pale pale BIG UP INSHAALAH MUNGU AKUPE UMRI MREFU NA ILMU YENYE MANUFAA.
 
Kahiyo ndio ulitengeneza hotuba ile! again backing off! Alaa kumbe hakuandikiwa akaenda kuusoma kama ulivyo! hapa mnakasha umefanya kazi. Tuendelee
 
Wakuu JokKuu na Jasusi, heshima mbele sana. Nawaombeni sana sana msielekee mtoni.

Kuna mtu kasema Ponda atafungwa na mfumokristo ili kuonyesha nguvu zake. Mtikila ambaye ni kiongozi wa mfumo naye alifungwa na mfumo huo huo kuonyesha nguvu zake.

Wakuu tuendelee na mnakasha tukiangalia tusijeingia mtoni na kuoga na watoto. Kuna vitu vinatia aibu na uvivu kuvijibu.
Naomba mviangalie tu mpite zenu! Ndio matunda ya mzee wetu hayo, kazi ya miaka 15 hiyo.
 

Wana jamvi,

Jambo la kufurahisha ni kuwa Mohamed na wafuasi wake kwa miaka 15 ya kupotosha umma leo wanakiri wazi kutambua mchango wa kanisa/wawakristu katika harakati za kudai uhuru,

Na wanakiri wazi kuwa kanisa liligharamia safari ya Mwalimu Nyerere UNO, lakini kiutu uzima hawawezi kukubali moja kwa moja angalau lazima wapindishe iwe safari ya pili japokuwa hawajui mantiki inabaki ileile,

Nimshukuru Mungu kwakuwafungua hawa viumbe akina Mohamed Said na wa aina yake.

Historia ipo, haiwezi kubadilishwa kwa hila na mtu mmoja ama kukundi kwa maslahi binafsi hata kwa chembe ya haradari.
 
Nguruvi3,
I am sick of this kinds of arguments raised by Ami!
Pamoja ni migawanyiko wa kidini ulimo kwenye hii thread, siamimi kama Big Show, Ritz na Shehe Said watakubaliana na hoja yako hii dhaifu.
Prof Lipumba hawezi kupata Urais kwa kuwa ni Muislamu! JK alibatizwa kabla ya kuchaguliwa kuwa Rais?
This is too low. Kama wenzako watakubaluna nawe kwa arguments na mitazamo ya aina yako, basi Waislamu wana safari ndefu sana...
 
Alikiri kinamna kwa sababu baada ya kushutumiwa hivyo na Kambona alipohutubia Jangwani hakuweza kukanusha.
Wewe umeamua kunijibu mimi hivyo hapa.Mbona ULISHINDWA KUMJIBU KADOGOO
Kwa hiyo nikikutukana kuwa wewe ni mpu*bavu na ukikaa kimya maana yake wewe ni........? What logic? Na ile ya Kadogoo nadhani sikuiona. Kuna threads naona ninaruka kwa sababu ya majukumu.
 

Ohh boy, this is nasty!! Is there an ambulance nearby?
 
gombesugu;6093671] Mbona leo ustaarabu na dasturi zako unataka kuziharibu ukubwani,si utawaangusha wana-Mjesani wenzio hivyo!?
Sisi wamjasani tunamsoma vema tu na kumwelewa, na si mjasani hata Potwe, Mkuzi, mashewa na Kicheba sote tunatumia macho na fikra zetu. Tunamwelewa wala hilo lisikutie wahka ustadh Gombesugu. Ni mnakasha tu.
Most peace loving,clear minded and impartial people,kama watayaona maandiko yangu machache humu na hasa ile bayana yangu ya mwanzo kwa Mohammed Said,basi nina hakika watanipa japo benefit of doubt kama si kukubaliana na mengi nilosema.
Mbona watu walishatoa benefit of doubt, bahati mbaya ukaiondoa mwenyewe. Ulisema hivi ''maandishi ya Mohamed yana makosa madogo madogo''.

Hukuwaeleza yapi ni madogo na kwa kigezo gani.
Mtu hawezi kuandika habari usiokuwa na ushahidi nayo ukasema ni kosa dogo.
Mtu hawawezi kutoa hukumu kwa mwingine huku akiwa ameficha ukweli ukasema ni kosa dogo.
Lakini uliposema kila mtu aende akaandike vitabu, laaa! hapo ndipo doubt ikanitoka Kosa! unachotaka kusema ni kuwa hapa JF mahali penye fikra huru pageuzwe kuwa na sehemu za watu wenye mrengo fulani pengine imani au ukabila ili wajadili kile wanachoona kinawafurahisha.
Hapana! utakuwa katika wrong forum na pengine fikiria kama unasababu za kuendelea kuwepo hapa.

Kufanya hivyo ni kuendeleza yale tunayoyakataa ya kubaguana kwa ''interest''.
Kwa taarifa yako hii ni mara ya tatu tumekuwa na uzi kama huu na Mohamed.

Tunachofanya hapa ni kuweka rekodi sawa sawa, kufahamishana, kueleweshana n.k. Kila mtu anajifunza kutoka kwa mwingine. Kwahiyo wazo la kuwa na uzi mwingine ni zuri lakini hilo halisababisha watu wasichangie kwa mitazamo, ukweli na maono yao.

Lau kana unataka mjadala na shule zaidi ya Mohamed kitabu kipo dukani mwaka wa 15 na unaweza kufanya PM hapa JF.
Ukishaweka mada,basi umealika ndugu jamaa na marafiki na hapo hakuna favor or fear.
Mada itahudumiwa kwa mujibu wa kanuni na taratibu, itapewa heshima stahiki bila kuangalia kigezo kingine isipokuwa mada Labda kama sijui maana ya typo error, ninachoweza kukuambia ni kuwa makosa ya Mohamed ni makubwa sana na ameyafanya maksudi.

Kitabu kipo toleo la nne laja sijui kwanini hajaweza kuona typo error!
Hawezi kuandika kuwa Warioba alitoka porini bila credential na hakujulikana katika Cabinet ukasema niyo typo error! haa!

Hawezi kuandika kuhusu maulidi na kusema aliyehudhuria alikuwa makamu wa Rais tena kuonyesha umuhimu wa mtu huyo na hoja yake halafu useme hiyo ni typo error! Yarabi.

Hawezi kuficha ukweli na kusema Nyerere alikuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka 1950 na kukutana na Sykes ukasema hiyo ni typo error!

Hawezi kusema Sheikh Amir alifukuzwa tu ukasema hiyo ni typo error
Hawezi kusema Hamza Azizi alitupwa na Nyerere na kuficha kisa cha ajali iliyompleleka ubalozi hilo likawa typo.
Hawezi kutoa madai ya kanisa kuua EAMWS bila ushahidi, hilo likawa typo.
Hawezi ukapachika manamba kutoka kichwani na kusema hiyo ni stats, ukasema ni typo error
Hawezi kudai sensa ya mwaka 1957 anayo peke yake ukasema ni typo
Hawezi kudai Sykes ndiye alianzisha AA na kuwa katibu peke yake ukasema hiyo typo
Hawezi kudai wazulu, wamanyema na wanubi ndio wamekomboa nchi hii ukasema hiyo typo.
Orodha inafika kurasa 17 kwa kutaja, leo unatufanya wajinga tuamini ni typo! skill yako ya analysis unaituimia wapi mkuu!

Kibaya zaidi hawezi akashindwa kusimama na kueteta hoja zake ukasema hiyo ni typo!
please please find the better word to please him and yourself not typo error. Absolutely anachronism

Kuhusu Nyerere, nadhani unakumbuka kuwa alipoacha utawala ni wakati huo magazeti na redio zilianza kuwa huru kama vyombo binafsi. Nyerere ameandikwa sana hata kutukanwa si kwa utawala bali hata kile kizuri alichofanya.
Nyerere ametukanwa ndani na nje ya nchi. Hata siku moja hukumsikia akisimama kujibu tuhuma za watu.

Mfano, wakati wa vyama vingi pale jangwani, watu wengi walitaraji Nyerere kumcharura sana mrema na upinzani.
Yeye alichokisema kilishangaza watu. Alisistiza umuhimu wa kujiandikisha na kupiaga kura. Akamalizia kwa kusema kama kuna mtu anataka kubebwa mwacheni amevunja sheria gani? Hapa alikuwa anaiasa serikali isilete fujo kwa wapinzani na si kwa mrema. Hizo ndizo tabia za statesman.

Sasa kama Nyerere alikuwa aje kujibu kitabu cha Mohamed sijui Mohamed ni nani wa kumlinganisha kwa fikra hoja na maono kama Nyerere. Hili nasema wazi kumweka Mohamed na Nyerere chungu kimoja ni kumdhalilisha sana Nyerere.
Nyerere na Mohamed hakuna mahali wanakutana ! hakuna, Nasema hakuna mahali wanakutana!

Nyerere kutojibu madai ya Mohamed ni sawa na yale yale aliyoyafanya kwa vyombo vya magharibi.
Busara ndizo zilikuwa zinamtangulia kwa kujua kuwa kujibizana na watu wanamna hiyo ni kuingia mtoni na watoto atachafuka.

Nyerere hana sababu za kumjibu Mohamed kwasababu matendo na kazi yake ndizo zinamjibu.
Muda wa kukanusha kuwa yeye alikuja Dar mwaka 1947 na si mwaka 1950 huo hakuwa nao na wala hafai kujibu tuhuma za kiupuuzi kama hizo.Nyerere alikuwa world figure na si mtu wa dunia ya Narung'ombe.

Kuhusu serikali kujibu madai ya waislam, hapa napata tabu sana. Kwanini Nyerere isakamwe kwa kutojibu madai hayo(kama Mohamed ndio Waislam as whole) halafu leo tunataka serikali ijibu.

Mohamed keshasema kuwa serikali ina taarifa, tumemeuuliza hili la serikali kujibu limeanza lini?
Mbona huko nyuma tuhuma zilikuwa za Nyerere na si serikali?

Nadhani nami naungana mkono na wewe na wengine kuwa sasa ni wakati Rais Jakaya Kikwete ajibu kama alivyokuwa anatuhumiwa Nyerere na wala si serikali ili tusiwe na double standard.

Kuhusu Warsha na kupata deportation, hilo tumelijadili sana na nadhani kwa ugeni wako umefikia conclusion kabla ya kupitia nyuzi kwa undani.

Aliyepewa deportation ni Maliki Mpakistani aliyekuja kufundisha watanganyika jinsi gani wanaonewa.
Alipewa PNG. Huyu ndiye mwanzo wa tatizo la chuki, fitna na farki.
Hawa akina Mohamed na Warsha ni mali ya Maliki FYI.
Ps:Nguruvi,Mag3
Naona Wataalamu mmenivamia kama nyuki,lakini haina neno najua tuko pamoja na tunaipenda nchi yetu!ahaha!!
Naheshimu sana michango yenu humu!
Nashkuru kwa taarifa. Naheshimu pia mawazo yako na sote ni Watanzania kwa lengo moja la kuishi kama ndugu.
 
Mkuu Mag3

Naomba nifanyie hisani ya kunifungua zaidi juu ya huyu Maliki FYI.
 
Nguruvi3 hapa umemaliza kila kitu Nyerere kweli wa kumjibu MS,----- kiss my a---

"Sasa kama Nyerere alikuwa aje kujibu kitabu cha Mohamed sijui Mohamed ni nani wa kumlinganisha kwa fikra hoja na maono kama Nyerere. Hili nasema wazi kumweka Mohamed na Nyerere chungu kimoja ni kumdhalilisha sana Nyerere.
Nyerere na Mohamed hakuna mahali wanakutana ! hakuna, Nasema hakuna mahali wanakutana! "
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…