Muheshimiwa Mwanakijiji,
Nashukuru sana kwa kunikaribisha. Nimekufahamu kiduchu kwenye maelekezo yako ulonipa.
Napata fadhaa kidogo unapoanza kwa kunishuku
Udini,lakini haina neno maana nahisi ndio mambo ya kwenye hii thread/JF.
Nilipoingia tu humu,kuna wale nao walonishuku hasa kutokana na ile bayana yangu ya mwanzo nilomwandikia
Mohammed Said . Labda na wao walipata elements fulani za
Udini kwenye maandiko yangu(wala silaumu saana,si unajua sisi watu wa Madrasa soote tunashabihiana kama ma-Chinese!). Kuna wengine pia wakahisi labda Mohammed Said anafanya
exit strategy kwa kutumia
multiple IDs! Once someone harbours that kind of childish thoughts, easily inclined to prejudice and bigotry,which more likely resulting to an
infectious mindset.
Nahisi na wewe Bwana Mwanakijiji labda una dasturi ile ile mnayosema kila mara dhidi ya
Mohammed Said,ati kwamba anafanya saana conclusions zenye kuangukia kwenye
Udini!? Kuna pahala umetaja na kujinasibu u-
Tanga wako na kuwa umelelewa na kukulia pale. Mbona leo ustaarabu na dasturi zako unataka kuziharibu ukubwani,si utawaangusha wana-
Mjesani wenzio hivyo!?
Most peace loving,clear minded and impartial people,kama watayaona maandiko yangu machache humu na hasa ile bayana yangu ya mwanzo kwa
Mohammed Said,basi nina hakika watanipa japo
benefit of doubt kama si kukubaliana na mengi nilosema.
Pale uliposema ati unajua "
damu nzito kuliko maji" na kunishuku kuwa sababu zangu za kumkubali Mohammed Said ni kwa sababu ya
Udini,hasha! Tatizo hili la fikara za Udini na kugawanya watu baina ya
wao na sisi,kila siku mnamlaumu
Mohammed Said kumbe na wewe pia unalo!? Infact, I'm little bit saddened with your choice of some words describing my thoughts. I think it is bordering question my analytical skills.
Ni muhimu pia utambue,mimi sipo hapa kwa malumbano wala
Udini. Nimesha-declare tangia kwenye ile bayana yangu ya mwanzo nilomwandikia Mohammed Said. Mintaarafu yangu ilikua kumshauri na kumsihi aachane na thread hii na afungue nyingine ili kuendelea na mafundisho yake ya
Historia. Maana nilishaona muafaka hapa aidha ni mdogo saana au hautakuwepo kabisa,matokeo yake kuna mengi yanasemwa na kashfa kutawala kwa watu kadhaa na Imani zeetu! Mimi binafsi bila ya kuficha kuna mengi nataka kuendelea kujifunza na kujua kutoka kwa
Mohammed Said, na ndo maana nikamwomba afungue thread/baraza nyingine ili kwa sisi tunaomkubali na kumtaka iwe wepesi kumsoma na kujadiliana kwa undani nae.
Hivyo vipengele ulivyoninyambulia na kuonyesha kwa madaha udhaifu wa hoja za Mohammed Said ,wala haina haja ndugu yangu. Maana nishaiona hiyo athari ya huo mzunguko na kurembeana kusokwisha baina yenu na
Mohammed Said.
Mwanakijiji, naona umetajwa mara kadhaa humu kuwa wewe ni
mwandishi na mtaalamu mahiri,sasa sijui hizo
ethics zenu za uandishi zinakua wapi pale unapoweka allegations/accusations nzito nzito kwa mwandishi/mtaalmu mwenzio,ati kisa mmekhitilafiana kwenye fani yenu au hukubaliani na hoja au maandiko yake fulani!? Si rahisi kama utakavyo kuwa kila atakaeingia humu hata bila ya Udini amkatae Mohammed Said kama unavyotamani. Na asipofanza hivyo inakuwa katweka maarifa,hana mantiki,haangalii mambo kwa utaalamu wa kisayansi n.k Hypotheticaly speaking,tujaalie waTanzania woote tuwe upande mmoja,halafu Mohammed Said awe yeye peke yake,sasa hiyo democracy ya kujadili mambo na kumkosoa kwa kina itatokea wapi!? Hapa unanikumbukusha ile
myth ya WWII.
Pia nimesoma pahala unajinasibu kuwa wewe ni mtoto wa
Mchungaji wa Kanisa na pia ilikua moja ya shughuli zako ni kushindana kwenye ile
mihadhara ya malumbano ya kidini pale viwanja vya Jangwani na kina Mwaipopo. Na unadai pia hawakufua dafu juu ya umahiri wako wa malumbano.
Ama kwa hakika niliathirika kidogo nilipoona jambo lako hili,I must admit that my sense of judgement has been coloured since!
Ama kwa hakika mimi ndio natakiwa niwe na shaka ya Udini juu yako na labda pia motives zako kwenye thread hii,not the other way round!
Mimi binafsi nilikua nikichukia saana yale mambo ya mabishano ya kidini,maana nilishajua athari na matokeo yake. Kumbe wewe
Mwanakijiji ndio ulikuwa mmojawapo wa vinara pale!? Halafu jinsi unavyomlaumu kila mara kina
Njozi,Dau,Mohammed Said na WARSHA ni kama vile wewe ni malaika,au kwa sababu umeshaacha na kujirekebisha!Tuacheni utoto jamani!
Ndugu yangu pia mmenisikitisha saana kumwacha
Gwalihenzi bila hata ya kumuasa, ajifiche nyuma ya pazia la ati kujifanya hana dini/Atheist,na kutukana
Uislamu/Waislamu humu pita kiasi mpaka nalipatwa na homa! Halafu mnadai ati manakumbuka saana mapenzi yalokuwapo zamani baina yetu na kuwa
Mohammed Said ndio mbaya na mchochezi!? Hivi nyinyi nyoote mmeshindwa hata kumuonyesha
RED au kumsihi kwa yale matamshi yake(nakumbuka mimi nilionyeshwa RED na ndugu yangu
JokaKuu pahala fulani,japo mimi bado ni mgeni saana humu)!? Maskini mkamwacha
Kadogoo peke yake amsihi na ndo pale
Gwalihenzi alizidi kibri,je tunaelekea wapi huko
waTanzania!?
Kwa wengi humu mnaompinga
Mohammed Said japo kwa dhamira njema,lakini huwa manapoteza credibility zenu pale mnapomsakama pita kiasi na hasa kwenye vijimakosa viduchu mno,kama vile minor typographical errors,halafu ndo watu kadhaa kushikilia ki-point hicho hicho na kufanya mdahala na darsa nzima kwenda out of context. Naona hii ndo inazidisha tafrani kwenye nyoyo za wengine na kuhisi labda kuna
hiden agenda/propaganda ya kutaka kumnyamazisha Mohammed Said na ndipo wengi saana wanataka kumsoma zaidi and in particular Muslims!?
Mwanakijiji; kama ni kweli kwa shutuma na wasiwasi ulotoa dhidi ya
Mohammed Said basi kipata fursa na wasaa nijaalie majibu japo kiduchu kwa haya hapa nchi yanayonitatiza:
- Hivi unahisi kuna mantiki gani ilomfanya Bwana Julius Nyerere ashindwe au asitake asilani kumjibu Mohammed Said kwa maandishi au japo kumkemea kwenye vyombo vya habari kwa miaka yoote ile!? Maana soote tunaaambiwa kuwa Nyerere kwenye ukweli, maslahi ya Taifa,na hasa kuhatarisha amani alikua hana ngoja ngoja!?
- Wengi wenu humu mmeonyesha umahiri na sifa kadhaa za Nyerere,na ukali wake,uadilfu na mengineyo mengi nami sina shaka nakubali ni kweli kabisa. Zaidi ya yoote tunaambiwa kuwa Nyerere aliipenda saana nchi na watu wake. Sasa inakuwaje huyo huyo Nyerere alijua fika kuwa Mohammed Said kaandika uzushi,Udini,kashfa,fitna na kumdhalilisha kihistoria yeye binafsi na family yake, na huenda pakawa na zogo au "janga" kwenye nchi kwa kitabu au habari hizo. Halafu yeye Nyerere akaamua kunyamaza tu!? Sasa hamuoni nyinyi ndo mmnavunjia hishma Nyerere kwa sababu mnaonyesha kuwa alikuwa ni mtu irresponsible na dhaifu na hakujali amani ya nchi!?
- Mbona Nyerere mara kadhaa aliweza kuwafokea Lowasa,Mwinyi na Malecela tena hadharani,ndio alishindwa "kumshughulikia" Mohammed Said!?
- Tunajua saana kuwa Nyerere hata alipostaafu lakini bado alikuwa anakubalika na wananchi wengi na pia alikuwa na inffluence kubwa saana kwa marais walomfuatia Mwinyi na Mkapa. Basi alishindwa hata kuwashauri hata wao kuondoa hilo "janga la kihistoria" toka kwa Mohammed Said. Maana mmetaja hapa kuwa WARSHA "ilishughulikiwa" kilivyo na wengine kupata deportation.
- Mwanakijiji,kuna wakati na kwa sababu uzijuazo wewe binafsi ulikua unahaha kutaka kuandika kitabu kuhusu Rostam Azizi(japo sina hakika kuhusu nini,au ilikua ni biography tu!?). Na ulikua unatafuta watu wowote walokua ati wanamjua kwa njia na nyakati tafauti(shule,Univ. au kikazi) na uliomba wakutafute kwa haraka,na uliacha mpaka contact details zako! Pia unadai ulikua unawafuatilia habari zao kwa makini kina Dau,Njozi,Mohammed Said na WARSHA na ulishajua athari zao kwa Taifa hili kipindi kirefu. Sasa mbona miaka yoote hiyo umekua kimya na hukumjibu kimaandishi/kitaalamu huyu Mohammed Said. Hivi kweli inaingia akilini,ati uwe na muda wa kuandika kitabu/habari za Rostam Aziz na uache kufanya uzalendo ili kepusha maafa/janga kwenye nchi yako kwa kumvunja kimaandishi "mchochezi" Mohammed Said!? Na mpaka sasa hivi bado unadai uko busy huwezi kumjibu,wakati unajua kuwa uandishi wako na utafiti ni muhimu zaidi kwa hivi sasa kutuepusha na hilo "janga" la Mohammed Said!?
- Kama kuna watu/kikundi hawakubaliani na maandiko ya Mohammed Said,kwanini isitumike Judicial System halafu mahakama ndo isikilize pande zoote kwa undani na kufanza maamuzi yake!?
- Kama kuna cross section of our society,inahisi kuonewa au kufaniwa dhuluma,na kila kukicha wanatoa malalamiko ambayo wanahisi ati ni ya msingi na ya kitambo na kuwa Serikali haiyashughulikii,sasa kuna ubaya gani wapewe nafasi ya kusikilizwa!? Na wewe unapodai kuwa ati hakuna tatizo kabisa,na wakati walalamikaji au wanaodai kuumia ni wengine!? Je hapa unatumia mantiki gani Mwandani wangu!? Je utajuaje kunguni wa kitanda usichokilala!?
Kwa ufupi,
Bwana Mwanakijiji kama kweli kama unavyodai kuwa kuna janga kubwa ndani ya maandiko ya
Mohammed Said,basi wa kulaumiwa ni wewe
Mwanakijiji na
Nyerere kwa kushindwa kumjibu kitaaluma tangia wakati huo! Japo inanilazim nimsamehe
Bwana Nyerere maana yeye kishatangulia mbele ya haki.
Hebu fikiria ule muda ulopoteza pale viwanja vya Jangwani wakati huo kwenda kushindana na kina Mwaipopo kwenye malumbano ya kidini,na kama ungeutumia kufanya utafiti wa kina na kuandika kitabu cha "kumshushua"
Mohammed Said kitaalamu,unafikiri leo yangefikia haya kweli!?
Ahsanta kwa kukubali kuelimishana.
CC;Ami,The Big Show,Kadogoo,Ritz,Sheikh Mohammed Said,Barubaru,Boko Haramu,Jokakuu,Nyambala
Ps:Nguruvi,Mag3
Naona Wataalamu mmenivamia kama nyuki,lakini haina neno najua tuko pamoja na tunaipenda nchi yetu!ahaha!!
Naheshimu sana michango yenu humu!