Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Muheshimiwa Mwanakijiji,
Nashukuru sana kwa kunikaribisha. Nimekufahamu kiduchu kwenye maelekezo yako ulonipa.
Napata fadhaa kidogo unapoanza kwa kunishuku Udini,lakini haina neno maana nahisi ndio mambo ya kwenye hii thread/JF.
Nilipoingia tu humu,kuna wale nao walonishuku hasa kutokana na ile bayana yangu ya mwanzo nilomwandikia Mohammed Said . Labda na wao walipata elements fulani za Udini kwenye maandiko yangu(wala silaumu saana,si unajua sisi watu wa Madrasa soote tunashabihiana kama ma-Chinese!). Kuna wengine pia wakahisi labda Mohammed Said anafanya exit strategy kwa kutumia multiple IDs! Once someone harbours that kind of childish thoughts, easily inclined to prejudice and bigotry,which more likely resulting to an infectious mindset.
Udini haujifichi; hisia ya ubora wa mtu na dini yake unakuwa wazi kama jua la asubuhi hata likifunikwa na mawingu.
Nahisi na wewe Bwana Mwanakijiji labda una dasturi ile ile mnayosema kila mara dhidi ya Mohammed Said,ati kwamba anafanya saana conclusions zenye kuangukia kwenye Udini!? Kuna pahala umetaja na kujinasibu u-Tanga wako na kuwa umelelewa na kukulia pale. Mbona leo ustaarabu na dasturi zako unataka kuziharibu ukubwani,si utawaangusha wana-Mjesani wenzio hivyo!?
Ustaarabu na desturi sikufundishwa na watu wa Tanga; nimefundishwa na familia yangu ambayo kwa asili inatoka bara. Tanga ni nimeongezea tu mambo ya elimu na mahusiano ya watu wengine lakini credit ya ustaarabu na desturi inawaendea watu wa bara. Of course, Tanga kwa kiasi kikubwa pana nafasi ya pekee moyoni mwangu.
Most peace loving,clear minded and impartial people,kama watayaona maandiko yangu machache humu na hasa ile bayana yangu ya mwanzo kwa Mohammed Said,basi nina hakika watanipa japo benefit of doubt kama si kukubaliana na mengi nilosema.
Kwa kweli baadhi yetu tulikupa benefit of the doubt and some of us still do. Unajitahidi kuwa balanced lakini mizani yako kama inavyojionesha hapa chini imeelemea upande fulani.
Pale uliposema ati unajua "damu nzito kuliko maji" na kunishuku kuwa sababu zangu za kumkubali Mohammed Said ni kwa sababu ya Udini,hasha! Tatizo hili la fikara za Udini na kugawanya watu baina ya wao na sisi,kila siku mnamlaumu Mohammed Said kumbe na wewe pia unalo!? Infact, I'm little bit saddened with your choice of some words describing my thoughts. I think it is bordering question my analytical skills.
As a matter of fact I do! I'm questioning not just your analytical skills but the lack of intellectual vigor of understanding the nature of Mohammed Said's argument against Nyerere, Christians and the Church in Tanzania. It seems for whatever reason you do not want to accept the fact (easily seen) that Mohammed Said's 'pseudo-history' is fundamentally based on his religious context. He has approached the whole subject with a mentality of "us versus them' where by the "us" are the Muslims and "them" the Christians. Kama hujaelewa hili na unakubali tu kuwa Mohammed Said ameandika kazi ya historia kwa sababu anataka kujazia pale palipopungua basi you very analytical skills need to be questioned and if or when necessary discredited.
Ni muhimu pia utambue,mimi sipo hapa kwa malumbano wala Udini. Nimesha-declare tangia kwenye ile bayana yangu ya mwanzo nilomwandikia Mohammed Said. Mintaarafu yangu ilikua kumshauri na kumsihi aachane na thread hii na afungue nyingine ili kuendelea na mafundisho yake ya Historia. Maana nilishaona muafaka hapa aidha ni mdogo saana au hautakuwepo kabisa,matokeo yake kuna mengi yanasemwa na kashfa kutawala kwa watu kadhaa na Imani zeetu! Mimi binafsi bila ya kuficha kuna mengi nataka kuendelea kujifunza na kujua kutoka kwa Mohammed Said, na ndo maana nikamwomba afungue thread/baraza nyingine ili kwa sisi tunaomkubali na kumtaka iwe wepesi kumsoma na kujadiliana kwa undani nae.
Naam!
Hivyo vipengele ulivyoninyambulia na kuonyesha kwa madaha udhaifu wa hoja za Mohammed Said ,wala haina haja ndugu yangu. Maana nishaiona hiyo athari ya huo mzunguko na kurembeana kusokwisha baina yenu na Mohammed Said.
Wewe ndiye uliyedai kuwa tunabishana juu ya maoni; hoja yangu ni kuwa hatubishanii maoni tunabishania facts; historical fact for that matter. Wewe kutokuelewa hilo na hata kukwepa kuangalia mifano niliyotoa (japo michache) kunaonesha tu you - like some of Mohammed's supporters - are not interested in facts but mere opinions on what has been claimed to be factual.
Mwanakijiji, naona umetajwa mara kadhaa humu kuwa wewe ni mwandishi na mtaalamu mahiri,sasa sijui hizo ethics zenu za uandishi zinakua wapi pale unapoweka allegations/accusations nzito nzito kwa mwandishi/mtaalmu mwenzio,ati kisa mmekhitilafiana kwenye fani yenu au hukubaliani na hoja au maandiko yake fulani!? Si rahisi kama utakavyo kuwa kila atakaeingia humu hata bila ya Udini amkatae Mohammed Said kama unavyotamani. Na asipofanza hivyo inakuwa katweka maarifa,hana mantiki,haangalii mambo kwa utaalamu wa kisayansi n.k Hypotheticaly speaking,tujaalie waTanzania woote tuwe upande mmoja,halafu Mohammed Said awe yeye peke yake,sasa hiyo democracy ya kujadili mambo na kumkosoa kwa kina itatokea wapi!? Hapa unanikumbukusha ile myth ya WWII.
"Myth of WWII" ... oh yeah? nitaiacha lakini inaelezea tu unasimamia wapi.. Lakini upande mwingine ni kuwa I don't consider Mohammed Said mwandishi wa historia; yeye ni msimulizi tu wa vitu ambavyo anatumia historia kuvipamba. Unapozungumzia 'ethics" siyo tu ethics za uandishi bali kuna ethics zinazosimamia uandishi wa historia. Mohammed Said ameshindwa kufuata kanuni na misingi ya uandishi wa kihistoria. Hata nikiamua kumkosoa yaani anaweza kukosolewa kwa pande zote mbili - on the substance of his works and on the methodology of his so called historical research.
Pia nimesoma pahala unajinasibu kuwa wewe ni mtoto wa Mchungaji wa Kanisa
Hapana ulinisoma vibaya; ni mjukuu wa Mchungaji...
na pia ilikua moja ya shughuli zako ni kushindana kwenye ile mihadhara ya malumbano ya kidini pale viwanja vya Jangwani na kina Mwaipopo.
Hapana kushiriki malumbano haikuwa mojawapo ya 'shughuli' zangu na wala haihusiani na mimi kuwa mjukuu wa Mchungaji. Nilikuwa nafanya kama hobby tu ya kukosoa watu wanaotoa hoja vibaya na wakaaminiwa. Ninachofanya leo ni mwendelezo wa kile kile nilichokifanya miaka karibu thelathini nyuma.
Na unadai pia hawakufua dafu juu ya umahiri wako wa malumbano.
Ama kwa hakika niliathirika kidogo nilipoona jambo lako hili,I must admit that my sense of judgement has been coloured since!
Pole sana ndugu yangu kwa kuathirika lakini nitakusaidia. Kinyume na watu wengine ambao wanashiriki malumbano ya kidini mimi sikushikiri kwa maana ya kubishania mistari ya Biblia na Qurani; au ya kushindana ni nani "nabii yule" au kama Mtume Mohammed alitabiriwa katika Biblia. Hayo ningeweza lakini kushiriki kwangu kulikuwa kwenye kukosoa ujengajo hoja wa watu kwa sababu ukishajenga hoja vibaya utafikia hitimisho baya. Hivyo nilichofanikiwa kufanya sana wakati ule ni kuwafanya watu waangalia wanavyojenga hoja na kuonesha makosa ya hoja zao na hivyo wao wenyewe kuweza kuona makosa ya mahitimisho waliyofikia.
Ama kwa hakika mimi ndio natakiwa niwe na shaka ya Udini juu yako na labda pia motives zako kwenye thread hii,not the other way round!
Mimi binafsi nilikua nikichukia saana yale mambo ya mabishano ya kidini,maana nilishajua athari na matokeo yake. Kumbe wewe Mwanakijiji ndio ulikuwa mmojawapo wa vinara pale!? Halafu jinsi unavyomlaumu kila mara kina Njozi,Dau,Mohammed Said na WARSHA ni kama vile wewe ni malaika,au kwa sababu umeshaacha na kujirekebisha!Tuacheni utoto jamani!
Ni matumaini yangu nimeshasahihisha hapo juu; sehemu ambazo nimejaribu kujadiliana na watu kuhusu substance za tofauti za kidini nimefanya hivyo chini ya kanuni kabisa za mijadala ya namna hiyo siyo yale ya Jangwani.
Ndugu yangu pia mmenisikitisha saana kumwacha Gwalihenzi bila hata ya kumuasa, ajifiche nyuma ya pazia la ati kujifanya hana dini/Atheist,na kutukana Uislamu/Waislamu humu pita kiasi mpaka nalipatwa na homa! Halafu mnadai ati manakumbuka saana mapenzi yalokuwapo zamani baina yetu na kuwa Mohammed Said ndio mbaya na mchochezi!? Hivi nyinyi nyoote mmeshindwa hata kumuonyesha RED au kumsihi kwa yale matamshi yake(nakumbuka mimi nilionyeshwa RED na ndugu yangu JokaKuu pahala fulani,japo mimi bado ni mgeni saana humu)!? Maskini mkamwacha Kadogoo peke yake amsihi na ndo pale Gwalihenzi alizidi kibri,je tunaelekea wapi huko waTanzania!?
Hili ni ukosoaji ulio sahihi kabisa; lakini utaniona pia sijakemea watu wanaowasema Wakristu vibaya au Ukristu vibaya au hata kuniita mimi mwenyewe majina mabaya kwa sababu ya tofauti. JIulize kwanini? Kwa sababu naamini tunazungumza na watu wazima kama watu wazima hawajui wenyewe kuchagua maneno ya kiubngwana kujadiliana na hawajui wenywee kubadilishana mawazo kama ndugu mimi nitajivika ukuu wa kuanza kukosoa watu wazima wengine. Hata kwenye siasa utaona malumbano ya watu binafsi siyaingilii kabisa kwa sababu le ile. Mtu mzima akija na kukuuambia utumia lugha nzuri au utumie uungwana manake ni kuwa anakuona uko chini yake ndio maana anakusahihisha. Haya miye nafanya kwa watoto wangu au wadogo zangu; watu wazima watajuana wenyewe vinginevyo tutaanza kutakana nani amkemee nani kama watoto wadogo wakicheza chandimu.
Kwa wengi humu mnaompinga Mohammed Said japo kwa dhamira njema,lakini huwa manapoteza credibility zenu pale mnapomsakama pita kiasi na hasa kwenye vijimakosa viduchu mno,kama vile minor typographical errors,halafu ndo watu kadhaa kushikilia ki-point hicho hicho na kufanya mdahala na darsa nzima kwenda out of context. Naona hii ndo inazidisha tafrani kwenye nyoyo za wengine na kuhisi labda kuna hiden agenda/propaganda ya kutaka kumnyamazisha Mohammed Said na ndipo wengi saana wanataka kumsoma zaidi and in particular Muslims!?
Sasa hapa Gombesugu unatudharau; hatubishani na makosa ya herufi; kusema Nyerere aliingia siasa mwaka 1952 wakati historia inaonesha kuwa alishaingia siasa miaka mingi nyuma siyo suala la herufi; tafadhali ndugu yangu.
Mwanakijiji; kama ni kweli kwa shutuma na wasiwasi ulotoa dhidi ya Mohammed Said basi kipata fursa na wasaa nijaalie majibu japo kiduchu kwa haya hapa nchi yanayonitatiza:
- Hivi unahisi kuna mantiki gani ilomfanya Bwana Julius Nyerere ashindwe au asitake asilani kumjibu Mohammed Said kwa maandishi au japo kumkemea kwenye vyombo vya habari kwa miaka yoote ile!? Maana soote tunaaambiwa kuwa Nyerere kwenye ukweli, maslahi ya Taifa,na hasa kuhatarisha amani alikua hana ngoja ngoja!?
- Wengi wenu humu mmeonyesha umahiri na sifa kadhaa za Nyerere,na ukali wake,uadilfu na mengineyo mengi nami sina shaka nakubali ni kweli kabisa. Zaidi ya yoote tunaambiwa kuwa Nyerere aliipenda saana nchi na watu wake. Sasa inakuwaje huyo huyo Nyerere alijua fika kuwa Mohammed Said kaandika uzushi,Udini,kashfa,fitna na kumdhalilisha kihistoria yeye binafsi na family yake, na huenda pakawa na zogo au "janga" kwenye nchi kwa kitabu au habari hizo. Halafu yeye Nyerere akaamua kunyamaza tu!? Sasa hamuoni nyinyi ndo mmnavunjia hishma Nyerere kwa sababu mnaonyesha kuwa alikuwa ni mtu irresponsible na dhaifu na hakujali amani ya nchi!?
- Mbona Nyerere mara kadhaa aliweza kuwafokea Lowasa,Mwinyi na Malecela tena hadharani,ndio alishindwa "kumshughulikia" Mohammed Said!?
- Tunajua saana kuwa Nyerere hata alipostaafu lakini bado alikuwa anakubalika na wananchi wengi na pia alikuwa na inffluence kubwa saana kwa marais walomfuatia Mwinyi na Mkapa. Basi alishindwa hata kuwashauri hata wao kuondoa hilo "janga la kihistoria" toka kwa Mohammed Said. Maana mmetaja hapa kuwa WARSHA "ilishughulikiwa" kilivyo na wengine kupata deportation.
Kweli Nyerere angemjibu Mohammed Said; Nyerere kasomea HIstoria na Falsafa; maandishi ya Mohammed Said hayakufuata kanuni zinazokubaliwa za uandishi wa historia na zimevunja vunja kanuni za logic; sasa Nyerere angemjibu kwa kuanzia wapi? Angempa heshima asiyostahili.
Lakini jiulize pia kuwa kwanini Mohammed Said hakumfuata Nyerere na kumhoji? Mohammed Said alifanya juhudi kubwa kweli kupata taarifa za Abdulwahid Sykes; lakini hakufanya hata juhudi moja ya kuwafuata watuw a karibu wa Nyerere. Hakumfuata Nyerere alipokuwa hai, hakumfuata Kawawa alipokuwa hai, hakumfuata Kambona aliyekuwa hai, hakumfuata Fundikira, hakumfuata mama Maria Nyerere ambaye bado yuko hai; wala hajajaribu kuwafuata watoto wa Nyerere. Kweli Nyerere angemjibu?
Lakini hujajiuliza mbona serikali imedaiwa mengi sana; umesoma maandishi yake kuhusu kile alichokiita "Christian Hegemony and the Rise of Islamic Militancy"? Umeona Serikali imemjibu? Amedai mengi kuhusu BAKWATA umeona BAKWATA wamemjibu? Amedai mengi sana kuhusu Kanisa umeona Kanisa limemjibu? Hata Prof. Njozi alidai mengi sana kwenye kitabu cha Mwembe chai madai ambayo ni more substantial kuliko ya Mohammed Said, CCM walisimama kumjibu? Kwanini hawa wote hawajibu? Hujajiuliza kwanini?
-
Mwanakijiji,kuna wakati na kwa sababu uzijuazo wewe binafsi ulikua unahaha kutaka kuandika kitabu kuhusu Rostam Azizi(japo sina hakika kuhusu nini,au ilikua ni biography tu!?). Na ulikua unatafuta watu wowote walokua ati wanamjua kwa njia na nyakati tafauti(shule,Univ. au kikazi) na uliombawakutafute kwa haraka,na uliacha mpaka contact details zako!
Kwani Rostam Aziz sasa ni Mbunge tena au ana nafasi yoyote ya kisiasa? Au unafikiria aliamua kuachilia tu kwa sababu ya uzuri wa mapenzi yake kwa Tanzania?
6. Pia unadai ulikua unawafuatilia habari zao kwa makini kina Dau,Njozi,Mohammed Said na WARSHA na ulishajua athari zao kwa Taifa hili kipindi kirefu. Sasa mbona miaka yoote hiyo umekua kimya na hukumjibu kimaandishi/kitaalamu huyu Mohammed Said. Hivi kweli inaingia akilini,ati uwe na muda wa kuandika kitabu/habari za Rostam Aziz na uache kufanya uzalendo ili kepusha maafa/janga kwenye nchi yako kwa kumvunja kimaandishi "mchochezi" Mohammed Said!? Na mpaka sasa hivi bado unadai uko busy huwezi kumjibu,wakati unajua kuwa uandishi wako na utafiti ni muhimu zaidi kwa hivi sasa kutuepusha na hilo "janga" la Mohammed Said!?
Swali zuri; bado sijaamua kama na mimi nimpe heshima ya kujibu histohisia yake au inatosha tu kujibu hapa hapa. NIkiamua kumjibu nitamjibu na kuvunja vunja hoja zake zote kwa urahisi tu kwani siyo hoja nzito kivile.
- Kama kuna watu/kikundi hawakubaliani na maandiko ya Mohammed Said,kwanini isitumike Judicial System halafu mahakama ndo isikilize pande zoote kwa undani na kufanza maamuzi yake!?
- Kama kuna cross section of our society,inahisi kuonewa au kufaniwa dhuluma,na kila kukicha wanatoa malalamiko ambayo wanahisi ati ni ya msingi na ya kitambo na kuwa Serikali haiyashughulikii,sasa kuna ubaya gani wapewe nafasi ya kusikilizwa!? Na wewe unapodai kuwa ati hakuna tatizo kabisa,na wakati walalamikaji au wanaodai kuumia ni wengine!? Je hapa unatumia mantiki gani Mwandani wangu!? Je utajuaje kunguni wa kitanda usichokilala!?
Lakini swali hilo hilo ungeliuliza kwa upande mwingine; kwani yeye anayetoa madai asingefuata njia ya judicial sytem kuleta madai yake. Sababu ni kuwa ushahidi wake hauwezi kusimama mahakamani; hakuna mtu katika mahakama anayeweza kuyachukua madai ya Mohammed Said kama ushahidi wa dhulma vinginevyo wangeshafungua kesi.
Lakini kama kweli ipo cross section ya watu wanaoamini wanadhulumiwa kwanini wasiende mahakamani wao kudai haki yao? Kama kuna ushahidi mzito (kama wadogo zetu kina Ami na Ritz wanaamini) kwanini wasifungue kesi mahakamani na walete ushahidi huo na upimwe kwa kipimo cha mahakama?
Kwa ufupi, Bwana Mwanakijiji kama kweli kama unavyodai kuwa kuna janga kubwa ndani ya maandiko ya Mohammed Said,basi wa kulaumiwa ni wewe Mwanakijiji na Nyerere kwa kushindwa kumjibu kitaaluma tangia wakati huo! Japo inanilazim nimsamehe Bwana Nyerere maana yeye kishatangulia mbele ya haki.
Hebu fikiria ule muda ulopoteza pale viwanja vya Jangwani wakati huo kwenda kushindana na kina Mwaipopo kwenye malumbano ya kidini,na kama ungeutumia kufanya utafiti wa kina na kuandika kitabu cha "kumshushua" Mohammed Said kitaalamu,unafikiri leo yangefikia haya kweli!?
Ahsanta kwa kukubali kuelimishana.
CC;Ami,The Big Show,Kadogoo,Ritz,Sheikh Mohammed Said,Barubaru,Boko Haramu,Jokakuu,Nyambala
Ps:Nguruvi,Mag3
Naona Wataalamu mmenivamia kama nyuki,lakini haina neno najua tuko pamoja na tunaipenda nchi yetu!ahaha!!
Naheshimu sana michango yenu humu!
Yaani wa kulaumiwa sisi? yaani badala ya kumlaumu mchochezi unataka walaumiwe wale wanaompinga au wanaosema kinachofanywa ni uchochezi? Kweli hii ndiyo analytical skills ambayo hutaki ihojiwe? lahaullah!