Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Mzee Mwanakijiji,

Waislam wanaitaji majibu kutoka serikalini kuhusu madai yao siyo kwenu nyie, ndiyo maana hata wewe ulipomwambia Kadinal Pengo atoe tamko ili serikali watoe majibu ingawa sisi tungeweza kukujibu lakini ulichokuwa unataka usikie sauti ya serikali. Ndivyo ivyo Waislam wanaitaji majibu ya serikali yao siyo majibu yenu Wakirsto.
 
Last edited by a moderator:

wanahitaji majibu ya nini yaani kitu gani?
 
Last edited by a moderator:

Ningetaka sauti ya serikali ningesema; nilitaka Pengo aseme. I was very specific. Nyinyi serikalini mnataka nani ajibu?
 
Son...
Ndipo mkutano wa kwanza wa kuunda African Association ulipofanyika.

Ukitaka habari zaidi msome Daisy Sykes katika Iliffe, Modern ''Tanzanzians''
''Kleist Sykes:The Townsman.''

Hiki kitabu ndio kimenifikia leo kikiwa miongoni mwa vile vitabu nilivyokuwa nimeagiza; kingine ni Tanganyika Under German Rule... Kumbe kina Kleist hawakusahauliwa na historia... wametajwa sehemu nyingi tu...
 
wanahitaji majibu ya nini yaani kitu gani?

Ndiyo maana nakuambia wewe huna uwezo wa kuyajibu hata ukipewa jibu lako kwetu halina maana.

Waislam walimpa Mkapa malalamiko yao na risala ya ilisomwa pale Diamond kwenye baraza la IDD.

Wewe ni raia tu wala Waislam hawaitaji chochote kutoka kwako wanataka kauli ya serikali baada ya hapo ndiyo watajua watafanyaje.
 
Nani katika serikali anatakiwa kuwajibu Waislamu? Waziri, Katibu Kiongozi, Rais, Bunge au nani hasa? Vinginevyo inawezekana ama wanategeana au wanatupiana mpira...

nimepata kusoma humu ndani kwamba Mkapa alitaka madai ya kisayansi akaletewa lakini akashindwa kujibu.

Sasa nashindwa kuelewa ni nani mwenye uwezo wa kujibu hayo madai kama Mkapa alishindwa!

Halafu nashindwa kujiuliza, sasa ikishindikana hayo madai ni nini kitafuata?
 
Wewe ni raia tu wala Waislam hawaitaji chochote kutoka kwako wanataka kauli ya serikali baada ya hapo ndiyo watajua watafanyaje.

Sasa kwanini Kikwete - Muislamu mwenzao - hawajibu? au wanataka PInda (Mkristu) ajibu ndiyo serikali iwe imejibu? Maana kama ni elimu yupo Kawambwa (Muislamu) hajajibu wanataka nani aje kujibu kuhusu hilo? Kwenye utumishi wa Umma yupo Hawa Ghasia (Muislamu) hajajibu mnataka nani ajibu?
 

najaribu reasoning lakini nashindwa kupata jawabu pia,kama ndio hivyo kwanini serikali ipo kimya?

Lakini pia nakumbuka imesha wahi nenwa humu, kipindi cha Julius majibu yalitakiwa yatolewe na Julius

Lakini kipindi cha Mwinyi majibu yalitakiwa yatolewe na Serikali... Kipindi cha Mkapa majibu yalitakiwa yatolewe na Mkapa

Lakini kipindi hichi pia nasikia majibu nasikia yanataka yatolewe na Serikali

Sasa najiuliza Serikali ni nani?
 

Kwa hiyo wewe unataka majibu ya Waislam yatolewe na Muislam siyo Mkirsto kama Nyerere, Mkapa, Mungai, Pinda, Sumaye, Sokoine, Msuya?
 

Mkuu Gombesugu,

Samahani nilibanwa na boksi kidogo. Anyways tuendelee.

Kama ulivyonena MS ana haki kuandika na kusema chochote anachojisikia, na si jukumu langu au lako kumpoka haki hiyo. Lakini masimulizi ya mzee Saidi kama ilivyo to any story has three sides unfortunately there’s very little coming from other side kwani wengi ni marehemu. But there are pro-second side kama walivyo pro-Mohamed Said. Some of us are into that third side called reality coming outta facts. I still believe you can see all the three sides. Umezungumza mengi kuhusu mataifa ya magharibi na hila zao, mgogoro wa Sudan and the so called mabaradhuli wa kizungu. (Though I believe baradhuli ni baradhuli tu, it doesn’t matter ni mzungu, mweusi, mchina etc.).

Sasa turudi kwa mzee wetu Saidi. Naweka haya nikiamini pengine hukupata nafasi kufahamu yaliyoendelea mijadala iliyopita. Simulizi za mzee Saidi zilianza kuhusu dhulma ya wakatoliki dhidi ya waislamu na watanganyika wengine (Pse note. Mimi si mkatoliki). Na hii narrative ilikuwa rahisi kuaminika usipofikiri kwa kina, Ofcourse Nyerere si mkatoliki, kuna Vatican, kuna kadrinali, kuna shule za wakatoliki etc. Ni wakatoliki tuuu kila mahali, why wakati wao ni wachache na sisi (Waislamu na wasio wakatoliki) ni wengi? He navigated thru these waters believing kuwa non-Catholics wataunga mkono hoja yake. Ifahamike kuwa non-Catholics mfano wasabato wana-“kritiki” mno mafundisho ya kikatoliki “kiimani”. And they have got heaps of books on that. Some go as far as portraying pope as the real Satan.

Simulizi za mzee Saidi zinaenda mbali na kuhitimishwa na mchakato wa “utakatifu” ndani ya ukatoliki, kwamba hiyo ni zawadi eti kwa kuwainua wakatoliki na kudhulumu waislamu. Sasa kwa watu wasiyofikirisha bongo zao ni rahisi kuamini hizi habari za kuunga unga. But wait a minute, kumbe hata Hugo Chaves anapendekezwa kuingia kwenye mchakato wa utakatifu? Huyu amedhulumu waislamu wepi? Ahmedinejad too compares him to saint and that he will return with Jesus hahahaha!!!!!!!. Je ni sawa kuwaita binadamu watakatifu? That is a question by itself, lakini hayo ni mambo ya kikatoliki tuwaachie wakatoliki. Sasa it is such an out-of-propotion insult kudai eti qualification mojawapo ya kuwa mtakatifu ni dhulma (regardless inahusu dini gani).

Mzee Saidi haishii hapo anakuja na simulizi nyingine kumuunganisha Mkapa na eti kuwa Nyerere alipokuwa akimkampenia Mkapa alikuwa akipokewa na kulala kwa maaskofu. Sasa si mnaona ukatoliki na mfumo kristo kiujumla unavyo-operate?

Miaka ikazidi kwenda Mzee Saidi baada ya kuona haungwi mkono na his narratives are becoming more and more incosistent akabadili dhana kwa ushahidi ule ule kuwa wakatoliki ni wakristo wote including wapagani (“hao ni walewale tumekwishawazoea”). Lakini pia tunagundua kutokana na maandishi yake mzee Saidi akisema waislamu si wote (japo kwenye stats) anamaanisha wote. Tunaambiwa kuna wasio wa kweli, wale wa bakwata, washirika wa Nyerere na wanaotofautiana na hoja zake. The way Mzee Saidi anavyoongelea kuhusu waislamu is as if they are all connected into this huge gigantic central brain of which he has the remote. Analysis ya mzee Saidi is based on Arabic and Europian names na watu kama hawa Jakaya Kikwete au Keith Ellison wasingekuwa maarufu jicho ya mzee Saidi isingewaona kuwa waislamu.

Mzee Saidi cha kushangaza anaiona hata corruption kidini dini, jambo la ajabu kabisa. Nilishawahi kumuuliza humu humu JF (2010/2011) kuhusu kwa nini hoja zake ni diiinii tu weee kila kukicha? Nikaendelea kwa kusema kuna mjadala humu kuhusu ufisadi wa EPA una maoni gani kuhusu hilo kama mtanzania? Mzee Saidi alinijibu “EPA nini?? Kwani sie tumo humo?”

Mzee Saidi is an intelligent man, and a distinguished scholar. Tatizo tu ni pale anapotaka ku-correlate matukio, watu, ajenda kwa jicho la kidini. Huu ni utamaduni mgeni kabisa kwa watanzania at least from what I know.

Jingine linalishangaza ni kuwa Mzee Saidi baada ya kuituhumu serikali kudhulumu waislamu kwa zaidi ya miaka 50 anategemea serikali hiyo hiyo imletee suluhisho. Mfumo kristo wakae chini kutafakari ni jinsi gani waache dhulma maana wadhlumiwa wameshtuka. That is soooo douche to begin with.

Saidi in recent times ameanza kutest drive a new narrative nayo ni kuwa eti Mtikila na Nyerere walikuwa wamoja kama agents wa mfumo kristo. Really? Mtikila aliyesimama majukwaani na kurekodi kanda lukuki kupinga utawala wa Nyerere na Nyerere mwenyewe hadharani? Nakumbuka alikuwa na usemi mmoja kuwa hivi huyu anaitwa baba wa taifa in maana alilala na akina mama wote Tanzania nzima kupata hiyo daraja? This is probably the only guy kufungwa kwa kosa la kumkashifu Nyerere baada ya kustaafu. Leo tuaanza kusimuliwa kuwa somehow ile ilikuwa geresha tu!!!!!!!! Huyu naye hakuwahi kujibiwa na Nyerere. Sidhani kama kuna mtanzania anamtuhumu dini ya Kawawa kwa lile zoezi butu la kuhamisha watu wakaunde vijiji vya ujamaa. It was such a stupid move ever to be done by a government.

Leo tunaambiwa eti kuna watu kwa sababu ya dini yao wanakuwa treated kama raia daraja la pili really? Ukweli ni kuwa daraja la pili Tanzania ni masikini no matter wewe dini gani, utawekwa ndani bila sababu, utanyang’anywa shamba lako na fisadi, utacheleweshewa mafao yako ya kustaafu etc.
Mfano ni hawa hapa chini.



Lakini pia tunapozungumzia shule za sekondari enzi zile kuna shule huko huko kwa wakatoliki wengi kabla ya shule za kata zilikuwa hazijawahi kutoa mwanafunzi hata mmoja kwenda sekondari in their entire history. Kuna wakati Tarafa nzima ilikuwa inatokea hakuna mwanafunzi aliyechaguliwa. Leo tunaliangalia hili kidini?

All in all matatizo ya watanzania wawe wakristo au waislamu hayatatatulika kwa kuumba umba, au kuunga unga simulizi ili ionekane watu fulani wanadhulumu wengine. That is just a recipe for disaster. Haishangazi kama alivyokuja kijana mmoja wa mzee Saidi akitokwa na povu kila tundu eti “ooh haya mambo ni serious kuliko unavyodhania”. Jambo serious ni jambo serious na linajipambanua lenyewe sasa mtu anapokuja na tisha toto badala ya kujenga hoja si kituko hicho?

Leo tunaambiwa kama hawa hapa chini (Igunga mjini hapa) eti wanafaidi keki ya taifa kwa sababu wanaitwa John au Charles, really?





Hivyo basi sisi kama vijana let’s digest and discuss nini kifanyikekuboresha huduma za jamii. Let’s talk about personal responsibilities. Let’s be there kama watanzania na matatizo tuyaone kama ya watanzania. Hii simulizi ya Saidi trust me inawaandaa wanaomuamini na hasa vijana wetu ku-fail kabla hata safari haijaanza.

Natanguliza samahani wakuu kwa kukuchosheni na bandiko reefu.
 

Mkuu Mag3,
Hilo ni jambo jema sana na hili litasaidia kwa wale "wanamashairi" walioingilia mjadala katikati kuelewa tulitoka wapi mpaka hapa tulipofika na ukweli ni upi.
 
Last edited by a moderator:
Sawa mkubwa tunasubiri hayo madai hatutaki matusi wala dharau!
 
Duh Mag3 kuwa na huruma kidogo mzee wetu Mohamed Said hawezi kubeba hili zigo limeshazidi uzito wapambe wake washamkimbia wamemwacha pekee bila usaidizi wa maana.


 
Last edited by a moderator:
Duh Mag3 kuwa na huruma kidogo mzee wetu Mohamed Said hawezi kubeba hili zigo limeshazidi uzito wapambe wake washamkimbia wamemwacha pekee bila usaidizi wa maana.

Mkuu Ngongo,

Mohamed Said ni habari ingine wala haitaji mtu yeyote kumtetea anasimama kwa miguu yake mwenye na anajenga hoja na anafanya mnakasha na kila mtu lugha yake ni ya kiungwana sana.

Hayo unayosema ni kujiliwaza na kujifariji tu.

Leo yupo humu miezi minne anasomesha watu wa kila haina wanapa Ilm bure kabisa na imani hata wewe umechota kidogo Ilm kutoka kwa Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:
Unajua kuna baadhi yao humu ndani wanadhani sisi tuko hapa tunampa backup Moh Said, Moh Said anahitaji Backup ya mtu?ndan ya miez minne sasa anafundisha na kuvumilia kejeli wanadhani ni kazi rahis? Anatoa darsa bila tozo bila masharti huku anavumilia matusi na kejeli,hakuna mtu anaempa backup,na wala yeye hahitaji backup ya yeyote, Na lazima watambue ya kwamba sisi ni fahari kwetu kuitwa wafia dini,walamba buti wa Moh Said,wanafunzi wake n,k n,k,as long as tunanufaika na Ilmu yake,kelele na matusi yao hayawezi kutupatia unyonge sisi,hata siku moja. Me nishawapuuzia tokea mda mrefu sana..
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Ritz ni kweli Mzee wetu Mohamed Said kajitahidi kutengeneza histohisia yake kaisimamia kwa zaidi ya miaka kumi na tano leo histohisia yake imebomolewa na Mag3 Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 Nyambala Son of Alaska Yericko Nyerere Jasusi JokaKuu Pasco ............... na wengineo wengi.

Mkuu Ritz Mzee wetu Mohamed Said kashindwa kwa kiwango cha kutisha kujibu hoja na wanajamvi niliowataja hapo juu.Sina haja ya kurudia hoja alizoshindwa kuzijibu kwakuwa najua wewe ni mmoja wa wanajamvi wanaotumia muda mrefu katika bandiko hili na umekuwa ukijaribu bila mafanikio kumtetea Mzee wetu Moh.Bila shaka umetambua Mzee wetu ana kipaji kikubwa katika fani ya uandishi lakini wakati huo huo hana ujuzi wa kutetea kile anachokiamini/anachokitaka pengine sababu kubwa ni kutofuata misingi ya utafiti kabla hajaandika kitabu chake au pengine alishakuwa na hitimisho na hivyo kulazimika kukwepa baadhi ya matukio muhimu ya historia ya Tanzania,hili la mwisho ndio hasa naliona wazi.Ikiwa Mzee Moh atapenda kuitendea haki nchi yake kabla hajamrejea muumba wake basi achukue maoni yote bila kinyongo hayaingize kwenye kitabu chake toleo lijalo,simlazimishi kufanya hivyo ni hiyari yake akishindwa hakuna wa kulaumiwa bali yeye mwenyewe.

Mohamed Said hakuwahi kukumbana na maswali mazito kama haya ya JF,alizoea kutoa mihadhara sehemu mbali mbali ndani ya nchi na nje bila kuulizwa maswali.alizoea kutoa mihadhara kwa watu wasioijua Tanganyika vizuri,alizoea kupigiwa makofi bila kuulizwa chochote na ikiwa aliulizwa basi maswali yenyewe yalikuwa rahisi rahisi au akitumia mbinu dhaifu kama anavyofanya hapa jamvini.





 
Last edited by a moderator:
Ha ha ha Mzee THE BIG SHOW uwanja huu haukufai wewe pambana gesi ya Ntwara isiende Dar.

 
Last edited by a moderator:
Wickama,
Yapo mengine hujasema.

Hebu isome kwa utulivu historia hiyo ya Abdu Sykes katika post hiyo.
Lipo kubwa la kusema zaidi.

Heshima yako Mzee MS, point yangu ni kuwa sijawahi ku-doubt dedication ya efforts za Sykes katika agenda unayoongelea, ile ya msingi kwangu ni kuwa he addressed all his challenges as a Tanganyikan to fellow Tanganyikans. Kama vile Paul Bomani au Bibi Titi. I see them as Tanganyikans. Shukran Mzee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…