Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Gombesugu,

Pole ndugu yangu, i can understand your feelings. Bwana, maumivu yako ni testimony ya kilio chetu, kuwa ukii-polarize society katika kuyaona mambo yake yote kwa lens moja basi mwisho wa siku hatasalimika mtu. Utanyimwa hata chumba cha kupanga kwa sababu umeenda kukiulizia kwa mwenyewe na huku umevaa msalaba. Na kama mwenye nyumba ni mwislamu pia basi huenda utakosa chumba sababu ya "Uanswari wako".

Kelele zilizoko humu Gombesugu, ni vilio vya baadhi ya watu kuwa direction hiyo haifai. Kuwa tuyaangalie mambo kwa lens zingine pia. Kwa sababu believe me, fanya utakavyotaka, dunia bado LAZIMA itabaki na watu wenye dini tofauti na yako. Dawa ni co-existence. Angalia tayari umeshaumia kwa jina la mtaa tu.

Sasa kama mtu ange-stereotype nasaba yako ungejisikiaje? Ndio maana nakumbusha tena; MDINI sio mtu anaye-practice dini yake; NO. Ni mtu anayetoa au kunyima fursa/kitu kwa mwingine kwa kigezo cha kufanana au kutofautiana katika dini. Anayekunyima heshima na sifa yako stahiki kwa vile wewe si mwislamu/mkiristo mwenzie ni mdini regardless amevaa nini au ana sauti gani. Pole Gombesugu, kazi buti safari bado.
 

Wickama,
Mjadala huu umetambaa parefu sana na mengi tumetumbukiza humo.

Hili linazua lile na lile linazua hili hadi hapa tulipofika. Hayo usemayo na katika huzo ''ukuti ukuti'' yaani tunazunguka hapo hapo.

Mie awali kabisa na ndiyo msimamo wangu ni kule kusema kuwa historia ya TANU imepotoshwa na madhumuni makubwa ilikuwa kufuta mchango wa Waislam.

Nikasema kuwa Nyerere si muanzilishi/muasisi wa TANU na hapo ndipo nikaja na Abdu Sykes na historia yake nzima toka utoto wake, Vita Vya Pili Vya Dunia, harakati zake za ''labor movement'' hadi kufikia kuingia katika uongozi wa TAA 1950 na kuasisi
TANU 1954.

Nikapingwa sana kwa watu kusema TAA hakikuwa chama cha siasa bali cha starehe nk. Mengi yakasemwa na nikajitahidi kutoa majibu kadri nilivyoweza.

Ikiwa wewe utamchukua Abdu kadri unavyoona anastahili mimi sina ugomvi na fikra zako. Sisi kama binadamu lazima tughitilafiane hatuwezi kuona mambo kwa jicho moja na lile lile.

Nadhani umenifahamu.
 
Ikiwa wewe utamchukua Abdu kadri unavyoona anastahili mimi sina ugomvi na fikra zako. Sisi kama binadamu lazima tughitilafiane hatuwezi kuona mambo kwa jicho moja na lile lile.

Nadhani umenifahamu.

Shukran Mzee MS, nimekuelewa where you stand and I have no problem with my own position. Ile post kuhusu hotuba; sijafuatilia tena ile thread lakini nilisoma something kwenye yale majadiliano.

Tasfri yangu ilikuwa kuna jitihada za kufifisha jitihada za Julius katika ile hotuba; in the event sivyo ile thread ilivyolenga then for sure una haki ya my apologies in case ni wewe uliipost na mliochangia ile mada, kama niko out of context. Jioni njema jamani.
 
This gombesugu needs help, porojo kwa kwenda mbele,i doubt if he knows what he is on about.

"Huyo Mwai Kibaki, wala sifa zozote za kuwa kiongozi mwadilifu au alofata uadilifu. Na hii ni kabla ya kuingia madarakani na mpaka kesho. Nafikiri mtakumbuka vitimbi vyao vingi enzi zao za u-playboy na akina D. Moi,Baraka H. Obama Snr na wengineo wengi pale Nairobi!? Mwai Kibaki hana credibility ya maana pahala pengi saana duniani,na hata huko kwao Kenya. Scandals zake na "udhalim" ni nyingi mno na unatisha saana.Hata self discipline yake na dignity yake binafsi ni utata mtupu!? Tuyaache hayo maana si yetu!

Ndo maana nilipostaajabu na kujiuliza hivi hao "viongozi wetu" na Serikali walitumia criteria na kufata taratibu, vipengele vipi mpaka walipoamua kumtunuku hiyo "zawadi"!? Lakini naona wenzangu hapo hamkuona uzalendo wangu bali udini tu!?ahaha!! Viongozi wengi wageni kama vile Patrice Lumumba,Augustino Neto,Ngouabi na wengineo nawakubali saana,lakini huyo Mwai Kibaki nafikiri ni Taifa/Nchi yetu kuzidi kujivunjia heshima tu".
 
Last edited by a moderator:
Hii nimeitoa jukwaa la historia kwa hisani ya mwenzetu The Fixer,



KATIKA kuyapuuzilia kwa mbali madai ya Waislamu imedaiwa kuwa matatizo ya Waislamu 'ni ya kihistoria'.

Ni kweli ni ya kihistoria. Historia ambayo Maaskofu waliziamrisha serikali za kikoloni - Ujerumani na Uingereza zisiwape elimu Waislamu na zikatii.
Hazikufanya ajizi, wala kubagua katika ukusanyaji wa kodi. Lakini shule chache zilijengwa na fedha nyingi zikatolewa kwa Makanisa. Kwa fedha hizo na misaada mingine Makanisa yakapewa uwezo wa kuendesha mashule mengi zaidi ya yale ya serikali, ili kuwalazimisha wananchi wengine wakabatizwe kwanza ndio wasome.
Hiyo ndiyo historia ya matatizo yetu. Ambapo serikali ya kikoloni iliweka sera maalum ya kufuga nguruwe katika maeneo ya Waislamu ili kuwaudhi na kuwatimua katika maeneo yao. Tazama Waraka wa serikali Na. 40 kuhusu agizo la Gavana wa Kijerumani kwa watendaji wake wa tarehe 13 Oktoba, 1913.
Ni kwa historia hiyo leo Rais anasema yeye ni Rais pia wa wala nguruwe, hivyo hatawagusa (hata kama wanaingilia haki na uhuru wa Waislamu) ila hatopuuza maoni ya Wakristo inapokuja sala la OIC.
Moja ya sababu ya wazee wetu kupigania uhuru wa nchi hii ilikuwa kuondoa historia hiyo ya kibaguzi. Lakini tumeshuhudia serikali ya awamu ya kwanza ikiimarisha utii wake kwa Kanisa kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni.
Ikavunja jumuiya za Kiislamu zilizokuwa zinasimamia ustawi wao katika elimu, afya na jamii. Na wakati huo huo kuzipa uwezo zaidi zile za Kanisa zizidi kujiimarisha.
Waislamu walizuiwa kuanzisha seminari. Wakristo wao wakapewa kila msaada ikiwa ni pamoja na kulifanya somo lao la 'divinity' kuwa moja ya somo linalokubalika kuingilia Chuo Kikuu.
Waislamu walipogundua udhalimu huu, na kufunga azma ya kuanzisha shule zao, ukatolewa Waraka wa kutozitambua shule hizo. Lakini nguvu za dola zilipotumika kuzivunja Waraka haukutumika tena kwa shule za Misheni.
Rais Mkapa anapodai matatizo ya Waislamu ni ya kihistoria, tunasema sadakta; na hii ndiyo historia yenyewe. Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam enzi za ukoloni wa Ujerumani, Askofu Cassian Spiss aliwaambia Wajerumani, msiwape elimu Waislamu. Na ikawa amri. Tazama Tanganyika Notes and Records No. 62/63, 1964. Kwa historia hiyo hiyo kujirudia kuwa kauli ya Kardinali au Askofu kwa serikali ni amri takatifu, hatushangai.
Wakati wa utawala wake, Rais, Alhaj Ali Hassan Mwinyi hakupuuza historia hiyo. Aliiendeleza; alimleta Pope, akaamrisha nguvu zote za dola ziwaangukie wale wanaowabughudhi wanaofuga nguruwe na kuweka bucha za nyama hiyo hadi kwenye vibaraza vya Misikiti.
Pia akaleta 'Memorundum of Understanding' ambapo sasa, serikali inawajibu wa kuzipa mabilioni ya fedha hospitali za Kanisa, kuyatafutia makanisa misaada na kuwapa upendeleo katika kusomesha wataalamu wao.
Lakini wakati akifanya yote hayo, kiongozi huyo wa awamu ya pili hakupuuza shinikizo la Maaskofu kwamba hakuna 'rukhsa' Tanzania kujiunga na OIC! Si hivyo tu, viongozi hao pamoja na kuujua ukweli huo wa "kihistoria" unaowanyima Waislamu haki ya kujiunga na OIC, kuvunja jumuiya zao na kufisadi mali zao za Wakfu, baadae hugeuka na kuwalaumu Waislamu eti hawana dira wala mipango ya kuendeleza jamii yao. Wakati mwingine kuwaambia Waislamu kuwa "wenzenu" wanaletewa misaada na "ndugu zao toka nje, nyie mbona hawaji kukujengeeni mahospitali makubwa". Mtadhani hawajui kuwa OIC ndio iliyotaka kuleta mahospitali hayo!
Zipo habari pia zinazosemekana kuwa Sheikh Mohamed bin Zayed wa Falme za Kiarabu alijitolea kujenga shule ya kisasa ya sekondari ya ufundi katika kisiwa cha Mafia, wakati wa kipindi cha serikali ya awamu ya pili, lakini serikali hiyo ilifanya ajizi baada ya kugundua kuwa wananchi wa Mafia ni asilimia 90 Waislamu. Kama ni kweli, nini kisa cha kuwalaumu Waislamu kuwa hawasaidiwi na ndugu zao?
Kinachofanyika leo kuna dalili zote za kuendeleza historia hiyo hiyo isiyowatakia kheri Waislamu. Ni jambo la kusikitisha na pengine kushtua kuona awali Mhe. Rais Mkapa aliyapokea madai ya Waislamu katika mazingira ya maelewano. Mazungumzo yaliyofuata pamoja na Halmashauri ya Waislamu yalidhihirisha pia kuwepo kwa maelewano, na zaidi kukubaliana katika mambo ya msingi yaliyotambua kuwepo kwa kasoro dhidi ya Waislamu.
Hali hiyo ya maelewano ndiyo bila shaka iliyowatia moyo Halmashauri ya Waislamu kumuandikia barua Rais Agosti 28, 1999 kuthibitisha muafaka wao na kupendekeza njia bora za utekelezaji wake.
Lakini majibu ya Rais katika barua yake ya Desemba 17, 1999 kwa Halmashauri hiyo ni kitendawili kikubwa. Ni nini kilitokea baada ya mazungumzo yale kiasi cha kumfanya Rais abadili msimamo wake wa awali. Barua yake imeonesha mgeuko mkubwa. Ni mgeuko wa U (U-turn). Hivyo tumelazimika kurejea kule kwenye historia yetu.
Kupiga marufuku EAMWS, kuzuia Chuo Kikuu cha Chang'ombe, kilichotaka kujengwa na Waislamu kwenye miaka ya 1960, kuzuia OIC, kukamata na kuwafunga Masheikh kwa mashinikizo ya Kanisa, na Padri wao (akina Lwambano) pamoja na kupiga hatua kidogo, kuua na kutojali sheria alimradi kiongozi wa Kanisa kaunga mkono kwa simulizi za Goliath.
Katika hali hiyo, ipo haja kwa Waislamu kuyarejea upya madai yao kama yalivyowasilishwa kwa Rais kwa maandishi na kuyatafakari upya majibu yake.
Jambo moja litadhihiri kuwa msamiati udini, umekuwa ukitumika kwa maana mbili tofauti lakini zote zikilenga kuuangamiza Uislamu na kuufanya Ukristo uwe dini rasmi.
Kwa upande mmoja, Muislamu hasa kiongozi wa serikali anayeonekana kuijali dini yake na kutoa haki sawa kwa wote bila kujali dini zao, huyu amekuwa akishutumiwa kuwa ni mdini.
Lakini kilicholengwa katika shutuma hizo ni kumfanya Muislamu huyu (asiyejiamini) aikane dini yake kimatendo, na kuifanya jambo la siri.
Awakimbie na kuwaona maadui Waislamu wenzake wanaoutekelezaa na kuupigania Uislamu wao. Lakini kubwa zaidi aungane na Wakristo kuona Ukristo ndio ustaarabu na ustaarabu wa Kiislamu ni jambo la kupigwa vita.
Ni Waislamu wachache katika masiku ya nyuma waliokuwa wameelewa mbinu hii iliyoasisiwa tangu enzi za awamu ya utawala wa Mwalimu Nyerere.
Na kwa sababu hiyo Waislamu wenyewe wakawa mstari wa mbele kumuunga mkono katika kuitumia mbinu hiyo dhidi ya Waislamu.
Ni kwa ajili hiyo walitumika pasipo kujua, na hivyo kumsaliti mwanaharakati, mpigania uhuru mzee wetu Shaahid Almarhum Sheikh Suleiman Takadir.
Aidha, bila ya kuelewa wakakaa kimya na kufumbia macho Masheikh Hassan bin Amir na wengineo walipokamatwa na kufungwa, kuteswa na baadhi yao kuhamishwa nchini mwaka 1964.
Wakati Waislamu walioko serikalini na kwenye uongozi wa siasa wakishughulishwa na propaganda za uzalendo huo, wenzao wa Kanisa Katoliki walikuwa wakiendelea na harakati zao za kihistoria. Waliendelea kukutana na kutekeleza maelekezo ya Kanisa na kisha kupeleka taarifa za utekelezaji Rome. Tazama Sivalon Uk. 15, na rejea yake Uk. 82 ambapo barua kumb. 15/9/9/173 ya Septemba 24, 1963 to Padri Welsh, Rome toka ofisi ya Mkurugenzi, Vice-President office. Tazama pia maoni ya Padri Welsh kwa wakoloni kuhusu Mwalimu Nyerere (Sivalon Uk. 21) na mikakati ya Padri Paul Crane (Sivalon Uk. 25).
Hapana shaka ni jinamizi hilo hilo la propaganda ndilo lililo wafumba macho baadhi ya Waislamu hususan waliopo serikalini wasiuone ukweli na hivyo wasitoke kwa nguvu zote kumhami Shahiid Prof. Kighoma Ali Malima alipoandamwa hadi kifo chake cha kutatanisha.
Kiwango cha kuzugwa na kurogwa bongo za Waislamu, kilidhihiri kupea kwake mwaka 1995, wakati wale wale waliyemuangamiza Sheikh Takadir na kina Sheikh Hassan bin Amir walipowafanya waone kuwa kila anayefuata mila ya Nabii Ibrahim ndiye mdini.
Ila aliye mzalendo ni anayefuata maelekezo kutoka Vatican na aliye mcha Mungu kwa vigezo vya Kadinali Pengo.
Hatujui wazalendo hao leo wanajisikiaje wanapogundua kuwa wao ndiyo walio tuundia serikali ambayo imepokea amri ya Paroko wa Kanisa Katoliki.
Msikiti ukavamiwa, Masheikh wakakamatwa, wanawake wakadhalilishwa na watu wakauliwa.
'Wazalendo' hao 'wasio na udini' wanajisikiaje leo wanapogundua mchango wao unakandamiza katiba na sheria isitumike kuhukumu kadhia ya Mwembechai.
Hapana shaka umati uliokusanyika Diamond siku ya Eid una ujumbe wake muhimu.
Kule watu kuacha mabaraza yao, na kuwa na Baraza moja, ile kukutana watu wa ngazi zote, Masheikh, Maustadh, wazee, wafanyabiashara ndogo ndogo na wafanyabiashara wakubwa, waajiriwa serikalini na katika sekta za umma wa ngazi za chini na juu na watalaamu mbalimbali wakiwemo wanasheria, wote hawa wakijadili madai ya Waislamu kuwa ipo dhulma na ubaguzi dhidi yao na hatimaye kulaani dhulma hiyo na kuahidi kupambana nayo, ni dalili njema.
Ni ishara tosha kuwa ile siri ya lile 'bangi' la kuwazuga Waislamu imefikia hatma yake.
Kila Muislamu sasa anajua, anayeshutumiwa kuwa na udini ni Muislamu yeyote anayependa dini yake na anayechukia dhulma dhidi ya Waislamu.
Kwa upande mwingine anayedaiwa kutokuwa mdini ni yule ambaye yupo tayari kulihami kanisa lake kwa gharama yoyote bila kujali katiba ya nchi, sheria na haki za binadamu.
Hilo tunaamini Waislamu wengi wamelielewa. Ila magugu na chuya hazikosekani. Hao ndio wale ambao Qur'an inasema:
"Na bila shaka tumewaumbia moto wa Jahanamu wengi katika majini na wanaadamu (kwa sababu hii): Nyoyo wanazo, lakini hawafahamu kwazo (Hawataki kufahamu kwazo), na macho wanayo, lakini hawaoni kwayo, na masikio wanayo, lakini hawasikii kwayo. Hao ni kama wanyama; bali wao ni wapotofu (wapotevu) zaidi. Hao ndio walioghafirika". (7:179)
 
Mie awali kabisa na ndiyo msimamo wangu ni kule kusema kuwa historia ya
TANU imepotoshwa na madhumuni makubwa ilikuwa kufuta mchango wa Waislam.

Ndio maana ya kwako inaitwa 'histohisia' yaani historia ambayo imeandikwa kwa kutumia hisia bila kujali ukweli wa matukio. Hakuna ushahidi wowote hadi hivi sasa ambapo unaonesha TANU ilijaribu kuficha au kudunisha mchango wa Waislamu. Hizi ni hisia tu hazina ushahidi. Nilikuwa namsoma Ali Ponda kwenye Iliffe hapa amesema wazi kabisa kuwa harakati za kupigania uhuru hazikuwa zikiongozwa na hisia ya dini. Hakukuwa na hisia kuwa Waislamu walikuwa wanachangia zaidi harakati hizo kuliko ndugu zao Wakristu na hivyo walistahili zaidi.




Kama Nyerere si muasisi wa TANU basi hakuna muasisi wa TANU. Na watu wakikubali hili inabidi wakubali kuwa Rais wa kwanza wa TANU alikuwa ni Abdulwahid Sykes na si Nyerere. Na kuwa Nyerere hakuwa na mchango wowote katika uasisi wa TANU.

Ikiwa wewe utamchukua Abdu kadri unavyoona anastahili mimi sina ugomvi na fikra zako.
Sisi kama binadamu lazima tughitilafiane hatuwezi kuona mambo kwa jicho moja na lile lile.

Nadhani umenifahamu.

Watu wanaweza kukhitalafiana kwenye maoni lakini si kwenye ukweli. Kusema kuwa Nyerere hakuwa muasisi wa TANU wala Mwanzilishi wake ni maoni tu hayana ukweli. Ukweli unaendelea kusimama kuwa Nyerere alikuwa ni muasisi wa TANU na Rais wake wa kwanza akizungukwa na waaasisi wengine ambao walitoa michango yao mbalimbali miongoni mwao ni Abdulwahid Sykes.

Sykes mwenyewe hajawahi hata mara moja kudai kuwa yeye ndiye aliyekuwa muasisi wa TANU; Nyerere hajawahi kudai hilo vile vile (mara zote alijiona ni miongoni mwa waasisi wa taifa letu). Hayo siyo maoni ni ukweli.
 
Mkuu Ngongo,

Pronunciation; Mad-rasah

Alternate Spellings; Madrassa, Madrassah, Madrsah.

watu hawaandiki Kiarabu hapa wanaandika Kiswahili; hivyo maneno yametoholewa vizuri tu. Anayeandika Darasa na anayeandika Darsa watu wameandika kitu kile kile. Watu hawaandiki Kiswahili kwa Kiarabu...( i know once upon a time that was the way to go but not anymore)
 

Wickama,
Kufifilisha ndiko kulikonifanya mimi niandike kitabu.

Matokeoa ya kitabu changu ndiyo haya leo tuko JF.

Mmesoma mambo ambayo hamkupata kuyasikia na msingeyasikia.

Kuhusu ile hotuba starehe yake ni si hotuba tu bali urudi nyuma ujifunze chanzo na historia ya hotuba ile.

Mambo kama haya ndiyo yamefanya leo wasikizaji wako 140,000 and counting...
 
Mzee Mwanakijiji

Kama Nyerere si muasisi wa TANU basi hakuna muasisi wa TANU. Na watu wakikubali hili inabidi wakubali kuwa Rais wa kwanza wa TANU alikuwa ni Abdulwahid Sykes na si Nyerere. Na kuwa Nyerere hakuwa na mchango wowote katika uasisi wa TANU.

hebu msome Nyerere mwenyewe kwenye maandishi ya blue

Ninasema yote haya kwa shukrani kwa wazee. Jamaa hawa walikuwa watu wazima wa Dar es Salaam, na mimi kijana mdogo Mzanaki, na Kiswahili changu si kizuri sana cha matatizo.

Nimekuja, natoka Ulaya, tena masomoni. Muda mfupi tu jamaa hawa wakaniamini haraka sana katika muda wa miezi mitatu. Wakanichagua Rais wa TAA. Hapo ndipo nilianza shughuli mpya ya kuandika katiba ya TAA na kuipa madhumuni hasa ya shabaha ya kuleta uhuru.

Baada ya miezi 13, hapo 1954, tukaanzisha TANU. Jina hili lilipendekezwa na akina Abdul Sykes. Walikuwa wamelifikiria tangu zamani, walipokuwa askari vitani huko Burma (Vita vya Pili).

Nyerere anaendelea kufunguka zaidi, Mag3, anasema mikutano mingi ilikuwa inafanyika Pugu kwa Nyerere ngoja tumsome Nyerere mwenyewe kwenye maandishi ya blue

Miezi minne baada ya kuanza kazi Pugu nikawa ninakuja Dar es Salaam, kwa mguu; kila Jumamosi. Baadaye wazee wakanipa baiskeli nikawa ninakuja mjini kukutana na wenzangu; kufanya mikutano.

Hivyo ndivyo tulivyofanya. Wazee wakaniamini upesi sana. Tukawa na uhusiano mkubwa sana. Wadogo wenzangu wengine walikuwa Abdul Sykes, Abass Sykes (mdogo wake), Dosa Aziz waliokuwa wengi ni wazee.

Nyerere anavyowalezea wazee wa gahawa
"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
 

Sawa Mzee MS, wazo lako nitalifanyia kazi Inshallah. Nimeitafuta sijaipata internet, muda haukunitosha kuperuzi sites fulani fulani. Ila sikuona mahali umeandika apology accepted!!!! hahahahahahah......." Kisha nauliza what happened to the other "original" founder wa TANU? (mzee Juma Mwinyikambi Mwananyamala house?)how did the story end?
 

Hivi umeniona post ya huyo "intellectual wanna be" na kani-Cc au maneno aliyotumia hapo hujayaona ila kwasababu ni Rapherl kajibu basi basi mmekurupuka kunisakama...anajifanya anabusara kumbe hakuna kitu...

Na kama ninawakera nivumilieni tu coz am here to stay

Jiangalie.
Cc: Ritz Son of Alaska
 
Last edited by a moderator:

Ritz, hongera kwa article nzuri yenye historia nzuri. Ila sikuona ikimpa Mkapa angalau credit ya kuwapa waislamu facility ya kuanzishia Chuo Kikuu pale Morogoro. Ni uungwana kuwa fair.
 

TAA Tabora and Dar es Salaam 1953

Ritz,Hebu soma na haya hapo chini ili tushereheshe hayo uliyoeleza hapo juu:

Tabora's reaction to the Governor's circular was unique.

An election was called which voluntarily voted out of power all civil servants and voted non-governmental employees into the Association's leadership.

Andrew Tibandebage, a teacher atthe St. Mary's School and a colleague of Nyerere, was elected Provincial President and Germano Pacha, Provincial Secretary.

In this way the top leadership of the Association went to Mission-educated Christians and the remaining posts went to Manyema Muslims.

Reacting further to this change inleadership, TAA in Tabora passed a resolution that stated among other things that in order to make TAA a strong organisation, there was need to transform it into an open political party.

Pacha was dispatched to the Association'sheadquarters in Dar es Salaam to deliver the proposal.

On arrival at therailway station Pacha was directed to go to the house of the Vice-President Abdulwahid at Stanley Street, who would receive him and put him in touch with Nyerere.

Abdulwahid informed Pacha in Dar es Salaam, and later Nyerere confirmed in Pugu, that the headquarters was at that moment drafting a constitution for a new political party which would be distributed to all TAA branches before the annual conference in July 1954.
[1]

Pacha remembers that it was on St. Francis' Day celebrations when he arrived atPugu to see Nyerere.

Many dignitarieswere invited at the school to mark the occasion and it was after the ceremony and after the distinguished guests had all gone back to Dar es Salaam that, inthe privacy of Nyerere's house he got the chance to deliver his message from TAA Tabora Branch.


[1] Pacha is in possession of the July conference minutes but not the draft constitution, whichcould not be traced at the Party Archives in Dodoma. Bukoba received the draft; see M.Lugazia to the Secretary, Bukoba Branch DC/HQ/BK/LP/897 May, 1954. Folio 16 TANU 16 but the draft constitution referred therein is missing in the covering letter.
 
Last edited by a moderator:
Nyambala, bandiko lako # 12361. Thank you!

Kuna kitu kimoja umekiongelea kuhusu Mohamed kuondoa baadhi ya madhehebu na kubaki na Katoliki.
Hili limefanywa makusudi kabisa kwasbabu kuu mbili.

1. Kwa vile mtuhumiwa namba moja wa matatizo ni Nyerere ambaye ni mkatoliki, kutaja madhahebu kama Sabato, Menonite, Lutheran n.k. kutavunja link kati ya Nyerere, serikali na dhulma.

Kwahiyo ni muhimu sana Katoliki wakawa centre and front of the discussion ili kuwe na link na continuity nzuri katika kujenga hoja zake, kwamba rais mkatoliki kafanya abcd kwa wakatoliki ili kudhulumu watu abcd.

2. Madhebu kama Yehova, Menonite, Sabato na Lutheran yana waumini wachache sana.
Kuwataja hao kutaondoa dhana ya kuwa nafasi na uonevu unafanywa na mfumo kwasababu nao kama wengine muonekano wao ni mdogo ''invisible minority''.

Kwa vile Katoliki ni wengi na ndio wenye umiliki wa taasisi kama shule na Afya ni rahisi sana kusema so and so ni mkurugenzi kwasababu ni mkatoliki. Kwahiyo ukatoliki anautaja kwa maana maalumu ya kujenga hoja kirahisi.

Kuhusu Keki ya taifa nadhani umemuonyesha vema kwa mfano wa Igunga. Lakini Mohamed ameulizwa mara zote, hivi hapo kariakoo bidhaa zinauzwa kwa kutumia majina au uteja? wapi mtu aliuziwa sukari kwa bei tofauti kwa kuzingatia dini yake. Tena basi wauzaji ambao ni wafanyabiashara wakubwa ni wale wale Mohamed anaosema wanaonewa.

Tukija katika mada ya Mag3, Mohamed ameandika kuwa Prof Malima alikuwa mwislam wa kwanza kupata nafasi hiyo tangu uhuru. Akaendelea kusema pale alipoleta mabadiliko alikiuka ''norms'' na hivyo kuondolewa.

Inashangaza kwasababu huko nyuma ameeleza kuwa Malima alikuwa mshauri wa Rais. Na waziri anateuliwa na Rais, na rais wakati huo alikuwa Ali Hasssan Mwinyi. Sijui nguvu ipi ilitumika kumlazamisha akubaliane na matakwa ya mfumo. Pengine inaweza kuwa ni shinikizo la vyombo vya usalama na ndani ya chama.

Kwa mukatadha huo, sasa hivi mkuu wa usalama, mkuu wa Polisi, waziri wa elimu, Makamu wa rais na Rais mwenyewe ambao kwa kiasi fulani ndiyo serikali ukiacha baraza zima ni waislam. Hadi hapo nguvu ya mfumo ni ndogo sana kama si kuwa haipo. Inashangaza bado Mohamed anasubiri serikali itoe majibu. Sasa hapa wa kunyooshewa kidole ni nani?

Huko nyuma ilisemwa mfumo ulimzunguka Mwinyi na Malima, mfumo huo haupo kwasasa. Je, ni kitu gani kinazuia serikali kutoa majibu.

Mohamed anatakiwa awe specific who is responsible kama alivyokuwa specific kwa suala la World Muslim League(WML) na Sheikh Rukara kufanya harakati za kisiasa akiwa si raia wa nchi,suala hili lilipaswa kutolewa ufafanuzi na wizara ya mambo ya ndani (na si serikali) kwa mujibu wa Mohamed.

Ni kwa mwendo huo huo anatakiwa aje na specific nani atoe majibu katika serikali kama alivyotoa kwa WML.

Lakini pia Mohamed anaposema kuna madai mazito na yenye ushahidi, wakati huo huo akishindwa kueleza nini suluhisho walilopendekeza ndipo hoja ya uchochezi wake inapotimia.

Kueleza tu kuwa kuna tatizo bila kueleza suluhu ni uchochezi ambao haswa ndio Yericko ameuandikia mada.
 
Last edited by a moderator:


Wickama,

Mzee Mwinjuma Mwinyikambi kwa ufahamu wangu alikuwa katika Baraza la Wazee wa TANU
chini ya Mwenyekiti wake Sheikh Suleiman Takadir.

UKitaka kujua waasisi wa TANU historia yao nakuwekea hapa chini kama kumbukumbu ili
utafakari:

Among the TANU founding members, it is only those from the headquarters who couldgive a correct account of the formation of the Party.

These are: John Rupia,Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Julius Nyerere, Dome Budohi, Abdulwahid and AllySykes.

The two Sykes brothers, Abdulwahid and Ally, have a family connection in the African Association, their father Kleist Sykes having been founder Secretary of the Association in 1929.

The Sykes files make very interesting reading for any researcher in the political history of colonial Tanganyika.

These records contain information on Nyerere's early political career and it is surprising that when Party historians were researching, these records, which have so much information about Nyerere, and the party itself, were not consulted.

No member of the family,including Ally and Abbas Sykes, the two surviving members of the three Sykes brothers, were interviewed.
 
Ritz, hongera kwa article nzuri yenye historia nzuri. Ila sikuona ikimpa Mkapa angalau credit ya kuwapa waislamu facility ya kuanzishia Chuo Kikuu pale Morogoro. Ni uungwana kuwa fair.

Wickama,

Si tu Mkapa atajwe kwa kuwapa Waislam chuo bali atajwe kama mmoja wa wale waliokuwa wakitumika kupiga vita EAMWS na kumpiga vita Sheikh Hassan bin Amir katika ''mgogoro'' wa EAMWS wa 1968.

Wakati ule akitumia nafasi yake kama Mhariri wa The Nationalist.

Mwingine aliyetumika kupiga vita Waislam alikuwa Martin Kiama Mkurugenzi wa Radio Tanzania.

Achilia akina Geofrey Sawaya waliokuwa wanatembea na fedha za serikali katika mikoba mikoani kuwahonga vibaraka waikubali BAKWATA.

Hii ndiyo historia ya Waislam ambayo leo tunashukuru JF imetupa nafasi kuieleza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…