Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
Waheshimiwa Nguruvi3 na Mag3,
I must admit that sometimes when I read your comments I get bit depressed. But still both of you have my utmost respect for your contributions in here.
Ile "habari ya Mwai Kibaki" kupewa jina la mtaa/barabara hapo Mzizima,mimi niliitaja sababu iliniumiza moyo kwa uzalendo na wala si udini,u-wana mjini au u-Dar Es Salaam. Nastaajabu yale maelezo marefu na dhana yalihusu nini!? Lakini haina neno, tuendelee na mnakasha.
Huyo Mwai Kibaki, wala sifa zozote za kuwa kiongozi mwadilifu au alofata uadilifu. Na hii ni kabla ya kuingia madarakani na mpaka kesho. Nafikiri mtakumbuka vitimbi vyao vingi enzi zao za u-playboy na akina D. Moi,Baraka H. Obama Snr na wengineo wengi pale Nairobi!? Mwai Kibaki hana credibility ya maana pahala pengi saana duniani,na hata huko kwao Kenya. Scandals zake na "udhalim" ni nyingi mno na unatisha saana.Hata self discipline yake na dignity yake binafsi ni utata mtupu!? Tuyaache hayo maana si yetu!
Ndo maana nilipostaajabu na kujiuliza hivi hao "viongozi wetu" na Serikali walitumia criteria na kufata taratibu, vipengele vipi mpaka walipoamua kumtunuku hiyo "zawadi"!? Lakini naona wenzangu hapo hamkuona uzalendo wangu bali udini tu!?ahaha!! Viongozi wengi wageni kama vile Patrice Lumumba,Augustino Neto,Ngouabi na wengineo nawakubali saana,lakini huyo Mwai Kibaki nafikiri ni Taifa/Nchi yetu kuzidi kujivunjia heshima tu.
Mag3:
Ile idea yako ya kuleta mada juu ya mada,nafikiri ni nzuri mno. Lakini nachelea isijeleta tafrani na songombingo, na kuzidisha "mtafaruku wa Juma Mbaruku". Nahisi la muhimu tuumalize huu ulopo hapa kwanza kabla hatuja tambukia pengine. Lakini hii shauri tu,nafikiri mtoa mada/shutuma Yericko Nyerere nae pia ashauriwe ili atujuze yakini yake!?
Ahsanta kwa kunisikiliza huo uchechefu wangu.
Gombesugu,
Pole ndugu yangu, i can understand your feelings. Bwana, maumivu yako ni testimony ya kilio chetu, kuwa ukii-polarize society katika kuyaona mambo yake yote kwa lens moja basi mwisho wa siku hatasalimika mtu. Utanyimwa hata chumba cha kupanga kwa sababu umeenda kukiulizia kwa mwenyewe na huku umevaa msalaba. Na kama mwenye nyumba ni mwislamu pia basi huenda utakosa chumba sababu ya "Uanswari wako".
Kelele zilizoko humu Gombesugu, ni vilio vya baadhi ya watu kuwa direction hiyo haifai. Kuwa tuyaangalie mambo kwa lens zingine pia. Kwa sababu believe me, fanya utakavyotaka, dunia bado LAZIMA itabaki na watu wenye dini tofauti na yako. Dawa ni co-existence. Angalia tayari umeshaumia kwa jina la mtaa tu.
Sasa kama mtu ange-stereotype nasaba yako ungejisikiaje? Ndio maana nakumbusha tena; MDINI sio mtu anaye-practice dini yake; NO. Ni mtu anayetoa au kunyima fursa/kitu kwa mwingine kwa kigezo cha kufanana au kutofautiana katika dini. Anayekunyima heshima na sifa yako stahiki kwa vile wewe si mwislamu/mkiristo mwenzie ni mdini regardless amevaa nini au ana sauti gani. Pole Gombesugu, kazi buti safari bado.