Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Hapana staajabu kabisa kwasababu unajua kuwa kuna upotoshaji sasa utauliza nini nawe upo katika ''mission''. Mohamed wewe kufahamu jambo si tatizo, tatizo ni pale lile unalolifahamu unataka kulifanya la kweli hata kama halina ukweli na unataka kupotosha hata kama unajua unapotosha.Nguruvi,
Utahangaika sana katika historia hii.Ridhika na unavyoona imekukalia sawa.Unajua kwa nini mimi niko bukheri wa hamsa ishirini?Naamini kile ninachokijua.Nakushauri na wewe amini unachoamini.Amini kuwa TANU iliasisiwa Pugu na hutopata shida ya kuniuliza hili wala lile.Hustaajabu kwa nini mimi siulizi mtu swali lolote?Siulizi kwa kuwa najua na ukijua unauliza nini?
Mfano, huwezi kuandika kuwa political career ya Nyerere imeanza baada ya kukutana na Abdul Sykes!
Ni wewe wewe uliyeandika kuwa Nyerere alikutana na Dosa katika national conference mwaka 1947.
Hapa si national conference ya chama cha mpira au wapiga soga ni ya chama cha siasa ambacho leo ndio matunda ya kazi yake yanaonekana.
Tunajua kuwa Nyerere alikuwa na harakati akiwa Makerere. Na zaidi ukasema alipokuwa ulaya alikuwa exposed katika international politics. Hilo lilitokea kabla ya kukutana na Sykes.
Sasa unaposema career yake imeanza wakati anakutana na Sykes yaweza kuwa kweli kwa mujibu wako, lakini si kweli kwa mujibu wa historia na mujibu wa maandiko yako.
Hapa ni jitihada za kumdhalilisha Nyerere na kujenga ngazi kwa Sykes. Nasema kila siku historia iandikwe kwa kila mtu na ushiriki wake si kwa kukumiza maneno ilimradi tu yale maana ya kile ulichokusudia.
The bottom line ni kuwa habari zako hazina mtirirko, ni rahisi sana watu kuchanganya watu.
Unafanya hivyo makusudi ili baadaye utakapochemeka agenda yako hakuna wa kuhoji maana una majibu either way.
Mohamed wewe huulizi kwasababu unajua kuwa swali lako litazaa maswali.
Unakumbuka tulianzia Annur na ilipofika World Muslim League umegota.
Unajua nini kimeendelea hadi WML wakafunga virago lakini husemi.
Unachosema ni kile cha makanisa kuruhusiwa kuwa na mahusiano ya kimataifa.
Sasa utauliza nini wakati unajua kuna unayoficha?