Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar




Vipi nikuongeze ya nne??
 
Platozoom,Kwani tatizo liko wapi ndugu zanguni?Nyie si mmekuwa na historia yenu ya Kivukoni nasi tunayo hii yetu.Kwa nini tugombane?
Mzee Sadi, sidhani kama busara zinaruhusu wewe kwa elimu na umri kutumia maneno hayo. Kwanza, tatizo lipo ambalo ni historia kutoandikwa kwa ukamilifu wake kama ilivyojieleza. Hili liwe la Kivukoni au maandishi yako.

Pili, unapotumia neno ''nyie'' una maana gani, yaani akina nani. Na unapotumia ''sisi'' unaa maana ya akina nani.
Kwa kufuatilia uzi huu sina shaka kuwa nyie ni nje ya waislam, na sisi ni waislam.
Hapa unaligawa taifa ''on line of religion'' kwamba unamfunga mkristo anayekubaliana nawe asikubaliane nawe na mwislam asiyekubaliana nawe akubaliane nawe.

Hiki ndicho ambacho kimekuwa tatizo kubwa katika uandishi wako.
Kwamba huamini kuwa maneno yako yanaweza kusimama yenyewe bila chembe za dini.

Ni kosa kwasababu sidhani kama waislam wote wanakubaliana nawe, au wakristo wote wanatofautiana nawe, sasa hili la ninyi na sisi linakujaje, na kuna busara yoyote katika matumizi yake?

Kibaya zaidi ni kuwa umejivika joho kuwa wewe ndiye waislam. Watu wanasema hivi you're entitled to your own opinion and not facts. Kwahiyo si busara kutumia neno sisi kwa mintaarafu ya waislam tena kwa kutumia maoni yako na kuyafanya maoni ya waislam. Ni makosa!

Vitabu vyako ni vitabu alivyoandika mwanadamu na hivyo visifungamishwe na dini kwa namna yoyote ile.
Hili ndilo unalotumia kuwatisha watu kuwa mtu akipingana na hoja zako anakuwa amekufuru.

Kwahiyo si kweli kuwa historia uliyoandika ni ya waislam ingawa ni kweli kuwa uliyoandika ni historia yako Mohamed ambaye ni mwislam kwa mtazamo wa kiislam kwa kutumia jina la Tanganyika hata kama haikuwa Tangayika iliyokusudiwa.
 
Hapa nina tatizo kabla sijachangia mchango wako. Hivi katika marais tuliowahi na tulio nao nani anaweza kuwa credited kwa kuongelea matatizo yanayodaiwa kuhusu waislam. Naomba msaada kidogo.
 

Mkuu Nguruvi mara kadhaa nilishamkataza Mzee Saidi kutimia hilo neno "nyie", maana kutokana na maandishi yake niligundua akisema nyie anamaanisha not only kutofautiana na hoja zake bali kuwa nyie ni ma-agents wa kanisa. Mzee Saidi hana tofauti na wale wakiona kampuni au TV show mfano haina weusi, au ni weusi watupu basi inaqualify kuwa ya kibaguzi. Ndiyo maana nikaandika kuwa yeye anapozungumzia waislamu is as if they are all connected with a central brain na yeye ndiye kashika remote. Si mara moja ametamka "nyie" mpo kila mahali, "sisi" tunaendelea kudhulumiwa, "nyie" haya hamuwezi kuamini. Infact this guy's statements are always too mean.
 
Tumeshawazoea! mkizidiwa hoja huwa mnaomba msaada wa Polisi!

Baada yote hayo halafu zinafuata kejeli na dharau eti mnakunywa kahawa na kashata hamuwezi..................
 

Nyambala,

Hilo neno stoliacha kulitumia.
Ukweli umeshadhihiri.

Hapa jamvini tuko kambi mbili.

Kuhusu nafasi yangu katika umma hilo
fanya utafiti wako mwenyewe utajua
nafasi yangu.

Waislamu wakitangaziwa kuwa leo nitazungumza
radioni au msikiti fulani huwa wanaitika vyema.

Huu ndiyo ukweli hata kama haukupendezi.

Nimehudhuria hafla kadhaa na huwa wapo wakubwa
wenye nafasi katika nchi.

Wanatambilishwa wakubwa na mwisho Waislam hunisimamisha
nami nikatambulishwa kwa mahaba makubwa.

Hii si ishara ya mie kupigwa pande.
 

Nguruvi3.

Moja la tatizo kubwa la waTanzania hususan wale kutoka upande wa pili wa Muungano nikimaamisha na tanganyika siku zote wamekuwa ni watu wa kutaka KUFICHO UKWELI. Na wanashindwa kabisa kufahamu kuwa huwezi hata sekunde moja kuuficha ikweli na ukidiriki kufanya hivyo basi kifo kitakuumbua.

Siku zote huko Tanzania kumekuwa na malalamiko lukuki ya Waislam kuhusu kudhulumiwa na wenzao wa dini nyingine na Serikali yenu na madai hayo yalianza kutolewa kwa Siri mpaka yakafikia dhwahiri na hata kubainishwa na kukabidhiwa Serikali wakti wa Mkapa lakin hakuna lolote. Jibu wanalopewa ni matatizo ya kihistoria tu hivyo hayana uzito. Wengi wa viongozi wenu hawaoni haya wala soni kutoa majibu mepesi kwa masuala magumu yenye wingi wa kufikiri.

Nguruvi3 sasa ndio mmefika pahala ambako hakuba siri tena. UDINI UPO KILA PAHALA. hata kama utausoma Mnakasha huu kwa kina utaona Upende wa MS ambao unatetea kitabu hicho wengi ni waislam na upande wa Yericho na wewe mwenyewe ni wakristo ndio mnaojitahidi kuuficha na kupingna na kitabu hicho. Hili nafikiri lipo wazi zaidi.

Vile vile kama mtu akianzisha Uzi wowowte ule wa kusema kasoro za Nyerere utaona dhwahiri kabisa wakristo watapinga hilo na kunena Nyerere hakuwa mkosefu na waislam wengi humu utaona wanakosoa mengi na kusahau japo yale mazuri aliowahi kufanya.

Kwa mantiki hiyo, Al Akhiy Mohamed Said ana haki kamili kunena Nyie kama wapingaji ambao ni wakristo na Sisi kama tunaokubaliana nae kama waislam kutokana na mtiririko mzima wa mnakasha huu.

Ili kutegua utata ni kwa Nyie kutunga au kuandika kitabu cheni ili kupingana na hizi tafiti za Ahali yangu Mohamed Said kinyume cha hapa mjiandae tu yote. Hizo kama hamtakubali kuwa Udini upo na umeenea kila kona na sasa kuanza kusaka suluhu za kuondoa udini huo katika jamii kwa njia za mijadala ya kitaifa ya wazi na kuweka tume ya maridhiano ili kuepusha balaa zaidi.

Mfano mdogo mumeona issue ya kuchinja na Hata Fatwa za viongozi wenu hususan wale vibaraka. Kwani wanakotaka kuwapeleka ni kubaya sana. Kwani kuruhusu kila dini ichinje maana yake ni kutenganisha waislam na wakristo. Kwani hakuna mwislam atakayekubali kula kilichochinjwa na Mkristo na halikadhalika Mkristo kula kilichochinjwa na Mwislam. Matokea yake kama Rais ataandaa sherehe lazima kuwe na Buffee mbili ya ile iliyochinjwa na waislam na ile iliyochinjwa na mkristo. Na hata mabuch itakuwa hivyo hivyo.

Bila kukubali ukweli mumekwisha. nawapa pole sana.

 

Swadakta Al akhiy Mohamed Said.
maneno yako ni mujarab kabisa kwani wao wamekuwa ni wenye kutaka kuuficha ukweli ambao sasa umedhwihiri dhwahiri shahir.

Enzi za kuogopa au kufichwa na Bakwata zimepitwa na wakti, watu wapo huru kujadili na kusema bayana na hata Bakwata Challli hawawezi tena kuwasemea waislam japo ndio sikio kuu la Serikali kuhusu waislam.

Hongera kwa kusema Kweli na Allah atakulipa Kwalo. Kwani amekataza kuificha haki kwa batwil kwa thamani ndogo ya kidunia.
 


Nami naungana nawe al akhiy MS kuuliza tupeni harakati za Nyerere huko makerere kama alivyobainisha hapo juu?
 
Hivi ile historia ya Chuo Cha Kivukoni iliandikwa na waandishi gani.

According to Mohamed Said Kitabu kiliandikwa/kilihaririwa na Abubakar Ulotu.

Na haya ninaongezea kuhusu Ulotu. He was a radical moslem ambaye miaka ya 90 alianzisha chama cha siasa cha NRA kilichokuwa na malengo ya kidini (kupendelea waislam). Chama kilipigwa marufuku mwaka 1995 kabla ya uchaguzi. Wale radical muslims waliokuwa wameingia kwenye NRA wakatangaza kuwa basi watahamia kwenye chama chenye mgombea urais ambaye alikuwa muislam pekee kati ya wale wanne (Mkapa, Lipumba, Mrema na Cheyo). Kutoka hapo, ukichanganya na hila za CCM-TISS, chama cha CUF (ambacho mwanzoni hakikuwa cha kidini) hakijaweza kujiondoa katika tope la kuhusishwa na dini fulani.

Sasa tukirudi kwenye hicho kitabu cha kivukoni, kimeandikwa na muislam tena mwenye siasa kali, lakini naona hakikumfurahisha mzee Moh Said, labda kwa vile hakikutaja watu kwa makabila (wamanyema, wanubi, wazulu) na wala kwa dini zao (wakristo, wapagan, waislam nk).
 
Last edited by a moderator:

Ami,

Salaam Al Akhiy.

Nimekuona na nakufuatilia kwa makini saana.
Hii minyambulisho na bayana zako hapa ni mubashar. Nina hakika ni bashraf tu. Kwa kifupi kuna vitu vingi mno humu viwazi kabisa,lakini inastaajabisha ati jamaa hawavioni!? Ama hakika "mioyo ya wenye kujua huwa na macho"!

Ahsanta.
 

Siyo kweli kuwa kitabu cha kivukoni kimeandikwa na Abubakar Olutu. Jaribu kuangalia vizuri rekodi zako.
 
Last edited by a moderator:

Nguruvi3,

Acha kufurukuta na kulikimbia swali alokuuliza Sheikh Mohammed Said. Tafadhali mtendee haki Maalim wetu na sisi wanajamvi wenzio.
Mara nyingi humu naona kuna jamaa wengi ni mahodari wa aidha kukwepa maswali na kukaa kimya kabisa au kujibu hoja kiujanjaujanja na kutia mkanganyiko na mbwembwe nyingi. Au ndo wamerithi ule "ustaarabu na hikma za Mwalimu"!? Lakini nina hakika wewe si miongoni mwao.

Narejea tena; Sheikh Mohammed Said alikutafadhalisha ulieleze jamvi ni zipi harakati za Nyerere alipokua Makerere kiasi zinawezwa kuandikwa historia kuwa zilikua na taathira kwa wakoloni!?
Nafikiri mwanzoni ulidai pia kuwa Nyeyere alikua akifanyia mikutano yake ya siasa huko Pugu! Sasa kipi kilichomsababisha imlazim kuja huku mjini Mzizima,tena miles nyingi saana na dhiki ya miguu,na mpaka Wazee wetu wakamhurumia na kumjaalia baiskeli!?
Tunaambiwa Nyerere ndie aliekua msomi,mwenye maarifa na mahiri kushinda wale Wazee wetu woote. Na tunajua kwa yakini kuwa baadhi ya Wazee wetu walikua na uwezo mzuri wa senti kujikidhi kwa wakati huo,na baadhi yao walihodhi motokari.
Sasa kwanini isiwe wepesi wao kumfuata Nyerere huko kwenye hiyo "mikutano ya Pugu" kuliko yeye Nyerere kutaabika, tena kwa miguu kuja mpaka Mzizima kuwafuata "wauza samaki na vinyozi"!? Hii inaashiria kuwa huko Pugu hakukuwa na mikutano ya siasa. Mikutano yoote ya siasa Nyerere aliikuta ikifanyika Mzizima kwa Wazee wetu,nae kwa kubaini umuhimu wa wale Wazee wetu na nafasi,jitihada na umahiri wao katika harakati zile ndipo nae akajiunga nao ndugu zake na wazalendo wenzie nao wakampokea bila ya kinyongo na ustaarabu mkubwa pasi mfanowe!
Ahsanta kwa kunisikiza huo uchechefu wangu.
 

Nanren,

Tuingie katika darsa na hapa chini nitakuwekea vitu nilivyoandika katika kitabu changu vikuongoze katika kulijua somo hili vyema Insha Allah:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD]In 1985, President Nyerere, while conferring an honorary degree on Basil Davidson, challenged the University of Dar es Salaamto write a correct history of Tanzania. In 1988, while commemorating thirty years of the Tabora Declaration, Nyerere in reference to early TANU members and as a tribute to them Nyerere asked the Party to take stock of those who joined TANU between 1954 and 1958. Nyerere said: “That was the most trying period in the history of our Party and few people were courageous enough to join and work for the Party.” [1]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]In supporting Nyerere for his recent call and taking up the challenge to record a correct history which he had for the first advanced in 1974 and again in 1985 the present author published an article in African Events [2] in which Abdulwahid and other forgotten TANU pioneers received prominence. In that article the author did what no other scholar had done before. He mentioned the fact that Muslims were in the forefront during the struggle for independence. It was at that time taboo to associate Islam or Muslims with the independence movement. The author received sharp rebuke from a Party historian, Dr Mayanja Kiwanuka, a leading member of the panel which wrote the Party book Historia ya Chama Cha TANU 1954-1977, the official history of the Party. The Party historian had this to say:
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD](the)... article...argues that although Muslims in Tanzania played a crucial role in the struggle for independence, there is a deliberate effort to downplay their contribution. Consequently, the entire article contains half-baked fairy tales to sustain his argument, more so by mentioning names of several TANU stalwarts who happened to be Muslims...The greatness of TANU, indeed that of its founder-leader, Mwalimu Nyerere, is that, in so short a time since its inception, it managed to weave together into a formidable, relatively homogenous nationalist movement, a people so ethnically, culturally and religiously diverse... Said’s major goal is to sow seeds of discord, and at any price, truth to him is a matter to be ignored. [3]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]This was the reaction from Kiwanuka, who supervised the research on the official history of the party, reducing a research article to what he called a ‘fairy tale’. The author was also accused of lying. Kiwanuka, not deviating from the Party stand, emphasised ‘the greatness of the party and its founder-leader’. Kiwanuka was at that time the Assistant Secretary in the Department of Political Propaganda and Mass Mobilisation of the Chama Cha Mapinduzi. Kiwanuka had as an undergraduate student at University of Dar es Salaam, written on post-independence Muslim-Christian relations. [4]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1]Daily News, 6 th October, 1988.
[2]See M. Said, ‘In Praise of Ancestors’ Africa Events, London, March/April 1988,pp. 37-41.
[3]See Africa Events,May, 1988, letter by Dr K. Mayanja Kiwanuka.
[4]K. Mayanja Kiwanuka, ThePolitics of Islam in Bukoba District (1973), B.A. Thesis, University of Dares Salaam.



Nanren,

Tusonge mbele na darsa letu:

Mtafute Abubakar Olutu hapa chini ambae aliandika kitabu chake ''Historia ya TANU'' Kilimanjaro Publiations 1980:
[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] ''The first serious attempt to record the history of TANU was done by none other than Abdulwahid himself. When TANU captured state power from the British in 1961 and was in the first phase of consolidating itself as a mass party, it is said that Abdulwahid was asked by Julius Nyerere, then Prime Minister of the country, to record the history of the struggle of the Africans of Tanganyika against the British. This, in essence, was to be the history of TANU. To assist him in the research was the late Dr Wilbert Kleruu, recently returned from studies in the United States.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Abdulwahid occupied his former office at the TANU headquarters; the one which he had occupied in the 1950s when he was TAA President. Abdulwahid’s personal files, dairies and his late father’s papers dating back to the days of the formation of African Association in 1929 were made available to researchers for the first time as primary sources of information. Abdulwahid’s version, analysis, presentation of facts and interpretation of forces at play which led to the rise of nationalism were, however, not acceptable to the TANU leadership. We shall see in the following pages reasons why Abdulwahid’s version of history could not be allowed to flourish. Abdulwahid abandoned the assignment after being convinced that the new leadership in TANU was not really interested in documenting an authenticated history of Tanganyika but was interested in merely creating a personality cult for President Nyerere. Dr Kleruu went ahead with the research and completed the work. This manuscript remains unpublished, at least in its original form. The manuscript disappeared from Party archives and was published for the first time in 1971 under a different name after changes had been done by the ‘author’ on the original manuscript to prevent detection by the Party. After the book was published, the Party silently tried to stop the second edition of the book from being published but failed. The work has now been published several times. The approach, style and analysis of the subject is not very much different from the book on TANU published in 1981 by the Party ideological college.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] However there is an anomaly in the book which the ‘author’ overlooked. The ‘author’, so to speak, writing in the first person, states that he wrote the book in 1964. In that particular passage the ‘author’ provides information from which by reading between the lines the reader gets an impression that the author is familiar and intimate with the Party members mentioned. But the ‘author’, in providing the date of his work, forgot that in 1964 he was a young boy in his teens and could not have known those people in 1950s nor have the intellect to undertake such an academic pursuit. The question is now, who is the real author of that passage? With the information now known, this could not even be the pen of Dr Kleruu writing that passage because he, like the ‘author’, was never part of that period. Only one person could have such information and mastery of issues of those times. This could only be Abdulwahid writing in 1964. The ‘author’ had carelessly copied a passage from Abdulwahid’s notes preserved in the TANU archives. And this was not done in 1964 either, but much later after his death.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] From that time Abdulwahid avoided involving himself in any discussion about the subject, although before his death he accepted an invitation and talked to the Historical Association of Tanzania (HAT). It has not been possible to get information on the topic presented for discussion, but it is said that one of the questions from the audience to him was whether it was not true that, Julius Nyerere had turned round the Party beginning in 1954. To this Abdulwahid gave an analogy of the astronaut John Glenn, the first American to go into outer space. Abdulwahid threw the question back to his audience and asked, “Where should the credit go, to the American scientists who designed and built the rocket, or to John Glenn who piloted it?”

Ikiwa hukuelewa darsa hii nifahamishe nikujuvye zaidi.
Ama kuhusu NRA, Prof. Malima, Waislam, CUF fungua uzi mpya Insha Allah nitakuja kutoa darsa.

Publishers wanagombana na mie wanasema watakuwa hawapati faida kwa kuwa hawatakuwa wanauza
sana vitabu vijavyo kwa kuwa natoa habari bure.

Jibu nimewaaambia hii ni hidaya kanipa Allah na ni amana kwa hiyo wenye amana yao wakija kuitaka
nawajibika kuwapa.

Allah ndiye mpaji wasahau hizo fedha kwa muda.

[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…