Mohamed, si umeandika na imeandikwa kwingineko kuwa Nyerere alikuwa katibu wa Tawi Tabora.
Kwani tawi lile lilkuwa la chama cha walimu, wacheza mpira au wafugaji! Jibu ni kuwa kilikuwa chama kile kile alichokiongoza Dr Kyaruzi na Abdul Sykes.
Na huko Makerere alipotaka kuanzisha chama cha TAWA aliambiwa tayari kupo kingine.
Hapa si kuwa alikuwa ameshaanza harakati za kuundoa ukoloni. Unless migomo ya Dockworkers ndiyo harakati pekee ukweli utabaki kuwa Nyerere hakuanza siasa na Abdul Sykes na wala Sykes hakumfundisha siasa.Nitty gritty
Ukitaka kujua harakati zake ni pale alipokuwa na uwezo wa kusoma katiba na kuilinganisha na za washirika wake wengine hadi kubadili chama kuwa movement ya kisiasa kabisa. Hilo liliwezekana kwasababu alikuwa Makerere anasoma na ndicho kilichomtfoautisha na wazee wake na wako aliowakuta Dar.
Hata wewe umeandika kuwa wazee wakow alimtaka kwasababu ya usomi wake.
Usomi huo haukupa Butiama bali Makerere na Scotland na ndio alioutumia ku-tranform siasa za wakati huo kuwa modern politics.
Kuanzia mwaka 1929 hadi 1950 alipokuatana na Sykes, na kuanzia 1952 hadi 1960 tulipopata madaraka ya ndani ni wazi muda aliotumia kuongoza alileta mabadiliko haraka zaidi kuliko muda wa nyuma.
Hili halimfanyi Nyerere awe superior au inferior kwa wengine ni mchanganyiko wa harakati.
Inategemea harakati unazitafsiri vipi lakini kwa mwenye kusoma, kutafakuri na kuelewa harakati ni ujumla wa mambo iwe umaarufu au usomi n.k.
Kuhusu WML ninaposema kugota nina maana hiyo uliyosema kwamba hujui.
Inashangaza unaweza kujua inside information za maeneo kama Laibon wakuu wa nchi walipokuwa wanaongea, habari za wizara ya elimu na funguo za Ikulu zilizoibwa wakati wa Mwinyi lakini la World Muslim League hulijui.
Si wewe Mohamed labda mwingine.
Ni hapo unapoongeza curiosity ya watu wengine kuwa uliwezaje kujua mashirika ya kanisa yaliayoandikishwa nchini wakati hujui WML inayokuhusu.
Unawezaje kujua habari za kanisa kuilazimisha serikali kufanya abcd wakati hujui harakati za Sheikh Rukara ambaye mlikuwa bega kwa bega katika kupigana na ''dhulma''.
Haiwezekani umfahamu Sheikh Malik Mpakistani ushindwe kujua habari za Sheikh Rukara.
Endapo hujui hilo la WML na Rukara,basi la Sheikh Amir na EAMWS utalifahamu vipi?
Hapa hakuna double standard ni hoja kwa hoja.
Nguruvi3,
Acha kufurukuta na kulikimbia swali alokuuliza
Sheikh Mohammed Said. Tafadhali mtendee haki
Maalim wetu na sisi
wanajamvi wenzio.
Mara nyingi humu naona kuna jamaa wengi ni mahodari wa aidha kukwepa maswali na kukaa kimya kabisa au kujibu hoja kiujanjaujanja na kutia mkanganyiko na mbwembwe nyingi. Au ndo wamerithi ule "
ustaarabu na hikma za Mwalimu"!? Lakini nina hakika wewe si miongoni mwao.
Narejea tena;
Sheikh Mohammed Said alikutafadhalisha ulieleze jamvi ni zipi harakati za Nyerere alipokua
Makerere kiasi zinawezwa kuandikwa historia kuwa zilikua na taathira kwa wakoloni!?
Nafikiri mwanzoni ulidai pia kuwa
Nyeyere alikua akifanyia mikutano yake ya siasa huko Pugu! Sasa kipi kilichomsababisha imlazim kuja huku mjini Mzizima,tena miles nyingi saana na dhiki ya miguu,na mpaka Wazee wetu wakamhurumia na kumjaalia baiskeli!?
Tunaambiwa Nyerere ndie aliekua msomi,mwenye maarifa na mahiri kushinda wale
Wazee wetu woote. Na tunajua kwa yakini kuwa baadhi ya
Wazee wetu walikua na uwezo mzuri wa senti kujikidhi kwa wakati huo,na baadhi yao walihodhi motokari.
Sasa kwanini isiwe wepesi wao kumfuata Nyerere huko kwenye hiyo "
mikutano ya Pugu" kuliko yeye
Nyerere kutaabika, tena kwa miguu kuja mpaka Mzizima kuwafuata "
wauza samaki na vinyozi"!? Hii inaashiria kuwa huko Pugu hakukuwa na mikutano ya siasa. Mikutano yoote ya siasa
Nyerere aliikuta ikifanyika Mzizima kwa Wazee wetu,nae kwa kubaini umuhimu wa wale
Wazee wetu na nafasi
,jitihada na umahiri wao katika harakati zile ndipo nae akajiunga nao ndugu zake na wazalendo wenzie nao wakampokea bila ya kinyongo na ustaarabu mkubwa pasi mfanowe!
Ahsanta kwa kunisikiza huo
uchechefu wangu.