Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

JokaKuu, hayo unayoyaona ni kwa vile umeweka fikra zako huru.
Kama umefungwa katika kufikiri basi kila kitu utakiona katika pembe tatu.
Kuna kitu wanasema paranoid, kwamba ninaweza kukuangalia basi ukadhani ninataka kukudhuru, kukuibia au kukukata kichwa hata kama nilikuwa sijakuona.

Hebu endelea kutoa shule maana wengine kiswahili ni kigumu na hakieleweki labda utaeleweka mkuu.
Hebu fikiri kuwa kama Kirinjiko inaweza kufanya vizuri kuliko shule zingine za kiislam sasa hapo kwanini mtu asione kuwa hoja ya kuonewa ni mufilisi? Tena anyetoa madai hayo anahibitisha kuwa usimamizi wa shule hiyo ni tofauti na ule wa BAKWTA. Ana jibu la tatizo lakini hakubali jibu hilo kwasababu kuna jibu ameshafundishwa hata kama akili yake haikubali

Shule ya Alharamain ilkuwa juu sana wakati fulani, tangu watu waache kuangalia kwanini inafanya vibaya wamekita akili NECTA ni kweli inaendelea kufanya vibaya, vicious circle

My message is, watu waende kwenye mzizi wa tatizo hizi habari za tumefanya tafiti za namba mbili tatu ni kuwadanganya tu! FEZA inafanya uzuri, Kirinjiko ndiyo hiyo inasemwa inafanya vizuri sasa kwanini kusiwe na hizo Tanzania nzima bali watu wakae wakiaminishwa kuwa ufaulu wa mitihani unategemea mkurugenzi ni nani.

Huko nyuma madai yalikuwa wizara haijawahi kuwa na waziri au katibu mkuu mwislam.
Sasa hivi madai yamerudi hakuna kamishna wa elimu mwislam na NECTA ni kigango.

Next time watapatikana waislam sijui madai yataelekezwa wapi, miaka inasonga watoto wanafeli.
Please watu waangalie tatizo wasitafute sababu za ku-justify tatizo.

Nimeangalia hizo shule za misheni, kuna moja wamefeli 100%. Maana yake ni kuwa kama hakuna maandalizi ni felia tu haichagui ni imani gani.

Endelee kutoa mwelekeo mkuu jokakuu
 

Wanajamvi,
Nitazangumza machache tu.

Kitabu cha Kivukoni kimekosea.

TAA haikuasisiwa 1927 bali 1929 wala hakikumtaja Dk. Aggrey katika
kuwashajiisha Waafrika wa Tanganyika waanzishe umoja wao.

Haya yalitokea mwaka 1924 Dk. Aggrey alipokuja Tanganyika kama
mjumbe wa Phelps Commission.

Kleist Sykes kaeleza mkasa mzima kwenye kumbukumbu zake aloacha
kabla hajafa 1949.

Kleist alifanya mazungumzo na Dk Aggrey.

Kumbukumbu hizi zinawezwa kupatikana Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
Maktaba, East Africana angalia "The Life of Kleist Sykes" seminar paper ya
Daisy Sykes 1968.

Pili TAA haikuanzishwa 1948 ni ile ile African Association ilibadili jina tu.
Ushahidi wa hili uko kwingi sana.

TAA si chama kipya wala huwezi kutenganisha na AA.

Jingine.

Mwaka 1929 wakati AA inaasisiwa Kleist alikuwa akijulikana kama Kleist
Plantan jina la baba yake mlezi Affande Plantan.

Hakuwa anaitwa Kleist Plantan Sykes kama ilivyoelezwa.

Alipokufa Affande Plantan mwaka 1914 ndipo Kleist akenda mahakamani kubadili jina na
kuanzia hapo ndipo akajulikana kama Kleist Sykes.

Wakati Affande Plantan anakufa Dar es Salaam Kleist na Schneider Plantan
walikuwa Tanga katika jeshi la Wajerumani wakipigana na Waingereza katika
Vita Kuu ya Kwanza.

Affande Plantan ndiye aliyekuwa mkubwa wa mamluki wa Kizulu walokuja Tanganyika na
Herman von Wissman 1890s kuja kuwasaidia vita dhidi ya Abushiri na Mkwawa.

Baada ya ushindi Wajerumani wakamfanya Affande Plantan kuwa mkuu wa German Constabulary.

Hawa wazee ni babu zangu wakuu na historia zao zimekuwa zikihadithiwa
ndani ya majumba yetu tukizisikia pamoja na yote walofanya toka tukiwa watoto.

Tatizo la Kivukoni ni kuwa walikuwa na hofu na hiyo hofu bado iko hadi leo,
uoga wa kusoma nyaraka aloacha Kleist Sykes katika historia ya Tanganyika na
historia ya AA.

Juhudi ni kutaka kumkata asiunganishwe na historia ya TANU na ndiyo maana zikafanyika
juhudi za kumfifilisha Abdu Sykes katika kuunda TANU.

Hii ndiyo sababu kuu ya huu mkanganyiko na mparaganyo ulioletwa hapa jamvini eti kuja
kumsahihisha Mohamed Said.

Kivukoni kitabu chao ni kichekesho.
Hayo mengine ya vyama vya ushirika na mengine yashachusha wala sina haja ya kuyasemea hapa.
 
Mzee Said, kuna hoja hapa unasemaje? Hizi zimetoka kwa J.Illife na Daisy ambazo umekuwa unanukuu kazi zao hamsa wa ishrin.
Hakuna swali, ni hoja tu, karibu sana.
 
Mzee Said, kuna hoja hapa unasemaje? Hizi zimetoka kwa J.Illife na Daisy ambazo umekuwa unanukuu kazi zao hamsa wa ishrin.
Hakuna swali, ni hoja tu, karibu sana.

Nguruvi,
Mimi sina tatizo.

Una haki ya kulichambua jambo kama akili yako inavyoliona.

Sijapinga alosema Illiffe.
Wala hapa sina haja ya kumkweza Kleist kuhusu mchango wake
katika historia ya Tanganyika.

Yote kayaeleza mwenyewe kwa kalamu yake kabla hajafa na ndiyo
maneno yake yakaja kuwa msingi wa maandishi ya Daisy na mwalimu
wake Iliffe.

Na nitamnukuu Daisy tena na tena kila nitakapokuwa naandika habari
za babu yake.

Lakini kubwa ni kuwa tuko katika merry go round na hili halinipi shida.
Napumzika narejea Insha Allah ninapoona ipo haja.
 
Sio kwamba tunpiga makofi tu bali tunashangilia ushindi.Hebu msikize Mohammed

Kivukoni kitabu chao ni kichekesho..!
Hata Mzee Mwanakijiji nae ni kichekesho!.Nakumbuka yale maneno yako siku ulipoalikwa ubwabwa kule Marekani,kwamba Marekani hakuna chakula cha bure.Inaonekana hata marehemu Sykes alipomualika Aggrey alikuwa na fikra kama hiyo na kweli ndiyo mantiki.
Kichekesho ni akina Mwanakijji kumpa hadhi mgeni kuwa ndiye aliyeatoa wazo la kuasisi AA kuliko mwenyeji wake.Kwanini isiaminike kuwa wazo hilo lilikuwa kwa Sykes na pengine tu lilipata nguvu kwa ugeni wa Aggrey?.

Kwa hili sheikh Mohammed :rockon::israel:
 

Naam! Naam! Nafyonza Ilm tu hapa bila wewe watu wasingetafuta vitabu kuwafahamu kina Kleist.

Leo hii watu ndio wanataka kujua habari za Aggrey wkt wewe umezielezea zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Endelea kutoa Ilm Mkubwa.
 
Wana jamvi,

Niwarejeshe nyuma kidogo,

Maandiko haya ni sehemu ya kitabu nilichokiandika mimi kiitwacho "vita dhidi ya ugaidi"



UHUSIANO WA SIASA ZA DUNIA NA DINI

Historia ya siasa duniani haitengani na historia ya dini. Vitu hivi vimekuwa sambamba na vyenye mafaa kwa jamii yoyote ile duniani, lakini vikileta matatizo makubwa sana katika baadhi ya nchi duniani, matharani ubaguzi wa kiimani umeleta machafuko na uharibifu mkubwa mali pamoja na mauti dhidi ya binadamu.

Vitu hivi imekuwa ni vigumu sana kutenganisha katika dunia ya leo huku machipuko ya kiimani yakija kwa kasi ya ajabu. Kwa upande wa Tanzania mfumo wa siasa umekuwa ni wa kuakisi kutoka mataifa ya Magharibi, na uakisi wake umekuwa ni kinyume. Tukiangalia historia ya binadamu tunaona yakuwa kabla binadamu hajajishughulisha na masuala ya siasa na utawala alikuwa anajishughulisha na maswala ya dini, binadamu akawa mcha-Mungu.

Ulipofika wakati wa uteuzi wa kiongozi wa jamii mtu aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo alikuwa ni yule aliyeonekana ni mcha-Mungu. Hata katika jamii zetu za kiafrika zilizotuletea kiongozi wa utawala, pia alikuwa kiongozi wa dini. Ni huyu aliyeongoza shughuli zote za utawala na za dini katika jamii. Itatumika biblia kutoa mifano hai kuthibitisha uhusiano wa dini na siasa. Hakuna ubishi dunia inakubali yakuwa Yesu Kristo ndiye mwanzilishi wa dini ya kikristo. Hii ni kusema kuwa Yesu Kristo alikuwa kiongozi wa dini. Kwaupande wa kabila Yesu alikuwa Muebrania.

Alipozaliwa nchini Uyahudi alikuta tayari watu wa kabila lake wanadini yao ya kiyahudi. Viongozi wa dini ya kiyahudi walikuwa pia watawala waliotawala kwa kutumia sheria za kiyahudi zilizomo katika kitabu chao cha sheria kiitwacho TORATI sheria hizo za dini zikawa pia sheria za utawala. Warumi walipoanzisha utawala wao, Wayahudi waliwaruhusu Warumi kufuata sheria zao za dini ambazo pia zilikuwa sheria za utawala wao wa jadi. Kuhani Mkuu ambaye alikuwa kiongozi mkuu wa dini, alikuwa mwenyekiti wa Baraza kuu la utawala lililoitwa Sanhedrin.

Ni baraza hilo ndilo lililotoa hukumu kuwa Yesu auawe (Math 26:65-69). Hata hivyo adhabu yoyote ya kifo iliyotolewa na baraza kuu la wayahudi ilibidi ithibitishwe kwanza na mtawala wa Kirumi kabla haijatekelezwa (Yohana 18:31). Kwa upande wa Yesu Kristo alipoanza kufundisha dini yake mpya alikosoa sheria za kiyahudi ambazo aliziona hazikuwasaidia binadamu kuishi kwa upendo na amani. Aliwataka wafuasi wa dini yake mpya wasiwe na tabia ya kulipa kisasi. Kwamfano sheria za kiyahudi zinasisitiza kauli ya jicho kwa jicho na jino kwa jino. Katika (Math 5:38-41) tunasoma yakuwa Yesu hakutaka sheria hizo, alisema, "Mmesikia kwamba imenenwa jicho kwa jicho na jino kwa jino, lakini mimi nawaambia msishindane na mwovu lakini mtu akupigae shavu la kuume mgeuzie na la pili na mtu atakaye kushitaki nakuitwaa kanzu yako mwachie na joho.

Uongozi safi wa kidini wa Yesu Kristu uliwavutia wayahudi wa kawaida hata wakaona anafaa kuwa kiongozi wa utawala, wakataka kumfanya awemfalme. Lakini Yesu hakuwa tayari kujiingiza mno katika masuala ya siasa na utawala (Yohana 6:15) alizoea kusema ufalme wake sio wa ulimwengu huu (Yohana 18:36) Katika mafundisho yake, Yesu hakuwahi kuwaambia wafuasi wake wasichanganye dini na siasa. Hata hivyo aliwataka wawe waangalifu katika kuyashughulikia masuala hayo mawili. Alisema, "Ya Kaisari mpeni Kaisari na ya Mungu mpeni Mungu". (Luka 20:25).

Hakuwahi kuwataka wafuasi wake washughulike na mambo ya mungu (dini) tu na wasijishughulishe na siasa. Katika hali hii niwazi kuwa kiongozi wa dini hatakiwi kuhubiri siasa katika jengo la ibada akaacha mambo ya mungu. Vilevile anapokuwa nje ya jengo la ibada hana mwiko wakutokuzungumzia masuala ya siasa na utawala. Baada ya kufa Yesu, wafuasi wake waliendelea kujihusisha na masuala ya dini na siasa, mambo ya utawala yakiendelea kuhusishwa na dini. "Iliaminika kuwa mamlaka yote yanatoka kwa Mungu (Warumi 13:1).

Katika hali hiyo kiongozi wa Katoliki duniani Papa wa Roma alipewa mamlaka makubwa ya utawala, eneo lake la Vatican likapewa hadhi ya utawala wa nchi. Eneo hilo likapewa mamlaka kamili yakupokea mabalozi wakigeni. Hatua hiyo ilichukuliwa kutokana na imani ileile iliyojengeka siku nyingi kuwa kiongozi wa dini ndiye anayefaa kuwa kiongozi wa utawala pia maana kwanjia hiyo atakuwa nanafasi nzuri ya kupambana na maovu. Lakini wakati Papa wa Roma anashughulikia zaidi masuala ya dini kuliko ya siasa na utawala, kuna viongozi wengine wa dini wamewahi kupewa madaraka kamili ya kushika utawala wa nchi. Mfano Askofu Mkuu Makarios wa kisiwa cha Cyprus ambaye aliwahi kutembelea Tanzania.

Wakati huohuo kuna nchi duniani ziliamua siku nyingi kuwa nchi za dini mfano Uingereza ni nchi ya kikristo ambapo mishahara ya maaskofu hulipwa na serikali. Pia nchi za Saud Arabia, Moroco na Libya ni nchi za kiislamu. Si hivyo tu pia kuna nchi ambazo vyama vya siasa vya kidini vinaruhusiwa mfano Ujerumani Christian Democratic Union (CDU). Kwa upande wa Tanzania nchi iliyozoea mapokeo, ni vigumu sana kupembua ni falsafa iliyotumika kutenganisha dini na siasa.

Kwakuanzia watawala wetu, wameshikilia kuwa dini na siasa ni vitu viwili tofauti kabisa, wanasema tusichanganye dini na siasa. Wanasema nchi yetu takatifu haina dini lakini watu wake wanadini. Huu ni ulaghai wa kimtazamo na kifikra, itakuwaje nchi isiwe na dini halafu watu wake wawe na dini?. Kunaumuhimu gani wa kuiombea mema nchi hii inayoaminika kuwa mungu aliiteua kuwa kisiwa cha amani na utulivu duniani ilihali wakaazi wa nchi hii wako mlengo wa kushoto na minajili ya munyazi mungu. Inafahamika yakuwa dini ilikuwepo hata kabla ya Yesu kristu na Mtume S.A.W hawajazaliwa. Kuna kitu kipo ndani yake, bora tuwe wawazi tuuambie umma kuwa Tanzania haina dini rasmi kama ilivyo na lugha rasmi ya Kiswahili.

Fikra za Mwalimu J.K Nyerere na wasaidizi wake ni vigumu sana kubeza kwani zilichambuliwa kwanza kabla ya maamuzi na ndiyo maana zinakuwa na mafaa mbele ya Tanzania yenye mshikamano, upendo, amani, utulivu na isiyo na udini wala ukabila katika kizazi hiki cha nyoka. Inaaminika kuwa mfumo uliotumika katika jambo hili ni fumbo la imani, na ndiyo siri ya amani na utulivu wa kisiwa hiki ambacho hakijawahi kuonja mtutu wa bunduki tangu enzi za akina Kinjekitile na akina Mkwavinyika (Mkwawa) kwani hata uhuru ulipatikana kwa sound (demokrasia).

Inatia simanzi na kufanya nyoyo za waungwana ziende kasi kanakwamba mtoa rohokashagonga hodi, pale inapodhihirika kuwa wale wanazuoni tuliowapa kibali cha kusimamia lile fumbo la imani, wanasimamia kinyume na maagano ya Mtakatifu Julius K. Nyerere. (Nimtakatifu kwasababu zilizo wazi). Aliwaamini, aliwapenda, akawapa elimu yakimagharibi bure kwa jasho la wananchi, lakini leo wamemsaliti! Wanataka kujua nini kilicho ndani ya fumbo la imani! Wanataka kujua uimara wa imani ya mtanzania! Tuliwapeleka wakasome magharibi, tena kwakuuza migomba na kuku huku tukijitunuku mshikamano na umoja wetu tukitumia dhana ileile iliyotupatia uhuru ya hakuna udini wala ukabila, leo wanakuja kufanyia field (mafunzo kwa vitendo) kwetu tena katikati ya mwamko wakiimani ya kila mmoja.

Kunaulazima wa kuwa na mahakama ya kadhi? Je mahakama zilizopo hazikidhi haja? Je kunaulazima wa mahakimu kujua biblia, au msahafu kuliko kujua sheria za nchi? Maswali yote hapo juu jibu lake wanalo wanazuoni. Leo wanazuoni hawa wanajaribu kila liwezekanalo kuisilimisha Tanzania, kwa shinikizo la Maulamaa wa umangani!, hii ni aibu na fedheha kubwa, Majuto yapo kwa wananchi tuliotoa leseni kwa wanazuoni hawa kutuongoza Shime! Watanzania tufikiri kabla yakuridhia majaribio ya wanazuoni hawa. Lakini wanazuoni wajue kuwa imani ya mtu haijaribiwi. Inasadikika na kuaminika kuwa Tanzania kuna dini kuu mbili, ambazo ni Uislamu na Ukristo.

Kinadharia na kivitendo hakuna dini ambayo ndiyo kioo cha Taifa kama ilivyo Lugha ya Kiswahili. Kujiunga na Jumuiya za Kiislamu (Afrika na Duniani) nikuzika umoja tulionao, Amani tuliyonayo na baadaye kuzalisha chuki na Udini ndani ya nyoyo zilizo katikati ya muhimili mkuu wa kiimani. Waislamu na Wakristo tusibariki majaribio haya, kwani wahanga wa machafuko ni makabwela, kwakuwa baada ya hali ya hewa kuwa mbaya, wanazuoni hawa utawaona wakiwa katika meza pana ya kutafunia kuku wakijinasibu kwa mapatano mseto, wakati tuliovunjika viuno tukiwa tunaugulia bila ruzuku wala kifuta jasho. Kwanadharia hiyo wanazuoni wanaandika barua za kuacha kazi!

Kwaheshima na taadhima, Nguvu ya umma izijibu barua hizo kwa kuweka ugoko juu ya mchakato mgando wa Kuisilimisha TZ.

Uwezo tunao, Nia tunayo na Sababu tunayo!!!!!!
 
Mzee wewe ni jasiri sana. Aliyekataa Abdu wako asiunganishwe na historia ya TANU ni nani? Hakutajwa kwenye kitabu cha Kivukoni? Uzuri mmoja wa kitabu cha Kivukoni kimeandikwa kitaasisi, kimeandikwa na vichwa vingi. Kimeandikwa KITAIFA. Historia ya NCHI au TANU haiwezi kuandikwa na kichwa kimoja, kwa kutumia kumbukumbu za familia moja.
 

Mohamed Said,

Tukiwaweka kando kwamda tu Daisy ambaye ndie nguzo ya simulizi lako na Iliffe kama mhariri wa maandishi ya Daisy, je unao ushahidi nje ya hao juu ya madai yako kwa AA, TAA, TANU, Nyerere na Sykes family?
 

Kadogoo
,


..acha ubishi ndugu yangu, Waislamu wa Machame, Usangi, Kagera, wanazingatia elimu kuliko wenzao walioko Pwani na Kusini.

Nafikiri rejea historia vizuri na pata data sahihi.

Wakti wa Muungano wa Tanganyika na Znz mwaka 1964. Zanzibar ilikuwa na wasomi wengi kuliko Tanganyika in terms of ratio. Mwaka 1963 Znz ilikuwa na wasomi wengi kuliko nchi yoyote katika Africa mashariki kwa maana ya tanganyika, kenya na Uganda.

Na Znz ni nchi ya Kiislam kwa maana raia wake kwa zaidi ya 99.7% ni waislam.

Kwa manyiki hiyo utaona huko Tanganyika wengi wa waislam walipenda kusoma lakin mifumo ya kiutawala iliwabana sana na kukosa fursa za kusoma kabla ya uhuru wenu labda kuanzia 1950 mpaka 1961.

Nikikupa mfano hai kabisa kabla ya uhuru kwa waislam waliokuwa wanatokea kanda ya Pwani kwa wanaume skuli yao ya Sekondari ilikuwa ni Mzumbe Tu na kwa wanawake ilikuwa mangamba girls sec (mbayo sasa inaitwa mtwara girls) na hizi zilikuwa zinachukua wanafunzi wote bila kujali dini zao. lakin kwa wazao wa dini nyingine walikuwa na minaki, Pugu, chidya, ndanda n.k ambazo zilichukua wakristo watupu.

Fursa ndio ilikuwa chanzo cha kukosa ilmu kwa waislam ukilinganisha kwa wakristo wakti huo lakin ilimu ingetolewa sawa basi kila dini ingechangamkia..
 
Mohamed Said,

Tukiwaweka kando kwamda tu Daisy ambaye ndie nguzo ya simulizi lako na Iliffe kama mhariri wa maandishi ya Daisy, je unao ushahidi nje ya hao juu ya madai yako kwa AA, TAA, TANU, Nyerere na Sykes family?

Siamini kama unaweza uliza suala kama hili !.

Kwani ushahidi huo haukutoshelezi? kivipi? au wewe weka ushahidi wako na reference zako kupingana na huo.

Pole sana

 
Naam! Naam! Nafyonza Ilm tu hapa bila wewe watu wasingetafuta vitabu kuwafahamu kina Kleist.Leo hii watu ndio wanataka kujua habari za Aggrey wkt wewe umezielezea zaidi ya miaka 15 iliyopita.Endelea kutoa Ilm Mkubwa.
Kleist na Aggrey sio majina mapya. Infact, upo mtaa hapa Dar unaitwa Aggrey miaka mingi kabla ya kitabu cha Mohamed. Majina mapya kwenye kitabu kile ni Kiyate, Mashado, Sheikh Amir,..., na Uislam wa TANU.
 

Kitabu chako kinapatika wapi na kilitoka lini?

Vipi mauzo yake sokoni?
 
Barubaru,Ni nani alitaifisha shule(skuli) za Pugu, Chidya, Ndanda, Minaki, Alliances za Dodoma na Musoma,..., na lizitaifisha kwa nini?
 
Kipo baadhi ya maduka hapa Dar,kama dar bookshop centre

Lakini waweza kukipata ukienda ubalozi wa USA, wao ndio wanakisimamia.

Yericko Nyerere,

Nimesoma hilo tangazo la "hadithi za kitabu chako". Vipi naona unaleta "mahubiri" na mikanganyiko mingi hapa jamvini. Hapo awali Mag3 nae pia alitaka kuleta "mada juu ya mada" lakini akatusihi kwa ustaarabu tutoe ushauri kama wanajamvi wenzie. Mimi binafsi nikamshauri kuwa isingekua idea njema maana, nalichelea kwenda nje ya hii mada/shutuma ulizoleta. Nastaajabu wewe unayafanza yaleyale!?

Nimejaribu saana kukufuatilia hapa jamvini,lakini kwa hizo "hadithi za kitabu chako" umejibainisha kwa yalo mengi. Kumbe ni wewe wala si Sheikh Mohammed Said aletae hasama baina yetu hapo nchini na chokochoko!

Lakini imekua vizuri kutujuza kuwa kumbe nyuma ya "pazia" ulojitahidi kujificha nalo kuna American Evangelism Ideology na State Dept. kwa kupitia ubalozi wao hapo nchini. Haina neno maana hizi chokochoko za wa-Amerika zinajulikana pahala pengi saana duniani na wamezianza karne kadhaa.

I'm afraid you failed terribly to prove most of us wrong...sorry!
 

JokaKuu,

Nakushukuru na nimekufahamu. Pia nafuatilia ule mjadala wa masuala ya elimu hapa jamvini baina yako na Kadogoo,unanifurahisha kumpa changamoto kwa njia ya ustaarabu ndugu yetu Kadogoo. Nae pia ni mahiri wa stats na maelekezo mazuri.

Nafikiri "baadhi yetu" yaelekea tunaanza kuelekea pahala pema na kusikizana. Nafsi ya kukubali kuwa kuna tatizo hapo nchini, na pia kukubali kuwa baadhi ya wenzetu walio wengi kwenye baadhi ya maeneo hususan waIslam, wanahitaji kusaidiwa na kushauriwa kwa njia mbalimbali. Ama kwa hakika hii ni dalili njema. Basi tuendelee na mnakasha.

Nakutakia siku njema.

Ahsanta.
 

Wewe huijui Bakwata! uliza Waislamu nini Bakwata! wala historia yake na harakati za Waislamu kutaka mabadiliko ndani ya chombo hicho kinacholindwa na Serikali huwezi kuamini! Msifumbe macho na someni Kitabu cha Profesa Hamza Njozi cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania ili kutambua nini Bakwata na juhudi za Serikali kuilinda dhidi ya Jumuiya yoyote ya Kiislamu!

Kama wewe unakiri kuwa Shule za Bakwata zinatia aibu kwanini Serikali inakubali kuilinda na kuitambua Bakwata ndio chombo halali cha Waislamu wakati Waislamu wenyewe hawaitaki? mwaka 1991 Waislamu wa nchi toka kila pembe ya nchi nzima walivamia Ofisi za Bakwata Kinondoni ili kuleta mageuzi lakini Serikali haikukubali na kulazimisha Ofisi irudi kwa wenyewe!

Siku hiyo Radio Tanzania msomaji wake akiwa Jackob Tesha saa 2 usiku taarifa habari wanatangaza Mapinduzi Bakwata! lakini baadae tumeona juhudi za Lyatonga Mrema kama Waziri wa Mambo ya ndani akitafuta mchango toka kanisani ili kuinusuru Bakwata!

Inaendelea........
 

Wild Card,
Reginald Mhango wa Daily News alipoogopa kuchapa kumbukumbu
ya kifo cha Abdu Sykes mwaka 1988 kwa hoja kuwa historia ya Abdu
imegungamana na historia ya Tanganyika kwa hiyo lazima apate kibali
kwanza kutoka Dodoma, alielezwa kuwa hiyo ndiyo historia ya Abdu
hakuna awezae kuibadili.

Sidai kuandika historia ya nchi kwa kumbukumbu za Abdu ila hayo
niloandika yote kayafanya kwa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ni majaaliwa tu kuwa historia ya maisha yake imefungamana na historia
ya kudai ukombozi wa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…