Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kipo baadhi ya maduka hapa Dar,kama dar bookshop centre

Lakini waweza kukipata ukienda ubalozi wa USA, wao ndio wanakisimamia.

Wanajamvi,
Ubalozi wa Marekani wanasimamia kitabu cha Yericko Nyerere!

Hii ngoma pevu.
Sasa ngoma inogile.

Ubalozi wa Marekani...
Sasa wanauza vitabu vya Yericko...

Hii nina hakika imevunja rekodi ya JF? Jamani msifanye maskhara hili jamvi zito.

Sasa barza itanoga.

Ritz hakikisha barza juisi na kahawa, haluwa havipungui.

Ama mja omba Allah akujaalie akili zilizotimia.
 
Duh Kadogoo naomba nimtete Mag3 kama hili hulijui ni vyema ukafuta ushauri wa Mag3 hakuna atakayekucheka huu mnakasha ni maji marefu sana.

MAG3;

Kama mmeshindwa kujibu hoja heri kunyamaza wala sio aibu!
 
Last edited by a moderator:
Gombe sugu kumbe na wewe ni muokoteza hoja kama Said, hahaha unamfahamu Lwakabamba lakini? Huyu aliwapa maisha wabongo pale Kist kuanzia malekchara, tvutorial assistants mpaka workshop instructors wa dini na makabila mbalimbali leo analinganishwa na huyo Rukala? ama kweli hili somo lenu la udini halina aibu.

Kuna kit nakisoma btn the lines, shule si mchezo bana yaani leo waliokuwa wa mjini kama nukuu lukuki za mchchezi said wanalamika kuonewa n a kudhulumiwa na mijitu isiyostaarabika kutoka bara hahahahahaha!!!!! Kweli waliosema elimu ufunguo wa maisha they were very right.

Cool Runnings,

Mbona nyinyi mna hulka ya kujibu kwa ghadhab na tashtit!? Naona umeanza kwa kutukashifu sisi na kumalizia kwa kujiadhiri nyinyi wenyewe!?
Ustaarabu gani huo,ati leo kutuona waTanzania wenzenu hatujui kusoma wala kuandika halafu mnatucheka na dhiki zimetujaa na nyie kutufanzia kebehi na mbwembwe nyingi!?

Wanapokuja "wageni" kama kina Alhaj Rukara na kuamua kutusaidia mnawatuhumu uchochezi,ugaidi na ushawishi!?

Kwa kukusaidia,ilitakiwa uniulize yale niliyokujuza na kumtuhumu Lwakabamba kama ni ya kweli,niliyatoa wapi au niliyajuaje,na labda nitoe details zaidi!? Sasa ilobaki ingekua ni amri yangu aidha kuitikia wito wako au kuyaacha kwa sababu kadhaa. Lakini najua wewe ni "miongoni mwa wale wapendao kujipunja".
Ulipofurukuta kujibu hoja yangu(najua nyingine ulimwachia mwenyewe Nguruvi3),unadai ati Prof. Silas Lwakabamba "amewapa maisha" saana waTanzania pale KIST,hususan ma-Lectures,Tutorial Assistants na hata Workshop Instructors.
Huoni kuwa hoja na maelekezo yangu bado inasimama palepale!?
Kwani hujui kuwa naye pia Alhaj Rukara anawafadhili,kuwasaidia na kuwafariji waTanzania wengi saana kupitia connections na influence zake pale Burundi!? Je hii ndiyo inamuondolea hizo tuhuma alizoshutumiwa na Nguruvi3!?(kama ni za kweli ,maana hatukuziona kuletwa hapa jamvini!)
Kumbuka mkimwaga ugali nasi tutamwaga "mboga",halafu soote tulale na njaa!

Evidently,you didn't get enough of an education yourself. If you can't even use spell check to deliver a sentence coherently and phonetically keep it to yourself. Embarrassing!

Love me or hate me,both are in my favour!

CC: mag3,nakusalimia Muheshimiwa naona umemwekea jamaa yako "LIKE" kwa majibu "murua" alonipa. Au unataka na mimi nipewe "adhabu" kama ndugu yangu Ritz!? Haina neno tuendelee na mnakasha.
 
Wanajamvi,
Ubalozi wa Marekani wanasimamia kitabu cha Yericko Nyerere!

Hii ngoma pevu.
Sasa ngoma inogile.

Ubalozi wa Marekani...
Sasa wanauza vitabu vya Yericko...

Hii nina hakika imevunja rekodi ya JF?
Jamani msifanye maskhara hili jamvi zito.

Sasa barza itanoga.

Ritz hakikisha barza juisi na kahawa, haluwa
havipungui.

Ama mja omba Allah akujaalie akili zilizotimia.

Hahaaahaa hili limekustua sana mpaka ukajizua ukashindwa mkuu,

Nilijua tu nikikupa hiyo lazima uhamaki.

Poleeeee mkuu kwakukukwaza.
 
Kinauzwa kiasi gani?

Kitabu ni cha kwako au cha ubalozi wa Marekani?

Ni chakwangu mkuu,

Haijawa rasmi wao kukiuza,

Wanajiridhisha kwanza kisha mchakato wa kukiweka kiwe kwa lugha ya kiingereza utaanza,

Nilivitoa vitabu vichache kama sehemu ya majaribio ya soko tu,

Nimeshafanya mahojiano na baadhi ya vituo vya tv hapa nchini na nje ya nchi kukielezea kitabu hicho.

Mchakato wa Ubalozi wa USA hapa nchini ukikamilika bila shaka kitakuwa hewani rasmi kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.
 
Kipo baadhi ya maduka hapa Dar,kama dar bookshop centre

Lakini waweza kukipata ukienda ubalozi wa USA, wao ndio wanakisimamia.

Yericko nae ana kitabu?
Cha ngano za mapenz kama mwanakijiji au?
Eti kinasimamiwa na ubalozi wa marekani..!
Naona umeamua kuja kudanganya ikhuani...
 
Yericko Nyerere,

Nimesoma hilo tangazo la "hadithi za kitabu chako". Vipi naona unaleta "mahubiri" na mikanganyiko mingi hapa jamvini. Hapo awali Mag3 nae pia alitaka kuleta "mada juu ya mada" lakini akatusihi kwa ustaarabu tutoe ushauri kama wanajamvi wenzie. Mimi binafsi nikamshauri kuwa isingekua idea njema maana, nalichelea kwenda nje ya hii mada/shutuma ulizoleta. Nastaajabu wewe unayafanza yaleyale!?

Nimejaribu saana kukufuatilia hapa jamvini,lakini kwa hizo "hadithi za kitabu chako" umejibainisha kwa yalo mengi. Kumbe ni wewe wala si Sheikh Mohammed Said aletae hasama baina yetu hapo nchini na chokochoko!

Lakini imekua vizuri kutujuza kuwa kumbe nyuma ya "pazia" ulojitahidi kujificha nalo kuna American Evangelism Ideology na State Dept. kwa kupitia ubalozi wao hapo nchini. Haina neno maana hizi chokochoko za wa-Amerika zinajulikana pahala pengi saana duniani na wamezianza karne kadhaa.

I'm afraid you failed terribly to prove most of us wrong...sorry!

Pole sana ndugu yangu kama nimekuudhi kweli,

Nimekileta hapa hicho kipande cha kitabu ili kusherehesha mnakasha na na kutia mbinyo wa hoja kuu.
 
Sio kwamba tunpiga makofi tu bali tunashangilia ushindi.Hebu msikize Mohammed

Hata Mzee Mwanakijiji nae ni kichekesho!.Nakumbuka yale maneno yako siku ulipoalikwa ubwabwa kule Marekani,kwamba Marekani hakuna chakula cha bure.Inaonekana hata marehemu Sykes alipomualika Aggrey alikuwa na fikra kama hiyo na kweli ndiyo mantiki.
Kichekesho ni akina Mwanakijji kumpa hadhi mgeni kuwa ndiye aliyeatoa wazo la kuasisi AA kuliko mwenyeji wake.Kwanini isiaminike kuwa wazo hilo lilikuwa kwa Sykes na pengine tu lilipata nguvu kwa ugeni wa Aggrey?.

Kwa hili sheikh Mohammed :rockon::israel:

Ami Wape Leso..!
Wakigoma waache machozi yawabubujike..
 
Ni chakwangu mkuu,

Haijawa rasmi wao kukiuza,

Wanajiridhisha kwanza kisha mchakato wa kukiweka kiwe kwa lugha ya kiingereza utaanza,

Nilivitoa vitabu vichache kama sehemu ya majaribio ya soko tu,

Nimeshafanya mahojiano na baadhi ya vituo vya tv hapa nchini na nje ya nchi kukielezea kitabu hicho.

Mchakato wa Ubalozi wa USA hapa nchini ukikamilika bila shaka kitakuwa hewani rasmi kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

Samahani lakini unasema kitabu ni chako mwenyewe kinaelezea ugaidi inakuaje mpaka mchakato wake wahusike ubalozi wa marekani. Labda tufahamishe marekani wana maslahi gani na kitabu chako wanakulipa au umejitolea.
 
  • Thanks
Reactions: Ami

Bila samahani mkuu,

Mimi nimewaomba wafadhiri huo mradi nao wakatoa mapendekezo yao ambayo kimsingi nilikubali,

Mda ukifika utakiona shekhe wangu,,
 
  • Thanks
Reactions: Ami
Kadogoo, Wickama,

..nadhani mwamko wa elimu ktk maeneo hayo ndiyo uliopelekea bakwata na taasisi nyingine nyingi kujenga shule huko.

..labda nikuulize; Bakwata mkoa wa pwani wana shule ngapi za sekondari, na wamezifungua lini? Kwa uelewa wangu mkoa wa Kilimanjaro ni kati ya mikoa yenye shule kongwe za sekondari za Bakwata.

..kuna jamaa yangu alinitonya kwamba, Kilimanjaro kulikuwa na shule ya misheni wakati wa mkoloni. Baada ya uhuru wazazi wakawa wanataka shule ya sekondari. What they did, ni kuikabidhi shule hiyo kwa Bakwata ambao walianzisha shule ya sekondari !! sasa tell me if that can happen ktk maeneo ya pwani.

..Shule za Bakwata zilizoko Kilimanjaro zinatia aibu kwasababu taasisi hiyo haina FUNDS za kutosha, pamoja UTAALAMU wa kuendesha shule hizo. Mimi nadhani wakiwezeshwa wanaweza kuwa wanatoa products nzuri tu.

NB:

..Nimeangalia matokeo ya Kirinjiko nimekuta wamefanya vizuri kuliko baadhi ya shule za misheni.

..Kwa kweli wanastahili pongezi kwa kuonyesha mfano kwamba INAWEZEKANA!!

..Sasa tunataka Feza na Kirinjiko zisambae kila pembe ya Tanzania.

cc: gombesugu, Nguruvi3

Joka Kuu ahsante sana.

Ndugu yangu Kadogoo, Attitude is everything. Hapa mjini Tanga nina rafiki zangu wa Kimachame waislamu wa kufa na kupona, lakini wote wanasomesha watoto wao kunakoeleweka. Ni hao hao wamefungua mabiashara, mashamba ya ngombe wa maziwa, nk, lakini swala tano ziko palepale.

Hakuna cha NECTA wala mjomba wake NECTA. Ukitaka majina sema. Siku zote tunasema vita vya panzi ni furaha ya kunguru. Kama waislamu wengi wanaaminishwa kuwa adui yao ni Bakwata ni lini ROHO zao zitatakasika kutafuta SOLUTION ya madhila ya jamii yao? Hata Bakwata itafikia mahali ikaanza kuwahofia wapiga yowe. Kumbuka MUDA hausubiri.

Mwenyezi Mungu ana kawaida ya kuzawadia bidii. Haiwezekani wazazi waliojenga shule wakatafuta waalimu na kuwahimiza watoto kufuatilia shule eti walingane na wasiofanya hayo hata kama wanavuta uradi. Hapo hamna cha dhehebu. Bila mtazamo chanya (+ve)hapa ipo hatari machozi ya majukwaani yatahamia kwa watoto na wajukuu, huku wenzao toka familia zilizoamua kujisweka mzigoni wakitinga UDSM, UDOM, SUA nk.

Kadogoo ukikutana na mwanangu tafadhali usimuanzishie stori eti Mkapa alivyokuwa Mhariri zamani leo kunamuathiri hadi anapata division zero. Kwa faida ya wanajamvi; Mwanza kuna shule ya Buhongwa Islamic ambayo baada ya kujipanga upya sasa nayo imeanza kuona positive results!!!! Ushahidi kuwa dawa ipo kwenye kujipanga na bidii sio majukwaa ya machozi.

Ajabu ni kuwa wanaochochea Simanzi/kukata tamaa/chuki ukiwauliza haya tufanye nini? HAWANA JIBU.
 
Ni chakwangu mkuu,

Haijawa rasmi wao kukiuza,

Wanajiridhisha kwanza kisha mchakato wa kukiweka kiwe kwa lugha ya kiingereza utaanza,

Nilivitoa vitabu vichache kama sehemu ya majaribio ya soko tu,

Nimeshafanya mahojiano na baadhi ya vituo vya tv hapa nchini na nje ya nchi kukielezea kitabu hicho.

Mchakato wa Ubalozi wa USA hapa nchini ukikamilika bila shaka kitakuwa hewani rasmi kwa lugha ya kiswahili na kiingereza.

Yericko, hongera sana kwa efforts. Binafsi i wouldnt care hata kama ningeambiwa review wanafanya ubalozi wa Cameroon. Issue kubwa ni kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa vitabu vya Watanzania worldwide ukilinganisha na wenzetu kama Kenya au Uganda au Ethiopia. Ukija kwenye published papers ndio usiseme tena trend ni hiyo pia. Kwa hiyo people like yourself au Mzee MS lazima kuwa commended kwa efforts zenu. Tuelekeze jinsi ya kukipata kikiwa in the open. Good Luck
 
Wewe huijui Bakwata! uliza Waislamu nini Bakwata! wala historia yake na harakati za Waislamu kutaka mabadiliko ndani ya chombo hicho kinacholindwa na Serikali huwezi kuamini! Msifumbe macho na someni Kitabu cha Profesa Hamza Njozi cha Mwembechai Killings and the Political Future of Tanzania ili kutambua nini Bakwata na juhudi za Serikali kuilinda dhidi ya Jumuiya yoyote ya Kiislamu!

Kama wewe unakiri kuwa Shule za Bakwata zinatia aibu kwanini Serikali inakubali kuilinda na kuitambua Bakwata ndio chombo halali cha Waislamu wakati Waislamu wenyewe hawaitaki? mwaka 1991 Waislamu wa nchi toka kila pembe ya nchi nzima walivamia Ofisi za Bakwata Kinondoni ili kuleta mageuzi lakini Serikali haikukubali na kulazimisha Ofisi irudi kwa wenyewe!

Siku hiyo Radio Tanzania msomaji wake akiwa Jackob Tesha saa 2 usiku taarifa habari wanatangaza Mapinduzi Bakwata! lakini baadae tumeona juhudi za Lyatonga Mrema kama Waziri wa Mambo ya ndani akitafuta mchango toka kanisani ili kuinusuru Bakwata!

Inaendelea........

Kadogoo nadhani una-point katika maelezo yako. Ila imagine wewe ni serikali unataka dialogue na waislamu. Haya utazungumza na wangapi? lazima mahali fulani pawe na aina ya uwakilishi. Mimi sitetei quality wala structure ya uwakilishi. Pili ni maumbile ya wanadamu kuzipenda nafsi zinazozifanyia hisani. Mtu anayepanda hadharani kukutusi una haja gani ya maongezi naye? Sishangai serikali kuwa karibu na bakwata. Lazima u-deal na yule ambaye hakukukwazi mno. Kisha nasema kama wewe na kila mwislamu jibu lake ni WEWE UNAIFAHAMU BAKWATA? tatizo litamalizika vipi? Vinginevyo basi tusubiri mpaka wafe wote, assuming ISRAIL ataanzia kwao sio kwako.
 
Yericko, hongera sana kwa efforts. Binafsi i wouldnt care hata kama ningeambiwa review wanafanya ubalozi wa Cameroon. Issue kubwa ni kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa vitabu vya Watanzania worldwide ukilinganisha na wenzetu kama Kenya au Uganda au Ethiopia. Ukija kwenye published papers ndio usiseme tena trend ni hiyo pia. Kwa hiyo people like yourself au Mzee MS lazima kuwa commended kwa efforts zenu. Tuelekeze jinsi ya kukipata kikiwa in the open. Good Luck

Asante sana mkuu,

Tutatoa taarifa ya pamoja pindi mchakato utakapokamilika.
 
Kadogoo ukikutana na mwanangu tafadhali usimuanzishie stori eti Mkapa alivyokuwa Mhariri zamani leo kunamuathiri hadi anapata division zero. Kwa faida ya wanajamvi; Mwanza kuna shule ya Buhongwa Islamic ambayo baada ya kujipanga upya sasa nayo imeanza kuona positive results!!!! Ushahidi kuwa dawa ipo kwenye kujipanga na bidii sio majukwaa ya machozi.

Ajabu ni kuwa wanaochochea Simanzi/kukata tamaa/chuki ukiwauliza haya tufanye nini? HAWANA JIBU.

Kumbe sio Waislamu wa Machame na Upare tu hata na Waislamu wa Mwanza wanamwamko pevu ktk elimu kuliko wa Pwani? vipi na Zanzibar nao mwamko wao ni vipi?
Lengo lenu sasa nimeshajua! mnataka kuwagawa Waislamu kimakabila na kikanda! ndio maana mnadai Waislamu wa Machame wanamwamko mkubwa kielimu kuliko Waislamu wa Pwani! hii ni siasa ya Divide and Rule! Ufahamu wenu finyu kuhusu Shule za Mudio na Kirinjiku wa kudhani zilijengwa na makabila hayo kwa lengo la kusomesha Wachagga na Wapare! Shule hizi zimejengwa kwa nguvu za Waislamu wote na kuzijenga ktk maeneo hayo hakuna uhusiano wowote na ukabila au ukanda!

Huenda mkaja na hoja kuwa MUM (Muslim University of Morogoro) imejengwa na Waislamu Waluguru au Thaqafa ya Mwanza imejengwa na Waislamu Wasukuma! hapa mnataka kuwagawa Waislamu lakini kimsingi haiwezekani kuwagawa kwani Waislamu wote ni ndugu! na Shule hizo wanapokea Wanafunzi wa Kiislamu toka popote!
 
Nafikiri rejea historia vizuri na pata data sahihi.

Wakti wa Muungano wa Tanganyika na Znz mwaka 1964. Zanzibar ilikuwa na wasomi wengi kuliko Tanganyika in terms of ratio. Mwaka 1963 Znz ilikuwa na wasomi wengi kuliko nchi yoyote katika Africa mashariki kwa maana ya tanganyika, kenya na Uganda.

Na Znz ni nchi ya Kiislam kwa maana raia wake kwa zaidi ya 99.7% ni waislam.

Kwa manyiki hiyo utaona huko Tanganyika wengi wa waislam walipenda kusoma lakin mifumo ya kiutawala iliwabana sana na kukosa fursa za kusoma kabla ya uhuru wenu labda kuanzia 1950 mpaka 1961.

Nikikupa mfano hai kabisa kabla ya uhuru kwa waislam waliokuwa wanatokea kanda ya Pwani kwa wanaume skuli yao ya Sekondari ilikuwa ni Mzumbe Tu na kwa wanawake ilikuwa mangamba girls sec (mbayo sasa inaitwa mtwara girls) na hizi zilikuwa zinachukua wanafunzi wote bila kujali dini zao. lakin kwa wazao wa dini nyingine walikuwa na minaki, Pugu, chidya, ndanda n.k ambazo zilichukua wakristo watupu.

Fursa ndio ilikuwa chanzo cha kukosa ilmu kwa waislam ukilinganisha kwa wakristo wakti huo lakin ilimu ingetolewa sawa basi kila dini ingechangamkia..

Barubaru,

..OK, ZNZ ilikuwa juu kielimu, leo hii imepitwa na Kenya na Uganda. sasa tunapaswa kujiuliza, WHAT HAPPENED??

..ZNZ hiyohiyo ambayo unasema ilikuwa mbele kielimu na ilikuwa na mwamko kwelikweli, wakati Univ of East Africa inaanzishwa, haikuwa na tawi lolote la taasisi hiyo. Uganda walikuwa na Makerere. Tanganyika walikuwa cha Kitivo cha Sheria. Kenya walikuwa na Faculty of Engineering. WHAT HAPPENED? WHY??

..Hoja yako nyingine ni kwamba hapa Tanganyika kulikuwepo shule zinachukua wanafunzi wa dini zote, halafu Wakristo wakawa na zao wenyewe kama Pugu[St.Francis], Minaki[St.Andrews], etc. Kukusahihisha tu hizo shule Waktisto zilikuwa zinachukua Waislamu wasiokwazika kwenda huko--pamoja na kwamba walikuwa wachache.

..Kama, Wakristo walikuwa wanashule zao wenyewe, nini kiliwazuia Waislamu kuwa na utaratibu kama huo?

..kuhusu MWAMKO WA ELIMU, hebu tuiangalie Kilimanjaro na Kagera. Hawa wenzetu kabla ya Uhuru walikuwa na vyama vyao vya ushirika. Vyama hivyo vilikuwa vinafadhili wanafunzi mpaka katika vyuo vikuu. Kuna wazee Kichaga walikuwa wanasomeshwa nje ya nchi na KNCU. Huoni kwamba huo ni mwamko wa elimu?? Je, ndugu zetu wa maeneo ya Pwani, Kusini, Kati, wamewahi kuwa na utaratibu kama huo???

..Pia utaratibu wa UPE na KISOMO CHA WATU WAZIMA ulikuwepo Kilimanjaro tangu enzi za mkoloni. The rest of Tanganyika ilikuja ku-catch up na Kilimanjaro ktk UPE 16 years after independence!!

..Mwisho, Muislamu/Muarabu alikuwepo hapa Tanganyika na Zanzibar miaka mingi sana kabla Mzungu/Mkristo hajafika. Sasa kwanini muda wote huo hakuwa na mfumo wowote ule wa elimu unaoeleweka?? Kwanini Pugu, Minaki, Magila, Makerere zijengwe na Mzungu/Mkristo na siyo Muarabu/Muislamu aliyekuwa amemtangulia??

..Binafsi nadhani tatizo la elimu linahitaji utulivu na tafakuri ya kina kulipatia majibu. Tuna bahati mbaya sana kwamba CCM na serikali zake wamekuwa wakishughulikia matatizo ya elimu kwa kusukumwa na siasa. since indepence we have had two false starts; the first time with UPE, and the second time with what has been called "sekondari za kata."

cc: Kadogoo, Wickama, gombesugu, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo nadhani una-point katika maelezo yako. Ila imagine wewe ni serikali unataka dialogue na waislamu. Haya utazungumza na wangapi? lazima mahali fulani pawe na aina ya uwakilishi. Mimi sitetei quality wala structure ya uwakilishi. Pili ni maumbile ya wanadamu kuzipenda nafsi zinazozifanyia hisani. Mtu anayepanda hadharani kukutusi una haja gani ya maongezi naye? Sishangai serikali kuwa karibu na bakwata. Lazima u-deal na yule ambaye hakukukwazi mno. Kisha nasema kama wewe na kila mwislamu jibu lake ni WEWE UNAIFAHAMU BAKWATA? tatizo litamalizika vipi? Vinginevyo basi tusubiri mpaka wafe wote, assuming ISRAIL ataanzia kwao sio kwako.

Wickama;

Hivi Serikali ikitaka kuzungumza na Wakristo wote huwa inazungumza na Kanisa Katoliki tu? mbona Waislamu wanajumuiya kubwa tu inayojumuisha Waislamu wote BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI TANZANIA yaani (Baraza Kuu) (sio Bakwata!) lakini Serikali haitaki kuwasiliana nayo hata kama imeandikishwa kisheria! kwanini Serikali, Wakristo na baadhi ya Wana JF akiwemo Mwanakijiji huwa wanaikumbatia na kuilinda Bakwata? naomba jibu!
 
Kadogoo nadhani una-point katika maelezo yako. Ila imagine wewe ni serikali unataka dialogue na waislamu. Haya utazungumza na wangapi? lazima mahali fulani pawe na aina ya uwakilishi. Mimi sitetei quality wala structure ya uwakilishi. Pili ni maumbile ya wanadamu kuzipenda nafsi zinazozifanyia hisani. Mtu anayepanda hadharani kukutusi una haja gani ya maongezi naye? Sishangai serikali kuwa karibu na bakwata. Lazima u-deal na yule ambaye hakukukwazi mno. Kisha nasema kama wewe na kila mwislamu jibu lake ni WEWE UNAIFAHAMU BAKWATA? tatizo litamalizika vipi? Vinginevyo basi tusubiri mpaka wafe wote, assuming ISRAIL ataanzia kwao sio kwako.

Wickama,
Usidhani kuwa serikali haijua haya yote ambayo Waislam wanasema.

Usidhani kama serikali haiko hadhir na historia ya BAKWATA na vipi ilikuja na nani kaileta.

Yote haya yanafahamika.

Kuna mambo wewe huyajui kabisa wala hayasemwi popote na nina hakika kama si JF wewe usingekutana na mimi na usingesoma haya yote niliyoandika humu.

Ngoja nikumegee kitu...

Hofu kuu ni vipi watamnasua Nyerere na Kanisa iwapo patakuwa na mazungumzo kati ya Waislam na Serikali kuhusu matatizo ya udini?

Si unasikia katika Bunge jana mbunge mmoja anasema matatizo haya yamekuja kwa kuacha mwendo wa Baba wa Taifa ambae hakuwa mdini...

Hapo sisi tunaojua historia ya nchi hii ndipo huwa tunakwenda msalani kucheka watu wasituone.

Nina mengi...
 
Yericko, hongera sana kwa efforts. Binafsi i wouldnt care hata kama ningeambiwa review wanafanya ubalozi wa Cameroon. Issue kubwa ni kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa vitabu vya Watanzania worldwide ukilinganisha na wenzetu kama Kenya au Uganda au Ethiopia. Ukija kwenye published papers ndio usiseme tena trend ni hiyo pia. Kwa hiyo people like yourself au Mzee MS lazima kuwa commended kwa efforts zenu. Tuelekeze jinsi ya kukipata kikiwa in the open. Good Luck

Wickama,
Usiniambie kuwa unaamini kuwa Ubalozi wa Marekani wanashughulika
na kitabu cha Yericko!

Ubalozi wa Marekani!
 
Back
Top Bottom