Kadogoo,
..sasa kama Waislamu wote ni kitu kimoja, kwanini unazungumza kama mtu anayeona fahari pale shule za Bakwata zinapofanya vibaya??
Mohamed Said,
..kwani wewe lengo lako ni kumnasa Nyerere na udini?
..zaidi, kwanini Waislamu wa Bakwata na Baraza Kuu hamkai pamoja na kumaliza tofauti zenu?
..
Jokakuu;
Mimi sifurahii kufeli kwa Wanafunzi wa Bakwata au wa Necta wote ni Wanafunzi wa Tanzania! uhasidi wa aina hiyo usininasibishe nao kabisa kwasababu Hasidi ni mtu mbaya kabisa! najua kuwa kufeli kwa wanafunzi ndio mwanzo wa kurudisha maendeleo ya nchi nyuma sababu tutakuwa na vijana wengi wasio na elimu nzuri na kusababisha umaskini ktk nchi yetu!
Tulimtimua mkoloni ili watoto wetu wote wapate elimu lakini tuliowakabidhi madaraka ya nchi walitugeuka na kufanya ubaguzi! sasa matokeo yake nchi ni maskini na imekuwa ombaomba kwasababu zaidi ya nusu ya raia wa nchi hii wamekosa elimu ambayo ingesaidia kujenga nchi yetu!
Tumejenga taifa la matabaka ya wenye haki ya kupata elimu na wasiostahili! kinyume chake tunaona nchi imeendelea kwa kuwa na idadi ya kutisha ya machinga, walalahoi, Mama ntilie, wapiga debe, wauza migahawa, barafu nk, nk,!
Jokakuu;
Waislamu wa nchi hii hakuna kitu kinawaudhi na kuwanyima usingizi kama kutengana ama iwe na Waislamu wenzao ama iwe ni Wa TZ wenzao! mfano mdogo kabisa ni Zanzibar, ambayo raia wake karibu wote ni Waislamu, pale walipokuwa ktk mgogoro mkubwa tangu mwaka 1995, Common Wealth walijaribu kuwapatanisha bila mafanikio! Serikali ya Mkapa nayo ikajaribu kupatanisha kiaina yake bila mafanikio! lakini mara walipoamua kupatana wenyewe, leo wanaishi kwa amani!
Bakwata haina support ya Waislamu bali inabebwa na mfumo Kristo kupitia Serikali ndio maana Mufti kapewa Mlinzi na anauwezo wa kumtia ndani Muislamu yoyote anapotaka! Sasa unaposhauri Baraza kuu wakae na Bakwata kumaliza tofauti zao sijui watamalizaje wakati kuna tofauti kubwa sana kati yao!
Mwaka 2012 Waislamu wote mpaka na Bakwata walikubaliana kuishinikiza Serikali juu ya Mahakama za Kadhi! baada ya muda mfupi wenzao Bakwata wakaitwa na Waziri Mkuu na kufanya nae kikao na kutangaza kuanzishwa kwa Mahakama za Kadhi zisizotambulika kiKatiba!
Sasa kama Bakwata ndio hiyo, muafaka utapatikana vipi? ndio maana Waislamu wameisusia na kuiacha Bakwata ishirikiane na Serikali na washirika wao!