Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kadogoo,

..sasa kama Waislamu wote ni kitu kimoja, kwanini unazungumza kama mtu anayeona fahari pale shule za Bakwata zinapofanya vibaya??

Mohamed Said,

..kwani wewe lengo lako ni kumnasa Nyerere na udini?

..zaidi, kwanini Waislamu wa Bakwata na Baraza Kuu hamkai pamoja na kumaliza tofauti zenu?
 
Gombesugu, mimi uliposema WML lipumzike kwasababu Mohamed hana majibu mazuri juu yake nililiacha.
Naona unalirudisha kwa mlango wa tuhuma. Siku zote wewe hunikabli kama mimi unazunguka zunguka.
Ndugu yangu sema Nguruvi3 amesema abcd.

Kuhusu sheikh Rukara nimweka wazi kuwa alikuwa anafanya harakati katika misikiti na Mohamed anajua hili ndio maana hataki kabisa kulijadili. Harakati zao ni za kisiasa zikihusisha dini.

Huyu alipewa passport na alikuwa karibu sana na serikali ya wakati huo ambayo ilijua kuwa ni Mrundi, anaendesha siasa misikitini na anaendesha siasa za vikundi vya Warundi.

Kuondoka kwa World Muslim League ni matokeo ya ufisadi mkubwa wa fedha uliofanywa na huyu sheikh.
Utanzania na uwakilishi kama Mtanzania aliupata kutokana na kuwa na mahusiano na viongozi wa juu wa serikali.

Kutokana na hilo yeye aliishi nchini si kama mfanyakazi wa WML bali Mtanzania. Kibali chake cha ukazi kiligeuzwa kuwa cha Uraia katika maingira ambayo hayaeleweki na yenye utata kwa kutumia mfumo ambao si kristo.

WML ni shirika la Kimataifa ambalo liliruhusiwa kufanya kazi hapa kama mashirika mengine.
Mohamed amedai katika maandiko yake kuwa mashirika ya waislam hayaruhusiwi kuwa na uhusiano na Tanzani.

Hili ni mfano mzuri wa uongo, uzushi na jinsi anavyofinyanga akili za watu ambao ni disadvantaged au wamegoma kabisa kutumia akili zao au basi tu wanachuki na Nguruvi kana wewe ndugu yangu.
Mohamed hataki kuzungumzia WML kwasababu anajua uchafu ndani yake.

Hakuna mwenye interest ya kujadili WML kwa kuzingatia kile kilichofanyika ikiwemo matumizi mabaya ya fedha za elimu, afya na misaada zilizotumika kujenga nyumba na si kuwaendeleza waislam.

Lakini basi kama mfumokristo upo na unafanya kazi ilikuwaje mtu huyu ambaye si raia akaachiwa kupata uraia, kukiuka taratibu za uhamiaji na ukazi bila kuchukuliwa hatua? Nguvu gani ilimlinda wakati huo!

Sasa kama unataka tuendelee kumchambua Rukara basi tutaishia kumwita jina la mtaani na si sheikh.
Mohamed anajua hili ndio maana hataki kabisa WML kujadili.

Gombesugu, kama kuna mkristo au yoyote aliyeishi maisha kama Rukara naye ni mhuni tu, hakuna mhuni mzuri au mbaya, mhuni ni mhuni tu.

Tatizo la watu wanaojenga hoja kwa ulinganifu kama wewe huishia kubomoa hoja zao hata kama zinamatiki.
Mfano waislam wanasema wanataka mahakama ya kadhi kama sehemu ya ibada jambo ambalo ni kweli kabisa.

Wanaonyesha mahakama hizo zisivyo na athari kama ilivyo kwa nchi zingine, jambo la kweli.
Wanabomoa hoja wanaposema tupewe pesa kama wakristo! maana yake si kwasababu ya ibada bali ulinganifu wa ''sisi na nyie''. Hoja inakufa kirahisi sana

Baadhi ya waislam wanahoji kwanini waislam wengi wapo magereza kuliko wakristo. Hapa wanaacha kutafuta tatizo na chanzo wanatafuta ulinganifu! kana kwamba kwenda magereza ni selection. Hoja inakufa kirahisi

Wanasema kwanini shule za wakristo zinafaulisha sana, hawajiulizi kwanini za kiislam zinafelisha. Hoja inakufa

Na wewe unasema Rukara '' ana haki'' kwasababu yupo mkristo alifanya abacd. Hoja inakufa.

Jaribu kujenga hoja isimame bila kuegemea mahali.

Sasa turudishe hili la WML kama una hoja zaidi.
 

Wickama,

Pamoja na hayo hebu wasikie Baraza Kuu la Jumuia na Tasisi wanasema nini:

Risala ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Kuhusu Kuunda Tume Huru Kuchunguza Baraza la Mitihani Tanzania

Ndugu Waziri,

Kwa muda mrefu sasa, kumekuwa na maswali mengi wakijiuliza Waislamu, moja likiwa inakuwaje katika maeneo yenye Waislamu wengi ambapo idadi ya wanafunzi Waislamu inakuwazaidi ya asilimia 70, lakini wanapochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya watoto wa Kiislamu huporomoka na kuwa chini ya asilimia 20. Swali na kitendawili hiki kimekuwepo kwa muda mrefu bila kupatiwa majibu. Hata lilipofikishwa Bungeni mwaka 1999 na aliyekuwa Mbunge wa Kigamboni, Mzee Kitwana Selemani Kondo, bado halikupatiwa jibu. Akihoji juu hali hiyo, Mzee Kitwana Kondo alitoa mfano jinsi hali ilivyokuwa katika shule ya Pemba Mnazi iliyokuwa na Waislamu watupu na kwa miaka mingi mfululizo kulikuwa hakuna hata mtoto mmoja aliyekuwa akichaguliwa kwenda sekondari kutoka katika shule hiyo. Aidha alisema kuwa, katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani, takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watoto wa Kiislamu katika shule za msingi ilikuwa zaidi ya asilimia 70 lakini inapokuja kuchaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Waislamu iliporomoka na kuwa chini ya asilimia 20. Akizungumza Bungeni tarehe 2 Februari, 1999 alisema kuwa katika watoto waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka 1998, idadi yaWaislamu ilikuwa asilimia 71 na Wakristo 29%. Hata hivyo akasema, ilipotoka orodha ya waliochaguliwa kwenda sekondari, idadi ya Wakristo ikawa asilimia 79 (79%) na Waislamu 21%.Je, hiyo ilikuwa na maana kuwa watoto wa Kiislamu kwa asili yao hawana akili? Alitaka kujua Mzee Kitwana Kondo. Lakini hakuweza kupatajibu.

Mheshimiwa Waziri,

Ni wazi kuwa Waziri wa Elimu au Waziri Mkuu ambaye ndiye msimamizi wa mambo ya serikali Bungeni asingeweza kutoa majibu ya uhakika kwasababu swali lilihitaji kufanyika uchunguzi huru wa kina na makini kwanza.

Mheshimiwa Waziri,

Mwaka 1987 aliyekuwa Waziri wa Elimu, Profesa Kighoma Ali Malima, aliweka utaratibu mpya wa ufanyaji wa mtihani wa darasa la saba ambapo namba zilitumika toka kufanya mtihani, kusahihisha na kuchagua wanafunzi wa kwenda kidato cha kwanza. Namba zilivishwa majina baada ya taratibu zote hizo kukamilika. Mwaka huo idadi ya watoto wa Kiislamu waliokwenda kidato cha kwanza iliongezeka kwa asilimia 40 ikilinganishwa na miaka ya nyuma. Hata hivyo, mara aliondolewa Waziri Malima katika wizara hiyo na utaratibu wa zamani ukarejeshwa ambapo yalikuwa yakichaguliwa majina naidadi ya Waislamu ikaporomoka na kurudi chini ya asilimia 20.

Mheshimiwa Waziri,

Hali kama hii hapana shaka inazua maswali mengi ambayo yanahitaji majibu na majibu hayo hayawezi kupatikana bila ya kufanyika uchunguzi.

Labda tuongeze mifano ili kuliweka wazi zaidi jambo hili. Mwaka 1983 mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Kopa Abdallah akisoma katika shule ya msingi Kichangani, Kilosa, alikosa kuchaguliwa kwenda sekondari. Yeye binafsi, wazazi wake na hata walimu wake hawakuamini matokeo yale kutokana na alivyokuwa akifanya vizuri kuliko wanafunzi wote. Baadae ilikuja kugundulika kuwa nafasi yake alipewa mwanafunzi aliyekuwa akiitwa Antoni Samirani ambaye alikuwa na uwezo mdogo sana ikilinganiswa na Abdallah. Kilichofanyika ni kuwa jina la Abdallah lilifichwa na baadae Antoni akapewa jina hilo kimya kimya na kwenda kusoma sekondari akitumia jina Abdallah wakati yeye ni Antoni.
Taarifa zinasema kuwa Kopa Abdallah alipogundua hakuweza kufanya kitu akaishia kuwa dereva. Hali kama hiyo ilimkuta pia Adam Ramadhani aliyekuwa akisoma shule ya msingi Rutihinda jijini Dar es Salaam na kumaliza darasa la saba mwaka 1999. Yalipotoka matokeo ya mtihani wa darasa la saba na kuonekana kuwa Adam hakuchaguliwa, baba yake hakuamini kuwa mtoto wake anaweza kufeli kutokana na uwezo aliokuwa nao na zaidi akitizama walivyochaguliwa watoto ambao Adam alikuwa mwalimu wao shuleni na mitaani. Katika kufuatilia suala hilo wizarani, ilikuwa aibu kwa wizara baada ya kuonekana kuwa walichaguliwa watoto wa Kikristo wenye alama za chini kabisa huku akiachwa Adam Ramadhani aliyekuwa na alama za juu kulikowote.

Mheshimiwa Waziri,

Mifano kama hii ni mingi mno na ipo katika ngazi zote kwamaana kutoka elimu ya msingi kwenda sekondari, kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano na kutoka kidato cha sita kwenda Chuo Kikuu. Kwamba hata kutoka kidato cha nne kwenda kidato cha tano, wapo watu waliopata kushuhudia majina yawanafunzi wa Kiislamu yakiwekwa pembeni japo walikuwa na sifa za kuchaguliwa.

Mheshimiwa Waziri,

Ukiacha hujuma katika kuwaacha wanafunzi Waislamu wenye sifa kuendelea na masomo, matatizo huanzia kwenye kuamua nani amefaulu na nani kafeli. Tuhuma zilizopo ni kuwa wapo wanafunzi wanapewa madaraja ya juu wakati alama zao ni za chini na wapo wanaopewa madaraja ya chini wakati alama zao niza juu. Na hii ni kwa masomo yote.

Mheshimiwa Waziri,

Kumekuwa na utamaduni katika nchi hii wa kukataa ukweli.Kufuatia uchunguzi uliofanywa na Kamati za Bunge, tumeshuhudia wizi na ufisadiwa kutisha ukifichuliwa Bungeni hivi karibuni hali iliyopelekea mpaka Mheshimiwa Rais kubadili Baraza lake la Mawaziri. Sasa baada ya kuyasema yote hayo, tunasema kuwa Baraza la Mitihani la Tanzania, limekuwa likilalamikiwa kwa zaidi ya miaka 30, lakini malalamiko hayo yamekuwa yakipokewa kwa sikio la uziwi. Imefikia mahalit unasema kuwa hatuna tena imani na Baraza hilo.

Mheshimiwa Waziri,

Ilikupata ukweli wa malalamikona shutuma hizi, na ili kujibu lile swali juu ya watoto wa Kiislamu ambalo halikupata jibu Bungeni, tunaitaka serikali kufanya yafuatayo.
Tume huru iundwe kuchunguza Baraza la Mitihani la Tanzania na utendaji wake kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita. Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaani na Baraza la Mitihani. Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa Kumpyuta ya Baraza la Mitihani nao wawajibishwe mara moja. Hatua za kisheria na kibinadamu zichukuliwe dhindiya watumishi wa Baraza la Mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii. Muundo wa Baraza la Mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea Baraza la Mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha Makatibu Wakuu Watendaji na Manaibu Katibu Wakuu wamekuwa Wakristona Wenyeviti wa Baraza hilo ni Wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hiileo na takwimu tunazo.

Mheshimiwa Waziri,

Tunaomba ieleweke kuwa tunachotaka ni kupatikana haki na kufanyika uadilifu kwa watu wote. Hatudai wala hatutaki upendeleo kwa Waislamu na wala hatutaki kuona mtu yeyote anaonewaau kuporwa haki yake, awe Mwislamu au mtu wa dini nyingine.Tunachoamini ni kuwa kama Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi haina cha kuficha, basi itaunda Tume hiyo kwaharaka na kuhakikisha kuwa ni Tume ya kuaminika itakayofanya kazi yake kwa umakini, kwa kina na kwa uadilifu wa hali ya juu kabisa. Lakini kama Wizara yako itaonakuwa haiwezi kuunda Tume ya uchunguzi, tunacho kuhakikishia ni kuwa sisi tutafanya kila liwezekanalo na kwa namna yoyote kuhakikisha kuwa Tume hiyo inaundwa. Na ikigundulika kuwa kuna hujuma zinafanyika katika utendaji wa Baraza, basi itabidi uwajibikaji uanze kwenye Wizara kabla ya kuwawajibishawatendaji wa Baraza la Mitihani.Ni imani yetu kuwa utayapokeamadai ya Waislamu na kuyafanyia kazi kwa umakini na kwa haraka ili kujenga mustakbali mwema wa nchi hii na watu wake.

Tunaomba kuwasilisha,

Mwenyekiti
Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisiza Kiislamu
Juni 8, 2012
 

Nguruvi,
Unazungumza na Gombesugu.

Mimi nimeingia kwa kuwa umenitaja.
Nakuambia tena sikupata kufahamiana na Rukara.

Mimi siogopi mtu wala sina la kuficha.
Sikumuogopa Nyerere aliyetetemesha wengi Tanzania hii.

Wewe binafsi ni shahidi.
Hapa JF nimekuwekeeni mengi ambayo yangewahofisha wengi.

Nachukia sana unaponing'ang'aniza jambo ambalo nishakueleza
ukweli wake.

Rukara sikupata kujuananae.

Nakusihi usirudie tena neno hili kwani kwa hakika linaniudhi kupita
kiasi.
 

Joka Kuu,
Anaswe mara ngapi?

Sisi hatushughulishwi na BAKWATA.
Sisi tunahangaika na ustawi wa Waislam.

BAKWATA hawana kitu wana ofisi utadhani
choo cha serikali.
 
Wickama,

Pamoja na hayo hebu wasikie Baraza Kuu la Jumuia na Tasisi wanasema nini:

Risala ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Kuhusu Kuunda Tume Huru Kuchunguza Baraza la Mitihani Tanzania

Heshima Kwako mzee MS, nashukuru kwa majibu mazuri. Ngoja niisome vizuri shukrani
 

Pamoja na majibu yako Mazuri na tishio juu yake,

Naomba kuuliza swali la nyengeza lenye kipengele a na b.

1) Je uliwahi kutambua uwepo nchini wa WML?

Kama jibu ni ndio,

A) Nani alikuwa kiongozi wao mwakilishi?

B) Kitendo cha Shehe Rukara kuwepo nchini kwa shughuli za kiroho kama ulivyodai awali, je hakikukusukuma wewe kumjua ama kujua taarifa zake, ikichagizwa kuwa wewe ni mdadisi wa masuala ya kiroho hasa uislamu?
 

Siku ya leo ni very productive. Tuendelee!!!
 
Wickama,
Usiniambie kuwa unaamini kuwa Ubalozi wa Marekani wanashughulika
na kitabu cha Yericko!

Ubalozi wa Marekani!

Ungesikiaje ungeambiwa ni ubalozi wa Pakistan au Misri, come clean, unataka kusema kitu hapa, what is it?
 
Wickama,

Pamoja na hayo hebu wasikie Baraza Kuu la Jumuia na Tasisi wanasema nini:

Mzee MS, ahsante, nimeisoma. Kwa vile majibu hayawezikuja na sasa hivi, ushauri ni kuwa mwanao kama una hakika anafanya vizuri na unahofu sana yatamkuta hayohayo basi nae atumie Stephen Owen, kama dharura wakati mna-sort ukweli wa chumvi iko wapi.
 
Mzee Mohamed,Baki naye Abdu wako moyoni. Hatukumwona katika mkutano wowote wa hadhara nchi hii akihutuibia kudai UHURU wa Tanganyika. Yeye alishiriki migomo ya kudai maslahi zaidi. Abdu hakuwa na elimu ya kutosha. Abdu alikuwa mtu wa starehe sana. Baada ya kushindwa ule uchaguzi wa KWANZA wa RAIS wa TANU, Abdu alianza kutokomea mbali kwenye siasa za nchi hii hadi kifo chake 1968.Simulizi zako zimejaribu kumnyanyua Abdu bila mafanikio kwani nafasi yake ilizibwa vilivyo na Mwalimu. Ulipombambika UDINI ukawa umemmalizia kabisa!
 

Hapo kwenye blue sio kweli.

Hapo kwenye red kwa maneno yako hayo lazima upate ufadhili Marekani.
 

Ningeshangaa kama ungeona point ya Mwanakijiji kwenye hilo bandiko!!
 

Ahsante sana Kadogoo. It is always a pleasure kukusoma. Huwa nafurahia sana jinsi unavyoweka mawazo yako. Bwana wee, mpe Mwanakiji nafuu, yeye sio serikali.

Ama baada; hebu check historia, huenda Bakwata ndio iliundwa kabla ya hilo baraza lingine (sina uhakika). Kama ni kweli basi upo uwezekana serikali ilishatengeneza mazoea na mazingira ya kufanya nao kazi. Sasa hata ukija na TAASISI ukaiita upendavyo lakini aliyetangulia katangulia.

Pili, HUENDA hata serikali inajua baadhi ya waislamu wanaichukia Bakwata, lakini dawa sio kuikacha na kuhamia kwa washindani wake. Hao jamaa wakitoana mkuku na bakora na kuivunja Taasisi jee? Utahamahama na kubadilisha watu wa kufanya nao kazi hadi lini? Hii inakuwa ngumu zaidi kama kauli za hao mbadala ni hizi tunazosoma humu kwenye threads za JF. Mi naamini sana dhana ya POSITIVE engagements. Lazima unajua kuwa Omar (ra) alimrudia kila mara positively Abubakar (ra) kwa hoja mpaka akakubali compilation ya msahafu. Hakuitisha mapinduzi ya Amir wala kumtusi. Ni juu ya Waislamu kujenga positive attitudes towards their institutions. Huwasikii wakiristo wakivurumishana matusi humu JF wala kwenye redio zao, lakini haina maana hawana tatizo. Wanayo. Lazima Waislamu wenyewe watafute a RESPECTABLE method ya kuwekana sawa. Open media sio chanzo kizuri cha kurebishana kwenye taasisi nyeti kama za dini. Kudai haki ni kitu kimoja, lakini jinsi unavyoidai ni kitu kingine. Kama unaidai katika hali ambayo mdaiwa wako lazima sasa awe dhalili mbele yako na umma basi usitarajie matokeo haraka au kwa ufanisi unaoutaka. Lakini pia sio kwamba kila conflict dawa yake ni taasisi mpya.

CONFLICTS ni sehemu ya uhai wetu. Pia lazima kujua kuwa tofauti za wakiristo wakati mwingine ni za kidhehebu kabisa (yaani doctrine ya kidini) kwa hiyo usishangae wakiomba forum tofauti na serikali. Ndio maana Catholics hawapo CCT ( i hope no error here)sasa i doubt kama Bakwata na hao unaowataja wana tofauti za kidini kiasi cha serikali kuona mantiki ya kukaa nao kama nambari 1`kama wanavyofanya kwa Bakwata.

Hapa nina maana kuwa sitegemei serikali ika-condone vikao na association nyingine (hata imesajiliwa) kuwa na wao ni wawakilishi wa Catholics wakati tayari ina mahusiana ya kikazi na kanisa hilo? Silifahamu vizuri hilo baraza. Lakini kama ni la waislamu wote basi niambie kuwa wamo waislamu wa Shia (aina zote), Ahmadiya, Wahabi, na Sunni wasio wahabi. Kama sio, nakuhakikishia ni mvinyo ule ule wa bakwata. Tofauti ni chupa tuu. By the way usijedhani kuwa wakiristo wao wanaula tu. Kuna dhehebu ambalo lilikuwa na msimamo tofauti sana kuhusu ama blood transfusions au kwenda kutibiwa hospitali kabisa na kama nakumbuka something was done about this. Na sio mara moja. Wenye data zaidi watanisaidia.
 

Barubaru, lets be honest here. Ukidiriki kuchukuwa idadi ya engineers wa kilimo, medical doctors, teachers, university lecturers, hata maustadh na fani yoyote ya wazenj, ukagawa kwa watu millioni moja (pemba na unguja), na ukachukuwa idadi ya professionals haohao huku bara ukagawa kwa watu millioni 43 (bara), bado kwa ratio Zanzibar ni better off.
 
Last edited by a moderator:
Unaijua taasisi ya World muslim League?
Mohamed, si wewe umesema ndiye kiongozi wa waislam!

**hapo nilipo bold, neno hilo halitumiwi na muungwana. Pale kwetu Makorora hilo ni tusi kumwambia mtu mzima.
 
Kipi kilichokusibu siku hizi za karibuni??
Umechuja sana na umekua dhaifu kama nyumba ya BUIBUI..
Mwenzako Gwlihenzi wa mkokoteni yuko wapi??
Naona mnaanza kupotea mmoja baada ya mwingine..
Poleni Sana..
THE BIG SHOW, uwezo wako wa kuelewa na kutafakari mambo ni mdogo mno! wala huwezi kujilinganisha na Mag3, mwenzio ni mlima Kilimanjaro wewe ni kakichuguu tu. Usijali mie nipo huku Nachingwea katika shughuri ya kuwahimiza hawa ndugu zako waache mambo ya unyago na warudi shule kwani kuna shule nne za sekondari zinakaribia kujifunga kwa kukosa wanafunzi! hivyo nipo huku na mkokoteni wangu nikigawa vitabu vya Physics na Basic Mathematics, cha ajabu walimu niliowakuta huku ni ile product ya University ya Morogoro inayoongozwa na mchochezi mwenzenu Hamza Njozi, badala ya kutoa taaluma wao wapo na uchochezi tuuu! ati wanafundisha Islamic Knowledge, wanashangaa kwanini tunapeleka vitabu vya sayansi vingi na kusahau vitabu vya Islamic Knowledge! Nakushukuru hata hivyo kwa kunikumba jamaa yangu!
 
Hapo kwenye blue sio kweli.

Hapo kwenye red kwa maneno yako hayo lazima upate ufadhili Marekani.

Spike,
Yericko hana ujanja wa kuzungumza na Wamarekani.

Kama anataka tuzungumze hayo ya ugaidi na afungue uzi mpya Insha Allah nitakuja
kutoa darsa.

Nakuwekea kitu hapa chini kutoka ''paper'' niliyotoa Chuo Kikuu Cha Ibadan 2006.
Paper hii iliniponza nikatiwa mbaroni uwanja wa ndege 2007 nilipokuwa narudi safari.

Huu ndiyo ulikuwa utangulizi wangu:
‘TERRORISM' IN EAST AFRICA - THETANZANIAN EXPERIENCE

Islam, Terrorism and African Development
Introduction
The current threat of attacks in countries whose governments have close alliances with Washington is the latest stage in a long struggle against the empires of the west, their rapacious crusades and domination. The motivation of those who plant bombs in railway carriages derives directly from this truth. What is different today is that the weak have learned how to attack the strong,and the western crusaders' most recent colonial terrorism exposes "us" to retaliation.

John Pilger – ‘The Unmentionable Source of Terrorism'

In order to understand the Tanzanian political environment and to appreciate and comprehend the impact of ‘terrorism' as defined by the United States, first we need to point out that this phenomenon was and still is a problem which involves the government of the United States and to a limited extent its allies.

The shock of 9/11 forced the United States to not only to include its allies in its war against terrorism but also other governments not forming part of the United States geo-political sphere like Tanzania.

It is in this way that Tanzania and other African countries were included in the war against terrorism.

Secondly, we have to look into the perception of associating Islam as an ideology which nourishes terrorism, the notion which seems to be gaining ground.

Thirdly, we have to qualify the notion of ‘terror.'

What kind of violence qualifies to be considered as an act of ‘terrorism' and therefore deserving condemnation?

At the moment it seems it is only when civilians are targeted for attack that the act assumes the connotations of ‘terror.'

This is in contrast where modern weaponry is used by nation states in annihilation of a people.
Examples of the latter are abound.

The sight of a suicide bomber in television screens is just as familiar as the sight of the Apache helicopters supported by heavy fortified tanks bombing, killing and maiming innocent civilians, be it in Afghanistan, Gaza or Iraq.

Now where do we draw the line between these two scenarios?


Spike,
Wakati nazungumza hayo hayo Wamarekani wenyewe ninao hapo ''cameras rolling...''
Wakaleta taarifa Dar es Salaam wapate habari zaidi za huyu ''terrorists sympathiser.''

Wakanivizia hadi wakanidaka Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere tena natoka Iran kwa
mwaliko wa Serikali ya Iran.

 
Unaijua taasisi ya World muslim League?
Mohamed, si wewe umesema ndiye kiongozi wa waislam!

**hapo nilipo bold, neno hilo halitumiwi na muungwana. Pale kwetu Makorora hilo ni tusi kumwambia mtu mzima.

Nguruvi,
Niwie radhi sikujua kama hilo ni neno baya.

Nisamehe sana ndugu yangu.
Kwetu ni neno la kawaida.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…