Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Hilo ni moja ya tatizo kuu la wachangiaji wengi ktk mnakasha huu.
 

umebanaaaa...sasa umeachia. wewe si ulisema utakuwa msomaji tu wa kufyonza elimu na hautafungamana na upande wowote?
Sasa imekuwaje tena?
 

Barubaru,
Amin.
 

Big Show, well said and Bravo. Now what do we DO?
 

Ha ha haaaa! sasa tumeijua rangi yako. kweli Nguruvi3 ni kiboko yenu. Naona umekuja kuokoa jahazi la mzeee wako MS baada ya kuona
linazama pamoja nawapambe wake wote....haya bwana tusalimie Chama wa Gongolamboto.
 

Mzee wetu ana data za kila kitu kama kipande hapo chini kutoka kwenye paper yake kinavyosema . Tatizo ni lilelile tulilolizoea. Ametumia njia gani kuzipata hizo data!?
 

Mr Barubaru, nashukuru sana kwa mchango wako. Nakukumbusha kuwa uislamu uliutangulia ukiristo katika nchi hizi kwa miaka karibu mia 600 au zaidi. Kama Waislamu wa huko bara ulikoenda hawakuwa na ari ya dini yao usirukie elimu yao, kwanini? wewe kama ulikuwa unaenda msikitini ulikuwa pia una questionnaire ya kujaza kazi na elimu za wanaoswali. Uliendea swala au udadisi wa hadhi ya wanaoswali? Hapa bwana huna point. Kama kuna udhaifu katika jamii za kiislamu kufuatilia dini yao wewe anzia chanzo. Uislamu ulianza 600 years kabla sasa iweje udhaifu huu. Jibu ni kuwa Barubaru uislamu ulienea through wafanya biashara (motive ilikuwa biashara ndugu yangu, uislamu ilikuwa ni by-product) ndio maana ya uislamu kuenea zaidi kwenye trading centres hapa nchini. Nani aliwazuia maustadh wa Pemba/Unguja for 500 years kufika Tarime/Njombe kueneza uislamu? Mbona pembe za ndovu walizifata? Mbona dhahabu ya zimbabwe waliifuata huko huko? Barubaru, usidhani watu wa bara ni wapungufu wa imani. Wala sio kweli kuwa mbora kidini yule mwenye idadi kubwa ya kuingia na kutoka msikitini. Lazima tupate na ushahidi kuwa matendo yako pia yanafuata subira, haki na yana nia njema. Na sidhani kwa kigezo kidogo kama hiki ninachokiona hapa Tanga na huu mwambao wote tokea LAMU hadi Mtwara jinsi mabinti wadogo wanavyoolewa na kutalakiwa kiholela na akina hamsa-salawat wakati mwingine ndio kwanza wametoka kujifungua, eti kuna mtu atajiita Mwuungwana hapa. Kama wewe umezaliwa kwenye familia na jamii yenye chanzo na malezi ya kiislamu mshukuru Mungu na wazazi wako lakini haina maana mwislamu msukuma wa kwimba ni mzembe kutokuwa kama wewe. Kwanza shukuru hajabadili dini!!!!! Wewe laumu maulamaa na maustadh waliopiga mizizi zenj (mara nyingi imejiita kitovu cha uislamu hapa afrika mashariki) na kuendekeza biashara za pembe za ndovu for 600 hundred years bila kujipanga kueneza dini ya kiislamu mpaka wakaja wamishionari na kukuta mteremko huku bara. Hakuna Lawama Barubaru, TOA SOLUTION.
 

Mohamed Said said:
While under JomoKenyatta and Daniel Arap Moi Kenya has experienced torture and executions,
Mohamed Said said:
Uganda experienced mass executions during the reign of Idi Amin Dada. In other words Africans have experienced terror even before the word ‘terror’ became fashionable.



Mohamed Said,

..zingatia hapo kwenye RED.

..hivi unasimama na kauli yako kuhusu Iddi Amin Dada?!

..kuna wa-Tanzania wenzetu wanamlaani Mwalimu Nyerere na kumsomea hitma Iddi Amin.

..je, una ushauri gani kwa ndugu zetu waliochukua uamuzi wa kumuenzi Iddi Amin Dada??

NB:

..Waislamu[at least kwa kuangalia majina] ndiyo waliathirika zaidi na shambulizi lililotokea ubalozi wa US-D'Salaam.

..sasa mimi nashangaa watu kama Mohamed Said wanapopinga sheria ya ugaidi.


cc: Jasusi, Kadogoo, THE BIG SHOW, Nguruvi3, Wickama, Mag3, Barubaru, gombesugu
 
Wanajamvi, naomba niwekane sawa na Mohamed Said, hasa juu ya dhihaka na hamaki yake niliposema kuwa nimeandika kitabu na kinafadhiriwa na ubalozi wa USA nchini,

Ndugu Mohamed, umeonyesha hamaki na dharau ya ajabu sana nilipokujuza kuwa mimi nimeandika kitabu kiitwacho Vita dhidi ya Ugaid,

Hilo naamini na nilitegemea iwe hivyo kwako, limekustua kwakuwa siku zote uliamini wewe ni alfa na omega,

Sasa na kazia kukujuza kuwa kwenye uwanda wa vita vya ugaidi na siasa za amerika kamwe wewe si wa HADHI yangu, nasema hivyo kwakuwa wewe si mbobevu wa siasa za Magharibi, bali siasa zako ni za Mzizima na viunga vyake tu, nje ya hapo ni dini na udini.

Hebu jisomee andiko hilo hapo chini kutoka kwenye kitabu changu kiitwacho "VITA DHIDI YA UGAIDI"



WAAFGHANISTAN 30 WALILIPWA NA CIA
Yote haya yalikuwa yamefanywa wakati wa kipindi cha Cliton, "kitu gain kinakusumbua sana siku hizi? Boren alimwuliza Tenet asubuhi hiyo. "Bin laden," Tenet alijibu akimanisha kiongozi wa ugaidi Osama Bin laden raia wa Saudi Arabian aliyekuwa akiishi ukimbizini Afghanistan ambaye alikuwa ameanzisha mtandao wa Al Qaeda dunia nzima neno ambalo kwa kiarabu linamaanisha " Kituo kikuu". "Oh, Tenet!" Boren alisema kwa muda wa miaka miwili iliyopita alikuwa akisikiliza wasiwasi wa rafiki yake kuhusiana na Bin laden, je, mtu mmoja binafsi angewezaje bila ya kutumia utajiri wa serikali ya kigeni akawa tishio kubwa kama hili? aliuliza, "huwezi kufahamu uwezo na kiwango cha yale wanayoyapanga", Tenet alisema.

Boren alikuwa na wasiwasi kwamba rafiki yake alikuwa ameamua kuwa na chuki za ajabu dhidi ya Bin laden. Karibu miaka miwili hapo nyuma muda mfupi tu kabla ya sherehe za kutimia kwa mwaka 2000 Tenet alikuwa amechukua hatua ambayo haikuwa ya kawaida kwa kumwonya binafsi Boren asisafiri au kutokea kwenye matukio makubwa ya wazi katika mkesha wa mwaka mpya kwa sababu alitegemea kungekuwa na mashambulizi makubwa. hNa siku za karibuni zaidi, Tenet alikuwa na wasi wasi kwamba kungekuwa na mashambulizi wakati wa sherehe za tarehe 4 Julai 2001. japokuwa hakuyafichua hayo kwa Boren, kulikuwa na matukio 34 ya habari zilizonaswa miongoni mwa washirika wa Bin laden zikielezea matamshi kama vile "siku ya kiama ni kesho" au "tukio la ajabu ni kesho" Kulikuwepo na unaswaji mkubwa wa habari kama hizi katika mitandao ya ujasusi na ripoti nyingi zilisema kulikuwa na shambulio kubwa dhidi ya balozi za marekani au dhidi ya makundi ya watalii wa marekani nchi za nje, lakini habari za kijasusi hazikuweza kufahamu ni lini wapi na kwa njia gani. Hapakutokea chochote, lakini Tenet alisema kwamba suala hilo lilikuwa linamfanya akose usingizi. Ghafla mara walinzi wa Tenet walikuja mbio kuelekea mezani alikokuwa.Uh-oh, Boren aliguna moyoni "Bwana Mkurugenzi", mmoja wao alisema "kuna tatizo kubwa". "Ni nini"" Tenet aliuliza akionyesha kwamba kwake ilikuwa ni vyema kumpa mtu uhuru wa kuzungumza bila woga . "mnara wa kituo cha Biashara umeshambuliwa." Mmoja wao alimpa Tenet simu ya mkono na akapiga simu makao makuu. "Kumbe wameigongesha ndege kwenye jengo lenyewe?" Tenet aliuliza akiwa haamini.

Aliamuru watu wake muhimu kukutana katika chumba cha mkutano kwenye makao makuu ya CIA, Akaagiza kuwa angekuwa amefika huko katika kipindi cha dakika 15 hadi 20. "Yote haya siku zote yamekuwa ni Bin Laden," Tenet alimwambia Boren. "Lazima niondoke" pia alifahamu kwamba uwezekano halisi ni kwamba CIA na shirika la upelelezi la Marekani (FBI) havikufanya yote yanayotakiwa ili kuzuia shambulio hilo la kigaidi." "Nashangaa," Tenet alisema, "iwapo hii inahusiana na jamaa huyu ambaye anachukua mafunzo ya kurusha ndege." Alikuwa akizungumza kuhusu Zacarias Moussaoui raia wa Ufaransa mwenye asili ya Morocco ambaye FBI ilikuwa imemtia kizuizini huko Minnesota mwezi uliopita baada yakuonyesha tabia za ajabu wakati akiwa katika shule ya mafunzo ya kurusha ndege.


Tukio hilo la Moussaoui likiwa bado liko katika mawazo yake. Mnamo Agosti, FBI ilikuwa imeomba CIA na wakala wa Usalama wa Taifa kufuatia simu zote ambazo Moussaoui alikuwa amezipata nchi za nje. Mtu huyo alikuwa tayari faili lake limetuna makaratasi ya unene wa inchi tano katika ofisi hiyo ya ujasusi wakati Tenet anaingia katika gari lake kwenda kwenye makao makuu ya CIA ambayo yana eneo la hekta 258 huko Langley Virginia, juhudi zake za kupigana dhidi ya ugaidi wa siku za nyuma zilikuwa zikipishana kichwani mwake. CIA ilikuwa inamwinda Bin laden kwa zaidi ya miaka mitano na juhudi hizo zikazidi baada ya ulipuaji mabomu wa mwaka 1998 wa balozi wa Marekani nchini Kenya na Tanzania ambao ulisimamiwa na Bin laden na kuacha watu zaidi ya 200 wakiwa wamekufa.
Wakati huo, Rais Clinton alielekeza jeshi la Marekani kufyatua makombora 66 katika kambi za magaidi ambako Bin laden anasadikiwa kuwa alikuawa akifanya mkutano muhimu.

Lakini ni wazi alikuwa ameondoka masaa machache kabla ya makombora hayo kufika sehemu hiyo. Mwaka 1999, CIA ilianzisha harakati za siri za kutoa mafunzo kwa makomandoo 60 kutoka katika shirika la ujasusi la Pakistan ili kuingia Afghanistan kumteka Bin laden. Lakini harakati hizo zilikwama kutokana na mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea nchini Pakistan. Njia nyingi zaidi na za hatari zilikuwa zimepangwa katika mfululizo wa mikutano na maofisa wa ngazi za juu wa usalama wa taifa katika utawala wa Clinton.
Moja ya chaguo ambalo lilikuwa limefikiriwa lilikuwa ni shambulio la usiku kutoka kwenye helikopta dhidi ya Bin laden kwa kutumia kikosi kidogo maalum cha Marekani chenye watu wapatao 40, shambulio hilo lingehitaji ndege kupatiwa mafuta zikiwa angani kwani helkopta hizo zingelazimika kusafiri kiasi cha maili 900. Lakini mpango huo ulivurugika kutokanaka na oparesheni "Desert One" ya mwaka 1980 ambayo Rais Carter aliamuru ifanywe ili kuwaokoa mateka wa Marekani waliokuwa wanashikiliwa nchini Iraq ambapo ndege kadhaa zilianguka jangwani na kuangushwa, kama helikopta mbili aina ya "Black hawk" nchini Somalia mwaka 1993 na kusababisha vifo vya Wamarekani 18.

Jeshi lilisema kwamba shambulio dhidi ya Bin Laden lingeweza kushindwa na kusababisha hasara kubwa kwa askari wa Marekani, Habari za kijasusi pia zilionyesha kwamba Bin Laden alikuwa akifuatana na familia yake, na Clinton alikuwa anapinga oparesheni yoyote ambayo ingeweza kuua wanawake na watoto.Kikosi maalum cha Marekani na askari wa jeshi la maji wenye uwezo wa kurusha makombora aina ya ‘cruise' waliwekwa katika tahadhari lakini walihitaji masaa sita hadi kumi kuweza kupata tahadhari ya mahali alipokuwa Bin Laden. Moja ya siri zenye kulindwa zaidi katika CIA ilikuwa ni ile ya mawakala 30 wa kijasusi wa Afghanistan waliokuwa wakiendesha shughuli zao chini ya maneno ya siri GE/SENIORS, ambao walikuwa wamepewa fedha kwaajili ya kufuata nyendo za Bin laden nchini Afghanistan. Katika miaka mitatu iliyopita kundi hilo ambalo lililipwa dola 10,000 kila mwezi liliweza kusafiri pamoja au kugawanyika katika vikundi vidogo vya watu watano.


CIA kila siku ilikuwa na vyombo salama vya mawasiliano "the Seniors" kama walivyokuwa wakiitwa, na walikuwa wamenunuliwa magari na pikipiki lakini kuzifuatia nyendo za Bin laden likawa jambo gumu zaidi kwani aliweza kusafiri bila mpangilio na kila mara akiondoka nyakati za usiku au kuwalamba chenga za visigino akipita milimani.
Kitu cha ajabu ni kwamba seniors hao waliweza kujua wakati wote mahali alipokuwa lakini kamwe hawakuweza kutoa habari thabiti za vitendo yaani kusema kithibiti kwamba angeendelea kukaa mahali hapo kwa muda unaotakiwa ili kuweza kulenga makombora ya ‘cruise' mahali hapo. Na CIA ilishindwa kupata mtu wa kuaminika ili kufanya ujasusi miongomi mwa watu wa Bin laden ambaye angeweza kuwadokeza kuhusu mipango yake. Kulikuwa na watu katika utawala wa Clintoni na vyombo vya usalama wa taifa walikuwa hawana imani na seniors kwa vile kuna wakati kulikuwa na habari za kupingana kuhusiana na mahali alipokuwa Bin laden.

Na nchini Afghanistan watu hususani wenye kuleta habari za kijasusi walikuwa wananunuliwa na kutoa habari kwa watu wengine .Hadi sasa, si Clinton au Bush waliokuwa wametoa madaraka kwa CIA kutuma seniors au mawakala wengine wenye kulipwa kwenda kumuua Bin laden. Amri ya kirais kupiga marufuku mauaji ambayo ilisainiwa kwanza na Rais Gerald Ford , ilikuwa na nguvu ya kisheria.
Katika kipindi kimoja kiongozi wa Seniors wa Afghanistan alikuwa amekutana mara kadhaa na mkuu wa kituo cha CIA kutoka Islamabad, Pakistan, ambaye alikuwa anawapa maelekezo na kuwalipa.

Kiongozi huyo wa seniors alidai kwamba walikuwa wameurushia risasi msafara wa Bin laden katika matukio mawili katika kujihami, jambo ambalo lilikuwa linaruhusiwa lakini alitaka kuufuatilia msafara huo kwa njia nyingine akiwa anapendekeza kuvamia kwa kushitukiza ambapo kitu chochote kilicho karibu kitapigwa risasi, kuua kila mtu na kisha kukimbia.Mkuu wa kituo cha CIA alisema, Hapana hamuwezi kufanya hivyo jambo hilo litavunja sheria za Marekani.
Kwa kutilia maanani fedha iliyokuwepo, vitengo mbali mbali vya siri na mazingira yaliyokuwepo, Tenet aliona kwamba CIA ilikuwa imefanya kila kitu kilichotakiwa kufahamika. Lakini kamwe hakuomba kubadilishwa kwa sheria alikuwa hajamwambia Clinton kuwepo kwa mfumo wa kijasusi ambao ungewaruhusu Seniors kumvamia kwa kumshambulia Bin laden.

Mwanasheria kwenye Wizara ya sheria Ikulu aliamini wangekataa na kusema kwamba hali hiyo ingekuwa imevunja sheria ya kupiga marufuku mauaji ya watu. Tenet aliona amefungamanishwa na msimamo wa Clinton na washauri wake.
Kila kitu kimefungiwa "sheria ya kufa", alikuwa akisema lakini na yeye pia alikuwa amechangia katika hali hiyo katika kipindi chake cha miaka mitano na nusu akiwa kama mkuu wa habari za Ujasusi wa Clinton na Naibu wa idara hiyo. Sheria ilikuwa inasema kwamba CIA ingeweza kumkamata Bin laden na kumfikisha katika vyombo vya sheria. Operesheni kubwa ya kufanya kazi hiyo iliwekwa katika ratiba za njama siri za idara hiyo.


Tenet alikuwa ana amini kwamba Bin laden asingekubali kuchukuliwa akiwa hai, hivyo operesheni kama hii, iwapo ingefanikiwa, ingepelekea katika mauti yake.Lakini wataalam wote wa CIA katika kurugenzi ya Uendeshaji walifikiri isingefanya kazi na kwamba ingesababisha watu wengi kuuawa na si lazima awemo Bin laden. Na Tenet alikubali Mpango huo kamwe haukuendelea zaidi ya hapo. Pendekezo la Saudi Arabia kwamba CIA iweke silaha maalum katika mizigo ya mama wa Bin laden ambaye alikuwa anasafiri kutoka Saudi Arabia kwenda kumwona mwanaye nchini Afghanistan, pia lilikataliwa kwa vile lingekuwa la hatari na kwamba lisingefanikiwa.


by YERICKO NYERERE
 

Pole sana mzee MS kwa hili hata mimi nakupa pole. From Emirates Air to some detention. Dunia Bwana. Wenyewe wanaita Collateral Damage kama ambavyo kombora la Drone likianguakia harusi ya watu. Pole sana. Yaelekea hukuwa na multiple passports ungejiita Milton Duncan .....hahahahahah. Pole bwana. Of course nadhani pole za Kadogoo zilishatangulia. Haya tuendelee na thread
 

Yericko, nadhani kwa kuzingatia kuwa kitabu kinajadili activities za taasisi kama CIA na FBI kwa operations za bin laden, Kwa maoni yangu ni vizuri umewapa draft ili ku-check factual errors ambazo usipofanya hivyo zinaweza kuku-embarrass.

Ama kuhusu chuki na Wamarekani au Umarekani just dont listen. Wewe huyo atakayekuja Kariokoo aue Watanzania 3500 kisha akimbilie Zambia halafu tumwache huru ni nani? wezi tuu wa benki pale Moshi walifuatwa hadi Kenya sembuse umeua watu?
 

Yericko,
Dhihaka ni kweli lakini kuhamaki hapana.
Huna uwezo wa kuandika kitabu kama hicho.
 
Yericko hiko kitabu chako nikikitia mikononi nakitia moto..!
Umeandika nini sasa.?ndio kitabu hiko?
Huna adabu kabisa,liombe radhi jukwaa hili..
 
Yericko Nyerere, hivi hiko kitabu chako kitapata wateja tanzania kweli, mbona kimekaa kama hadithi za sinema za kina Rambo na Jack Chain. Nimesoma huo ukurasa wako naona unazunguka tu na Osama mwanzo mwisho huelezi ugaidi ni nini.
 
Yericko Nyerere, hivi hiko kitabu chako kitapata wateja tanzania kweli, mbona kimekaa kama hadithi za sinema za kina Rambo na Jack Chain. Nimesoma huo ukurasa wako naona unazunguka tu na Osama mwanzo mwisho huelezi ugaidi ni nini.

fyonza ilm kijana...
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Nimejaribu kukufahamu. Nafikiri kulikua na minor misunderstanding. Mimi nilipokuomba uache kusakama na kuuliza "lile suala", nashukuru kuwa ulitumia "ustaarabu" wako na ile issue tulishamaliza. Lakini kama unavyojua "ustaarabu" wa hapa jamvini; ghafla alikurupuka jamaa fulani kujiingiza ati kutaka kujibu/kuchangia tena kwa kashfa. Ndipo ilinilazim "kumnyooshea maneno" huyo jamaa na ikalazim nikutaje maana wewe ndie uliyekua kinara wa "ile issue".

Tatizo lako Nguruvi3,unapotoa maelekezo au kujibu hoja unakuwa-too sensitive na pia too defensive. Labda hizi ni mojawapo ya mbinu zako pale unapojitahidi kuvunja hoja za wenzio!?ahahaha!! Nashangaa pia unadai kuwa nilisema ati Alhaj Rukara ana haki, na pia umeyachukua yale maelekezo yangu yoote out of context na unajuwa wazi hilo!? Tafadhali acha utoto mimi nakuheshimu na nimeshakwambia hilo mara kadhaa! Hatuna haja ya kusababisha distraction hapa jamvini bila sababu za msingi ndugu yangu.

Kwa hiyo nachukua tena fursa hii kukuhakikishia kuwa sina kabisa chuki na wewe binafsi,kama unavyodai kwenye huo ujumbe wako wala yeyote hapa jamvini. Naamini sisi soote ni ndugu,hizi "rabsha chache" zilizomo humu binafsi wala hazinishughulishi.
La muhimu tuendelee na mada kwa kustahamiliana,japo nahisi kwa sasa pana mkanganyiko kiduchu na mada zimekua nyingi mpaka tumefikia kwenye ugaidi!


Ahsanta.
 
Yericko hiko kitabu chako nikikitia mikononi nakitia moto..!
Umeandika nini sasa.?ndio kitabu hiko?
Huna adabu kabisa,liombe radhi jukwaa hili..

duh! Kwahiyo Yericko kuandika kitabu chake ndio hana adabu...

Na wewe toa cha kwako, ngojea nikusaidie title kiwe hivi GAS INATOKA AU HAITOKI?

Baada kumtia mtu moyo nyie mnamkatisha tamaa...
 
Yericko hiko kitabu chako nikikitia mikononi nakitia moto..!
Umeandika nini sasa.?ndio kitabu hiko?
Huna adabu kabisa,liombe radhi jukwaa hili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…