Zipo thread za Mwalimu humu nyingi tu. Hili limejadiliwa sana huko. Ushahidi ni wazi. Ameondoka madarakani tukaanza chokochoko. Sasa hivi tunachinjana kabisa. Siri ilikuwa moja tu. Mwalimu aliapa kuilinda na kuitetea KATIBA ya JMT. Alifanya hivo kweli.
Mwalimu alichukia wizi, rushwa, uporaji wa rasilmali za nchi, udini, ukabila. Mwalimu aliongozwa na sheria za nchi. Pale alipopotoka alikiri hadharani, akarekebisha, akasonga mbele
Hivi mnapata wapi ujasiri wa kusema Nyerere alichukia wizi, rushwa, uporaji wa rasilmali za nchi, udini na ukabila? Utawala wake vitu hivyo vyote vilishamiri na kuota mizizi.
Kuhusu wizi yeye ndiye aliyeasisi wizi hapa Tanzania. Alinyang'anya mali za watu kwa kisingizio cha ujamaa. Huu ulikuwa wizi wa mchana kweupe. Mali alizozinyang'anya akawapatia makada wa chama chake ili waziendeshe. Makada hawa wakaanza kuiba mali ya umma na kufilisi mali karibu zote zilizotaifishwa. Huu ni wizi wa pili aliouasisi ambao sasa hivi tunauita ufisadi.
Kuhusu rushwa kipindi chake ilikuwa ni ya hatari sana. Ulikuwa huwezi kupata huduma hata za msingi kama unga, sabuni, mchele bila kulanguliwa. Ilikuwa ukitaka kununua tuseme gunia la unga lazima upate kibali ambacho huwezi kupata kama huna connection ya kada.
Kuhusu uporaji wa rasilimali za nchi yeye amepora sana rasilimali za Tanzania na kuzisambaza maeneo mengine barani Africa kwa ajili ya crusade yake. Ni vigumu kuweza kukuta kuna vita ilipiganwa wakati ule barani Africa bila yeye kuwa na mkono wake kwa njia moja au nyingine. Vita za Zanzibar, Uganda, Burundi, Rwanda, Nigeria n.k kote huko ana mchango wake na alikuwa anatumia kasma ya kodi za Watanzania kufadhili vita hizo matokeo yake taifa la Tanzania likabaki taifa maskini la kutupwa wakati lilikuwa na kila rasilimali za kuliwezesha kuwa taifa lenye neema. Watanzania wengi wamekufa katika vita hizi zisizokuwa na kichwa wala miguu na matokeo yake mataifa hayohayo yaliyotumia rasilimali zetu kufikia malengo yao leo yanatudharau na yenyewe yamepiga hatua kubwa ya maendeleo ukilinganisha na sisi.
Kuhusu udini hilo nimeshalieleza sana na mpaka sasa hakuna mtu aliyejibu hoja zangu hivyo sina haja ya kurudia kwamba Nyerere alikuwa zaidi ya mdini. Alikuw mmadhehebu kwa kuupendelea Ukatoliki dhidi ya dini zingine na madhehebu mengine ya Kikristo na alifanikisha hali hiyo kwa kutumia kodi za wananchi kuwawezesha Wakatoliki ili wawe na nafasi ya kuwa juu zaidi ya wengine. Kitendo cha yeye kumpigia debe Mkapa Mkatoliki mwenzake na kuwawekea kiwingu Wakristo wengine wakati ule wa Uchaguzi ambapo Mkapa alipita ni dhahiri kwamba huyu jamaa hana hata soni kwenye kuupendelea Ukatoliki waziwazi. Maana kama angekuwa na soni basi angesema angalau awache kipindi kile atawale Mkristo mwingine ambaye siyo Mkatoliki kwani walikuwepo wengi tu wenye uwezo wa kutawala na hasa ukichukulia kwamba yeye kama Mkatoliki amekaa pale Ikulu zaidi ya miongo miwili.
Kuhusu ukabilia huyu jamaa alikubuhu kwa hilo. Neno Erro hapa Tanzania linatumika kuwatambulisha Wanajeshi na polisi kwani alikuwa amewajaza Wakurya kule kila kona. Huu ulikuwa ni ukabila wa waziwazi. Ukabila mngine wa hatari aliouasisi na mpaka leo bado unaisumbua CCM ni ule wa kuyatenga makabila makubwa kama Wahaya, Wachaga, Wasukuma, Wanyakyusa katika nafasi nyeti za uongozi kwenye nchi hii, hasa kwenye ulingo wa siasa kwa sababu ya inferiority complex yake ya kutotaka kukaa na watu waliomzidi ujuzi na maarifa karibu nao ili yeye ndio aonekane kama mjuzi wa kila kitu na wengine wote ni watu wa kujifunza kutoka kwake.
Kusema kwamba mwalimu aliongozwa na sheria za nchi huu ndio mzaha wa mchana kweupe. Yeye alikuwa dicteta wa kuburuta kila kitu. Alikuwa yeye ndiye sheria na sheria ni yeye. Hata kwenye hotuba zake aliwahi kuthibitisha hili pale aliposema kwamba alimtia ndani jamaa mmoja aliyetamba kwamba aliiweka mfukoni serikali yake na alimtia ndani bila kufuata sheria za haki za binaadamu. Kilichomuokoa yule jamaa ni Kanisa Katoliki lilipomuombea kwa Nyerere ili amuachie. Na huu ni uthibitisho mwingine kwamba Kanisa Katoliki lilikuwa linaendesha nchi hii kwa remote control kupitia Nyerere. Mifano ipo mingi hapa ya yeye kutoheshimu utawala wa sheria. Alipiga marufuku mashindano katika ngazi ya Urais na ikawa ama unamchagua yeye au kivuli wakati katiba ya nchi ilikuwa inatoa haki kwa wote kuweza kuchagua au kuchaguliwa. Hii ni dhambi kubwa aliyotutendea Watanzania. Alikua anatishia watu kijinga mno. Kwa mfano aliwahi kusema kwamba mmeniita majina mengi lakini hilo la haambiliki litaondoka na mtu. Kwa maana hiyo alikuwa tayari kuua mtu kwa ajili tu ya kuambiwa haambiliki, jina ambalo alilistahili kwa kila hali. Bado kuna mifano mingi ya Watanzania waliouawa, kuwekwa kizuizini bila kufuata kanuni za sheria n.k