Nyie mbona mmeungana kumshambulia Mohamed Said kutoka na dini yake. Umeishajiuliza kwa nini mmeungana Wakiristo wote na watu wa Musoma kumtetea Nyerere.
Sikujua kama mada ni kumpinga Nyerere na hiyo kwenye "
bold" utakuwa umeongezea kutokana na darasa alilotoa
Wickama kuhusu
EAMWS ila mimi nakuhakikishia wanaopinga uchochezi wa
Mohamed Said, wanatoka dini zote, makabila yote na kanda zote bila kubaguana kwa namna yoyote ile...turudi kwenye mada.
Na mimi naongezea kidogo...mitafaruku baina ya Waislaam, wenyewe kwa wenyewe, ilianza zamani sana. Kubwa ni wakati jumuiya ya
Ismaili Khoja chini ya
Aga Khan wakifungua tawi la
EAMWS Tanganyika mwaka
1945. Ugomvi mkubwa ulianzia hapo wa nani watambulike kama wawakilishi wa Waislaam na hili
Mohamed Said hathubutu kuliongelea, hapana, lita"
dilute" sumu ya ngano zake. Iliyojulikana kama
Al Islamia Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika haikufurahishwa na ujio wa
EAMWS na kusababisha uhasama mkubwa baina ya hizi jumuiya mbili. Huu uhasama uliendelea hadi tunapata uhuru mwaka 1961.
Mwanzoni mwa mwaka
1968, serikali ilitaka sana kushirikiana na
EAMWS na iliiona jumuiya hii kama mwakilishi rasmi wa Waislaam kitaifa wa kuweza kuongea kwa niaba yao. Bahati mbaya baada ya chama cha
AMNUT kuzikwa rasmi miaka michache nyuma, wale wote waliokuwa na malengo ya kuipinga serikali walihamia
EAMWS. Ghafla mgogoro mkubwa ukazuka ndani ya jumuiya hii kati ya Waislaam walioiunga mkono na Waislaam walioipinga
TANU, chama kilichounda serikali
. Ili kuepusha shari na hali ya hatari iliyojitokeza baina ya kundi hizi mbili, serikali kwa ushauri wa viongozi Waislaam iliipiga marufuku
EAMWS.