Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Sikujua kama mada ni kumpinga Nyerere na hiyo kwenye "bold" utakuwa umeongezea kutokana na darasa alilotoa Wickama kuhusu EAMWS ila mimi nakuhakikishia wanaopinga uchochezi wa Mohamed Said, wanatoka dini zote, makabila yote na kanda zote bila kubaguana kwa namna yoyote ile...turudi kwenye mada.

Na mimi naongezea kidogo...mitafaruku baina ya Waislaam, wenyewe kwa wenyewe, ilianza zamani sana. Kubwa ni wakati jumuiya ya Isma'ili Khoja chini ya Aga Khan wakifungua tawi la EAMWS Tanganyika mwaka 1945. Ugomvi mkubwa ulianzia hapo wa nani watambulike kama wawakilishi wa Waislaam na hili Mohamed Said hathubutu kuliongelea, hapana, lita"dilute" sumu ya ngano zake. Iliyojulikana kama Al Islamia Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika haikufurahishwa na ujio wa EAMWS na kusababisha uhasama mkubwa baina ya hizi jumuiya mbili. Huu uhasama uliendelea hadi tunapata uhuru mwaka 1961.

Mwanzoni mwa mwaka 1968, serikali ilitaka sana kushirikiana na EAMWS na iliiona jumuiya hii kama mwakilishi rasmi wa Waislaam kitaifa wa kuweza kuongea kwa niaba yao. Bahati mbaya baada ya chama cha AMNUT kuzikwa rasmi miaka michache nyuma, wale wote waliokuwa na malengo ya kuipinga serikali walihamia EAMWS. Ghafla mgogoro mkubwa ukazuka ndani ya jumuiya hii kati ya Waislaam walioiunga mkono na Waislaam walioipinga TANU, chama kilichounda serikali. Ili kuepusha shari na hali ya hatari iliyojitokeza baina ya kundi hizi mbili, serikali kwa ushauri wa viongozi Waislaam iliipiga marufuku EAMWS.

Tutajie ni nani au yupi aliejitambulisha kwa iman ya uislam kwenye huu mnakasha anaempinga Mohamed Said,na yupi aliejitambulisha kwa imani ya kigalatia pia anaemsapoti na kukubaliana na Moh Said??
Tutajie,kama wewe ni miongoni mwa wale wasemao kweli basi..
Mufilisi...
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: Ami
Zali;Umejitahidi. Ni article nzuri. Sasa kwa vile katika posting yako ya #13365 umeonyesha tayari huyu Nyerere kapigwa laana hadi kufa kwa ukosefu wa kinga mwilini na tena polepole akipumulia mashine kama adhabu toka Mola wake, sasa tuna cha ku-debate tena hapa?

Pumba Pumba Pumba...!
Tulia Zali la Mentali akulambishe dawaa...
 
Last edited by a moderator:
WAnaotaka kuzungumzia uhalali wa Mapinduzi ya Zanzibar walete hoja tuzungumze -anzisheni thread yenu tuwashushie hoja. Haijalishi nani aliongoza yale mapinduzi, yalikuwa halali na ya lazima na ambayo yasingeweza kuepukika. Kwa hapa tunajadili na tumeshaonesha vya kutosha tu kuwa Mohammed Said ni mchonganishi katika jamii ya Watanzania. Mnaotaka kuzungumza juu ya failures za Nyerere (ambazo mnaziona) zipo threads kadhaa hapa kachangieni maana tulishavunja hoja zenu zamani.

Kinachojadiliwa hapa na ambacho kimeweza kuonesha pasipo utata ni kuwa

a. Mohammed Said hajaandka historia; ametumia matukio ya historia kuelezea hisia zake dhidi ya Kanisa, Wakristu na hasa hasa dhidi ya Nyerere

b. Mohammed Said ameingiza dini katika harakati za kupigania Uhuru huku akitukuza na kuinua mchango wa wazee wetu Waislamu dhidi ya mchango wa Watanzania wengine wote.

c. Madai mengi ya Mohammed Said yanatokana na masimulizi amnbayo hayawezi kuthibitishwa; madai hayo hayawezi kusimamia uchunguzi wa kihistoria (historical scrutiny). Ni madai yanayotokana na hisia za mtoto aliyeumizwa baada ya kusimuliwa na wazee wake kuwa wazazi wake walionewa na Nyerere na yeye kaamini kabisa...

d. Maandishi mengi yamejaa hisia za kuchochea chuki baina ya Wakristu na Waislamu huku akijitahidi kuwaaminisha Waislamu kwua wameonewa na kudhulumiwa na ndugu zao Wakristu. Leo wapo vijana na labda wazee (na wengine tunawaona hapa) ambao wanaamini WAislamu wamedhulumiwa na hivyo wanadai "haki" yao.

Hapa ndipo mgogoro ulipo.

Mzee Mwanakijiji,

Hebu angalia kichwa cha habari ya huu uzi "Uchochezi wa Mohamedi Saidi na dhihaka ya Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar."

Sasa wewe hutaki watu wajadili mapinduzi ya Zanzibar, Hakuna anayepiga vitabu vya Judith na Illife kuna vitu vingine hawavifahamu kama haukuwa na hawa wazee unaweza kuamini kila kitu kutoka Judith na Illife bila kupinga kama wewe na Jasusi.

Mfano mdogo wewe unajua kuwa mwaka 1965 Sheikh Takadir alikuwepo sababu umemsoma Judith lakini Mohamed Said anakuambia mwaka 1965 Sheikh Takadir hakuwepo alikuwa ameishafariki wewe kwa akili yako utamuamini nani hapo Mohamed Said au hao wazungu.
 
Last edited by a moderator:
Sikujua kama mada ni kumpinga Nyerere na hiyo kwenye "bold" utakuwa umeongezea kutokana na darasa alilotoa Wickama kuhusu EAMWS ila mimi nakuhakikishia wanaopinga uchochezi wa Mohamed Said, wanatoka dini zote, makabila yote na kanda zote bila kubaguana kwa namna yoyote ile...turudi kwenye mada.

Na mimi naongezea kidogo...mitafaruku baina ya Waislaam, wenyewe kwa wenyewe, ilianza zamani sana. Kubwa ni wakati jumuiya ya Ismaili Khoja chini ya Aga Khan wakifungua tawi la EAMWS Tanganyika mwaka 1945. Ugomvi mkubwa ulianzia hapo wa nani watambulike kama wawakilishi wa Waislaam na hili Mohamed Said hathubutu kuliongelea, hapana, lita"dilute" sumu ya ngano zake. Iliyojulikana kama Al Islamia Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika haikufurahishwa na ujio wa EAMWS na kusababisha uhasama mkubwa baina ya hizi jumuiya mbili. Huu uhasama uliendelea hadi tunapata uhuru mwaka 1961.

Mwanzoni mwa mwaka 1968, serikali ilitaka sana kushirikiana na EAMWS na iliiona jumuiya hii kama mwakilishi rasmi wa Waislaam kitaifa wa kuweza kuongea kwa niaba yao. Bahati mbaya baada ya chama cha AMNUT kuzikwa rasmi miaka michache nyuma, wale wote waliokuwa na malengo ya kuipinga serikali walihamia EAMWS. Ghafla mgogoro mkubwa ukazuka ndani ya jumuiya hii kati ya Waislaam walioiunga mkono na Waislaam walioipinga TANU, chama kilichounda serikali. Ili kuepusha shari na hali ya hatari iliyojitokeza baina ya kundi hizi mbili, serikali kwa ushauri wa viongozi Waislaam iliipiga marufuku EAMWS.

Tuna miezi minne kwenye huu mnakasha ukimtoa Mkandara ambaye anajulikuna jamvini alivyokuwa na mahaba na Nyerere hebu nitajie Muislam yeyote kwenye huu uzi ambaye anakubaliana na "nyie" kama siyo huyo jamaa wa Musoma ambaye anamuona Nyerere ni nabii.

gombesugu, Ami, Zali la Mentali, Kadogoo, THE BIG SHOW,
 
Last edited by a moderator:
Tutajie ni nani au yupi aliejitambulisha kwa iman ya uislam kwenye huu mnakasha anaempinga Mohamed Said,na yupi aliejitambulisha kwa imani ya kigalatia pia anaemsapoti na kukubaliana na Moh Said??
Tutajie,kama wewe ni miongoni mwa wale wasemao kweli basi..
Mufilisi...

kwani Mkandara yeye ni imani ipi? Lakini kwani huwa anakubaliana na hii historia 100%

halafu hivi wagalatia ndio akina nani? Au imani ya kigalatia ndio ipi hiyo?
 
Last edited by a moderator:
kwa hiyo yeyote ambaye hakubaliani na nyie sio Muislamu?
Hivyo ndivyo walivyo Mkuu wa chuo ...kutwa kudai Waislaam wanaoiunga mkono Bakwata si Waislaam, Waislaam wanaoiunga mkono serikali (?) si Waislaam, Waislaam wanaoiunga mkono Chadema si Waislaam, Waislaam wanaopinga ngano za Mohamed Said si Waislaam na Waislaam wanaoshirikiana na Makafir si Waislaam.
 
Last edited by a moderator:
Umeishajiuliza kwa nini nyie Wakiristo wote mnampinga Mohamed Said na kumtetea Nyerere kama mtakatifu wenu.

tunamtetea Nyerere kwenye nini? Kwani Mohamed Said na Nyerere ni nini tunachowalinganisha?

Mpaka ukasema tunamtetea Nyerere? Tumia akili ku reasoning sio ubishi tu.

Mimi kama mimi nipo hapa nasoma, na nawasoma wote.

Pia licha ya hivyo nafanya reasoning pia, simezi mambo mazima mazima
 
Mzee Mwanakijiji,

Hebu angalia kichwa cha habari ya huu uzi "Uchochezi wa Mohamedi Saidi na dhihaka ya Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar."

Sasa wewe hutaki watu wajadili mapinduzi ya Zanzibar, Hakuna anayepiga vitabu vya Judith na Illife kuna vitu vingine hawavifahamu kama haukuwa na hawa wazee unaweza kuamini kila kitu kutoka Judith na Illife bila kupinga kama wewe na Jasusi.

Mfano mdogo wewe unajua kuwa mwaka 1965 Sheikh Takadir alikuwepo sababu umemsoma Judith lakini Mohamed Said anakuambia mwaka 1965 Sheikh Takadir hakuwepo alikuwa ameishafariki wewe kwa akili yako utamuamini nani hapo Mohamed Said au hao wazungu.

Ritz,
Hata sijui hawa ndugu zetu wamepagawa na zohari gani.

Siku zote nawaambia mimi sina tatizo na mtu kuona historia niielezayo hapa ni uongo.
Na mara kadhaa nimewaambia ikiwa mnaona mie muongo hebu leteni nyie huo ukweli.

Hadi leo hamna kitu.
 
tunamtetea Nyerere kwenye nini? Kwani Mohamed Said na Nyerere ni nini tunachowalinganisha?

Mpaka ukasema tunamtetea Nyerere? Tumia akili ku reasoning sio ubishi tu.

Mimi kama mimi nipo hapa nasoma, na nawasoma wote.

Pia licha ya hivyo nafanya reasoning pia, simezi mambo mazima mazima

Wewe endelea kusoma hakuna aliyekukataza.
 
Mohamed,
Hiyo ya mwaka 1965 ni kosa langu. Ni wakati kitabu chake kilichapishwa. Ndiyo maana niliiweka kwenye mabano.

Jasusi,
Hapana tabu.

Nakuongezea kitu.
Judith Listowel alikuja Tanganyika 1962 kuja kufanya utafiti wake.

Aliyempokea ni Ally Sykes kwa kuelekezwa na Peter Colmore.

Nimesoma barua za ''aerogram'' ambazo Listowel alikuwa akimuandikia
Ally Sykes kutoka London katika nyaraka za Sykes.

Hizi zipo pamoja na barua za Chief Thomas Marealle na Rashid Kawawa.
Barua hizi zina mengi.

Jasusi najua ungependa kujua vipi Chief Thomas Marealle alivyokuwa
akimchukulia Nyerere.

Zipo habari za Nyerere katika moja ya barua hizi ambapo Chief Marealle
alimtakidi Ally Sykes kuwa rafiki kipenzi wa Nyerere.

Hii ilikuwa miaka michache kabla ya uhuru.

Katika barua hii alimwambia Ally Sykes kuwa ipo siku tukipata uhuru aitataka
aje azunguze habari zile.

Historia ya TANU ina wachezaji wengi, ina visa vingi vya dhahir na vingine
vilivyojificha.

Mzungu hawezi akavipata na ndiyo maana unaona Iliffe na Listowel wana
mambo hawakuweza kuyajua.

Kuna rafiki yangu hapa anataka kunibeza ati siwezi kujua habari za wazee
wangu hata kama niliishinao.

Ati mimi nimemuiga Iliffe.
Mie nimuige Iliffe...

Ama akutukanae...

Namshauri asome kisa cha Abdulwahid Sykes na Dockworkers Union nilichoandika
mimi kisha asome kisa hicho hicho kama alivyokiandika Iliffe aone tulivyoghitilafiana.

Iliffe kamtoa Abdulwahid katika kisa kile.
Mimi nimemrudisha tena kwa taarifa nyingi sana.

Kile kisomo cha Shamba kwa Mohamed Abeid kapuruzia mie nimeeleza hadi
maana kwa nini Waislam wakati wa harakati dhidi ya ukoloni walikuwa hawafanyi
jambo sharti watawasul.

Isomwe Qur'an kwanza ndipo waingie vitani.

Mimi nimemueleza Hamilton jinsi alivyokuwa ndumila kuwili yeye hilo hakulipata.
Yote haya kanihadithia mzee wangu Islam Barakat aliyekuwa bega kwa bega na
Abdu Sykes katika ''labour movement'' kuanzia 1948 hadi 1950 na kashuhudia
migomo yote.

Wanajamvi kisa hicho nimekiweka chote hapa jamvini.
Kisomeni.

Ninayo mengi.

Si kitu Ritz kanishauri nijaribu kuandika riwaya za mapenzi.
Naufikiria ushauri wake kwa bidii sana.

Naanza kupitia vitabu vya Barbara Cartland kwa kuanzia huenda nikapata
vitu vya kunisaidia.
 
Edward Massengo alipofariki mimi ndiye nilimpa taarifa Ally Sykes. Nilifanya naye interview juu ya maisha yake na Edward Massengo. Peter Colmore miaka miwili kabla alinipa tapes za muziki wa Massengo. Naye nikampigia simu Nairobi nikafanya naye interview juu ya maisha yake na Massengo. Siku ambayo Massengo anazikwa kwao Lubumbashi radio Ngoma Africa FM walitumia interview yangu na kuirudia mara kwa mara. Mtangazaji mmoja baadaye akanipigia simu akasema wanae Massengo wameshangaa nimepata wapi ule muziki wa baba yao. Nina deni la safari Lubumbashi, tuombe uzima.
Kuhusu Marealle ningependa kujua tofauti zake na Nyerere na jinsi TANU ilivyoweza kupenyeza uchagani licha ya kwamba Marealle alipingana na juhudi hizo.
 
Ritz, Hata sijui hawa ndugu zetu wamepagawa na zohari gani.
Aliyepagawa hajifichi...wingi wa post lazima zimuumbue mtu, kula kulala JF!
Siku zote nawaambia mimi sina tatizo na mtu kuona historia niielezayo hapa ni uongo.
Si kweli, una tatizo sana hadi ukaunda eti "shit list". Kuukabili ukweli uso kwa uso kwa silaha ya uongo kunahitaji ujasiri mkubwa!
Na mara kadhaa nimewaambia ikiwa mnaona mie muongo hebu leteni nyie huo ukweli. Hadi leo hamna kitu.
Uongo, chuki na uchochezi kweli hupofusha! Yaani ukweli wote unaotolewa humu huuoni, wewe unapishana nao tu!

Burudika na huu wimbo wa Edward Masengo, "mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichana"
 
Nyie mbona mmeungana kumshambulia Mohamed Said kutoka na dini yake. Umeishajiuliza kwa nini mmeungana Wakiristo wote na watu wa Musoma kumtetea Nyerere.

acha kupotosha umejuaje kama wote ni wa musoma na wakristo. Weka udini leta hoja. Kama huwezi soma kwa faida ya ubongo kama sie.
 
Wickama, katika bandiko lako#13364 umeandika mengi muhimu sana, nakushukuru sana.
Hoja ambayo Mohamed hajaweza kuiongelea ni kuwa endapo EAMWS ilipigwa marufuku huko kwingine ilizuiliwa na nani?

Kuna hoja ya sheikh kupewa wadhaifa na kuukataa, kwa upande wa kumuonyesha Nyerere alivyo mbaya Mohamed anadai wazee wote walitupwa na vyeo kupewa wakristo. Sasa hili lipo wazi na amekaa kimya kwa kutambua kuwa kuligusa kutazua mambo mengine.

Katika mgogoro wa Issilamiya fil Tanganyika washiriki wake ndio wale waliounda AMNUT.
Hoja ambayo Mohamed hajathubutu kuiongelea ni kwanini katika chaguzi AMNUT ilishindwa.

Kuna tatizo moja kubwa sana ambalo wengi hawapendi kulisikia lakini ni vema kulisema.
Leo BAKWATA ikizikwa kabisa bado kutakuwa na migogoro ndani ya chombo kingine.

Hii inatokana na ukweli kuwa waislam wa Tanzania hasa wasomi wa kiislam wameacha mambo yanayowahusu kwa ima wasio na ufahamu au half baked kama tunaoona hapa.
Narudia tena wasomi na watu wenye weledi wamechukua back seat.

Endapo kungekuwa na wasomi walio mbele basi wangeshampiga break Mohamed na wafuasi wake kwa kumwambia aseme na awaambie watu ukweli wa matatizo yao na wala si kueneza usengenyaji, uongo na chuki.
Kwa bahati mbaya wanaogopa pengine kufanya hivyo ni kukufur.

Ujenzi wa hoja wa kundi hili la Mohamed ni wa kiwango cha kusikitisha ndugu Wickama.
Hili wanalomlaumu Nyerere kuhusu Mapinduzi utashangaa kuwa lina sura tatu.
Kundi la kwanza ni hili la Mohamed linalomuandama Nyerere. Kundi la pili ni lile linalosema Mapinduzi daima na kundi la tatu ni la wale wasiokubali kuhusu Nyerere na wasiokubaliana na kundi la pili.
Hoja inajiua hata kabla haijajadiliwa. Pengine utafunguliwa uzi tujadili

Kwahiyo kuna tatizo la kiuongozi na hili linatokana na kukosekana kwa wasomi. Wasomi nina maana watu wenye weledi uwe wa dini au elimu nyingine. Imekuwa proved kuwa Ponda ambaye ni swahiba yake Mohamed hana elimu ya dini wala ya kawaida(dunia). Lakini ndiye yupo katika steering wheel.

Watu wanaonekana kuwa na weledi ndio hawa ambao mstari mmoja unaua hoja nzima. Hapo hamuoni tatizo.
Hawafikiri kwa upana zaidi ya kujifungia na kutunga hadithi! Hao ndio wasengenyaji wakubwa, wenye farki na chuki na ni hao hao wanaoongelea dhulma kana kwamba kuna kadhambi kadogo na dhambi kuubwa!
 
Aliyepagawa hajifichi...wingi wa post lazima zimuumbue mtu, kula kulala JF!
Si kweli, una tatizo sana hadi ukaunda eti "shit list". Kuukabili ukweli uso kwa uso kwa silaha ya uongo kunahitaji ujasiri mkubwa!

Uongo, chuki na uchochezi kweli hupofusha! Yaani ukweli wote unaotolewa humu huuoni, wewe unapishana nao tu!

Burudika na huu wimbo wa Edward Masengo, "mapenzi ni kikohozi hayawezi kufichana"

Wanajamvi,

Kazi na dawa.

All work and no play make Jack a dull boy.
Nimependa hapo kwa Eduardo Massengo.

(Check spelling ya ''Edward'' hivyo ndivyo Masengo alivyokuwa akiandika jina lake)

Hebu tusome kwa furaha habari hii kuhusu Massengo na promoter wake Peter Colmore.
Haya mambo yametokea katika miaka ya 1950 mjini Nairobi:

I sat behind the Mercedes with Peter Colmore.

His chauffer was dressed in khaki suit complete with cap.

He knew quite a lot about me from Ally Sykes.

Ihave never seen such an organized person in my life.

(Among the white people I had known in my life two of them stand out - Peter Colmore and Jim Bailey, the owner of Drum Magazine. These two gentlemen were all introduced to me by Ally Sykes and our friendship endured until when they passed away).

Colmore had catalogued newspaper cuttings, photographs, records in wax, CDs, tapes, films, etc, he wasa walking encyclopedia of the music and entertainment history in East Africa.

I had planned to interview Peter Colmore for three days and my area of interestbeing the 1950s.

Whatever I had wanted to know was in his finger tips, he would give me a cutting or play a tape for me or give me a narration in his upper class English accent.

Colmore could also speak Kiswahili well together with other local vernaculars.

I had all I wanted in less than a day and had lunch together.

I spent the rest of my time with him in his library going through his book collection and listening to very old recordings by Eduardo Massengo andMwenda Jean Bosco.

olmoresigned Eduardo Masengo the gifted guitarist from Elizabethville, Belgian Congo to promote Coca-Cola.

Masengo had come to Nairobi with a group called ‘Je-Co-Ke' meaning, Jean Comedian Katanga.

Colmore who was already inbroadcasting was informed that there was a young man in town who played terrific guitar.

Colmore went to the hotel where Masengo was lodging.

There hefound Masengo in a filthy hotel at River Road.

He was sitting on the floor playing his guitar with people around him listening to his music.

This was the beginning ofthe association between Colmore and Masengo.

Growing up in Dar es Salaam of 1960s I remember very well the famous poster of Masengo in stripped blazer with his guitar and holding a bottle ofCoca-Cola.

There was also the famous photograph of Msafiri Morimori the trombone player.

These photographs were familiar in all newspapers in East Africa.

This had a dual effect to themusicians as well as to the products.

First the sales of the product rose asthe market responded to the idol, and second the music of the artist himself was promoted through his personality being associated with the product.

The artists made money, the industries made profit and more people wereemployed.

The quality of life of the people improved and at the end of the day everybody was happy more so HighFidelity Productions.

Wanajamvi,

Hivi ndivyo tunavyoyaona mambo mimi na ndugu zangu hapa jamvini.

Wao wanapita kijuujuu tu.
Mimi hawa watu waliotengeneza historia nilikuwa naishinao.

Hakika kwa hili namshukuru Allah.
Insha Allah watazamaji ndani ya uwanja watafika 200,000.

Kila siku Insha Allah nitawapa mambo mapya hawajapatapo kusikia.
 
Edward Massengo alipofariki mimi ndiye nilimpa taarifa Ally Sykes. Nilifanya naye interview juu ya maisha yake na Edward Massengo. Peter Colmore miaka miwili kabla alinipa tapes za muziki wa Massengo. Naye nikampigia simu Nairobi nikafanya naye interview juu ya maisha yake na Massengo. Siku ambayo Massengo anazikwa kwao Lubumbashi radio Ngoma Africa FM walitumia interview yangu na kuirudia mara kwa mara. Mtangazaji mmoja baadaye akanipigia simu akasema wanae Massengo wameshangaa nimepata wapi ule muziki wa baba yao. Nina deni la safari Lubumbashi, tuombe uzima.
Kuhusu Marealle ningependa kujua tofauti zake na Nyerere na jinsi TANU ilivyoweza kupenyeza uchagani licha ya kwamba Marealle alipingana na juhudi hizo.

Jasusi,
Hii mambo yako ya kuniwekea mitego mie sipendi.

Nani kakuambia kama Marealle na Nyerere walikuwa hawawivi?
Hahahahahahahah!

Jasusi,
Nitashukuru kama utanipatia hiyo clip ya Masengo interview yako
na muziki wake.

Insha Allah nitakueleza vipi TANU iliingia Uchagani.
 
Hivi mlitaka kumwambia Nyerere nini? Mzee Bomani aliwahi kuniambia kwamba wote wale wanaomwita Nyerere haambiliki ni watu ambao walikuwa na uwoga wa kujenga hoja. Inaonekana na wewe ni mmoja wao. Nyerere alikuwa haburuzwi.
Na kama kutosikiliza kwa Nyerere ndio kumetuletea matatizo mbona miaka karibu 30 tangu aondoke mamlakani mambo Tanzania yamezidi kuwa mabaya? Jiulizeni ninyi mnaoambilika what has gone wrong?

Mpaka sasa hivi tangu nimeingia kwenye mkanasha huu sijajibiwa hoja yangu hata moja. Kutokana na maneno ya Bomani, na ninyi ni watu waoga wa kujenga hoja na wewe ni mmoja wao. Mnafahamu mimi siburuzwi.

Sasa kusema kwamba Nyerere kaondoka tangu miaka 30 hayo unaweza ukaongea na mkeo nyumbani lakini sio kwenye ukumbi huu. Nyerere aliwaweka Mwinyi na Mkapa kwa mabavu na kwa hiyo ali extend utawala wake kupitia kwa hawa marais. Alikuwa akiwakemea na kuwakosoa anavyotaka. Viongozi hawa wa kuchaguliwa na Nyerere hawakuweza kufanya maamuzi yao binafsi bila Nyerere kuwaingilia katika utendaji wao wa kazi. Hivyo Nyerere katawala nchi hii miaka zaidi ya miaka 40. Nchi hii effectively ina awamu mbili tu. Awamu ya kwanza ni ya Nyerere ambayo imegawanyika sehemu tatu ambazo ni Nyerere, Nyerere kupitia Mwinyi na Nyerere kupitia Mkapa. Awamu ya pili ni hii ya Kikwete.

Sasa utumbo alioufanya Nyerere kwa zaidi ya miaka 40 kati ya miaka 50 ya Uhuru mnategemea Kikwete afanye maajabu gani kufunika mashimo yote hayo yaliowachwa katika awamu ya kwanza? Bado mifumo ya kiukandamizaji aliyoiacha Nyerere inamuandama Kikwete katika utawala wake hasa Mfumo Katoliki.

Hivyo hiyo hoja yenu mnayotumia kumtetea Nyerere kwamba mbona kaondoka mda mrefu ilhali mambo bado mabaya tu ni hoja ya kitoto.
 
Nyie Wakirsto mlikuwa mnajidanganya Dr Slaa atakuwa rais. Hata siku moja Tanzania hawezi kutawaliwa na padri.
Hivyo ndivyo udini ulivyochochewa na wanamtandao wa Kikwete kwa kuwatumia akina Mohamed Said, Ritz, Ponda, Illunga... mambo yamekuwa na kuwafanya wadini kuanza kuwachinja wachungaji na mapadri, Kikwete anashangaa!
 
Back
Top Bottom