THE BIG SHOW
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 16,950
- 13,527
Sikujua kama mada ni kumpinga Nyerere na hiyo kwenye "bold" utakuwa umeongezea kutokana na darasa alilotoa Wickama kuhusu EAMWS ila mimi nakuhakikishia wanaopinga uchochezi wa Mohamed Said, wanatoka dini zote, makabila yote na kanda zote bila kubaguana kwa namna yoyote ile...turudi kwenye mada.
Na mimi naongezea kidogo...mitafaruku baina ya Waislaam, wenyewe kwa wenyewe, ilianza zamani sana. Kubwa ni wakati jumuiya ya Isma'ili Khoja chini ya Aga Khan wakifungua tawi la EAMWS Tanganyika mwaka 1945. Ugomvi mkubwa ulianzia hapo wa nani watambulike kama wawakilishi wa Waislaam na hili Mohamed Said hathubutu kuliongelea, hapana, lita"dilute" sumu ya ngano zake. Iliyojulikana kama Al Islamia Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika haikufurahishwa na ujio wa EAMWS na kusababisha uhasama mkubwa baina ya hizi jumuiya mbili. Huu uhasama uliendelea hadi tunapata uhuru mwaka 1961.
Mwanzoni mwa mwaka 1968, serikali ilitaka sana kushirikiana na EAMWS na iliiona jumuiya hii kama mwakilishi rasmi wa Waislaam kitaifa wa kuweza kuongea kwa niaba yao. Bahati mbaya baada ya chama cha AMNUT kuzikwa rasmi miaka michache nyuma, wale wote waliokuwa na malengo ya kuipinga serikali walihamia EAMWS. Ghafla mgogoro mkubwa ukazuka ndani ya jumuiya hii kati ya Waislaam walioiunga mkono na Waislaam walioipinga TANU, chama kilichounda serikali. Ili kuepusha shari na hali ya hatari iliyojitokeza baina ya kundi hizi mbili, serikali kwa ushauri wa viongozi Waislaam iliipiga marufuku EAMWS.
Tutajie ni nani au yupi aliejitambulisha kwa iman ya uislam kwenye huu mnakasha anaempinga Mohamed Said,na yupi aliejitambulisha kwa imani ya kigalatia pia anaemsapoti na kukubaliana na Moh Said??
Tutajie,kama wewe ni miongoni mwa wale wasemao kweli basi..
Mufilisi...
Last edited by a moderator: