Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Sasa wakati unatafakari unamwaga matusi si ndio?

Mwanzoni nilikukasirikia lakini sasa imebidi nicheke! Japo si kicheko cha furaha.
 
Je kenya na Uganda hakukuwa na machifu?

Je unaweza nitajia makabila 20 tu ya kenya na 20 ya Uganda?

Je unaweza niambia Lugha ya taifa (local language)ya kenya na Uganda ni ipi?

Na kwanini lugha ya Taifa ya Tz ni kiswahili?

Majibu yako rahisi sana. Kenya kuna makabila yalikuwa na machifu. Wanandi ni mojawapo ya makabila hayo.. Lakini kwa sababu Kenya ilikuwa ni koloni machifu hawakuwa na mamlaka makubwa kama waliyokuwa nayo machifu wa Tanganyika na Uganda. Uganda uchifu uliwatesa mpaka Obote alipopambana na Kabaka mwaka 1966 na kumlazimisha kabaka kukimbilia Uingereza. Museveni alirudisha uchifu lakini wamebaki kuwa ceremonial heads kwani mamlaka yote yamo kwenye serikali yake. Kwa sababu katika Tanganyika utawala wa Waingereza ulikuwa indirect rule machifu walijikuta wakiwa very powerful. Na kuhusu lugha ya taifa, Uganda ni Kiingereza na Kiganda wakati Kenya walipitisha Kiswahili kuwa lugha ya taifa licha ya upinzani wa akina Charles Njonjo. Hata Museveni alipendekeza Kiswahili kiwe lugha ya taifa lakini kuna upinzani mkubwa kutoka kundi la Baganda. Umesema nikutajie makabila 20 ya Uganda? Haya: Acholi, Alur, Baamba, Babukusu, Bagisu, Bakiga, Banyankole, Banyoro, Banyole, Baruli (hawa wako Musoma pia) Basoga, Bateso, Batoro, Karamoja, Langi, Lugbara, Nubi, Pokot (hawa wako Kenya pia) Banyabindi, Banyaruguru, Banyabutumbi, Barundi. Sijui ni wangapi hao, lakini inakupa picha kuwa kuna makabila 64. Na kwa nini Kiswahili ni lugha ya taifa Tanzania hilo na wewe nina hakika unalo jibu lake. Capice?
 
Wickama,
Nifafanulie sielewi "kubana" umekusudia nini.

Wala sijafahamu mie nitafute kitu kipi.

Uliniambia ulibanwa ndio maana ya kuandika masuala ya mboga na kupishwa chumba JKN, sasa ndio maana nikasema basi nawe jitahidi umbane mtu!!!! Hakuna zaidi ya hapo
 
Mwanzoni nilikukasirikia lakini sasa imebidi nicheke! Japo si kicheko cha furaha.

Quotations zisizohusiana na hoja husika zinalenga kuwapotosha watu. Badala ya kujibu hoja unakimbilia kuunganisha vipande ambavyo havihusiani ili angalau uonekane unachangia kwenye hoja nilizoweka. Hapa hatupo kwenye mchezo wa kuigiza. Ama unajibu hoja au unakaa kimya kama huna ubavu wa kujibu kama wenzako wengi niliowauliza wameamua kukaa kimya. Wewe unapokuja bila hoja humu halafu unaanza kujichekesha unamchekea nani?
 
Hatrage! Hate aginst Nyerere, kila mtu analeta sehemu aliyokwazwa na Nyerere na kupitia hizo chuki wanaungana kuwa kitu kimoja.

Nyani haoni kundule. Nyinyi wote mmeungana pamoja mmesahau tofauti zenu mnamshambulia Mzee Said. Kichwa cha thread hii tu kinaonyesha kwamba angekuwapo Nyerere mngekwisha mmaliza. Mtu anatoa mawazo yake mnaita uchochezi. Acheni hizo chuki zenu zilizojaa na njaa ya kunywa damu za watu wasio na hatia.
 
Hatrage! Hate aginst Nyerere, kila mtu analeta sehemu aliyokwazwa na Nyerere na kupitia hizo chuki wanaungana kuwa kitu kimoja.

Nyie mbona mmeungana kumshambulia Mohamed Said kutoka na dini yake. Umeishajiuliza kwa nini mmeungana Wakiristo wote na watu wa Musoma kumtetea Nyerere.
 
Kwani wewe umegeuka kuwa prefect wa jukwaa hili? Ebo!
 

Short and clear,asante kwa ilm
 

Hivi Barubaru makabila huwa yanapungua na kuongezeka?
Ni lini Kenya ilikuwa na makabila 11? Miye kwa kumbukumbu zangu kwa haraka nawaona: Wajaluo, Walhuya, Wakikuyu, Wagiriama, Wamasai, Wakurya, Wakisii, Wataita, Waturkana, Wamijikenda, Wakamba, Wakalenjin (Jamii ya Wanandi), Wakipsigis, Wameru, Wsamburu, Tharaka, Pokomo, Wadigo, Duruma, Waborana, Waorma na orodha inaendelea.

Na Tanzania tumekuwa na Makabila 120 hata kabla ya Uhuru.

Kama unajenga hoja juu ya Wingi ama uchache wa Makabila ni vyema kufikiri kwanza kabla ya kuandika. Na siku hizi hata
google zinasaidia.
 

Jasusi,
Wewe umepokea kwa Judith Listowel.

Mimi nimekaa na Sheikh Haidar Mwinyimvua.
Sheikh Haidar Mwinyimvua ni mmoja wa wajumbe wa Baraza la Wazee.

Halikadhalika alikuwa rafiki wa Sheikh Suleiman Takadir kisha wote ni
wa TANU Mvita Branch moja ya matawi yaliyokuwa na nguvu Tanganyika
nzima.

Wazungu waijue historia ya TANU kunishinda mie mjukuu wa mashujaa hawa?
Huo ni muhali.

Sheikh Haidar Mwinyimvua ni katika watu wa mwanzo kufahamiana na Nyerere.

Na ndiye alikuwa fundi wake wa kushona suti kwani Sheikh Haidar alikuwa fundi
cherehani mzuri wa wakati wake.

Sheikh Haidar alikuwapo siku ile Sheikh Takadir alipomtuhumu Nyerere kuwa hatowajali
Waislam.

Si Listowel wala Iliffe anaweza kuwajua watu hawa kunishinda.
Mie nimeishi na wazee hawa toka udogo wangu hadi hawa wazee walipoondoka duniani.

Walinipa mengi kuhusu TANU na Nyerere.
Sahihisho kwa Lady Listowel.

Mwaka 1965 Sheikh Takadir alikuwa hayupo duniani.
 
Uliniambia ulibanwa ndio maana ya kuandika masuala ya mboga na kupishwa chumba JKN, sasa ndio maana nikasema basi nawe jitahidi umbane mtu!!!! Hakuna zaidi ya hapo

Wickama,
Ahsante nimefahamu.

Mimi huingia katika mjadala kusoma na ikibidi nisomeshe.

Sheikh wangu kaniusia anasema,"Ingia katika mnakasha usome
au usomeshe. Usiingie kutafuta ubishi kwani ilm ya ubishi haina
baraka."

Mie simo humu kutafuta ushindi.
Nataka nikupeni yale yaliyokuwa mageni kwenu.
 
Mohamed,
Hiyo ya mwaka 1965 ni kosa langu. Ni wakati kitabu chake kilichapishwa. Ndiyo maana niliiweka kwenye mabano.
 
WAnaotaka kuzungumzia uhalali wa Mapinduzi ya Zanzibar walete hoja tuzungumze -anzisheni thread yenu tuwashushie hoja. Haijalishi nani aliongoza yale mapinduzi, yalikuwa halali na ya lazima na ambayo yasingeweza kuepukika. Kwa hapa tunajadili na tumeshaonesha vya kutosha tu kuwa Mohammed Said ni mchonganishi katika jamii ya Watanzania. Mnaotaka kuzungumza juu ya failures za Nyerere (ambazo mnaziona) zipo threads kadhaa hapa kachangieni maana tulishavunja hoja zenu zamani.

Kinachojadiliwa hapa na ambacho kimeweza kuonesha pasipo utata ni kuwa

a. Mohammed Said hajaandka historia; ametumia matukio ya historia kuelezea hisia zake dhidi ya Kanisa, Wakristu na hasa hasa dhidi ya Nyerere

b. Mohammed Said ameingiza dini katika harakati za kupigania Uhuru huku akitukuza na kuinua mchango wa wazee wetu Waislamu dhidi ya mchango wa Watanzania wengine wote.

c. Madai mengi ya Mohammed Said yanatokana na masimulizi amnbayo hayawezi kuthibitishwa; madai hayo hayawezi kusimamia uchunguzi wa kihistoria (historical scrutiny). Ni madai yanayotokana na hisia za mtoto aliyeumizwa baada ya kusimuliwa na wazee wake kuwa wazazi wake walionewa na Nyerere na yeye kaamini kabisa...

d. Maandishi mengi yamejaa hisia za kuchochea chuki baina ya Wakristu na Waislamu huku akijitahidi kuwaaminisha Waislamu kwua wameonewa na kudhulumiwa na ndugu zao Wakristu. Leo wapo vijana na labda wazee (na wengine tunawaona hapa) ambao wanaamini WAislamu wamedhulumiwa na hivyo wanadai "haki" yao.

Hapa ndipo mgogoro ulipo.
 

Ndio maana nimesema huko nyuma Mwalimu wako wa mantiq angekuwa wa kwanza kucharazwa bakora; what kind of reasoning is this? Kwani dagaa akikaa na mamba anajua yote ya mamba? Jiwe likikaa mtoni muda mrefu linageuka samaki? Umekaa na wazee wamekupigisha stori nyingi na wewe umeziamini kuwa ni "kweli tupu" kiasi kwamba kutokana na mapenzi yako kwa hao wazee umeshindwa kuyafanyia upembuzi yakinifu.

Yaani unawabeza LIstowell na Iliffe wakati kitabu chako kwa asilimia kubwa ni marudio ya kazi za kina Iliffe? Kama hatuwezi kuwaamini hawa kuhusu mambo ya Tanganyika wewe unawaamini kwa misingi gani?
 
Nyie mbona mmeungana kumshambulia Mohamed Said kutoka na dini yake. Umeishajiuliza kwa nini mmeungana Wakiristo wote na watu wa Musoma kumtetea Nyerere.
Sikujua kama mada ni kumpinga Nyerere na hiyo kwenye "bold" utakuwa umeongezea kutokana na darasa alilotoa Wickama kuhusu EAMWS ila mimi nakuhakikishia wanaopinga uchochezi wa Mohamed Said, wanatoka dini zote, makabila yote na kanda zote bila kubaguana kwa namna yoyote ile...turudi kwenye mada.

Na mimi naongezea kidogo...mitafaruku baina ya Waislaam, wenyewe kwa wenyewe, ilianza zamani sana. Kubwa ni wakati jumuiya ya Isma’ili Khoja chini ya Aga Khan wakifungua tawi la EAMWS Tanganyika mwaka 1945. Ugomvi mkubwa ulianzia hapo wa nani watambulike kama wawakilishi wa Waislaam na hili Mohamed Said hathubutu kuliongelea, hapana, lita"dilute" sumu ya ngano zake. Iliyojulikana kama Al Islamia Jamiatul lslamiyya fi Tanganyika haikufurahishwa na ujio wa EAMWS na kusababisha uhasama mkubwa baina ya hizi jumuiya mbili. Huu uhasama uliendelea hadi tunapata uhuru mwaka 1961.

Mwanzoni mwa mwaka 1968, serikali ilitaka sana kushirikiana na EAMWS na iliiona jumuiya hii kama mwakilishi rasmi wa Waislaam kitaifa wa kuweza kuongea kwa niaba yao. Bahati mbaya baada ya chama cha AMNUT kuzikwa rasmi miaka michache nyuma, wale wote waliokuwa na malengo ya kuipinga serikali walihamia EAMWS. Ghafla mgogoro mkubwa ukazuka ndani ya jumuiya hii kati ya Waislaam walioiunga mkono na Waislaam walioipinga TANU, chama kilichounda serikali. Ili kuepusha shari na hali ya hatari iliyojitokeza baina ya kundi hizi mbili, serikali kwa ushauri wa viongozi Waislaam iliipiga marufuku EAMWS.
 
Last edited by a moderator:
Je kenya na Uganda hakukuwa na machifu?
Je unaweza nitajia makabila 20 tu ya kenya na 20 ya Uganda?
Je unaweza niambia Lugha ya taifa (local language)ya kenya na Uganda ni ipi?
Na kwanini lugha ya Taifa ya Tz ni kiswahili?
Majibu yako rahisi sana...
Jasusi, una roho ngumu!...yaani unahangaika kujibu hayo maswali ya kipuuzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…