Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Naomba mimi ndugu zangu msinihusishe na hii historia ya ''kaptula.''
Kwa kweli hainipendezi na inanivunjia muruwa wangu.

Nihusisheni na historia ya kudai uhuru hilo ndilo somo ninalojua.
 
Tena kaweka wazi kabisa. Ndio maana nilisema lile bandiko lake la ukurasa fulani hapo nyuma sijui aliliweka kwa makusudi au bahati mbaya.

Limeonyesha hata Nyerere alivyokaa na akina Sykes kutafuta mstakabali wa Tanganyika siyo Waislam.

Nimejibu hii kuwa nimeweka nikiwa hadhir kabisa kwa sababu huo ndiyo
ukweli na mkono wangu ndiyo uloandika maneno hayo.

Narudia kusema kuwa siko hapa kufanya ubishi.

Niko hapa kufahamisha ile historia ambayo wengi hawakuwa wakiijua.

Laiti kama nisingeandika historia hii...
Mengi muhimu yasingefahamika.
 
umeshindwa hoja unaanza kejeli na kashfa.Kinachofurahisha mpaka sasa hamjatoa historia mbadala iliyosahihi.Nyinyi mnapinga yaliyoelezwa na Mohamed Said.Haya basi leteni hiyo historia iliyo sahihi hamna.Mjadala mmeuanzisha wenyewe sasa unawatoa jasho.

Ungekuwa unamsaidia kujibu maswali yaliyomshinda ningekuona wa maana sana zaidi ya hapo hauna jipya unaruka ruka tu hapa
 
Last edited by a moderator:
Niko hapa kufahamisha ile historia ambayo wengi hawakuwa wakiijua.

Laiti kama nisingeandika historia hii...
Mengi muhimu yasingefahamika.

Historia haiwi historia kwa sababu wewe umeita historia. Leo hawezi kuja mtu na kusema vita ya Kagera ilipiganwa kati ya 76 na 77 na akasema ndiyo historia kwa vile kasimuliwa hivyo na wazazi wake walioshiriki vita hiyo. Akija hapa na kusema hivyo watu watahoji 'historia' hiyo. Sasa hawezi kung'ang'ania kuwa "hiyo ndiyo historia na huo ndio ukweli wake kwa sababu wazazi wangu walinisimulia, kubali msikubali habari ndiyo hiyo.

Historia yako ingekuwa kidogo ina nguvu kama ungekuwa unakubali masahihisho na siyo kung'ang'ania kuwa kwa vile umesema ni historia basi isihojiwe.

Maswali yaliyoulizwa kwako ni ya msingi kabisa katika simulizi lako.

Nimekuuliza huko mwanzoni: Ni wapi Nyerere alisema kuwa yeye ndiye aliyeanzisha TANU na kuwa kabla yake hakukuwa na watu wengine - hakuna jibu na likitolewa linasema "soma kile kitabu cha Kivukoni" lakini tukikuambia andika hiyo nukuu kwenye hicho kitabu ili na wale ambao hawajakiona wasome utatuambia "kakitafuteni wenyewe".

Kweli mzee tukubali maneno yako kwa sababu umeyasema tu au tuyakubali kwa sababu yanakubalika hata kama yangesemwa na kichaa kwani ushahidi wake uko dhahiri na unaweza kufikiwa na watu wengine. Haiwezekani ushahidi wa hoja unazotoa utoe kwenye maandishi yako mwenyewe kama ushahidi.
 
Labda tumuulize Bw. Said swali jingine la moja kwa moja: Je Dossa Aziz aliwahi kukutana na Nyerere au kushiriki na Nyerere mkutano wowote wa TAA kabla ya 1953? Wapi na Nyerere alishiriki kama nani?

Vitu vidogo vidogo ambavyo kwa kweli linaua raha ya darsa.
Hiki si kitu kikubwa.

Nimeeleza kuwa Dossa kakutana na Nyerere Dodoma mwaka
1946 katika mkutano wa African Association.

Kwani hili ni jambo muhimu kiasi swali linarudiwa mara kwa mara,
mara kwa mara...

Vitu vizito ninavyokuwekeeni hapa hamuulizi.
Nimeweka nyaraka kati ya Ally Sykes na Kenneth Kaunda 1953.

Kimya.

Nimeeweka hapa mkutano wa Abdu Sykes na Kenyatta, Kungu
Karumba, Bildad Kaggia...1950.
Kimya.

Nimeeleza mambo mengi.
Kimya.

Muhimu ni lini Dossa alikutana na Nyerere.
Nimeeleza Dossa alikuwa tajari sana na alisaidia mno TANU.

Dossa kafa masikini katika hali ya kutisha.
Hakuna maswali nini kilitokea.

Sasa hata kama nia ni kusema kuwa Nyerere akijulikana Dar es Salaam
pale TAA New Street basi ndiyo kweli kwa kujuana na Dossa Dodoma 1946
ndiyo atakuwa maarufu Dar es Salaam nzima?

Mnanistaajabisha sana.
 
Naomba mimi ndugu zangu msinihusishe na hii historia ya ''kaptula.''
Kwa kweli hainipendezi na inanivunjia muruwa wangu.

Nihusisheni na historia ya kudai uhuru hilo ndilo somo ninalojua.
Unakwepa kitu ulichokizungumza wewe mwenyewe? Umesahau uliposema uvaaji wa kaptula halikuwa jambo la ajabu kwa tanganyika?

Umesahau uliposema umeishi Scotland na umeona ni washamba tu?

Yani unakana vitu ulivyovitamka wewe mwenyewe hapa?
 
Naomba mimi ndugu zangu msinihusishe na hii historia ya ''kaptula.''
Kwa kweli hainipendezi na inanivunjia muruwa wangu.

Nihusisheni na historia ya kudai uhuru hilo ndilo somo ninalojua.

Hapana mzee hili ni muhimu; wewe umekusanya historia ya wazee wako wa Dar tangu wakati Nyerere anakuja na tumeona baadhi ya video ambapo baadhi ya watu mbele zakow anasema kwa kejeli kuwa Nyerere alifundishwa kuvaa suruali na wazee hao na wewe hujakanusha. Ama unakubali kuwa ni kweli au hujathubutu kuwauliza wazee wako ili uwasahihishe hawa wanaosema hivi.
 
Hivi na wewe umefatilia huu mnakasha toka mwanzo??aiseee!!!alafu mnalalamika NECTA wanawafelisha!smh
 
Vitu vidogo vidogo ambavyo kwa kweli linaua raha ya darsa.
Hiki si kitu kikubwa.

Nimeeleza kuwa Dossa kakutana na Nyerere Dodoma mwaka
1946 katika mkutano wa African Association.
.

Hii inaenda katika kiini cha simulizi lako. Kama Dossa Aziz alikutana na Mwalimu mwaka 1946 kweli unataka watu waamini Dossa hawakuwa impressed na Nyerere huyu? au Mwapachu anapokutana na Mwalimu wakiwa masomoni habari za Nyerere hazijafika kwa wazee wao Dar?

Hivi umeuliza mzee John Rupia alisikia habari za Nyerere kwa mara ya kwanza wapi?
 
Unakwepa kitu ulichokizungumza wewe mwenyewe? Umesahau uliposema uvaaji wa kaptula halikuwa jambo la ajabu kwa tanganyika?

Umesahau uliposema umeishi Scotland na umeona ni washamba tu?

Yani unakana vitu ulivyovitamka wewe mwenyewe hapa?

Sikutaja kaptula kama tusi.
Soma vyema post yangu.

Yericko una pupa sana.
Jitulize, soma, kisha andika.
 
Hivi hatuwezi kutoka hapa tukasonga mbele katika mambo muhimu
yaliyopitika katika historia ya Tanganyika.

Mbona sipati maswali kuhusu watu muhimu sana lakini hata siku moja
hawakupata kusikika.

Mathalan.

Huyu Idd Faiz Mafongo alikuwa na umuhimu gani kiasi kuwa yeye akabidhiwe
kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO?

Huyu Idd Faiz ndiye alikuwa mweka hazina wa TANU 1954 na hapo hapo mweka
hazina wa Al Jamiatul Islamiyya...

Huyu Idd Faiz alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnatouglo...

Huyu Idd Faiz na nduguye Idd Tosiri ndiyo waliomtambulisha Nyerere kwa Sheikh
Mohamed Ramia wa Bagamoyo ambae alikuwa ndugu yao.

Hawa walikuwa Wamanyema kizazi cha pili kuzaliwa Tanganyika.

Yote haya hamyaoni umuhimu wake.
Nyie ni Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Hamtaki kujua habari za wale waliokuwa pamoja na yeye.

Ajabu sana.
Nini kinakutisheni?
 
Mohamed,
Hakuna mtu anayelazimisha kila kitu kianze na Nyerere. Lakini hata kama kila kitu kilianza na wazee wako wa Gerezani, hiyo ilikuwa ni chapter one tu katika kitabu kizima cha harakati za uhuru wa Tanganyika. Na katika chapta zote, baada ya kumaliza chapter one na wazee wako wa Gerezani, by the time unafika chapter seven, wazee wako watakuwa wameshasahauliwa kwa sababu dynamics za harakati zilikuwa zimeshabadilika na kupanuka Tanganyika nzima, ambako wazee wako wa Gerezani hawakufika, lakini Nyerere alifika. He no doubt was the star of the Tanganyika independence movement. Hiyo haiwezi kubadilishwa. He was chosen by history to play that role and he will forever remain so.
Kuna wakati Mugabe alikuwa analalamika sana kwamba anakuwa sidelined baada ya Mandela kutoka jela. Nilipata bahati ya kuongea na Mwalimu Nyerere juu ya malalamiko ya Mugabe. Mugabe alifikiri kuwa kwa sababu Zimbabwe imepata uhuru kabla ya Afrika kusini, yeye ndiye aliyepaswa kuwa kama prominent leader na amu-overshadow Mandela. Mwalimu alinijibu kuwa "historia ndiyo iliyom-assign Mandela the role of prominence" na hata Mugabe akilalamika kwa kiasi gani hawezi kubadilisha hiyo role ya historia. The same applies to Mwalimu and the wazee wa Gerezani.
 
Utajibu swali mtu lenye tija na maana.
Huwezi kujibu kila kitu.

Huwa vilevile sijibu kejeli na matusi.

Hebu tafakari haya hapo chini:

Hivi hatuwezi kutoka hapa tukasonga mbele katika mambo muhimu
yaliyopitika katika historia ya Tanganyika.

Mbona sipati maswali kuhusu watu muhimu sana lakini hata siku moja
hawakupata kusikika.

Mathalan.

Huyu Idd Faiz Mafongo alikuwa na umuhimu gani kiasi kuwa yeye akabidhiwe
kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO?

Huyu Idd Faiz ndiye alikuwa mweka hazina wa TANU 1954 na hapo hapo mweka
hazina wa Al Jamiatul Islamiyya...

Huyu Idd Faiz alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnatouglo...

Huyu Idd Faiz na nduguye Idd Tosiri ndiyo waliomtambulisha Nyerere kwa Sheikh
Mohamed Ramia wa Bagamoyo ambae alikuwa ndugu yao.

Hawa walikuwa Wamanyema kizazi cha pili kuzaliwa Tanganyika.

Yote haya hamyaoni umuhimu wake.
Nyie ni Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Hamtaki kujua habari za wale waliokuwa pamoja na yeye.

Ajabu sana.
Nini kinakutisheni?
 
Kwakuzingatia hoja yako ya awali kuwa Nyerere aliingizwa katika siasa na Abdu mwaka 1952, na kwakuzingatia kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa hafahamiki na yeyote katika wale wazee wa AA na TAA,
Je mwaka huo 1946 Mwalimu Nyerere alihudhuria mkutano huo wa AA huko Dodoma kama nani na alikuwa akitokea kanda ipi?
 
Hilo ulosema ni kweli lakini si kweli yote.
Hakuwa peke yake katika safari.

Wapi umemsikia Ali Migeyo wa Bukoba akitajwa na yeye alipigana bega kwa bega
hadi 1961 uhuru unapatikana.

Wapi katajwa Mzee Yusuf Ngozi wa Moshi.

Wapi katajwa Hamisi Kheri wa Tanga.

Kuna mengi msiyoyajua ndiyo maana hamshangazwi.
 
Inaelekea hili swali mmelipenda sana.
Soma nyuma nimetoa maelezo.

Hivi hatuwezi kutoka hapa tukasonga mbele katika mambo muhimu

yaliyopitika katika historia ya Tanganyika.

Mbona sipati maswali kuhusu watu muhimu sana lakini hata siku moja
hawakupata kusikika.

Mathalan.

Huyu Idd Faiz Mafongo alikuwa na umuhimu gani kiasi kuwa yeye akabidhiwe
kukusanya fedha za safari ya Nyerere UNO?

Huyu Idd Faiz ndiye alikuwa mweka hazina wa TANU 1954 na hapo hapo mweka
hazina wa Al Jamiatul Islamiyya...

Huyu Idd Faiz alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU pale Arnatouglo...

Huyu Idd Faiz na nduguye Idd Tosiri ndiyo waliomtambulisha Nyerere kwa Sheikh
Mohamed Ramia wa Bagamoyo ambae alikuwa ndugu yao.

Hawa walikuwa Wamanyema kizazi cha pili kuzaliwa Tanganyika.

Yote haya hamyaoni umuhimu wake.
Nyie ni Nyerere, Nyerere, Nyerere...

Hamtaki kujua habari za wale waliokuwa pamoja na yeye.

Ajabu sana.
Nini kinakutisheni?
 
Tatizo lao wao wamemezeshwa nyerere tu hawataki kusikia mtu mwingine ktk harakati za uhuru.
Akili zao zina wigo.Angalia maswali yao na maelezo yao yote ni kuhusu nyerere tu,kana kwamba ndiye 'aliyepigania' uhuru peke yake.
 
Kama watu wanatukana vipi unihusishe mimi?
 
Ndugu yangu Mohamed Said, nakuuliza swali wewe unaweka hadithi za alfu lela ulela?

Ulichojibu mbona hakiendani kabisa na swali nililokuuliza ndugu,

Hivi ukikiri kuwa kunamakosa katika uandishi na uelewa wako nini utapungukiwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…