Wanajamvi, kumbukeni kuwa huu ulikuwa mkutano mkuu wa TAA April 1946. Ni matarajio kuwa mkutano mkuu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka makao makuu. Kama nimeelewa vema mkutano mkuu ulihudhuriwa na Kasella, Dossa na Phombeah. Sasa soma hii tenaKumbe basi Nyerere alishaanza siasa akiwa katibu wa AA Tawi la Tabora. Kwa vile alikuwa katibu wa tawi muhimu namna hiyo vipi baadaye TAA makao makuu wasiwe wamesikia habari zake? Hapa Mohamed anakiri kuwa wanafunzi wa Makerere akiwemo Mwapachu na Nyerere tayari walikuwa katika msisimko wa kisiasa. AnaendeleaKwamba alichofanya Abdu Sykes si kuwaingiza katika siasa ili waanze kama anavyodai Mohamed katika majibu mengine bali kuwashirikisha katika siasa za jiji.Hapa Mohamed anamlenga Nyerere kwa kusema kila aliyetoka bara alifika kwa Abdul Sykes ili kupata ufahamu wa siasa kwanza. Alichosahu ni kuwa Nyerere huyo huyo alikuwa katibu wa AA Tabora(kwa maneno yake) na alianza siasa tangu Makerere (kwa maneno yake Mohamed).
Hakuishia hapo aliendelea kumnanga Nyerere kama hivi Mohamed anasema Ahaa1 kumbe walikuwepo akina John Rupia,Stephen Mhando katika subcommitee, sasa iweje Mohamed atambe kuwa baraza la wazee wa TANU iliyokuja baada ya TAA ilikuwa na Waislam walioleta Uhuru? Halfu hapa tunaona majina zaidi ya yale ya Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi. So far kuna Rupia, Dunstan Omar, Stephen Mhando, Clement Mtamila. Sasa inakuwaje Mohamed aseme wazee wake ni waislam na si wazee wote? Mohamed is on offensive against Nyerere, soma hii Hapo Mohamed ametumbukiza ukatoliki wa Nyerere kwanza, kisha kumwekea maneno kwa kutumia neno ''inasemekana''. Mohamed hakuwahi kumhoji Nyerere lakini alifahamu vema kuwa alikuwa mnyenyekevu wa kanisa na Serikali ili kulinda kibarua chake. Ni Mohamed huyo huyo alitueleza kuwa akiwa Makerere na Tabora Nyerere tayari alikuwa katika siasa, kwanini basi aanze kuhofia kibarua, serikali na Kanisa alipofika Dar? Maana yake ni kutaka kumshusha katika watu waliopigania uhuru kama anavyosema hapa Halafu akaendelea na chuki dhidi ya Nyerere na dini yake Hapa Mohamed anasahau kuwa Dr Vedastus Kyaruzi aliwahi kuwa kiongozi wa TAA licha ya Ukristo wake. Amewasahau akina John Rupia, Stephen Mhando na Clement Mtamila kuwa kwa Nayakati fulani walikuwa viongozi katika mji ule ule ambao Nyerere asingeweza kuwa kiongozi kwa ukristo wake.
Fikiria wakati unasoma, ukimeza bila kutafuna utajikuta umemeza ''Ngano'' kama si Mashudu.