Labda tumuulize Bw. Said swali jingine la moja kwa moja: Je Dossa Aziz aliwahi kukutana na Nyerere au kushiriki na Nyerere mkutano wowote wa TAA kabla ya 1953? Wapi na Nyerere alishiriki kama nani?
Vitu vidogo vidogo ambavyo kwa kweli linaua raha ya darsa.
Hiki si kitu kikubwa.
Nimeeleza kuwa Dossa kakutana na Nyerere Dodoma mwaka
1946 katika mkutano wa African Association.
Kwani hili ni jambo muhimu kiasi swali linarudiwa mara kwa mara,
mara kwa mara...
Vitu vizito ninavyokuwekeeni hapa hamuulizi.
Nimeweka nyaraka kati ya Ally Sykes na Kenneth Kaunda 1953.
Kimya.
Nimeeweka hapa mkutano wa Abdu Sykes na Kenyatta, Kungu
Karumba, Bildad Kaggia...1950.
Kimya.
Nimeeleza mambo mengi.
Kimya.
Muhimu ni lini Dossa alikutana na Nyerere.
Nimeeleza Dossa alikuwa tajari sana na alisaidia mno TANU.
Dossa kafa masikini katika hali ya kutisha.
Hakuna maswali nini kilitokea.
Sasa hata kama nia ni kusema kuwa Nyerere akijulikana Dar es Salaam
pale TAA New Street basi ndiyo kweli kwa kujuana na Dossa Dodoma 1946
ndiyo atakuwa maarufu Dar es Salaam nzima?
Mnanistaajabisha sana.