Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Swali zuri sana mzee MS hakuna mhariri anayeweza kumpa huyu mtu ukurasa labda TANZANIA DAIMA!
Boko Haram,
Kwanini Tanzania Daima lina sifa gani inayomwenea Jericko?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali zuri sana mzee MS hakuna mhariri anayeweza kumpa huyu mtu ukurasa labda TANZANIA DAIMA!
Yericko,
Kweli tuwekana sawa.
Wewe hivyo ndivyo ujuavyo na mimi nimeeleza niyajuayo.
Sote tuna haki ya kueleza historia hii na kusikilizwa.
Hakuna wa kumnyanyasa mwenzake wala kumbughudhi.
Kuna wasikilizaji sasa 175, 000 + wanatusoma.
Hawa ndiyo waamuzi wetu.
Tuwaachie wasome historia hizi mbili za uhuru wa Tanganyika.

Mkuu, hii sio kweli, waingereza kwa miaka mingi walichinjana kule Irend kwa jina la kiristo!
Sijajihusha na magazeti ya kitaifa,
Nimehadhiri katika luninga za kitaifa na kimataifa,
Nimealikwa maadhimisho ya kumbukumbu za mashambulio ya september 11, 2001 pale Pentagon!
Nimezungumza na mabingwa wa vita vya ghuba na wabobevu wa ujasusi wa kimataifa!
Anga nilizokanyaga yaweza kuwa ni mswahili pekee kuzifikia japo sina uhakika kama yupo na mwingine aliyewahi kupita nyayo hizo!
Kimsingi Mohamed Said, ugaidi huu unaopiganwa chini ya mkono wa USA wewe huuwezi na huufahamu!
Kualikwa Ibadan wala haina impact hasa kama wanaokualika ni wale wakufanana na wewe kimlengo!
Radical Muslims wote duniani wanafanana!
Yericko we ni kiboko! umealikwa Pentagon! tufanyie hisani utuwekee na picha basi ulizopiga Pentagon!
Kwamara ya sita tangu tuanze mjadala huu unaomba tena picha za tukio hilo!
Swali moja kwako,
Je uliwahi kuomba picha zangu nje ya hilo?
Zitakusaidia nini wewe ukiziona?
Ili niamini kweli ulialikwa Pentagon! hilo ni ombi tu una haki ya kukataa kutuwekea picha hakuna ugomvi mkuu!
Boko Haram,
Kwanini Tanzania Daima lina sifa gani inayomwenea Jericko?
Mzee MS huyu mtu ni mjanja sana nafikiri wewe unatembelea huu uzi tu laitiungekuwa unapitia uzi zote huku jf ungemjua huyu jamaa ni nani, hawa ni mapro wa hiko kikundi kinacho toa hilo gazeti ni jamaa zake nje ya hapo hana ubavu. Kaombwa picha za ushaidi kuhusu alivyo kuwa anaongea na hao watu kuhusu ugaidi povu linamtoka eti picha zitakusaidia nini wala hizo picha hana mjanja mjanja tu na akiziweka naritadi sasa hivi!
Mzee MS huyu mtu ni mjanja sana nafikiri wewe unatembelea huu uzi tu laitiungekuwa unapitia uzi zote huku jf ungemjua huyu jamaa ni nani, hawa ni mapro wa hiko kikundi kinacho toa hilo gazeti ni jamaa zake nje ya hapo hana ubavu. Kaombwa picha za ushaidi kuhusu alivyo kuwa anaongea na hao watu kuhusu ugaidi povu linamtoka eti picha zitakusaidia nini wala hizo picha hana mjanja mjanja tu na akiziweka naritadi sasa hivi!
Vema sana ndugu,
Lakini kuna hoja hapo nimeziweka kutokana na madai ya wewe kuwa ni safari ya pili ndio kanisa lilisaidia,
Zifanyie hisani kwakuzijibu mzee wangu!
Haka katabia kakulialia kanawafanya wapumbavu wachache tu ndani ya uislama mudharirishe uislamu!
Hivi ukiulizwa kuwa serikali ikitaka kuzungumza na wakristu hutumia chombo kipi kati ya ulivyovitaja hapo juu?
Je vyombo hivyo ili viwe hai vimesajiliwa na serikali kama unavyolia kuwa na nyinyi mruhusiwe kuwa na vyombo vyenu tena visajiliwe na serikali?
Watanzania tanaangamia kwakukosa maarifa!
Huu upuuzi ulioandika ndiyo umepewa mualiko Marekani...Ha haa haa haa.Mohamed Said
Wewe juu ya anga za ugaidi kwakweli hujui kitu,
Kuwa muungwana jitulize na uombe kufundishwa, usijifanye kila kitu wakijua wewe, ona sasa unaumbuka bila sababu za msingi!
Hebu kata kiu hapa chini!
VITA DHIDI YA UGAIDI
Marekani iko katika Bara la America ya kaskazini, iko katika longtudo 120% Mashariki, na Latitudo 40% Kaskazini. Ilipata uhuru mwaka 1789 kutoka kwa Waingereza, Rais wake wa kwanza alitwa George Washington Upande wa kaskazini imepakana na Canada, Mashariki inapakana na Bahari ya Atlantic, Kusini inapakana na Mexico na Magharibi inapakana na bahari ya Pasifiki. Marekani ni moja kati ya nchi zilizo mstari wambele katika kupinga utengenezaji wa silaha za maangamizi. Ni moja kati ya mataifa tajiri duniani na ni moja kati ya mataifa makubwa duniani. Kiungo kikubwa cha serikari kimeegemea katika ubepari,na nimoja kati ya nchi zilizo mstari wa mbele katika kutetea haki za binadamu kinadharia.
Kwa mtazamo wa karibu utaona kuwa Marekani imekuwa ikipata ubavu wa kiuchumi, kisiasa na kijeshi kwa kupitia mwavuli wa umoja wa Mataifa ambao makao makuu yake ni Marekani, Pia unaweza kupata maswali mengi yasiyo na majibu "mfano au kwa kuwa mkubwa duniani ni mmoja baada ya muungano wa kisovieti kuvunjika? Au Tamaa ya malighafi katika nchi husika?, au kutaka kujaribu silaha zao?
Kuwait itaikumbuka Marekani kwa msaada ilioutoa mwaka 1991 – 1992 wakati nchi hiyo ilipovamiwa na Iraq. Katika suala la kutetea haki za binadamu, Marekanai imekuwa kikwazo kwa mataifa ya mashariki ya kati (ya kiarabu) ambayayo yanatajwa kuwa yanaukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Historia inaonyesha kuwa Marekani imepigana vita kati ya Cuba, Cosovo, Vietnam, Pama, na Iraq. Na inaonyesha kuwa baadhi ya vita hivyo Marekani imekuwa ikiingilia kati tena bila idhini ya Umoja wa Mataifa. Suala linabaki palepale kuwa Marekani kama taifa tajiri na kubwa duniani, haina budi kuingilia kati panapotokea mgogoro katika nchi, uwe wa kisiasa au kiuchumi.
Tulishuhudia wale waliokuwa wanapinga vita vya Afganistan na Iraq wakiomba Marekani itume askari wake kutuliza vita vya wenyewe kwa wenyewe kule Liberia chini ya utawala wa Charles Teyller, na hao hao tena wakishinikiza USA isimamie mpango wa amani (Road map) Mashariki ya kati. Kama kweli walikuwa wanapinga vita basi tungeshuhudia kambi za kijeshi katika baadhi ya nchi zilizopinga vita zikiondolewa pamoja na balozi za USA zikifungwa, lakini katika hali ya kushangaza watu walipinga vita kinadharia. Ifahamike kuwa mkubwa ni jalala, haohao waliopinga vita wangekuja kuishutumu USA kuwa kama taifa kubwa duniani kwa nini ilishindwa kuingilia kati migogoro ya nchi ndogo na maskini duniani?
Mwaka 1994 dunia ilishuhudia mauaji ya halaiki ya kimbali ya Rwanda, na Marekani ilikuwepo katika sayari hii, lakini katika hali ya kustaajabisha Marekani haikutia mguu katika ardhi ya akina Byerihimana kuzuia mauaji hayo. Wachambuzi wa siasa za ndani na nje za Marekani wanasema Marekani huendesha siasa zake za nje kwa faida zaidi, tofauti na wanavyojinadi kwa umma wa dunia.
Mwandishi mwenye mlengo wa kushoto na siasa za Marekani bwana Thomas Schelling katika kitabu chake cha (Siasa za nje za Marekani) anamnukuu Naibu Waziri wa Ulinzi Paul Wolfowitz ambaye mwaka 2007 alikumbwa na kashfa ya kumzawadia mpenzi wake vyeo na mshahara uliovunja rekodi yamishahara katika Benki ya Dunia akiwa Rais wa Benki hiyo, katika vikao vya faragha vya kumun'goa Saddam, "Nivema tukazingatia kila tulifanyalo liwe na faida kwa kizazi kijacho, historia isije kutusuta tukiwa kama Amerika."
Inawezekana walichanganua nakuona hakuna faida kwa kizazi chao cha baadaye ndio maana walishindwa kwenda kuzuia mauaji Rwanda, wakati mwaka 1991-92 walikuwa Kuwait nchi inayomwaga mafuta kwa wingi duniani wakiipiga tafu kukabiliana na mkono wa chuma (Saddam Hussein) nchi hizo ni wazalishaji nguli wa mafuta ndio maana Marekani iliyaona matatizo hayo yaliyo kwenye mwanga vizuri kuliko Rwanda kwenye giza lililo zingirwa na umasikini wenye asili ya kiafrika. Baadhi ya viongozi waliopata kuwa madikteta ni kama Benito Mussolin (Italy) 1922-1943, Francico Franco (Hispania) 1939-1975, Chanceller Otto Von Bismak (Ugerumani) 1862 – 1890, akapindulia na mbabe kijana Williami wa pili, akaja Chanceller Adolf Hiltler. Huyu ndiye dikteta anayetajwa kuwa na sifa mbaya zaidi duniani aliyetaka kuutawala ulimwengu na kusababisha vita kuu ya pili ya dunia.
Hata hivyo alikuja kubanwa mbavu na majeshi ya Urusi na kuamua kujiua pamoja na mke wake Bi Eva Brown mwaka 1945 mjini Bellin.Jen B.Bokasa wa Jamuhuri ya Afrika ya kati, Mobutu Seseseko wa Zaire ya zamani, Anua al –Saadat wa Misri, Yasser Arrafat wa Palestina, Rais wa zamani wa Peru Alberto Fujimori, Saadam Hussein na Idd Amini wa Uganda aliyeonywa na Mwalimu Julias Nyerere kuto uleta utemi Tanzania kwakupewa uhamisho wa kwenda kuishi Umangani na kutuacha wenye hekima tuendele kupeta.
Kutoka katika hatua ya kupinga udikteta, Marekani imeingia katika suala la ugaidi. Kwa upande wa magaidi wamekuwepo wengi sana, na kinara wao mkuu awali alikuwa Irich Ramizez Sanchez ‘Carlos' raia wa Venezuela aliyeutingisha ulimwengu kiasi cha waandishi kutoa vitabu vingi kuelezea kashikashi zake na kuonekana kana kwamba zilikuwa ni hadithi za kufikirika hadi alipokamatwa nchini Sudani 1994, Jonas Savimbi aliyeongoza mapigano ya muda mrefu nchini Angola baada ya uhuru hadi alipouawa mwaka 2002 na majeshi ya serikali kufuatia mapigano makali, Joseph Konny kiongozi wa waasi kaskazini mwa Uganda anayetaka kuitawala Uganda kwa amri kumi za mungu.
Akaja gaidi mwingine ambaye ni hatari zaidi kuliko waliomtangulia, Osama Bin Laden, ambeye siyo tu wababe walishindwa kumtia mbaroni bali kwa mara nyingine aliuthibitishia ulimwengu kwamba nguvu bila kutumia akili siyo ujanja akiwa mafichoni katikati ya nchi ya Afghanishan. Osama bin Laden gaidi mkuu, ndiye aliye ipeleka Marekani katika vita nchini Afghanistan pamoja na vita vya Iraq ambavyo Marekani ilisema ni vita vya ukombozi na wengi wakadai ni vita vya uvamizi. Hiyo yote inatokana na mashambulio ya kigaidi ya Sept,11/2001 Washington na New York nchini Marekani
Katika vita vya Ugaidi nchini Afghanstan, Marekani ilifanikiwa kuung'oa utawala wa Taleban bila kumpata mlengwa (Osama ben Laden) na kilichoifanya Iraq kuvamiwa na Marekani ni madai ya USA kuwa Iraq inamiliki silaha za maangamizi ambapo timu ya wakaguzi wa silaha za maangamizi ikiongozwa na Hans Blax mkaguzi mkuu wa silaha za nyukilia na Ell Barlldei mkaguzi mkuu wa silaha za kibaolojia walipelekwa nchini Iraq na kabla ripoti ya mwisho haijatolewa Marekani ikaanzisha vita vya kumng'oa madarakani kiongozi wa nchi ya Iraq Saddam Hussein. Kiongozi huyu ambaye aliitawala nchi ya Iraq kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1979 mpaka Machi 2003 anazungumuziwa kama ni dikteta, gaidi na haini mkubwa ambaye Marekani ilidiriki kusema Hitller wapili.
Saddam Hussein alizaliwa mwaka 1937. Katika historia ya maisha ya awali ya Saddam, kulingana na taarifa ya kitengo kimoja cha masuala ya akili cha Marekani inasema, kutungwa kwa mimba pamoja na kuzaliwa kwake kulitokea baada ya kufariki kwa kaka yake aliyeitwa Sanakher Hussein aliyekuwa na umri wa miaka 12 kutokana na maradhi ya saratani. Baba yake alifariki wakati mama yake akiwa na ujauzito na mama huyo alichanganyikiwa akawa anapewa ushauri nasaha hasa baada ya kutaka kuitoa mimba ya Saddam. Baada ya kujifungua alikataa kabisa hata kumtazama mtoto wake. Akakua na kulelewa na mjomba wake mjini Tikrit
Na Yericko Nyerere
Kutoka "Vita dhidi ya Ugaidi"
Huu upuuzi ulioandika ndiyo umepewa mualiko Marekani...Ha haa haa haa.
gombesugu, Zali la Mentali, THE BIG SHOW, Kadogoo,
Yericko,
Ikiwa wewe ueniona mimi sijui kitu katika ugaidi lakini ukweli utabakia
kuwa mimi nilialokwa Chuo Kikuu Cha Ibadan na nikatoa mada kuhusu
ugaidi.
Hayo unayoandika wewe ni manyumbulisho kutoka vyanzo vingi.
Kitabu hakiandikwi hivyo.
labda nikuulize umapata kuandika chcochote kikachapwa katika majarida
au magazeti?
Young Boy anasikitisha sana,,,
Basi tumwache ajifurahishe...
Huu upuuzi ulioandika ndiyo umepewa mualiko Marekani...Ha haa haa haa.
gombesugu, Zali la Mentali, THE BIG SHOW, Kadogoo,
The Big Show,
Katika ujana wangu kulikuwa na kundi moja la muziki likkitwa Earth, Wind and Fire.
Hawa jamaa walikuwa na nyimbo yao moja nikiipenda ikkitwa ''Illusions.''
Huu upuuzi ulioandika ndiyo umepewa mualiko Marekani...Ha haa haa haa.
gombesugu, Zali la Mentali, THE BIG SHOW, Kadogoo,
Nikweli huo ndio upuuzi ulionifikisha katika ground zero!
Ndio huo ulinikutanisha uso kwa uso na Bob Beqeen
Huo ndio ulionifikisha mezani pamataifa!
Wasomi hukaa kwenye mantiki sio kwenye herufi!
Uzuri nikuwa umeelewa mantiki