Nguruvi3,Sasa suala langu ambalo nilikuuliza Waislam wa Tz bara wamewekewa Bakwata ikague na kuithinisha misaada yao kama ulivyo eleza. Suala langu nilikuuliza JE WAKRISTU ni nani anayethibiti misaada yao kutoka nje?
Si sahihi misahama hiyo kudhibitiwa na BAKWATA.Hilo ni jukumu la serikali husika. Ninachoelewa ni kuwa misaada hiyo lazima ipitie taasisi zinazojulikana na zilizosajiliwa na kama BAKWATA ndiyo inayojulikana, hilo si tatizo la serikali ni tatizo la waislam kwasababu wale BAKWATA ni waislam unless usimame hapa na kusema siyo.
Misamaha ya kodi inatumiwa vibaya na watu wa dini, narudia dini zote isipokuwa wapagani na wasioamini.
Nakaumbuka kama si Rais JK ni Mkapa aliwahi kuonyesha misaada hiyo inavyokuwa misused na taasisi.
Kwamba magari yanaingia kama ya taasisi za dini kumbe ni ya watu binafsi.
Siku zote huwa nasema misamaha ya kodi lazima iwe na udhibiti wa hali ya juu sana ili kuzuia kufujwa na baadhi ya watu. Nimekonyesha kuwa misamaha inayotolewa lets say kwa BAKWATA hutumika kwa waislam kwahiyo hakuna sababu ya kusema hilo ni jambo la uonevu.
Ndivyo ilivyo kwa imani zingine na ndio sababu nasema misamaha ni ukwepaji kodi isipokuwa ile inayodhibitiwa kikamilifu.
Umeongelea kwanini kuwe na udhibiti. Kuna jambo unalosahau hapa. Kauli na matendo ya watu vinatosha sana kuwa na shuku juu ya misaada. Nimekuuliza hivi ukisikia Maliki ametoa dollar milioni 1 kwa ajili ya maendeleo kupitia wanafunzi wake utakuwa na imani kweli. Wanafunzi hao ndio wanasema ''tafuta mtu fulani ua kwa siri'', ndio hao wanakuwa wazushi kila alfajiri hadi isha wakienda hadi China si kuitafuta elimu bali kueneza chuki na uongo.
Si kweli kuwa kuna udhibiti kwa waislam. Hivi karibuni kuna taasisi imejenga misikiti 700, visima na maji mbona hawakudhibitiwa? Kuna akina African Muslim agency na World muslim league mbona hawakuwahi kudhibitiwa.
Nenda ndani ya baadhi ya taasisi hizo uone uchafu unaofanyika halafu urudi na kuniambia hiyo ni sehemu ya Uislam.
Na mwisho huko nyuma uliongelea TAMPRO. Nadhani hii taasisi inapoteza maana yake kwa namna fulani.
Wao kama professionals wanapaswa waongoze waislam katika mambo mengi badala ya kukaa pembeni na kuwaachia wahuni wachache.
Haiwezekani siku ya Ijumaa igeuzwe siku ya fujo na maandamo bila sababu za maana wala za msingi.
Ni hawa ninaoita wahuni ndio wameshika usukani wa kupotosha watu.
TAMPRO inapaswa itumike kama msaada mzima wa kuchukua ajenda na kuziangalia, kuzitathmini na kuzifanyia kazi kiweledi bila tafrani.
Sijui hebu nieleweshe viongozi wa TAMPRO ni akina nani ili niweze kuielewa vema
Anyway ni maoni tu.
Ukisema BAKWATA ni tatizo nitakuuliza WML ilifanya nini na iliondokaje, maana mzee mzima hakujibu!
Sitetei BAKWATA ninachosema hapa ni kuwa tatizo linaonekana kama BAKWATA lakini ni zaidi ya hapo na ni kubwa sana