mshikachuma
JF-Expert Member
- Dec 2, 2010
- 2,853
- 627
Ndugu yangu, hakuna asiyependa kujua historia ya nchi yake na hakuna anaepinga tu maandiko yako bila kuwa na mantiki stahiki,Sina ugomvi na uchambuzi wako.
Hatuwezi sote tukaona mambo kwa jicho moja.
Kinachonistaajabisha ni hizi hamaki mlokuwanazo
katika mjadala huu.
Lugha za "uongo," "uchochezi" hakika si maneno ya
kiungwana.
Sasa mbona hamgusi kwa kina Idd Faiz, Idd Tosiri na
Idd Tulio?
Hamna maswali kwa watu hawa?
Hampendi kujua kile kisichojulikana na wengi?
Hampendi kuwajua marafiki wa Nyerere katika siku zile
ngumu na za hatari za mwanzo 1955.
Mbona hamshangazwi kuwa mashujaa hawa hawajaenziwa
hadi leo?
Hampendi kujua nini ilikuwa hatima yao katika TANU?
Je hampendi kujua nyaraka za Nyerere za enzi ya TAA na TANU
anazo nani hii leo?
Je hamtapenda kujua nini kilitokea baada ya uhuru Nyerere
alipoziomba zile nyaraka?
Wanaukumbi hamtaki kujua "kisa cha ugomvi wa nyaraka?"
Hamtapenda kujua walokuwa na nyaraka zile kwanini walikataa
kumpa Nyerere nyaraka zile za TAA na TANU?
Mkijifunga katika maswali ya kujibizana yale ya nipe nikupe
mtapitwa na mengi.
Ahaaaa utakuja na ID zako zote 2 lakini ukweli ni kwamba umeshindwa kwa nguvu za hoja na sasa unaleta viojamzee Mohamed Said,
kwanza Assalam Alykum
Natumai hali yako ni murwa
Swali kwa hao wanaoita kitabu chako Alf Lela... Ni akina nani walimsaidia Hayati Mwalimu Julius Nyerere mpaka Tanganyika inapata Uhuru? Katika orodha yenu, mnawatambua wazee aliyowataja mzee Mohamed Said au la?
Naomba majibu
cc Barubaru Do santos Ritz
Mzee Mwanakijiji Nguruvi3 Jasusi Mag3 Yericko Nyerere na mkuu Sweke wakuu mmejenga hoja za maana sana ila nasikitika maswali humu hayajibiwi kabisa inasikitisha kama mtu anashindwa kutetea kitabu chake,nazidi kujifunza hapa asanteni sana kwa hili darasa
Wanajamvi, kumbukeni kuwa huu ulikuwa mkutano mkuu wa TAA April 1946. Ni matarajio kuwa mkutano mkuu ulihudhuriwa na wajumbe kutoka makao makuu. Kama nimeelewa vema mkutano mkuu ulihudhuriwa na Kasella, Dossa na Phombeah. Sasa soma hii tenaKumbe basi Nyerere alishaanza siasa akiwa katibu wa AA Tawi la Tabora. Kwa vile alikuwa katibu wa tawi muhimu namna hiyo vipi baadaye TAA makao makuu wasiwe wamesikia habari zake? Hapa Mohamed anakiri kuwa wanafunzi wa Makerere akiwemo Mwapachu na Nyerere tayari walikuwa katika msisimko wa kisiasa. AnaendeleaKwamba alichofanya Abdu Sykes si kuwaingiza katika siasa ili waanze kama anavyodai Mohamed katika majibu mengine bali kuwashirikisha katika siasa za jiji.Hapa Mohamed anamlenga Nyerere kwa kusema kila aliyetoka bara alifika kwa Abdul Sykes ili kupata ufahamu wa siasa kwanza. Alichosahu ni kuwa Nyerere huyo huyo alikuwa katibu wa AA Tabora(kwa maneno yake) na alianza siasa tangu Makerere (kwa maneno yake Mohamed).
Hakuishia hapo aliendelea kumnanga Nyerere kama hivi Mohamed anasema Ahaa1 kumbe walikuwepo akina John Rupia,Stephen Mhando katika subcommitee, sasa iweje Mohamed atambe kuwa baraza la wazee wa TANU iliyokuja baada ya TAA ilikuwa na Waislam walioleta Uhuru? Halfu hapa tunaona majina zaidi ya yale ya Clement Mtamila na Vedastus Kyaruzi. So far kuna Rupia, Dunstan Omar, Stephen Mhando, Clement Mtamila. Sasa inakuwaje Mohamed aseme wazee wake ni waislam na si wazee wote? Mohamed is on offensive against Nyerere, soma hii Hapo Mohamed ametumbukiza ukatoliki wa Nyerere kwanza, kisha kumwekea maneno kwa kutumia neno ''inasemekana''. Mohamed hakuwahi kumhoji Nyerere lakini alifahamu vema kuwa alikuwa mnyenyekevu wa kanisa na Serikali ili kulinda kibarua chake. Ni Mohamed huyo huyo alitueleza kuwa akiwa Makerere na Tabora Nyerere tayari alikuwa katika siasa, kwanini basi aanze kuhofia kibarua, serikali na Kanisa alipofika Dar? Maana yake ni kutaka kumshusha katika watu waliopigania uhuru kama anavyosema hapa Halafu akaendelea na chuki dhidi ya Nyerere na dini yake Hapa Mohamed anasahau kuwa Dr Vedastus Kyaruzi aliwahi kuwa kiongozi wa TAA licha ya Ukristo wake. Amewasahau akina John Rupia, Stephen Mhando na Clement Mtamila kuwa kwa Nayakati fulani walikuwa viongozi katika mji ule ule ambao Nyerere asingeweza kuwa kiongozi kwa ukristo wake.
Fikiria wakati unasoma, ukimeza bila kutafuna utajikuta umemeza ''Ngano'' kama si Mashudu.
Si Darasa ni Darsa mkuu...
Unajuwa unajichanganya sana. Kwa bahati sana nakifahamu kisa hichi ndani nje nje ndani. Na unaposeme Ukonga Banana enzi hizo kulikuwa na Bar ya SHUMA iliyoitwa Banana. Na wengi sana maofisa wa jeshi hususan kutoka Air wing walikuwa wanakunywa hapo. Na hata akina Rodric Robarts, Harry Hans Pope, Suleiman Matusela Komando na wengine walioachiwa baada kukosekana ushahidi kama akina Abdu Feshi Nketo walitokea Airwing 603KJ. Sasa wewe tuwekee hilo jina tulichambue. Kumbuka nilikuwa karibu sana na kisa hichi sababu mke wangu wakti huo alikuwa akifanya sharia pale UDSM. hivyo nilikuwa karibu katika kumsaidia skuli yake. Lete jina tulijadili.Ndugu zangu Barubaru, Kichwakigumu na Do santos, Kabla sijawajibu swali lenu naomba niwape kazi maalumu, 1) Baada ya maasi yale ya Ukonga Banana mwaka 1982, nani alikwenda kuwa balozi wa Nigeria, Msumbiji, na mwingine kuwa sehemu ya wanadhimu wa Ikulu? Majibu yenu ndio JIBU kuu langu la swali mama.
darsa ni kiarabu na darasa ni kiswahili kwahio usitulazimishe sie wabara kutamka lafudhi ya kiarabu
Waliofungwa ni waliokuwa jeuri tu, wapo (wakuu wa maasi) waliojirudi na kuomba msamaha hasa walipopelekwa IKULU, Nitakujuza wote subiri...
Unajuwa unajichanganya sana. Kwa bahati sana nakifahamu kisa hichi ndani nje nje ndani. Na unaposeme Ukonga Banana enzi hizo kulikuwa na Bar ya SHUMA iliyoitwa Banana. Na wengi sana maofisa wa jeshi hususan kutoka Air wing walikuwa wanakunywa hapo. Na hata akina Rodric Robarts, Harry Hans Pope, Suleiman Matusela Komando na wengine walioachiwa baada kukosekana ushahidi kama akina Abdu Feshi Nketo walitokea Airwing 603KJ. Sasa wewe tuwekee hilo jina tulichambue. Kumbuka nilikuwa karibu sana na kisa hichi sababu mke wangu wakti huo alikuwa akifanya sharia pale UDSM. hivyo nilikuwa karibu katika kumsaidia skuli yake. Lete jina tulijadili.
Asante sana mdau kwa kuthamini mchango wetu hapa jukwaani, watanzania tushirikiane kuilinda historia ya nchi yetu takatifuNimesoma kwa makini sana hoja za Mohamed Said na wachangiaji mbali mbali kuhusu maada hii. Hakika nimeshangaa sana madai ya Ustadh Mohamed Said, sijatofautisha sana madai yake na haya ambayo tumekuwa tukiyasikia sana katika misikiti karibu nchi nzima. Kwa kweli huyu mkuu amemwaga sumu mbaya sana na kama si sisi wana JF kuwa ni watu wa kuzungumza kwa uwazi na kwa kumbukumbu mbalimbali huyu jamaa anapotosha umma wa Tanzania......
Nimesoma kwa makini sana hoja za Mohamed Said na wachangiaji mbali mbali kuhusu maada hii. Hakika nimeshangaa sana madai ya Ustadh Mohamed Said, sijatofautisha sana madai yake na haya ambayo tumekuwa tukiyasikia sana katika misikiti karibu nchi nzima. Kwa kweli huyu mkuu amemwaga sumu mbaya sana na kama si sisi wana JF kuwa ni watu wa kuzungumza kwa uwazi na kwa kumbukumbu mbalimbali huyu jamaa anapotosha umma wa Tanzania.....
Tayari nimekupeni majibu, ona kwa jicho la tatu ndugu
Kwa yote haya, ilikuwa muhimu ahojiwe Nyerere kabla hajafa, pia Kawawa. Kama kuna wengine waliobaki wa kipindi hicho wahojiwe upesi sana.
Ingawaje mimi si 'mdini' (kwa maana ya kukashifu dini za wengine), ila ni kweli nikitazama hali za Waislamu Tanzania hadi miaka ya 90, huwezi kusema walikuwa wana haki zote. Haya yamekiriwa hata na Mkapa! Ikiwa haya yalikuwa yanafanywa makusudi au ni kwa sababu za Waislamu wenyewe, hilo ndio jambo halisi la kufanyiwa utafiti wa kina na kuhojiwa wale wanaohusika. Haiwezekani watu wenye akili timamu wakazuka tu na madai!
Nimesoma kwa makini sana hoja za Mohamed Said na wachangiaji mbali mbali kuhusu maada hii. Hakika nimeshangaa sana madai ya Ustadh Mohamed Said, sijatofautisha sana madai yake na haya ambayo tumekuwa tukiyasikia sana katika misikiti karibu nchi nzima. Kwa kweli huyu mkuu amemwaga sumu mbaya sana na kama si sisi wana JF kuwa ni watu wa kuzungumza kwa uwazi na kwa kumbukumbu mbalimbali huyu jamaa anapotosha umma wa Tanzania.
Namshukuru sana MwanaJF kwa kutoa somo la Historia kwa mhusika na nina dhani mhusika anatakiwa kufuta kauli zake kwa jamii. Kuhusu kitabu alichokuwa amekiandika hilo tuiachie jukumu serikali kwani lengo la huyu jamaa ni kufuta historia ya nchi yetu kwa maufaa yake na familia yake. Aliandika akiwa na maono binafsi ili aweze kuganga njaa. Sisi wananchi wa Tanzania tunatoa tamko kwamba historia yetu isipindishwe na mtu ambaye kwanza amezaliwa juzi juzi na amejifunza katika vitabu na amejitahidi kupindisha kwa njaa aliyonayo.
Mengi yamekuwa yakianzia katika mahubiri ya kukashifu dini nyingine ama serikali, ni jukumu la serikali kuanza kuzuia mihadhara hii ambayo haina tija kwa jamii.