Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kama wewe ulivyo kuwa sawa na Nguruvi,Mag3 wote kitu kimoja munachuki na mzee MS na uislamu!
 
gombesugu,

..Casimiro Montero, jasusi wa Kireno, ndiye anayenyooshewa kidole kuhusika na mauaji ya Mondlane.

..sasa kama una taarifa mpya kwamba Mwalimu Nyerere ndiye mhusika basi JF kuna watu wengi very open minded tunaweza kuziangalia kama zina ukweli au la.

..lakini wakati utakapozileta naomba nikuulize: movite ya Nyerere kumuua Mondlane ilikuwa ni nini haswa?

..zaidi, what r u trying to prove here, ukizingatia hoja yako ni Mwalimu kumuua Mondlane, na badala yake kushiriki kumsimika ktk uongozi Samora Machel ambaye alikuwa Maxist??

cc: Jasusi, Nguruvi3, Kudi Shauri, Wickama, Mag3
 
Last edited by a moderator:

Yericko Nyerere,

Usipende kusafiria nyota za watu unatumia maandishi ya watu bila kumtaja muhusika jina huu ni ujinga na upuuzi wa hali ya juu.

Watu wanaumiza vichwa kufanya utafiti kuandika makala za historia, hili bandiko siyo lako ukibisha tawaonyesha wanaukumbi ulipo liiba.

Unajifanya mwandishi kumbe una lolote unaiba kazi za watu.

Angalia mimi naleta bandiko humu na nimtaja mwandishi.

Mohamed Said, Barubaru, Kadogoo, gombesugu, THE BIG SHOW,
 
Last edited by a moderator:
jokaKuu,
How can you take anybody seriously who claims that Nyerere conspired with Kennedy to kill Lumumba. Now he must have also conspired with PIDE, the secret Portuguese police to kill Mondlane. And for what reason? Really?
 


...huna tofauti na wanawake wa vilabuni....! maana wale kwa maneno machafu....sion tofauti yao na yako
 
Nimeamua kuuweka huu unaoitwa mpini na Ritz kwa namna rahisi kidogo ili wanajamvi wausome tena taratibu na kwa umakini mkubwa. Sina hakika na huu mpini wa Ritz kama na wenyewe unaelezwa kama historia ya kweli ya Mapinduzi Zanzibar. Baadaye nafasi ikipatikana huu mpini nao utachambuliwa taratibu kama mpini wa Mohamed Said kuhusu alichodai ni historia ya kweli ya harakati za uhuru wa Tanganyika ulivyochambuliwa na unazidi kuchambuliwa.

Hata hivyo kabla ya uchambuzi huo kufanyika natoa tahadhari kwa wana JF; ni vizuri kufahamu malengo na nia za watu kama hawa ambao wako tayari kuita mchana usiku, mwanga giza na cheupe cheusi. Mohamed Said anadai BAKWATA haiwawakilishi Waislaam Tanzania bali ipo inautumikia mfumo Kristo; kwa maana nyingine kama unakubaliana na BAKWATA, kama ni kiongozi wa BAKWATA au kama wewe ni mwanachama wa BAKWATA basi Uislaam wako una walakini.

Hoja hii ya nguvu imetumika kuwadanganya, kuwasuta na kuwatisha Waislaam wasiokubaliana na mahubiri yake ya chuki. Kwa nini nasema hivi? Labda tuanze na NATIONAL MUSLIM COUNCIL OF TANZANIA (BAKWATA) ni nini, hapa naona nianze kwa kunukuu maelezo yaliyotolewa na jumuiya yenyewe miaka ya nyuma kidogo;

Swali kwa wanajamvi; tumweleweje mtu ambaye anao ujasiri wa kudai kuwa BAKWATA si chombo cha Waislaam wala kinachowawakilisha Waislaam bali ni chombo kinachoongozwa kwa maelekezo ya Kanisa? Je mtu huyu analitakia mema taifa hili? Kwamba Sheikh Mkuu wa Tanzania anatekeleza majukumu yake kwa maelekezo ya Kanisa! Kwamba kiongozi Mkuu wa serikali na jemadari Mkuu wa taifa, Al Haj Dr. Jakaya Mrisho Kikwete anatekeleza wajibu wake kwa matakwa ya Kanisa! Huyo ndiye Mohamed Said.

Baada ya hiyo tahadhari, naendelea kuutafakari mpini ulioletwa na Ritz akiwanukuu Dr. Ghassany na mwandishi anayeitwa Ahmed Rajabu. Kama isingekuwa kuwa madai yaliyotolewa hayatoi mwanya wa kutafsiriwa vibaya na watu wenye uelewa mdogo na hivyo kuweza kutumika kichochezi, wala hata nisingehangaika kuyajibu, ningebaki tu nacheka kwani simulizi utadhani ni hekaya za Abunwasi...hadithi njoo, uongo njoo, utamu kolea!
 
...huna tofauti na wanawake wa vilabuni....! maana wale kwa maneno machafu....sion tofauti yao na yako

kumbe mkuu wewe ni mtu wa vilabuni sana, Sasa jitahidi mida hii ukiwa unatoka kilabuni usiwe unapost maana unaharibu mjadala.

Mwalimu wangu wa jamvini alinifundisha mtu akikutukana ulevini na wewe mrudishie hapo hapo, kesho asije akasema alikuwa amelewa.
 

Dilikeni,
Amin, Amin, Amin.
 

Yericko,
Stizai ndiyo mwenza kwa yule ambae hakufikwa.

Tumekusomeni hapa mkikejeli, mkikebehi na mwisho
mkitukana.

Waswahili tuna msemo.
Mdomo haumkatai bwana wake.

Hakuna wa kukuzuia kumpa sifa Okello.

Lakini historia ya Zanzibar tunaijua siyo kwa kuwasoma
Wazungu bali kwa kuishi ndani yake.

Rejea mabandiko yangu niloweka kuhusu historia ya mapinduzi
kisha fananisha na usemayo kuna jambo utaliona dhahir shahir.
 

Tatizo lako hii historia huijui bali unajikita kwa USHABIKI tu kuwa katika taifa la Znz ambao wengi waislam UHURU wao uliletwa na Mkristo tena mmoja ambaye ni mgeni asiye na hata konde hapo Unguja.

Vile vile unatakiwa kujua kuwa Uhuru wa Tanganyika wamepewa ofisini kwani nchi hiyo iliwekwa chini tu ya uangalizi wa wAingereza. sasa inapotokea mtu kujiita baba wa Taifa kwa sababu ya kusafirishwa na kwenda kupewa uhuru ofisini je ni Ubaba gani huo. hebu niambie baba wa Taifa lolote unalolijua wewe ambaye Uhuru alipewa ofisini.

lakin na la kujiuliza Je ni kikao gani halali cha Bunge kilichopitisha kuitwa Nyerere baba wa Taifa. nafikiri hizo ni baadhwi tu ya wanafunzi wake ambao aliowaangalia kwa jicho la huruma na kuwapa madaraka ndio hao vinara wa kumpa kila cheo.

je una taarifa na sasa baada ya Kufariki anataka kupewa cheo kingine cha Mwenye kheir?

Ushauri wangu kama utaondoa USHABIKI na Pupa nafikiri utafunzwa mengi hapa kwani unachoandika wengine kimetutokea na tumekishuhudia mchana kweupeeee si wewe wa kuhadithiwa na kuwekewa chumvi.

Jitulize usomeshwe.

 

Swadakta Al Akhiy Mohamed said.

Mimi nimemnasihi Atulie kitako tumpe darsa hapa kwani yeye amehadithiwa lakin wengine tumeyashuhudia kwa macho yetu.

lakin siku zote ukikumbwa na USHABIKI na pupa basi ilmu itakupita pembeni kwani siku zote ilmu bora ni ile unayotulia na kuipokea tartibu kwa mpangilio na mtiririko wake.

Tumpe pole na kumnasihi aache jazba ili adarsishwe hapa. na akiondoa Ushabiki basi ataelewa zaidi.

Ahsantum Al Akhiy .

 

Naona huu "Mpini" umekuchanganya kabisa mpaka hujitambui unajifanya unacheka wakati nafsi inalia.

Naona unakunywa sumu kwa maziwa...ha haa ha.

Cc.. gombesugu,
 
Last edited by a moderator:

Mbona unaropoka kwa hamaki hivyo?

Wapi nimesema mimi ndie mwandishi?

Hukuona makala zingine zote nilizoleta hapa nilikuwa naweka jina langu mwisho?

Usiwe na papara kijana, tulia soma na ujue mantiki!

Musimulizi wa hayo ni Barghash:
 
Last edited by a moderator:
Hii shule tunayopata kwenye huu mjadala ni kali,kumbe Field Marshall OKELLO ndio baba wa taifa wa zanzibar-asanteni wachangiaji
 

Alichoeleza Ahmad Rajab ni sahihi kabisa kwani ndio kwani yeye mwenyewe ni mmoja walioshuhudia mapinduzi hayo akiwa na Rafiki yake Salem Saleh mitaa ya shanghani.

Kwani mambo haya yanataka umakini sana katika mapokeo yake lakin utapata machungu sana kama utaingiza ushabiki.

Kumbuka kuwa Brig Yusuf Himid ndie aliyakuwa Mkuu wa kwanza wa majeshi upand ewa Znz na akina Seif Bakari ( nilizowea kumwita mndengereko wa jang'ombe) alikuwa msaidizi wake.

Ahsantum Ritz kumwekea historia toka kwa mtafiti ambaye alishuhudia tukio hilo.

 


Kwani Nyerere ni nani mbele ya watu hao mpaka wamchukie.

kumbuka kuwa matendo yako na tarbia zako ndio zinazokuhukumu. na Nyerere anahukumiwa kwa matendo yake alotenda na si vinginevyo.

tafadhwali usimtukuze mtu kiasi cha kukufuru na kumpa swifa za uungu kama unavyotaka kumpa Nyerere.

Pole sana
 
Mbona unaropoka kwa hamaki hivyo?

Wapi nimesema mimi ndie mwandishi?

Hukuona makala zingine zote nilizoleta hapa nilikuwa naweka jina langu mwisho?

Usiwe na papara kijana, tulia soma na ujue mantiki!

Musimulizi wa hayo ni Barghash:

Sikiliza dogo hapa unaongea na vichwa vya Madrassa usilete ujanja ujanja.

Mohamed Said, kakuuliza kama unajua chochote kuhusu mapinduzi weka ulivyokuwa kauzu umejitapa kisha ukamjibu kwa maandishi ya mtu mwingine kwa kuwa wewe huna unachokijua.

Bila mimi kusema ungemtaja mwenye maandishi wa hiyo makala? Acha utoto.

Cc.. gombesugu, Barubaru,
 
Last edited by a moderator:

Shariff Barubaru,

Kuna vitu vingine inabidi ujifunze kutoka kwa wahusika haiwekani mtu anatoka Mwitongo au Magu au Kemendo, anataka kuelezea historia ya mapinduzi ya Zanzibar.

Mimi binafsi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar nimejifuza kutoka kwa wahusika wenyewe waliokuwepo.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…