Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Wanajmvi,
Nakumbuka mwaka jana tulikuwa na mjadala huu wa mapinduzi na ushiriki wa Nyerere. Katika mjadala huo swali langu lilikuwa lile lile '' kwanini wznz wanasherehekea na kutukuza mapinduzi'' yaliyokuwa na dhima ya kuua Uislam?
Swali la pili likiwa ''kwanini kuna wznz wanasema mapinduzi daima, na wengine wanasema mapinduzi haram''?
Baada ya kukosa majibu, Ahmed Rajab kwa kutumia gazeti la Raia mwema alitoa majibu.
Ingawa hakusema ni kujibu JF mnakasha, dhahiri ilikuwa na lengo hilo kwa mwenye akili.
Ahmed alisema, inategemea wakati wa mapinduzi nani alikuwa upande gani. Akasema wapo walioona mapinduzi yalikuwa na mnaufaa na wapo waliosema hayana manufaa kwa kuzingatia masilahi ya kila mmoja kwa wakati ule.
Hakuweza kusema ni halali au siyo zaidi ya habari nyingine.
Leo nimemsoma Mohamed Said kurasa chache zilizopita. Yeye anatamba kutaja majina ya waliohusika na punda waliohusika nadhani akimaanisha waislam walioshiriki kama ndivyo.
Ukisoma maelezo ya Ahmed na Mohamed yanatofautiana sana na ni wazi kuwa kwa hili kila mmoja anavutia upande wake ingawa wana common interest ambayo ni mashambulizi dhidi ya Nyerere. Kwa Ahmed si makali kama Mohamed.
Mohamed anasema yeye ni mtafiti na amefanya utafiti. Kitu cha kushangaza ni kuwa utafiti siku zote hueleza pale ambapo utafiti zaidi unahitaji au kama hakuna basi conclusion ya ule uliopo.
Sasa utafiti wa Mohamed ni pamoja na kupata majina ya waliohusika hata kufahamu nani alilala kwa bibi au babu yake.
Yote hayo ni kheri. Kinachosumbua sana katika utafiti wake ni pale ambapo utafiti unashindwa kujibu hoja muhimu sana.
Anadai Nyerere alipeleka wamakonde wa Kipumbwi kwenda kupindua serikali ya Sultan kwa lengo la kuua uislam.
Kwa maneno mengine mapinduzi ni haramu kwasababu hayakutokana na wznz bali Nyerere na ukatoliki wake.
Sasa tunapomuuliza conclusion ya maneno yake hana jibu anakimbia huku na huko akitaja majina ya watu.
Mohamed, Je, unawaambia nini wznz, kwamba mapinduzi ni haramu na waache kuyatukuza?
Haiwezekani iwe haramu kufanya mapinduzi kulikotokana na Nyerere halafu ikawa halali kwa waislam wa znz kutukuza mapinduzi haramu!!!
Wapi haram ilikuwa halali kisa imeshikwa na mwislam?
Contradictions kama hizi zinafanya watu wahoji, nini maana ya utafiti kama hauna answer to the question.
Is it not fabrication?
Bottom line, Je, mzanzibar ana uhalali wa kushangilia na kutukuza mapinduzi? Kama ni ndiyo,je, Nyerere apongezwe au alaumiwe? kama ni hapana mapinduzi ni haram? Jibu likiwa ndiyo, halali ya waislam 99 wa znz kuyashangalia inatoka wapi?
Wanajamvi,
Kuna kijembe "Karume kalala kwa bibi yangu" kimerudiwa mara kadhaa.
Nilisema siku ile ya mapinduzi Karume alikuwa kalala nyumbani kwa mmoja
wa wazee wangu.
Mtu yoyote mwenye utambuzi wa kawaida angejua kuwa hiyo mipango ya
kupindua serikali ilimjumuisha huyu mzee wangu.
Nitafunguka bila kumtaja jina.
Huyu mzee wangu alikuwa mmoja wa waasisi wa TANU.
Lakini ilipokujamdhihirikia yale mauaji yalotokea Unguja yeye alijuta na hadi
leo amekataa kabisa kueleza mchango wake katika mapinduzi yale.
Ila kitu nilichoweza kukipata kutoka kwake ni kuwa hadi yanatokea yale mauaji
hakuwa anajua kuhusu kambi ya Kipumbwi na jeshi la Wamakonde.
Haya mauaji bado yanamchoma moyo hadi leo.
Swali la kutukuza mapinduzi jibu lake jepesi.
Unahitaji kuwasikiliza wenyewe Waunguja leo wanasema nini.