Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Hii shule tunayopata kwenye huu mjadala ni kali,kumbe Field Marshall OKELLO ndio baba wa taifa wa zanzibar-asanteni wachangiaji

Karibu sana dada jackline1,

Huo ndio ukweli mchungu kwa baadhi ya wahafidhina wa Zanzibar!

Wanalijua hilo lakini kwao wanaona ni aibu,

Wacuba leo hii baba wa taifa lao ni mgeni kabisa Ernest Che Guevara,

Imewalazimu kwa heshima ya kutambua mchango wake wamesafiri mpaka Argentina kufukua kaburi la Che-Guevara nakuja kulizika kitaifa nchini Cuba!

Sasa leo wazalendo hawa wa Zanzibar wakiamua kumuenzi mkombozi wao dhidi ya minyororo ya utumwa kuna ubaya gani kwao?
 

Wewe dogo mbona muongo muongo sana, hujui historia ya Guevara.

Kwanza siyo Ernest ni Ernesto Guevara wala hakufia Argentina alifia Bolivia.

Nifunguke zaidi nikupe darsa?

Hivi unajua historia ya taifa la Cuba au unaropoka tu.

Baba wa Taifa wa Cuba ni Carlos Manuel De Cespedes.

Umeipata wapi kuwa Che Guevara ni raia wa Cuba?
 
Field Marshal John Okello yawezekana wapo watu wakajidanganya kuwa wanaweza kufuta historia yake lakini dunia itaendelea kumkumbuka kama huyu mbunge wa Uganda alivyoandika Jumapili Octoba 7, 2012 wakati wa kusherehekea siku ya uhuru wa Uganda.

 
Hahaa mkuu, wanajamvi wanakusoma wazi!

Kumbuka maelezo yako ya mwanzo ulisema hutaki kabisa kuzungumzia mapinduzi yale chini ya Okello ukisema wazi yalipoteza watu wengi sana wakiwemo ndugu zako wa damu,

Lakini baada yakumsoma mpotoshaji mwingine Ahamed Rajab umegeuka na kuwa upande wake,

Unanishangaza kwa hilo mkuu, kumbuka wewe uliyashuhudia mapinduzi yale
 
Field Marshal John Okello yawezekana wapo watu wakajidanganya kuwa wanaweza kufuta historia yake lakini dunia itaendelea kumkumbuka kama huyu mbunge wa Uganda alivyoandika Jumapili Octoba 7, 2012 wakati wa kusherehekea siku ya uhuru wa Uganda.

Mkuu kwakweli inachekesha hasa ukiwaona hawa ndugu zangu wanapopika data za uongo na ngano kibao ilimradi kupotosha umma na kumuondoa Okello katika historia ya Zanzibar!

Ukweli histori hujiandika, na huwa haibadilishwi bali hujibadilisha yenyewe!

Kamwe huwa haifuti ama kujifuta!
 
Sayyid Jamshid bin Abdullah Al Said hawezi kumsahau Field Marshal John Okello, Dunia haiwezi kumsahau Field Marshal John Okello, Afrika Mashariki haiwezi kumsahau Field Marshal John Okello na Zanzibar ndiyo kabisa haitaweza kumsahau Field Marshal John Okello. Kama si hekima na juhudi za Mwalimu Nyerere ya kumshawishi Okello aje Dar es Salaam na kumpa nafasi Karume apumue, mambo yangekuwa mengine kabisaaa.
 

Hili darasa linanizidi kimo- kwa hiyo wa kulaumiwa ni nyerere????? kwa kumuondoa okello katika historia kama inavyodaiwa alivyowaondoa wazee wa gerezani?????????
 
Hili darasa linanizidi kimo- kwa hiyo wa kulaumiwa ni nyerere????? kwa kumuondoa okello katika historia kama inavyodaiwa alivyowaondoa wazee wa gerezani?????????

Hehee dada mada hii ni nzuri na chungu kwa wabora sisi,


Ukipekua ukura wa pili ama wa tatu nyuma hapo nimeweka makala inayoeleza wazi utawala wa Okello wa miezi sita ulivyokuwa mgumu kwa watu na sababu za Mwalimu kutumia turufu ileile aliyotumia kumshawishi Gavana Twaining wa kutupa nchi yetu ndipo akamshawishi Okello aje ikulu Dar na maridhiano ya kukabidhi madaraka kwa karume yakatukia!


Karume asingeguza ikulu ya zanzibar na kuwa rais bila mwanadiplomasia mahiri wa afrika Julius Kambarage Nyerere!
 
kwa hiyo kiuhalisia rais wa kwanza wa zanzibar ni Okello???


"According to Zanzibari historical sources, during a speech on radio after the takeover, Okello dubbed himself the "Field Marshal of Zanzibar and Pemba". In fact, some political analysts consider/considered him as the first President of the new Revolutionary Government of Zanzibar"
 
Hili darasa linanizidi kimo- kwa hiyo wa kulaumiwa ni nyerere????? kwa kumuondoa okello katika historia kama inavyodaiwa alivyowaondoa wazee wa gerezani?????????
jackline, kwanza mpe heshima kidogo Baba wa Taifa...ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Pili tarehe 9/12/1961 Tanganyika ikijikomboa kutoka mikononi mwa mkoloni mwingereza, aliyeongoza mapambano alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Tatu, tarehe 12/1/1964 Zanzibar ikijikomboa kutoka mikononi mwa mkoloni mwarabu, aliyeongoza mapambano alikuwa Field Marshal John Okello.




Iti is Field Marshal John Okelo who named the leader of the Afro-Shirazi Party, Abeid Karume as President. Karume was residing in Tanganyika, but returned to Zanzibar, where he was welcomed by Okello.
 
Last edited by a moderator:
Hivi kuna swali limenijia;

Abdulwahid Sykes alikuwa upande gani ilipoundwa AMNUT?
Abdulwahid Sykes alikuwa upande gani ilipovunjika EAMWS?

(Alisema nini kuhusiana na yote haya mawili?)
 
Wanajmvi,
Nakumbuka mwaka jana tulikuwa na mjadala huu wa mapinduzi na ushiriki wa Nyerere. Katika mjadala huo swali langu lilikuwa lile lile '' kwanini wznz wanasherehekea na kutukuza mapinduzi'' yaliyokuwa na dhima ya kuua Uislam?

Swali la pili likiwa ''kwanini kuna wznz wanasema mapinduzi daima, na wengine wanasema mapinduzi haram''?
Baada ya kukosa majibu, Ahmed Rajab kwa kutumia gazeti la Raia mwema alitoa majibu.
Ingawa hakusema ni kujibu JF mnakasha, dhahiri ilikuwa na lengo hilo kwa mwenye akili.

Ahmed alisema, inategemea wakati wa mapinduzi nani alikuwa upande gani. Akasema wapo walioona mapinduzi yalikuwa na mnaufaa na wapo waliosema hayana manufaa kwa kuzingatia masilahi ya kila mmoja kwa wakati ule.
Hakuweza kusema ni halali au siyo zaidi ya habari nyingine.

Leo nimemsoma Mohamed Said kurasa chache zilizopita. Yeye anatamba kutaja majina ya waliohusika na punda waliohusika nadhani akimaanisha waislam walioshiriki kama ndivyo.

Ukisoma maelezo ya Ahmed na Mohamed yanatofautiana sana na ni wazi kuwa kwa hili kila mmoja anavutia upande wake ingawa wana common interest ambayo ni mashambulizi dhidi ya Nyerere. Kwa Ahmed si makali kama Mohamed.

Mohamed anasema yeye ni mtafiti na amefanya utafiti. Kitu cha kushangaza ni kuwa utafiti siku zote hueleza pale ambapo utafiti zaidi unahitaji au kama hakuna basi conclusion ya ule uliopo.

Sasa utafiti wa Mohamed ni pamoja na kupata majina ya waliohusika hata kufahamu nani alilala kwa bibi au babu yake.
Yote hayo ni kheri. Kinachosumbua sana katika utafiti wake ni pale ambapo utafiti unashindwa kujibu hoja muhimu sana.

Anadai Nyerere alipeleka wamakonde wa Kipumbwi kwenda kupindua serikali ya Sultan kwa lengo la kuua uislam.
Kwa maneno mengine mapinduzi ni haramu kwasababu hayakutokana na wznz bali Nyerere na ukatoliki wake.

Sasa tunapomuuliza conclusion ya maneno yake hana jibu anakimbia huku na huko akitaja majina ya watu.
Mohamed, Je, unawaambia nini wznz, kwamba mapinduzi ni haramu na waache kuyatukuza?

Haiwezekani iwe haramu kufanya mapinduzi kulikotokana na Nyerere halafu ikawa halali kwa waislam wa znz kutukuza mapinduzi haramu!!!

Wapi haram ilikuwa halali kisa imeshikwa na mwislam?

Contradictions kama hizi zinafanya watu wahoji, nini maana ya utafiti kama hauna answer to the question.
Is it not fabrication?

Bottom line, Je, mzanzibar ana uhalali wa kushangilia na kutukuza mapinduzi? Kama ni ndiyo,je, Nyerere apongezwe au alaumiwe? kama ni hapana mapinduzi ni haram? Jibu likiwa ndiyo, halali ya waislam 99 wa znz kuyashangalia inatoka wapi?
 

Huo ndio ukweli pekee unaokwepwa bila sababu za msingi!

Field Marshal John Okello au Mungu wa Afrika ndie BABA halisi wa Taifa la Zanzibar,

Ulie, ukatae, unune, ususe huo ndio ukweli!

Na wazanzibar wanayo fursa ya kumuenzi kama mkombozi wao sio kuyaenzi tu mapinduzi yake kwa mgongo wa chupa!
 

Sasa wewe unashukuru, mara unasifia, nani kakupa kazi ya kuwa kama mgeni rasmi aliealikwa kufungua na kufunga mijadala? huna lolote unalochangia ktk mnakasha huu wa Yericko juu yakile kinachoitwa uchochezi wa MS! kazi yako wewe ni kudandia na kuteremka! we una tuwekea Conclusion hapa kama nani?
 
Yan Yericko sasa amefikia hatua mbaya sana,anatufananaisha Moh Said na vijana wake sawa na wanawake wa saluni??
Kweli kakosa malezi ya baba,si bure..!
 
Hivi kuna swali limenijia;

Abdulwahid Sykes alikuwa upande gani ilipoundwa AMNUT?
Abdulwahid Sykes alikuwa upande gani ilipovunjika EAMWS?

(Alisema nini kuhusiana na yote haya mawili?)
Mzee Mwanakijiji, Abdulwahid Sykes alipata nafasi tatu za kuonesha alivyo maarufu kisiasa, mahiri kiuongozi na mashuhuri kijamii.

  1. Nafasi ya kwanza ilijitokeza mwaka 1950 alipogombea nafasi ya uongozi wa juu wa TAA katika uchaguzi uliofanyika kumpata kiongozi mwenye sifa zote hizo.
  2. Nafasi ya pili aliipata mwaka 1953 uchaguzi wa TAA ulipofanyika kumpata kiongozi mwenye "vision" ambaye angeweza kuiwezesha TAA kukabiliana na changamoto mpya zilizoikabili
  3. Nafasi ya tatu ilijitokeza mwaka 1954 chama cha TANU kilipozaliwa na kutakiwa kiongozi ambaye angeweza kusimamia imara harakati za kisiasa katika kudai uhuru.
Baada ya hapo? Your guess is as good as mine...a boxful of disappointment. Je kitu gani kilifuatia baada ya hapo? Hizi simulizi za Mohamed Said nadhani zinatupa kwa mbali taswira ya yaliyomsononesha Abdulwahid Sykes. Je kama kungetokea chama pinzani na TANU, angekiunga mkono hata kama si kwa waziwazi? Ni nini chanzo cha machungu yaliyomo ndani ya simulizi alizokuwa akipewa Mohamed Said utotoni? Ni kitu gani kiko nyuma ya malalamiko yale? Mathalani mwaka 1958 tunawaona waliokosa uvumilivu kama Chamwenyewe wakiaasisi AMNUT kwa imani kwamba kitaungwa mkono na waumini wenzake halafu kinakataliwa na hao hao waumini...disappointment on top of disappointment! As I said before, your guess is as good as mine.
 

Nasisi wengine tuna fyonza ILM toka kwa MS na yeyote mkweli!
 
Baubau, Sikajiji ameuliza swali rahisi sana. ''Je wewe unadhani Nyerere aliinjinia Mapinduzi''
Hayo maelezo yako hapo juu hayajibu swali.

Katika maelezo yako hapo juu unajaribu sana kuweka fikra zako zaidi ya ukweli licha ya kukimbia swali la msingi.
Nakuomba uzirejee sababu zilizopelekea Karume kukubali muungano. Katika hili lazima uwafikirie akina A.Babu na Uslama wa Karume.

Lakini basi kama Nyerere alitaka kuwalaghai waislam wa Tanganyika, je hiyo ndiyo sababu ya yeye kuinjinia Mapinduzi?

Mzanzibar anaposhindwa kuieleza historia ya nchi yake inashangaza na kusikitisha
 

Wanajamvi,
Abdu Sykes hakupata kuipa mgongo TANU kwa mapenzi wala ufadhili.

Katika Tatizo la AMNUT yeye alikuwa upande wa Nyerere kama wenzake
wote alioundanao TANU toka enzi za TAA 1950s hadi rasmi walipoiunda
1954.

Kuhusu EAMWS hili alikuwa upande wa Waislam na nimeeleza katika kitabu
mazungumzo yake na Nyerere Ikulu kuhusu kuandamwa Waislam siku chache
kabla hajafa.

Abdu hakuwa mtu aliyechangia kuasisi TANU kwa kukamata nafasi za uongozi.
Abdu yeye sifa yake kubwa ni kile kipaji chake cha kusuka mipango dhidi ya
Waingereza na kufadhili harakat.

Haya yote nimeyaeleza katika kitabu toka alipokuwa Burma hadi alipohusika
na mgomo wa makuli 1947, kuleta mageuzi ya uongozi TAA 1950 na mwisho
kuasisi TANU 1954 kadi yake ikiwa na 3, mdogo wake Ally Sykes kadi na 2 na
Nyerere kadi na 1.

Said Chamwenyewe hakupata kuwa mwanachama wa AMNUT yeye alikuwa Congress
na Zuberi Mtemvu.

Juu ya maelezo haya mtu bado yuko huru kuamini historia aionayo imemkalia vizuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…