Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wazee wako walilisukuma hilo gurudumu bila usukani hadi mwaka 1952. Kuanzia mwaka 1953 Mwalimu akashika USUKANI hadi tulipopata uhuru. Wazee wako wachache wakabaki kama utingo, wengine konda na wengi wakawa abiria na kulala kabisa kwenye viti hadi mauti.


Historia ni katili hivo wakati mwingine. Anayeanza sio lazima amalize akiwa wa kwanza.
 
gombesugu,

..inategemea umemuita Mnyasa ktk mazingira gani.

..katika mazingira ya Znz na ubaguzi uliopo pale unapomuita Mnyasa inamaanisha hastahili kuitwa Mzanzibari.

..sasa Karume anaitwa Mnyasa, halafu Shamte anaitwa Mzanzibari!! huoni kuna hitilafu hapo??

..Sheikh Mohamed hajakosea kuwataja hao Wamakonde waliopewa "tender" ya kumpindua Sultani.

..mimi sijakisoma hicho kitabu, lakini kwa jinsi watu wanavyokitaja hapa JF, nadhani nitalazimika kukisoma.

..tatizo ni kwamba karibu kila m-Znz ana ajenda yake. wakitaka kumshutuma Nyerere na Ukatoliki basi wanadai yeye na Okello ndiyo wamepindua. wakitaka kuutukuza uzanzibari wanadai waliopindua ni umma party.
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,

..duh!!

..punguza udini.

..tatizo lako ni kufikiri kila anayepingana na wewe basi ana chuki dhidi ya Uislamu.

..hebu ona hapo unamuita mchangiaji mwenzako "Muislamu" wenu.

..hivi ni uungwana kweli kufanya hivyo??





..

JokaKuu,

Nakuomba ndugu yangu upitie posts zangu ambazo si nyingi asilan,halafu uone jinsi gani nilivyojieleza kuhusu Udini na family tree yangu ilivyo....

Watu wanaonifahamu na close friends wangu watakucheka na kukushangaa wakikusikia ati unanishutumu mimi Udini!?

Wewe kwanza ulitakiwa ukemee matusi dhidi ya Dini zoote hapa Jamvini....unakumbuka vizuri jinsi nilipojiunga hapa Jamvini/JF jinsi Gwalihenzi alivyokua anamtukana Allah na Mtume wetu Mtukufu constantly for almost a week....na hakuna hata mmoja wenu alothubutu kukemea zaidi ya kuweka LIKE!?

Hii issue nilishawahi kumwandikia rasmi Nguruvi3 na Mwanakijiji,kwa sababu nilihisi labda kutokana na hishma yao ya ki-Chadema wangeamua kukemea na kusikilizwa!

Sasa ndo maana nikakwambia pitia posts zangu zoote na uone hayo yoote na pia majibu yao hao Nguruvi3 na Mwanakijiji kuhusu suala hilo!

Ndo maana wakti mwingi kutokana na baadhi ya matendo yenu hapa jamvini, mimi nawahisi nyinyi hamna nia thabit na ya dhati kutaka amani na hiyo nchi yetu!

Kuhusu huyo "Muislamu" wenu,embu angalia post za awali jinsi alivyomnyambua Mufti Sheikh Hassan Bin Ameir....hivi unafikiri ni Waislamu wangapi wana Acess na JF,ambao labda hata pia si members. Na unajua hishma ya huyo Sheikh Hassan Bin Ameir katika umma wa Waislamu hapo Tanzania!?

Na kama ulivyoona jinsi alivyoizungumza Ayat za Quraa'n kwenye zile posts ya siku chache tu ilopita. Angalia jinsi nyinyi mlivyoweka LIKE!?

Unajua inalazim muwe serious na mtumie common sense,kama kweli mko humu kutafuta amani na usalama wa nchi.
 
Mkuu Zumbemkuu, ulikuwa wapi? kimya kingi kina mshindo?
mkuu nipo na wala siogopi kung'olewa kucha na meno kwa makoleo, hahahahahahaha!
nilijipumzisha na stress za siasa tu kwa mda. nafuatilia kwanza BANGE la jamhuri kule dodoma.
 

JokaKuu,

Ndugu yangu niwie shukran.

Maana tayari inalazim niondoke. Lakini numefurahi mno kuzungumza nawe.

Mimi binafsi nakuheshimu saana hapa jamvini,na napenda pia nakustahi mno kwa ustaarabu na stahamala ulonayo.

Ahsanta tutamalizia siku nyingine.
 
gombesugu,

..nimekusikia mkuu.

..kila mwana JF yuko responsible na majibu yake.

..ushauri wangu ni kwamba ukiona mtu ana hoja za ajabu ajabu[kutukana dini za wenzake] wewe mu-ignore tu. wengi wao huwa wanatafuta attention tu.

..kuhusu huyo "Muislamu" wetu, na jinsi alivyoizungumzia Ayat za Quraa'n je unafikiri ni suala la dharau na kashfa au huenda ni mapungufu tu ya kibinadamu ktk kutoa tafsiri sahihi ya Ayat husika??

..anyway, mimi nadhani tuyaache haya. turudi kule kwenye suala letu la Msumbiji nadhani kule tulielewana zaidi.
 
Last edited by a moderator:
Mnakasha unazidi kunoga,kuna mtu anaitwa gombesugu ananifanya nicheke sana,sasa na hii Al akhy maana yake nini? Ritz
 
Last edited by a moderator:

Huyo Muislam wao toka alete bandiko lake humu ukumbini kumkashifu Mufti Sheikh Hassan bin Amiri, kuanzia siku iyo nikamuweka kwenye list yangu "Abuu Jahali list"

Marehemu Sheikh Hassan bin Amir kwetu sisi Waislam ni mtu ambaye ametuachia athari nyingi katika mafundisho ya Uislam. Kafundisha Masheikh wengi Tanzania.

Halafu anakuja kauzu mmoja analeta kashfa huku anajinasibisha na Uislam.

Marehemu Sheikh Mohamed Ayoub kutoka Tanga alikuwa anatokwa na machozi Masheikh wakidhalilisha na wale wanaojiita Waislam.
 
Kijani, Njano, Nyeusi na Nyekundu!

Uhuru kamili wa Rege!

Nawasalimu wote katika jina la Jah!

Naam nilijipa likizo kidogo leo, na sasa nimerejea!

Naona mjadala juu ya Zanzibar bado ni mzito, hamaki na fura naona vimepungua, ustaarabu umechukua mkondo wake!

Jah akisimama nasi bila shaka tutazidi kupevuka!
 


Gombesugu,
Profesa Ibrahim Lipumba na chama chake cha CUF wakiambiwa wafuasi wao wengi ni Waunguja, Wapemba na Waswahili hawakasiriki! lakini hembu mwambie Jokakuu na Mbowe kuwa Chadema kina wafuasi wengi wa Chaga na baadhi! ya Wambulu uone utakavyotukanwa!
 

Wild Card,

Mie nafurahi kufanya mjadala na wewe ila pale ghafla unapoghadhibika na kuja na lugha za kejeli.

Historia wala si katili.

Si hiyo umeona tunawataja wazee wetu na kuwarehemu.
Leo nimeweka hapa habari za ''Mole,'' Idd Faiz Mafongo,
Rashid Ali Meli, Mwalimu Kihere...

Mnawasoma na kujua historia zao.

Wala wazee wetu hawakuishia 1952.

Walipigania uhuru hadi ukapatikana 1961.
 
Kadogoo,
Nilikuambia usikose kutembelea Greco Roman Museum iko Alexandria.

Shekh Mohamed Said,

Nashukuru Shekh wangu kwa kunikumbusha ila bado nakumbuka sehemu nyingi tu ulizonijulisha hapo kabla na nimeziandika ktk notebok yangu na inshaallah nikipata wasaa ntatembelea.
Kwa kweli Shekh wewe ni hazina yetu hapa JF kila nikiona post yako humu nazidi kupata faraja kuwa leo nachota ILM!
Alla ndie mlipaji we tenda wema wende zako usingoje shukrani za akina Yericko naona sasa karudi na viapo vya Jaa!
Al jumaa karim Shekh!
 
GOMBESUGU,
nimefurahi umenikumbusha Home na vitumbua vya Waswahili! bado niko Madrasa za cairo najifunza nahau na historia ya ulimwengu wa Kiislamu na utamaduni wake!
Nikirudi home nitakujulisha inshaallah!

Kadogoo,

Ndugu yangu wewe mwenyewe unajua Marwadhi yangu umenitajia vitumbua umenitamanisha.

Vitambua vya mayai ya kienyeji vipoe kidogo na chai ya maziwa ya ngamia walaahi hatari.

Cc.. gombesugu,
 
Last edited by a moderator:

Mohamed Said,

Usiwadanganye wanajamvi na watz kwa ujumla,

WAASI WOTE hawakuionja pepo ya UHURU!

Nakujuza kuwa sio kweli kuwa hao unaowaita ni "wazee wako" walikwenda sambamba na speed ya Julius Nyerere mpaka 1961,

Shehe Hassan bin Amir, Shehe Takadir, Waikela na wengine hawakushuhudia hata sherehe za uhuru,

Waasi hao walianza chokochoko baada ya uchaguzi wa 1953 wakiongozwa na Abdul Syke, na ilipofika 1958 katika uchaguzi wa kura tatu ndipo sasa kundi hilo lilipoanza rasmi kuendesha uasi wao waziwazi, wakitoka katika siasa za kizalendo na kwakuwa wengi wao walikuwa ni waislamu waliingia misikitini kupandikiza chuki zao!

Chuki hizo, ndizo mlizorithi vijukuu vyao ukiwemo wewe Mohamed Said na wenzio na kuanza kulichochea taifa kwa chuki za kidini hivi sasa!
 


Mimi naamini wazi siku zote swadaka inaanzia nyumbani.

Kwa mwenye akili timamu hawezi hata siku moja kuona kwake kuna mgogoro na yeye anakimbilia kusuluhisha kwa jirani. Huo ni upunguani kama si uhayawani wa hali ya juu sana.

Binafsi kila siku nimekuwa namlaumu Nyerere kuwa ni msomi mzuri na alipenda wananchi wake wasome. NI VIPI YEYE ALISHINDWA KUSOMESHA WATOTO WAKE HATA MMOJA KUFIKIA JAPO FIRST DEGREE.

NI VIPI ALIKIMBILIA KULETA UHURU NCHI NYINGINE WAKTI KWAKE HUKO MKOA MARA MAUAJI KILA SIKU.

Je huyu kweli ni wa maendeleo kweli.

Kumbukeni madhila yote pamoja na umasikini wa nchi yenu yeye ndio chanzo. Alipenda sana kusifiwa na wazungu na kudharau nyumba /chi yake.

Hakuwa mzalendo hata kidogo kwa nchi yake.
 
Kadogoo,

..wanaosema hivyo wanataka CDM kionekane chama chenye malengo ya kikabila[kichaga,kimbulu].

..kama Prof.Lipumba anafurahi chama chake kikituhumiwa kwa mambo kama hayo basi hiyo inadhihirisha kwamba huyu msomi huko kwenye siasa ana "buz-buz" tu.

cc😡gombesugu, Nguruvi3, Mag3, Ritz, Wickama
 
Last edited by a moderator:


Ritz,

Hakika ulipomtaja tu Almarhum Sheikh Mohamed Ayoub umenikumbusha dua yake hii kila wakti alikuwa akipenda kuisoma.
Allah humma as'aluka ziyaddatan fi diin, wa barkatan fil umr, wa swih'attan fil jasad, wa wasiatan fi rizq, wa taubatan kabla al maut,wa shahadatan indal maut, wa afwan indal hisaab, wa amaana minal adhab, wa naswiiban minal jannah, warzuqna nnadhara ila wajhikal kareem biramatika yaarhama r'ahimin.

Ni dua nzito sana al marhum akipenda kuomba kila wakti.

nami nawaombea hivyo na kumuombe Sheikh Allah ampe darja la juu katika janna.

Cc. Mohamed said, Ritz, Gombesugu, Big Show.

 


Yericko,
Mie sina sababu ya kudanganya wala sina hamaki kama
zako katika kuhadithia habari hizi.

Wala simtukani mtu.

Ninaeleza kile nikijuacho kama wewe ulivyoeleza fikra
zako hapa.

Wala mimi sitosema wewe unadanganya.
Hayo ndiyo uyajuayo na wewe una haki ya kuyaeleza.

Waamuzi wetu ni hawa wasomaji ambao sasa wamefikia
185, 000.

Hawa wanatusoma na wataamua ni historia ipi wanaiona
ina ukweli.
 
Barubaru,

..sasa mambo ya kusomesha watoto yameingiaje hapa??

..nani amekwambia wanawe Mwalimu hawajasoma, na hakuna aliyefika chuo kikuu?

..hivi unafikiri kila mzazi anayependa mwanawe afike chuo kikuu, anafanikiwa ktk lengo hilo?

..mimi namshukuru Mwalimu kwamba wakati wa utawala wake elimu ya Tanzania ilikuwa ni ya viwango.

..ilikuwa ukihitimu form 4, 6, University, kweli unakuwa umewiva kulingana na daraja ulilofikia siyo kama miaka hii.

..kuhusu mapigano mkoani Mara, wakati wa Mwalimu hali haikuwa mbaya kama sasa hivi. wakati wa Mwalimu hali ya usalama ilikuwa nzuri kuliko sasa hivi.

..wewe mwenyewe si ulikimbia kwenu Znz kuja kuishi na kusoma huku Tanganyika?? Sasa hata kwa hilo humshukuru hata kidogo Mwalimu Nyerere??

cc😡Jasusi, Mag3, Wickama, Kadogoo, Ritz, Nguruvi3
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,
..haina tabu.
..sasa kama una data nyingine za uhakika zaidi ziweke hapa tuone kama ni tofauti na hicho kilichokuwa posted wikipedia.
JokaKuu, huyo gombesugu ni mtu wa ajabu sana; katika posti yake ya kwanza alisema hivi, nanukuu;

Nilimstahi sana gombesugu nilipomezea upotoshaji mkubwa ailoufanya hapo juu; amechanganya ama kwa makusudi au kwa kutojua chaguzi mbili zilizofanyika Zanzibar...ule wa mwaka 1961 na ule wa 1963. Kama amefanya kwa kutojua namsamehe lakini kama kafanya kwa mtindo ule ule wa mwalimu wake wa darsa, simwachi ng'o...kama nilivyowahi kusema, uongo ukiachwa na kurudiwa rudiwa mwishowe huwanasa wasiofanya jitihada za kuhoji na hapo ndipo mimi huamua kuliita koleo kwa jina lake.

Hapa chini narudia matokeo ya chaguzi zote mbili...katika uchaguzi wa mwaka 1961 ZPPP na ZNP zilikubaliana kuachiana nafasi wakati huo Abdulrahman Babu akiwa bado ni mwanachama wa ZPPP. Matokeo ya uchaguzi huo ni kama inavyooneana hapa chini;

Uchaguzi wa mwaka 1961

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD] [TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
Chama
[/TD]
[TD]
Kura
[/TD]
[TD]
%
[/TD]
[TD="width: 54"]
viti
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ASP
[/TD]
[TD="width: 78"]
45,172
[/TD]
[TD="width: 84"]
50.6%
[/TD]
[TD="width: 54"]
10
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ZPPP​
ZNP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
31,681​
12,411​
[/TD]
[TD="width: 84"]
35.3%​
13.9%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
13
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kuhama kwa Abdulrahman Babu na kuanzisha chama cha UMMA Party kulileta athari kubwa kwa chama ZPPP kwani kwenye uchaguzi wa mwaka 1963, UMMA Party waliiunga mkono ASP ingawa nayo ZNP iliweza kufaidika japo kidogo kama inavyoonekana hapa chini; (to tell the truth ZNP wa arab-dominated)

Uchaguzi wa mwaka 1963

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
Chama
[/TD]
[TD]
Kura
[/TD]
[TD]
%
[/TD]
[TD]
viti
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ASP
[/TD]
[TD="width: 78"]
87,085
[/TD]
[TD="width: 84"]
54.21%
[/TD]
[TD="width: 54"]
13
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ZNP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
47,950​
[/TD]
[TD="width: 84"]
29.85%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
12​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ZPPP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
25,609​
[/TD]
[TD="width: 84"]
15.84%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
6
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sasa shuhudieni hivi viroja; inakuwaje ASP ipate kura 87,085 lakini iambulie viti 13 huku ZNP iliyopata kura 47,950 ikizoa viti 12? Hizi ndizo kura eti zilizompa Sultani uhalali wa kuendelea kuvikalia kimabavu visiwa vya Zanzibar! Hizi kura zina tofauti gani na zile za Kaburu Voster wa Afrika Kusini au mlowezi Ian Smith wa Rhodesia? Yaani kura moja ya mwarabu ni sawa na kura mbili za mwafrika!
JokaKuu, mwambie Al Akhiy gombesugu kwamba madhila waliyofanyiwa ndugu zake hayafikii yale waliyofanyiwa waafrika wa Zanzibar chini ya wakoloni kutoka Oman kwa karne nenda rudi. Wakati akitafakari la kufanya mpe pia info kwamba si wote wanaompinga Mohamed Said ni Wakristo ama wana Chadema, ni kwamba tu adui wa adui yako mwombee heri; kwangu hakuna adui wa hili taifa langu ninalolipenda zaidi ya CCM.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…