Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Usikonde; Jaribisha hii, simu nyingi zinaipata, imem-cover JOHN OKELLO vizuri sana. Kuna mahali anazichapa kavukavu (hahahahahaha) Mimi nimeifurahia Good nite

Top 100 Goals of the Year 2012 - YouTube

cc Gombesugu

ha haa haaa!! naangalia fainal ya Copa del Rey, Real Madrid na Atletico Madrid huku nacheka peke yangu.

Hiyo YouTube ya Okello imerekodiwa mwaka 1964?

Hollywood Cinema wamekushikia akili... Ha haa haaa! unajua video za Okello zipo ngapi?

Jipange siyo unakurupuka.

Cc.. Barubaru, gombesugu,
 
Last edited by a moderator:
In the name of jah!
We trust!

Karibu kwenye ibada ya kirasta fari kesho mkuu,

Kanisa la RastaFarian lipo Kigamboni Mbutu, nyimbo bora kabisa za rege zitatumbuizwa kumsifu jah,

Pia weed ya kutosha itatolewa kama sehemu ya sakramenti kuu

Mkuu Yericko nashukuru sana ningependa tujumuike pamoja...
Jah bless you...
 
Wewe ndiyo MUONGO mkubwa nisome upya unielewe kuliko kuropoka ovyo.

Nimekuambia mie naishi Musoma? Nilichomjibu JokaKuu alisema bara wao wanajuana kwa makabila nikamwambia mie mbona sijaulizwa kabila langu.

Hivi bara ni kwenu Musoma tu? Maeneo mengine hakuna bara, kwa taarifa yako nimefika Mara na nikaulizwa kabila langu nikajibu mimi siyo mtu wa Mara.

Naona mipini imekuingia kisawasawa mpaka unaropoka ovyo.

Cc.. gombesugu,

RITZ; NIMEKUKUBALI MSHIKAJI; WEE BURUDIKA, MBONA NI MGENI WANGU? LAZIMA NIKUKARIMU. NDIO MWENDO MDUNDO HIVYO

https://www.youtube.com/watch?v=YXb7kdnDsEU

CC GOMBESUGU
 
Last edited by a moderator:
Jokakuu,
Hapa sio suala la tuhuma! ndio ukweli halisi usizibe masiko na kujifanya kipofu! Chadema kina wafuasi wengi wa Chagga na Wambulu! mimi naishi Moshi na naona hali halisi! Cuf kina wanachama wengi Zanzibar na mikoa ya Pwani huku bara! sijasema kuwa vyama hivi havina wanachama sehemu zingine za nchi! naona unataka kunibambikizia kauli ambayo si yangu!

Wala si ajabu kwa vyama hivi kuwa na wafuasi wengi maeneo hayo kwani hata Tanu ikianzishwa ilikubalika kwa haraka zaidi ktk jamii ya Kiislamu kuliko wenzao Wakristo ndio maana Wazee wapigania uhuru wakamkaribisha Mwalimu Nyerere kujiunga na harakati za kupigania uhuru ili kuongeza wigo na kuifanya Tanu iwe ya kitaifa zaidi kuliko kionekane ni chama cha Wazee wanywa gahwa tu!

Jokakuu, sijasema Profesa Lipumba anafurahia Cuf kuhusishwa na Zanzibar na mikoa ya Pwani tu! la! Profesa kafanya kazi kubwa sana kuitangaza CUF kila kona ya nchi hii na kafanikiwa sana kuijenga CUF na pamoja na vita kali toka Chadema na wapinzani wengine CUF iliweza kuwa chama cha kitaifa na hata kufika mpaka Bukoba na kunyakuwa ubunge! sikuambii kichekesho cha kunyakua kiti cha Kigamboni dhidi ya Mzee KK!

Ninachosema Profesa ni tofauti na Jokakuu au Mbowe wanapoambiwa Chadema ni chama kinachoungwa mkono na Wachagga au Wambulu wengi au Wakristo wengi huwa mnakasirika na kutokwa na povu! sababu yake siijui!

Jokakuu, Profesa Ibrahim Haruna Lipumba ni msomi mahiri, mchapakazi, msafi kimaadili na mwenyekipaji cha uongozi ndio maana kila uchaguzi unapofika chama chake kinamchagua tena ingawaje yeye angependa wengine wagombee! kama ungependa kumjua Profesa niko tayari kukutumia CV yake uone jinsi ilivyonona! nakuomba mpe heshima yake maana watu kama hawa ni wachache sana ktk nchi yetu!
Kadogoo,

..U r not going to fool me na maneno matamu.

..mimi siyo Mchaga, lakini nafahamu vita wanayopigwa Wachaga, na kwamba kampeni za kuinasabisha CDM na Wachaga ni jitihada za kukiua chama hicho.

..hata CUF nao zilifanyika kila juhudi kukinasabisha chama hicho na Wapemba na Waislamu, na madhara ya kampeni hiyo sote tunayajua.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu wa Chuo,
nawewe umejiunga na dini inayoruhusu uvutaji wa midaharati! ndio maana ulikiri kuwa wewe ni Mkuu wa ....!!! haa, haa, haa.

Kadogoo
Mihadarati ni mirungi ambayo mimi situmii na huwa haivutwi
 
Last edited by a moderator:
Jasusi na Jokakuu; Huku sehemu zingine hawajui kuwa mapigano ya mkoa wa Mara sio kwamba makabila kama mabila wanachukiana. Suala ni raslimali na biashara zingine zisiwezo kuwekwa wazi. Kwa mfano wilayani tarime kuna mapigano yalichangiwa sana ama na wizi wa mifugo au kilimo cha bangi. Sasa kwa asiyejua ataona mambo mengine. Kuna wale WAONGO wenye kudanganya watu kama RITZ. Awali amesema yeye hajawahi hata siku moja kuulizwa kabila lake. Kisha kasema katembea sana Mkoa wa Mara na makabila kayataja VIZURI sana. Anasema huko watu WANATAMBUANA/KUJUANA KWA MAKABILA YAO. Tayari CONTRADICTION. Sio kwamba haelewi kwanini duniani kuna makabila na utaifa/mataifa, ANAJUA. Ila Mwongo utamjua. Kumbe hujawahi kuulizwa hata na watu wa Mara kabila lako ulipokuwa huko, sasa Agenda ni nini?
Wickama, unajua kuna watu ambao wapo tayari kuridhika na udanganyifu hata kama fikra zao hazikubaliani.

Jasusi #15050 kaweka dhahiri shahir kuhusu watoto wa Nyerere, sasa Barubaru aje akanushe kama si kweli.

Baada ya jitihada za kumshambulia Nyerere kwa masimulizi, ngano na mikoba kushindwa sasa wanamgeukia kuhusu watoto wake.
Tumesikia kuhusu Virago vya mwalimu, mtaa na chumba alichoishi. Tena tukatajiwa hata siku tumbo lilipochafuka!
Hizo zote ni hila na mbinu chafu walizofuzu kutoka kwa mzee kwa ubani wa ''kufyonza ilm''

Kuhusu mapigano ya wakurya, nimempa challenge moja tu. Kwamba, anitajie taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migongano! ninataka taifa moja tu.

Anasema Nyerere hakuwa mzalendo, basi kama ni hivyo taifa hili halijawahi kuwa na kiongozi mzalendo!
 
Nguruvi3 umechuja sana,umechooka na kunyong'onyea kabisaa,ungelog out kwa sasa na kubakia as a GUEST ungekuwa umejitendea haki sana...
Kila napokuona na bandiko lako nazid kuingiwa na mshangao wa hali ya juu,kimekusibu nini??
 
Last edited by a moderator:
JokaKuu,
Barubaru ni miongoni mwa wale ambao wanaamini ukisema uwongo mara kwa mara inageuka kuwa ukweli. Watoto wa Mwalimu, Andrew Nyerere alikuwa mwanajeshi, John alikuwa air force. Makongoro sote tunajua. Emi Magige ni engineer. Madaraka amesoma Canada, anayo M.A. Anna Nyerere anazo digrii mbili alisomea Canada. Sasa sijui anazungumzia watoto wa Mwalimu gani. Lakini tumeshamzoea huyu kwa kauli za uwongo. Na kuhusu mapigano ya Mara yameanza miaka kumi na sita iliyopita. Wakati wa Mwalimu Wakurya walikuwa wakiogopa sana kwani akisikia kuna chokochoko alikuwa anawasomba viongozi wote wa koo na kuwaweka likizo. Lakini tumeshamzoea Barubaru, na hatutachoka kumsahihisha na kumpa elimu.

Nashukuru sana mkuu kwakuamua kulijibu swali hili,

Niliamua kujiepusha nisimjibu lakini nimefurahishwa sana najinsi ulivyojibu kwa ufasaha kabisa!

Zaidi ya mara tatu huyu bwana Barubaru analirudia tena kwa dhihaka sana,

Kuna watu hapa huishi kwa hisia tu!

Asante sana mkuu!
 
Wickama, unajua kuna watu ambao wapo tayari kuridhika na udanganyifu hata kama fikra zao hazikubaliani.

Jasusi #15050 kaweka dhahiri shahir kuhusu watoto wa Nyerere, sasa Barubaru aje akanushe kama si kweli.

Baada ya jitihada za kumshambulia Nyerere kwa masimulizi, ngano na mikoba kushindwa sasa wanamgeukia kuhusu watoto wake.
Tumesikia kuhusu Virago vya mwalimu, mtaa na chumba alichoishi. Tena tukatajiwa hata siku tumbo lilipochafuka!
Hizo zote ni hila na mbinu chafu walizofuzu kutoka kwa mzee kwa ubani wa ''kufyonza ilm''

Kuhusu mapigano ya wakurya, nimempa challenge moja tu. Kwamba, anitajie taifa moja tu duniani ambalo jamii zake hazina migongano! ninataka taifa moja tu.

Anasema Nyerere hakuwa mzalendo, basi kama ni hivyo taifa hili halijawahi kuwa na kiongozi mzalendo!

Kwa sababu Musoma makabila wanauwana kwa kuchinjana unataka kulazimisha kila nchi zina ugomvi wa kikabali mie nakutajia kwa uchache nchi ambazo hazina migogoro ya kikabila.

1) Tuwalu

2) Nauru

3) Vatican

4) Brueni

5) Luxembourg

Kama hutaitaji zingine takutajia wewe umeita moja mie nimekupa tano.
 
Nguruvi; Shukran. Kwanza hata kama Nyerere asingefikisha watoto vyuo vikuu, what has this got to do with the liberation ya watu weusi wa Zenj waliokuwa wanaitwa WAKATA MAJI? au wanaambiwa watamke HALUA ili wajulikane kama ni wenyeji? (yaani neno HALUA ndio ID!!!!!)Waone watu wametulia, wanauwezo wa kunyanyasa wenzao utashangaa.
 
JokaKuu,

Wewe kwanza ulitakiwa ukemee matusi dhidi ya Dini zoote hapa Jamvini....unakumbuka vizuri jinsi nilipojiunga hapa Jamvini/JF jinsi Gwalihenzi alivyokua anamtukana Allah na Mtume wetu Mtukufu constantly for almost a week....na hakuna hata mmoja wenu alothubutu kukemea zaidi ya kuweka LIKE!?

.
gombesugu, sikupendezwa na lugha ya Gwalihenzi, lakini niwewe huyohuyo gombesugu uliyemuunga mkono mtukanaji mwingine aliyejiita Zali la Mentali aliyekuwa anashusha matusi ya nguoni dhidi ya Nyerere bila hata chembe ya aibu mpaka alipopigwa ban!Allah na mtume wana nguvu ya kujitetea na kutoa adhabu kwa Gwalihenzi! lakini Nyerere aliyetukanwa na Zali la Mentali kwa jina la kuutetea uislam atasaidiwa na nani? gombesugu ndugu yangu acha hiyo double standard.
 
Kwa sababu Musoma makabila wanauwana kwa kuchinjana unataka kulazimisha kila nchi zina ugomvi wa kikabali mie nakutajia kwa uchache nchi ambazo hazina migogoro ya kikabila.

1) Tuwalu

2) Nauru

3) Vatican

4) Brueni

5) Luxembourg

Kama hutaitaji zingine takutajia wewe umeita moja mie nimekupa tano.

Unajua maana ya nchi?

Vatican ni nchi?
 
JokaKuu, huyo gombesugu ni mtu wa ajabu sana; katika posti yake ya kwanza alisema hivi, nanukuu;

Nilimstahi sana gombesugu nilipomezea upotoshaji mkubwa ailoufanya hapo juu; amechanganya ama kwa makusudi au kwa kutojua chaguzi mbili zilizofanyika Zanzibar...ule wa mwaka 1961 na ule wa 1963. Kama amefanya kwa kutojua namsamehe lakini kama kafanya kwa mtindo ule ule wa mwalimu wake wa darsa, simwachi ng'o...kama nilivyowahi kusema, uongo ukiachwa na kurudiwa rudiwa mwishowe huwanasa wasiofanya jitihada za kuhoji na hapo ndipo mimi huamua kuliita koleo kwa jina lake.

Hapa chini narudia matokeo ya chaguzi zote mbili...katika uchaguzi wa mwaka 1961 ZPPP na ZNP zilikubaliana kuachiana nafasi wakati huo Abdulrahman Babu akiwa bado ni mwanachama wa ZPPP. Matokeo ya uchaguzi huo ni kama inavyooneana hapa chini;

Uchaguzi wa mwaka 1961

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
Chama
[/TD]
[TD]
Kura
[/TD]
[TD]
%
[/TD]
[TD]
viti
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ASP
[/TD]
[TD]
45,172
[/TD]
[TD]
50.6%
[/TD]
[TD]
10
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ZPPP

ZNP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
31,681

12,411​
[/TD]
[TD="width: 84"]
35.3%

13.9%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
13
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Kuhama kwa Abdulrahman Babu na kuanzisha chama cha UMMA Party kulileta athari kubwa kwa chama ZPPP kwani kwenye uchaguzi wa mwaka 1963, UMMA Party waliiunga mkono ASP ingawa nayo ZNP iliweza kufaidika japo kidogo kama inavyoonekana hapa chini; (to tell the truth ZNP wa arab-dominated)

Uchaguzi wa mwaka 1963

[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
Chama
[/TD]
[TD]
Kura
[/TD]
[TD]
%
[/TD]
[TD]
viti
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
ASP
[/TD]
[TD="width: 78"]
87,085
[/TD]
[TD="width: 84"]
54.21%
[/TD]
[TD="width: 54"]
13
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ZNP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
47,950​
[/TD]
[TD="width: 84"]
29.85%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
12​
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
ZPPP​
[/TD]
[TD="width: 78"]
25,609​
[/TD]
[TD="width: 84"]
15.84%​
[/TD]
[TD="width: 54"]
6
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sasa shuhudieni hivi viroja; inakuwaje ASP ipate kura 87,085 lakini iambulie viti 13 huku ZNP iliyopata kura 47,950 ikizoa viti 12? Hizi ndizo kura eti zilizompa Sultani uhalali wa kuendelea kuvikalia kimabavu visiwa vya Zanzibar! Hizi kura zina tofauti gani na zile za Kaburu Voster wa Afrika Kusini au mlowezi Ian Smith wa Rhodesia? Yaani kura moja ya mwarabu ni sawa na kura mbili za mwafrika!
JokaKuu, mwambie Al Akhiy gombesugu kwamba madhila waliyofanyiwa ndugu zake hayafikii yale waliyofanyiwa waafrika wa Zanzibar chini ya wakoloni kutoka Oman kwa karne nenda rudi. Wakati akitafakari la kufanya mpe pia info kwamba si wote wanaompinga Mohamed Said ni Wakristo ama wana Chadema, ni kwamba tu adui wa adui yako mwombee heri; kwangu hakuna adui wa hili taifa langu ninalolipenda zaidi ya CCM.

Muheshimiwa Mag3,

Nashukuru kwa kunitumia salaam kupitia kwa ndugu yetu JokaKuu,nami nimekuja mwenyewe ili tuamkuane uzuri.

Kwa kifupi hiyo Historia ya Zanzibar nami pia naijua kwa kina na kiundani mno kwa minajil ya uwezo nilojaaliwa nao. Japo hii haina maana yakuwa ati wewe nawe hujui kitu,hasha mwandani wangu!

Tatizo ni yakuwa tuna mitazamo tafauti,ambalo pia ni jambo jema sana khasa kitaaluma.

Lakini tatizo jingine linipalo dhiki na madhila mengi,ni yakuwa nakuhisi wewe ndugu yangu Mag3 ni Mbaguzi wa rangi. Jambo ambalo ni hatari na khasara kwa Taifa letu changa.

Hayo majedwali yako hapo juu mimi binafsi na wewe ndugu yangu twajua yakuwa hizo informations/statistics ni fake na ni upotoshwaji wa Historia mkubwa mno!

Lakini napenda fursa kwa leo nirejee kiduchu kwenye huo ubaguzi wako wa rangi. Hivi Mag3 na wenzio woote hapa jamvini tangia lini mmeanza kuwa na Imani,huruma,majonzi,empathy,sympathy,sikitiko na labda pia kufikia kilio cha "ndugu zenu WaZanzibary Weusi"!? Halafu hizi definitions zenu za "Arabs","Africans","Bantu","Comorians" na mengineyo mengi,ndio mwanzo wa machochezi na kuhatarisha amani ya nchi.

Kuna baadhi ya Thread humu ndani nimeona ati huyo Mwanakijiji,amefikia hadi ya kujipa dhamana na authority ati ya kujua ni kiwango gani cha senti,hao WaZanzibary walipwe ili watolewe kwenye muungano!? Yaani imefikia huyo Mwanakijiji anajifanya yeye ni Fiscal Activist na kupangia Taifa/WaZanzibary kiasi gani cha senti wapewe ili waondoshe "gubu lao" kwa WaTanganyika!? Ama kweli hapa JF pana viroja vingi mno!

Ndo maana mimi binafsi,huwa nakuoneni yakuwa wengi wenu ni Wazandik tu. Yaani mnakuwa upande wa WaZanzibary pale tu inapo-suit matakwa na vigezo vyenu vya kibaguzi!? Sisi watu wa Madrassa hiyo tunaita Fitnatil Al Maaarifa.

Haya si ndo mambo mlokua mkimfanyia kebehi Sheikh Mohammed hapa jamvini,alipokua akitaja baadhi ya Makabila ya wenye mji/Wazee wetu hapo Mzizizma!?

Kama nilivywahi kunena hapo awali,haya majambo ya Race Issue ni very complex subject. Inalazim muwe waangalifu japo kiduchu,khasa mnapokua kwenye Public Forum kama hapa.

Mimi nina personal experience kutokana na family background yangu,kwa hiyo nazungumza kitu ninachokifahamu kwa undani na khatari zake kwenye Family au Taifa letu.

Nipo huku nje ya nchi kwa miaka mingi mno,tangia nakaribia "Alamatu'l Bulugh". Na nimetembea pahala na nchi nyingi mno kutokana na kibarua/Taaluma yangu. Nimekutana na watu na Historia nyingi zisizo mipaka na nimeona athari nyingi saana zitokanazo na huo ubaguzi wa rangi na ukabila ulokuingia kichwani.

Nilialikwa kupitia hapa kibaruani pangu,kwenye zile sherehe za ule "Uhuru wa South Sudan". Yaani nilitokwa na machozi mengi. Niliona vituko na mambo mengi kwa zile siku chache nilizokuwapo pale. Nilithibitisha zaidi jinsi gani Wazungu/Wakoloni walivyo mahiri na mastadi kwenye kutumia "Government machines" zao,influences na massive contacts walizonazo...ili kuendeleza madhila kutugombanisha WaAfrika,na wao wakiendela kuchota hizo rasilimali zilizopo hapo. Hii nayo pia ni topic ndefu mno,na bila ya shaka wewe mwenzangu itakuwa waijua uzuri zaidi yangu kutokana na huo umri wako ulowahi kukutajia hapa jamvini!?

Kwa kumalizia napenda kama kipata fursa japo kiduchu,rejea baadhi ya bayana zangu za awali khasa ile niliyokua nikijadiliana na ndugu yangu Nyambala,na nilijaribu kuweka tahadhari kwa Taifa letu WaTanzania,kwa kutumia kigezo/mfano wa nchi ya Sudan.

Nakuheshimu saana ndugu yangu,na pia napenda kuchukua fursa hii kukupa mwaliko rasmi katika Thread yetu mimi na ndugu yangu JokaKuu itakapokua tayari. Itahusu na kunyambua kiundani Nyerere na Mozambique,walakin tumekubaliana yakuwa ndani yake tutaweka na vikorombwezo vingi,khasa hiyo khabari ya Race Relation/Issue.

Lazim leo ninene hapa barazani;yaani kuna wakti nafikira kama siku tukijaaliwa kukutana popote pale basi hata mimi pia waweza kuniona au kuniita yakuwa sio MTanzania/MTanganyika, khasa kutokana na hizo definitions zenu za urangi na Makabila. Jana nilikua nawasomea wanangu/wajukuu zako ambao ni viduchu mno khadith za kulalia/bed time reading. Basi ghafla nikakukumbuka wewe Babu yao Mag3,je utakubali kuwa wao nao pia ni WaAfrika/WaTanzania siku ukiwaona/wakija kukuamkua!?

Kaa chini kwa utuvu ufikirie haya majambo kwa kina...huna haja ya kujilazimisha kujibu kwa pupa na zogo. Tumia busara nyingi ulonazo kwa utaratibu na madhubuti.

Insha Allah tuendelee na mnakasha,na nakutakia w'end njema.

Ahsnata.

Cc;Ritz
 
gombesugu, sikupendezwa na lugha ya Gwalihenzi, lakini niwewe huyohuyo gombesugu uliyemuunga mkono mtukanaji mwingine aliyejiita Zali la Mentali aliyekuwa anashusha matusi ya nguoni dhidi ya Nyerere bila hata chembe ya aibu mpaka alipopigwa ban!Allah na mtume wana nguvu ya kujitetea na kutoa adhabu kwa Gwalihenzi! lakini Nyerere aliyetukanwa na Zali la Mentali kwa jina la kuutetea uislam atasaidiwa na nani? gombesugu ndugu yangu acha hiyo double standard.

Maulaga,

Naomba uonyeshe hapa hadhwaran,pahala gani nilipompa LIKE huyo "mtukanaji". Au umechanganya yale majibizano ya kisiasa na hoja dhidi ya Nyerere na matusi!?

Tafadhali,mimi niko karibu mno na huyo Nyerere kuliko unavyofikiri na namtetea huku nje na kumlindia hishma yake kila kukicha kwa niyajuayo mema alofanza na nilikua nakubaliana nae. Kuna vitu mambo mengine/facts nijuazo sitaweza asilan kuyaweka hapa jamvini hata iweje. Kama vile asemavyo Sheikh Mohammed,yakuwa hawa ni Wazee wetu na wajibu wetu kuwastiri.

Kipata fursa kiduchu pitia bayana zangu za awali kwa Ihsan yako ndugu yangu Maulaga.

Kwa kifupi kwa hapa jamvini,zaidi ya huyo Jasusi labda na Andrew Nyerere ambae sijamuona kuchangia tangia nimefika hapa;basi hakuna mwengine ambae anaweza kunishinda kwa kumjua na ukaribu nilokua nae huyo Nyerere wako.

Hicho ni kwa kifupi tu ndugu yangu,na nimependa mno jinsi ulivyonikanya nami natumai utafurahia majibu yangu kwako.

Ahsanta na tuendelee nam mnakasha.
 
Back
Top Bottom