JokaKuu, huyo
gombesugu ni mtu wa ajabu sana; katika posti yake ya kwanza alisema hivi, nanukuu;
Nilimstahi sana
gombesugu nilipomezea upotoshaji mkubwa ailoufanya hapo juu; amechanganya ama kwa makusudi au kwa kutojua chaguzi mbili zilizofanyika Zanzibar...ule wa mwaka
1961 na ule wa
1963. Kama amefanya kwa kutojua namsamehe lakini kama kafanya kwa mtindo ule ule wa mwalimu wake wa darsa, simwachi ng'o...kama nilivyowahi kusema, uongo ukiachwa na kurudiwa rudiwa mwishowe huwanasa wasiofanya jitihada za kuhoji na hapo ndipo mimi huamua kuliita koleo kwa jina lake.
Hapa chini narudia matokeo ya chaguzi zote mbili...katika uchaguzi wa mwaka 1961
ZPPP na
ZNP zilikubaliana kuachiana nafasi wakati huo Abdulrahman Babu akiwa bado ni mwanachama wa
ZPPP. Matokeo ya uchaguzi huo ni kama inavyooneana hapa chini;
Uchaguzi wa mwaka 1961
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[/TR]
[TR]
[TD][TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD="width: 78"]
[/TD]
[TD="width: 84"]
[/TD]
[TD="width: 54"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Kuhama kwa Abdulrahman Babu na kuanzisha chama cha UMMA Party kulileta athari kubwa kwa chama
ZPPP kwani kwenye uchaguzi wa mwaka
1963, UMMA Party waliiunga mkono
ASP ingawa nayo
ZNP iliweza kufaidika japo kidogo kama inavyoonekana hapa chini; (to tell the truth
ZNP wa
arab-dominated)
Uchaguzi wa mwaka 1963
[TABLE="class: MsoTableGrid"]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[TD]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
[/TD]
[TD="width: 78"]
[/TD]
[TD="width: 84"]
[/TD]
[TD="width: 54"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
[/TD]
[TD="width: 78"]
[/TD]
[TD="width: 84"]
[/TD]
[TD="width: 54"]
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 79"]
[/TD]
[TD="width: 78"]
[/TD]
[TD="width: 84"]
[/TD]
[TD="width: 54"]
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Sasa shuhudieni hivi viroja; inakuwaje
ASP ipate kura
87,085 lakini iambulie viti
13 huku
ZNP iliyopata kura
47,950 ikizoa viti
12? Hizi ndizo kura eti zilizompa Sultani uhalali wa kuendelea kuvikalia kimabavu visiwa vya Zanzibar! Hizi kura zina tofauti gani na zile za
Kaburu Voster wa Afrika Kusini au mlowezi
Ian Smith wa Rhodesia? Yaani kura moja ya mwarabu ni sawa na kura mbili za mwafrika!
JokaKuu, mwambie Al Akhiy
gombesugu kwamba madhila waliyofanyiwa ndugu zake hayafikii yale waliyofanyiwa waafrika wa Zanzibar chini ya wakoloni kutoka Oman kwa karne nenda rudi. Wakati akitafakari la kufanya mpe pia
info kwamba si wote wanaompinga Mohamed Said ni Wakristo ama wana Chadema, ni kwamba tu adui wa adui yako mwombee heri; kwangu hakuna adui wa hili taifa langu ninalolipenda zaidi ya
CCM.
Muheshimiwa Mag3,
Nashukuru kwa kunitumia salaam kupitia kwa ndugu yetu
JokaKuu,nami nimekuja mwenyewe ili tuamkuane uzuri.
Kwa kifupi hiyo
Historia ya Zanzibar nami pia naijua kwa kina na kiundani mno kwa minajil ya uwezo nilojaaliwa nao. Japo hii haina maana yakuwa ati wewe nawe hujui kitu,hasha mwandani wangu!
Tatizo ni yakuwa tuna mitazamo tafauti,ambalo pia ni jambo jema sana khasa
kitaaluma.
Lakini tatizo jingine linipalo
dhiki na madhila mengi,ni yakuwa nakuhisi wewe ndugu yangu
Mag3 ni Mbaguzi wa rangi. Jambo ambalo ni hatari na khasara kwa
Taifa letu changa.
Hayo majedwali yako hapo juu mimi binafsi na wewe ndugu yangu twajua yakuwa hizo
informations/statistics ni fake na ni upotoshwaji wa Historia mkubwa mno!
Lakini napenda fursa kwa leo nirejee kiduchu kwenye huo
ubaguzi wako wa rangi. Hivi
Mag3 na wenzio woote hapa jamvini tangia lini mmeanza kuwa na Imani,huruma,majonzi,empathy,sympathy,sikitiko na labda pia kufikia kilio cha
"ndugu zenu WaZanzibary Weusi"!? Halafu hizi definitions zenu za
"Arabs","Africans","Bantu","Comorians" na mengineyo mengi,ndio mwanzo wa machochezi na kuhatarisha amani ya nchi.
Kuna baadhi ya
Thread humu ndani nimeona ati huyo
Mwanakijiji,amefikia hadi ya kujipa
dhamana na authority ati ya kujua ni kiwango gani cha senti,hao
WaZanzibary walipwe ili
watolewe kwenye muungano!? Yaani imefikia huyo Mwanakijiji anajifanya yeye ni
Fiscal Activist na kupangia
Taifa/WaZanzibary kiasi gani cha senti wapewe ili waondoshe
"gubu lao" kwa
WaTanganyika!? Ama kweli hapa JF pana viroja vingi mno!
Ndo maana mimi binafsi,huwa nakuoneni yakuwa wengi wenu ni
Wazandik tu. Yaani mnakuwa upande wa
WaZanzibary pale tu inapo-suit
matakwa na vigezo vyenu vya kibaguzi!? Sisi watu wa Madrassa hiyo tunaita
Fitnatil Al Maaarifa.
Haya si ndo mambo mlokua mkimfanyia kebehi
Sheikh Mohammed hapa jamvini,alipokua akitaja baadhi ya Makabila ya wenye mji/
Wazee wetu hapo
Mzizizma!?
Kama nilivywahi kunena hapo awali,haya majambo ya
Race Issue ni
very complex subject. Inalazim muwe waangalifu japo kiduchu,khasa mnapokua kwenye
Public Forum kama hapa.
Mimi nina
personal experience kutokana na family background yangu,kwa hiyo nazungumza kitu ninachokifahamu kwa undani na khatari zake kwenye Family au
Taifa letu.
Nipo huku nje ya nchi kwa miaka mingi mno,tangia nakaribia
"Alamatu'l Bulugh". Na nimetembea pahala na nchi nyingi mno kutokana na kibarua/Taaluma yangu. Nimekutana na watu na
Historia nyingi zisizo mipaka na nimeona athari nyingi saana zitokanazo na huo
ubaguzi wa rangi na ukabila ulokuingia kichwani.
Nilialikwa kupitia hapa kibaruani pangu,kwenye zile sherehe za ule
"Uhuru wa South Sudan". Yaani nilitokwa na machozi mengi. Niliona vituko na mambo mengi kwa zile siku chache nilizokuwapo pale. Nilithibitisha zaidi jinsi gani Wazungu/Wakoloni walivyo mahiri na mastadi kwenye kutumia
"Government machines" zao
,influences na
massive contacts walizonazo...ili kuendeleza madhila kutugombanisha
WaAfrika,na wao wakiendela kuchota hizo rasilimali zilizopo hapo. Hii nayo pia ni topic ndefu mno,na bila ya shaka wewe mwenzangu itakuwa waijua uzuri zaidi yangu kutokana na huo
umri wako ulowahi kukutajia hapa
jamvini!?
Kwa kumalizia napenda kama kipata fursa japo kiduchu,rejea baadhi ya
bayana zangu za awali khasa ile niliyokua nikijadiliana na ndugu yangu
Nyambala,na nilijaribu kuweka tahadhari kwa Taifa letu
WaTanzania,kwa kutumia kigezo/mfano wa nchi ya
Sudan.
Nakuheshimu saana ndugu yangu,na pia napenda kuchukua fursa hii kukupa mwaliko rasmi katika
Thread yetu mimi na ndugu yangu
JokaKuu itakapokua tayari. Itahusu na kunyambua kiundani
Nyerere na Mozambique,walakin tumekubaliana yakuwa ndani yake tutaweka na
vikorombwezo vingi,khasa hiyo khabari ya
Race Relation/Issue.
Lazim leo ninene hapa barazani;yaani kuna wakti nafikira kama siku tukijaaliwa kukutana popote pale basi hata mimi pia waweza kuniona au kuniita yakuwa
sio MTanzania/MTanganyika, khasa kutokana na hizo
definitions zenu za urangi na Makabila. Jana nilikua nawasomea wanangu/wajukuu zako ambao ni viduchu mno khadith za kulalia/bed time reading. Basi ghafla nikakukumbuka wewe Babu yao
Mag3,je utakubali kuwa wao nao pia ni WaAfrika/WaTanzania siku ukiwaona/wakija kukuamkua!?
Kaa chini kwa utuvu ufikirie haya majambo kwa kina...huna haja ya kujilazimisha kujibu kwa pupa na zogo. Tumia busara nyingi ulonazo kwa utaratibu na madhubuti.
Insha Allah tuendelee na mnakasha,na nakutakia w'end njema.
Ahsnata.
Cc;Ritz