Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Wickama,
Mtemvu hakupinga kujikomboa kutoka ukoloni.

"..........Mwaka wa 1960 kwenye mwezi wa tisa [Septemba] kama hivi, walitolewa vijana wawili kati ya Zuberi Mtemvu na Chipaka, kuja eneo la Wete, Pemba, kuja kufanya kampeni. Hawa walichukuliwa na chama cha Zanzibar Nationalist Party (ZNP) kuja kufanya kampeni ili kuonekana chama cha TANU kibaya. Zuberi Mtemvu alisema mnachokifata si chama cha haki, mnafikiri ule msikiti mkubwa ulojengwa Tanga msikiti, lakini si msikiti ule wanasali Waislamu na Wakristo. Kwa hivyo kama mnafuata TANU mmepotea ndugu zetuni, wa visiwani. Nyinyi ni Washirazi, waumini, leo mnaweza kuungana na chama dhaifu kama TANU ambapo kiongozi wao hana maadili ya Kiislamu"

Kwaheri Uhuru...pg 54

Good nite
 

Vema sana,

Nitajibu kwakifupi kulingana na maswali yako yalivyo mkuu!

1) Hakukuwa na uhusiano wowote wa siri nje yakuwa muamini wake, alilitambua kuwa kanisa ni taasisi ya kiroho yenye kusaidia maendeleo ya jamii husika!


2) HAPANA, hakuwa na upendeleo wowote kwa wakristu ama waislamu, aliingili na kusuluhisha popote kati yapo patokeapo mgogoro wa kidini, rejea mapigano 1980 baada ya uchaguzi wa TAG chini ya Mch Moses Kurola na Mch Emanuel Razaro, serikali iliingilia kati kwakuunda turu huru ya kimahaka na kumaliza ugomvi ule, hatimae ikazaliwa EAGT ya Mchungaji Moses Kurola!

Vivyo hivyo rejea mgogoro wa waislamu mwaka 1964 ulimalizika kwakuzaa BAKWATA, zote hizo ni juhudi za serikali na hekima za Hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere!


3)Inatosha dhahiri shahiri kuonyesha kuwa Mwalimu alikuwa mzalendo wa kweli, haihitaji mtu kuwa na elimu ya PHd kubaini hilo!
 

Huo ni msumari kwa radicals hawa
 

Barubaru,
Nina hakika. Anna alikuwa Canada 1974-1977. Nilimtembelea mara kadhaa pale. Madaraka vile vile alisoma Canada lakini sina hakika jina la chuo. Na si kila mtu aliyesomea nje alishindwa kujiunga UDSM. Mimi nimesomea nje wakati kaka zangu wawili walisoma UDSM. Barubaru, wewe ni msomi, tena nasikia una Phd. Sasa kwa watu kama wewe mnategemewa kuwa wabobeaji kwenye utafiti na ukileta habari hapa ziwe za uhakika siyo zile za kijiweni . Na kuhusu tv ya Mwalimu hayo unayosema ungo mkubwa nyumbani kwake ni hadithi nyingine ya kijiweni. TV ya Mwalimu aliyokuwa nayo alinunuliwa na balozi Bomani baada ya ziara yake hapa Marekani 1977. Kuna video nyingi zilirekodiwa na vipindi mbalimbali wakati wa ziara hiyo na Mzee Bomani akasuggest kununua TV hiyo pamoja na video hizo ambazo zilikuwa kwenye American system NTSC. Haikuwa tv ya kuangalia matangazo hata kidogo. Haya, lete stori nyingine ya kijiweni kuhusu Mwalimu nikuweke sawa.
 

Jasusi,

Samahani lakini hivi Yericko Nyerere, huwa naye ni ndugu yenu mwanafamilia.
 
Last edited by a moderator:
kwi!kwi!kwi! Ritz, wewe mchokozi kweli kweli. Tuzungumzie mambo ya Mukendo Street, Musoma.

Safari hii nataka kuja Maryland nikija takutafuka kaka...bado unafunga mzuzu...ha haa haaa.
 

Aksante ndugu yangu kwa majibu musharab kabisa haya.. Lipo jambo moja zaidi ambalo ningependa kujua., tafadhali usinichoke.
Aliyeongoza Mapinduzi ya Zanzibar alikua ni Field Marshal John Okelo. Karume hakutajwa popote wakati wa masimulizi ya siku ya mapinduzi. Kuna pahala nalipata kusoma kuwa, Karume alikuwa mtanganyika na alipandikizwa tu Zanzibar.. Naomba ufafanuzi juu ya hili mzee mwenzangu...
 
Jasusi, it's all spinning. Huko nyuma Barubaru alisema hakuna mtoto aliye na degree wala kumaliza highschool. Akadai Nyerere amesomesha wengine akaacha wake. Sasa anakuja na suala la kwanini hakusomesha UDSM.
Kumbuka huyu ndiye yule alisema Nyerere alitelekeza wanawe.

Ninashangaa sana, unaposema ana PhD! Mkuu Barubaru hebu itendee heshima club ya PhD, hadithi za mitaani achia akina Al-akhyi. Come forward cogently and boldly. The street rumors belong to the street!

Narudia tena baada ya kushindwa kumshusha, kumdhalilisha Nyerere kuanzia Virago na chumba, senti za vitoweo na ''uwakuja'' wake, Nyerere stands tall. Sasa wanageukia watoto wao.

Kuhusu TV, hebu niulize hizi zilizopo zinaisaidia vipi jamii, maana wakati wa Nyerere literacy level ilikuwa above 85 sasa hivi pamoja na TV sijui tupo wapi. Swali ni je, TV ilikuwa muhimu kuliko bwawa la Mtera, Nyumba ya mungu au Kidatu!!
Sina jibu

By the way siku hizi watoto wa viongozi ndio wanasoma huko nje, vipi la Nyerere lionekana kama balaa! kisa Nyerere.
Chuki ni maradhi mabaya sana!
 
Naam na znz yenu yenye maendeleo itapatikana mkiwa nje ya muungano!

Kwabahati mbaya hilo halitatokea kwasababu ninyi ndio waumini wa muungano wa Uswiss, Hong Kong na China n.k. Hamtaki kuondoka katika muungano mkifahamu wazi kuwa hayo ni maumivu tena makali.

Kuhusu wznz kupigwa, hilo halina taabu. Hakuna sababu za wnz kuandamana kudai znz.
Wanaweza kuipata znz bila tusi achilia mbali kurusha jiwe.

Ni hivi, mwambieni makamu wa rais aliyepatikana kwasababu ya uzanzibar, mawaziri waliopatikana kwasababu ya uzanzibar(na si weledi au usomi), wabunge walioko Dodoma kwasababu ni wzn, maafisa wanaofanyakazi katika serikali ya muungano kwasababu ni wznz, wanafunzi wanaosoma bure kwasababu ni waznz na wafanyabiashara, wote kwa pamoja waondoke warudi kuijenga znz yenye maendeleo. Hadi hapo muungano utakuwa umekufa.

Si hapo tu, washawishini wajumbe 15 wa tume ya warioba waondoke katika tume.
Mshaurini Maalim arudishe kitambulisho alichochukua Karimjee.
Fungeni biashara na mawasiliano na Tanganyika. Muungano utakuwa umekufa

Ima hayo ni magumu, nendeni katika baraza la wawakilishi mkiwa na mswada wa kuvunja muungano.
Kabla wabunge wa Dodoma hawajaondoka kurudi kwao, watoe mswada wa kuvunja muungano

Ima hawataki basi anayeng'ang'ania si Mtanganyika aliyeko nyumbani kwakwe ni mzanzibar aliyekuja kuhemea huku akiacha nchi ya neema na yenye maendeleo

Hadi hapo unajitaji maandamano ?

Kuhusu maendeleo, takwimu zipo wazi kuwa katika muungano mnachangia pato la billion 24.
Mapato ya znz kwa mwaka ni 120 billioni, bajeti ni 630 billioni, jilize hilo pengo anaziba nani?

Hapo ukae ukitambua kuwa hakuna bajeti ya ulinzi na usalama, elimu ya juu, na mishahara ya SMZ.

Mna hiari muondoke mkatafute maendeleo, hakuna anayewazuia. Ule muda wa kulia na kupewa pipi sasa basi.

Jaji Warioba, hawa watu wana 50% katika tume! tunakutahadhirisha kuwa kila jambo liangaliwe kwa 50% kama wanahitaji msaada wa kuwa nasi. Rasimu ya kumbeba mznz itakufa kabla ya kusomwa
 
Juu ya Karume

Ninachofahamu kwa kabila ni Mnyasa,alikuwa mfanyakazi wa bandari (kuli) na alikuwa mwanachama mtiifu wa ASP,

Kuingia kwake madarakani kulitokana na ASP chama kilichoungwa mkono wazalendo wengi napia kiliungwa mkono na Tanganyika (Julius Nyerere),

Karume hakuingia mtaani kupambana na Sultan, Siku ya mapinduzi yeye alikuwa Dar,

Karume alikabidhiwa madaraka mizi sita baada ya mapinduzi, hilo lilitimia kutokana na juhudi za Julius Nyerere kumshawishi Okello akabidhi madaraka kwa chama kinachoungwa mkono na wengi, kumbuka Okello hakuwa na chama chochote cha siasa!
 



Tunataka source ya hizo takwimu zako,
Hatupo hapa kuangalia mapambo yako ya majedwali bila kutupa references na sources za statistics zako,
Tuna akili zetu timamu sisi...
 


Hilo la TV nalo pia mwakanusha??
Kuleta hoja inayohusu kusomesha watoto wake nako pia ni kumdhalilisha?
Hata angekuwa nani,kuja kututambia na uwongo mwingi kwa kutumia advantage ya ushamba na ujinga wetu pale tunapoondokewa na ujinga plus ushamba wetu kwanin tusiwmone ni CHAKUBIMBI??

Kuna kosa hapo??
 
Tunataka source ya hizo takwimu zako,
Hatupo hapa kuangalia mapambo yako ya majedwali bila kutupa references na sources za statistics zako,
Tuna akili zetu timamu sisi...

Mjadala huu ni mkubwa kwako mkuu,

Mpaka dakika hii ikiwa ni siku ya nne takwimu hizo zinatiririka hapa lakini bado hujajua wapi chanzo?


Hahaahaa waombe msaada wenzio akina Ritz na GumbeSugu si unaona wapo kimya juu ya kisu hicho?

Wameujua ukweli!
 


Mjadala huu ni kweli unaweza kuwa ni mkubwa kwangu,na ndio kwa maana nipo hapa masaa 24 na nimehamishia dinning room,bathroom,sitting room hadi na godoro langu pia ili nikae hapa nimsome Moh Said namimi niweze somesha wajukuu zangu hapo mbeleni insha allah.,

Tujaalie ni kweli hayo unayoyasema,mimi pia sijaona hoja zako ni zipi hadi sasa,uchochez wa moh said hujatuonesha,nasaba yako kwa julius hujatuonesha,hueleweki kipi sasa unachokisimamia,,

Haitoshi ukaja na mauza uza yako ya kitabu cha ugaid,and thanks god umeshayatupa jalalani sasa baada ya kuona kwamba hayana tija yoyote,watu wapo hapa kwa heshima ya Moh Said young boy yericko...

Na tunazid kukushaur ya kwamba status na heshima hupatikana kwa kujitoa kweli kweli,kujitoa kusaka elimu na maarifa kwa udi na uvumba,pamoja na hekima,na haiapatikana kwa ujanja ujanja wa kudandika nasaba za watu...

Mimi sijaona source kwenye hilo bandiko la Mag3,kama ipo na sijaiona ndio uiweke au unijuze...

Mwisho Julius kambarage nyerere hakuacha mtoto anaeitwa Yericko hata Jasusi analifaham hilo...

Acha kujipendekeza pendekeza...
 

Hata Dr Slaa ana data zake anasema alishinda uchaguzi.

Hayo matokeo ya Mag3 wala hakuna jipya uki-google utayapata matokeo zaidi ya mia wewe mwenyewe utaamua uchukue yapi ambao yanakupendeza.

Nikikuuliza unamjua mkuu wa tume ya uchaguzi Zanzibar aliyetangaza hayo matokeo ututajie hata jina hujui. Kazi yako kufuata mkumbo tu.
 

Pole sana,

Sitashughulishwa na porojo zingine bali upate chanzo cha takwimu hizo tu!

Haya msome mnywa kahawa mwenzio hapa chini,

Atakusaidia!

Hawezi kuweka source mie nafahaumu anapookoteza hizo data zake data hazina uhakika.
 


Hana lolote analolijua huyo,
Mauza uza yake ya kitabu cha ugaidi yameonekana yanachomwa moto huko Damponi TABATA...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…