Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kuna sehemu huko nyuma nilikwambia kuwa itendee haki jf,

Hivi wewe mwenyewe umesema wazi kuwa gogu inakupatia hizo takwimu za uchaguzi, sasa iweje upate takwimu za chaguzi hizo na kisha ushindwe kupata majina ya wenyeviti wa chaguzi hizo?

Lazima upevuke ndugu!

Kimsingi Qualification za mjadala huu, ndiomaana sometimes unapuuzwa na ukijibiwa basi mjibuji aliona hana kazi kwa mda ule!
 

Ni kweli mie mnywa kahawa tena ni kichwa cha madrassa.
 
Nitajitahidi kutafuta kwenye hifadhi za kumbukumbu,

Mshume Kiyate inafahamika wazi kuwa alikuwa rafiki wa karibu na mzee, nitajitahidi kupata picha zao pia.


Ha haa haaa, mimi na wewe nani wa kupuuzwa humu ukumbini.

Wanaukumbi hebu msomeni wenyewe huyu jamaa anajifanya mtoto wa Julius Kambarage.

Cc.. gombesugu, THE BIG SHOW, Kadogoo,
 
Last edited by a moderator:
Ha haa haaa, mimi na wewe nani wa kupuuzwa humu ukumbini.

Wanaukumbi hebu msomeni wenyewe huyu jamaa anajifanya mtoto wa Julius Kambarage.

Cc.. gombesugu, THE BIG SHOW, Kadogoo,

Nini chaajabu kwako hapo?

Ninaposema Mwalimu Nyerere ni Mzee wangu, Joseph Warioba ni mzeee wangu, Paul Boman ni Mzee wangu, Joseph Butiku ni Mzee wangu, Abdul Sykes ni Mzee wangu, Kingunge Ngombalemwiru ni Mzee wangu, unaelewa nini hapo?

Usiwe mkubwa wa mwili na umri tu lakini akili za kijiko cha chai!

Mohamed Said anaposema Shehe Hassan Bin Amir ni mzee wake unaelewaje?

Wewe unaposema Abdul Sykes ni mzee wako unaelewa maana yake!

Nilishasema huna Qualification za kujadiliana na mimi, nakustahi kwakuwa ni binadamu unaepumua!

Kimsingi nakupuuza! Na sitakujibu kwa upuuzi wako huo!
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed Said nimefarijika sana hili haujalikanusha,wapo baadhi ya wanajamvi wasiotaka kushughulisha akili zao walitaka Nyerere awachekee Masheikh waliotaka kuyumbisha usalama wa nchi.

Yericko,
Huyo anazungumza ni Mohamed Omari Mkwawa.

Dk. Ghassany kaweka yote kama yalivyokuwa ili
historia ikae sawa kwa wasomaji wa kitabu chake.
 
Last edited by a moderator:

Swadakta,

Wanakumbi mtaamua wenyewe hapa tena Yericko anajinasibisha kuwa Julius Kambarage ndiyo baba yake walikuwa wakiishi pamoja.

Siku zote ukiwa muongo unapoteza kumbukumbu, tawaletea kisa kingine cha huyu dogo analazimisha nasaba.

Anaenda mbali zaidi kuwa Nyerere alikuwa akimuadithia habari za marafiki zake kina Mshume Kiyate kwenye viwanja vya Ikulu, ha haa haa teh teh!
gombesugu, Jasusi,
 
Last edited by a moderator:

Bado unazidi kuonyesha ulivyo na upeo finyu,

Watanzania mamia wamekuwa wakimiminika Nyumbani kwa Hayati Mwalimu Nyerere, najiuliza sana, Niini kinachokustua nikisema nitakwenda kupata picha hiyo?

Hhivi wewe huna uwezo wa kwenda Butiam nyumbani kwa Hayati Mzee Nyerere na ukapata data yoyote unayoitafuta tena data yenyewe ni picha?

Mimi kila mwaka huwa nakwenda kuhiji pale kaburini, ukitaka wasiliana na mimi twende wote mwezi wa sita kesho kutwa tu!



Pole sana! Naishia hapo juu ya hili sitakujibu
 
Last edited by a moderator:

Bora ukimbie maana mipini ikikuwa inakuja tena kupitia mabandiko yako mwenyewe unanadhani watu wajinga humu unaweza kuongea pumba zako bila kuhojiwa.

Mbona haujawaambia wanaukumbi habari za Mshume Kiyate, Nyerere alikuwa akikuadithia wapi kwenye viwanja vya Ikulu au Butiama.

Yericko usikimbie mnakasha watu wanataka utupe habari za mzee wako.

Cc.. Ben Saanane,
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere,

Dawa siyo kukimbia jibu hoja wewe ndiyo umejinasibisha na Nyerere kama mzee wako mbona unakuwa tena mkali ukihojiwa.

Mbona Jasusi, tunamuhoji mambo ya ndani ya Nyerere pamoja na familia yake anatoa ushirikiano kama mwanafamilia.

Wewe unataka kumuhoji Mohamed Said, kuhusu wazee wake anakujibu pamoja na kutoa kejeli kuwa wazee wa vibarazani wanywa kahawa na watu wa madrassa.

Wewe tumekuomba tu kwa faida ya wanaukumbi tujuze Nyerere alikuwa anakuadithia wapi habari za Mshume Kiyate.

cc.. gombesugu, Jasusi,
 
Last edited by a moderator:
Mzee Mohamed Said nimefarijika sana hili haujalikanusha,wapo baadhi ya wanajamvi wasiotaka kushughulisha akili zao walitaka Nyerere awachekee Masheikh waliotaka kuyumbisha usalama wa nchi.

Ngongo,
Tatizo la Baraza la Wazee wa TANU na Nyerere halina
uhusiano hata chembe na usalama wa nchi.

Ilikuwa ni hofu tu kuwa Waislam wakiwa na nguvu kama
ile waloonyesha wakati wa kupigania uhuru ukristo utakuwa
mashakani.

Waislam walimpenda sana Nyerere.
Isome historia niliyoandika hili liko wazi kabisa.
 

Hapo swadakta.. Narudi kidogo kwenye uhuru wa Tanganyika., Hili pia ningependa na Mzee wetu Mohamed Said alitolee ufafanuzi. Katika mojawapo ya maandiko ya wanazuoni nguli wa Zanzibar niliyopata kuyapitia kwa umakini mkubwa yanaelezea namna ambavyo Baba wa Taifa, akiwa katika TANU alivoanza kuwa na mgogoro na baadhi ya wazee wa kiislamu.

Anaeleza kuwa, mara tu baada ya Uhuru, mwalimu alikutana kwa siri na baadhi ya viongozi wa juu wa kanisa katoliki, hasa maaskofu na waliliweka Taifa la Tanganyika chini ya usimamizi wa Bikira Maria, na hii ikafanywa kuwa formal kabisa.

Baadae alipowaomba kuzikabidhi shule za makanisa chini ya Serikali haikuwa vigumu kwa kuwa tayari walikuwa "wanazungumza lugha moja". Tukio hili la kuliweka taifa chini ya Bikira Maria lilifanywa kwa siri kubwa, lakini kwakuwa ndani ya Serikali walikuwepo viongozi wa kiislamu kama vile akina Mzee wetu Mkwawa (R.I.P), Zilivuja na kuwafikia baadhi ya masheikh wakubwa Tanganyika hasa wa Tabora na Dsm..

Hawa wasingekubali kunyamaza, na huo ukawa mwanzo wa maelewano tete kati ya mwalimu na wenzake wa TANU, hasa wale waislamu. June 1962, masheikh hawa waliamua kuonana na Mwalimu ili kuweka wazi madukuduku yao.. Hata hvo, yasemekana mwalimu alikuwa na baadhi ya masheikh ambao "wangemtetea popote hata kupinga imani zao", na hata katika mazungumzo hayo, walisimama kidete kumtetea mwalimu.

Sina shaka hili pia lilihusishwa na uundwaji wa BAKWATA, na waliotengeneza BAKWATA ya mwanzo walikua hawa ambao waliiva katika chungu kimoja na Mwalimu, wakati wengine walipinga vikali uanzishwaji wake.


Hebu wanazuoni wangu naombeni mnichambulie vizuri hii habari ya Bikira Maria kufanywa msimamizi wa Taifa na mgogoro kati ya mwalimu na masheikh., pana ukweli ama ni porojo za kwenye gahawa?
Kwako
Yericko.
Mohamed Said,
Ritz,
Nguruvi na wengine wote...
 
Tunataka source ya hizo takwimu zako,
Hatupo hapa kuangalia mapambo yako ya majedwali bila kutupa references na sources za statistics zako,
Tuna akili zetu timamu sisi...
Upo sahihi mkuu, lakini naomba umshauri ndugu yetu Ritz naye atuletee source ya taarifa hii nyeti;
 

Maulaga,

Salaam sana ndugu yangu.

Nashukuru mno kwa ustaarabu na maneno yako mema ulotumia. Huo ndo ubin-Adam na weledi wa hali ya juu.

Nami sitagusa wala kuongeza lolote katika hayo ulonena,zaidi ya kukwambia yakuwa nimefarijika mno kutambuana na muungwana kama wewe hapa jamvini.

Kabla ya kukuacha,takupa usia kiduchu. Hayo ulonena yakuwa "macho ya mwana-Adam hayana uwezo wa kumwonyesha yanyuma huyo alonayo". Hili ni kweli nami nakuunga mkono. Lakini taratibu hapa jamvini, pana jamaa waweza kutumia neno hilo hilo kukudhihaki yakuwa ati hujapitia au hujasoma mnakasha woote,sasa yanini kukurupuka au kuchangia hoja!...wenyewe wana msemo wao ati "umedandia Train kwa mbele" nafikiri!?

Nimekupa usia huo kwani mimi binafsi yalinikuta wakti najiunga na kuanza kuchangia hapa jamvini!

Nakutakia siku njema ndugu yangu natuendelee na mnakasha,kwa hishma na mahaba.

Shukran.
 
Jasusi,
Ninashangaa sana, unaposema ana PhD! Mkuu Barubaru hebu itendee heshima club ya PhD, hadithi za mitaani achia akina Al-akhyi. Come forward cogently and boldly. The street rumors belong to the street!

Muheshimiwa Nguruvi3,

Salaam.

Unafahamu nini maana ya Al Akhiy kwa utuvu,na kama unafahamu mbona unafanya tashtit zisizo maana "ndugu yangu wa Kicheba"!?

Napenda kukufahamisha yakuwa Al Akhiy Barubaru,siye pekee mwenye hiyo PhD hapa jamvini(kama PhD ndio kigezo chako cha kumuhishimu mtu na kumuona wa maana au msomi zaidi).

Hata hao "ma-Al Akhiy" unaowadharau na kuwabeza nao pia wanazo hizo "PhD zako" unazoziabudu.

Kama kuitendea haki "Club ya PhD",mbona unamuonea Barubaru peke yake!?

Kwani hujapata khabari kuna watu wa "Club" hiyohiyo ya PhD,wananyang'anya Wake za watu na kuwafanza Vimada wao...je ushawahi kuwaambia lolote!? Kumbuka udhaifu ni kwa mwana-Adam yeyote.

Hivi karibuni takujibu ile hoja yako,nisamehe nimezongwa na vijishughuli kiduchu.

Nashukuru kwa kunisikiza.
 

Yericko Nyerere,

Naomba ufafanuzi japo kiduchu,hivi unafahamu nini maana ya neno "Kuli"!? Je pia unaweza kutofautisha vipi kati ya "Kuli" na "Hamali"!?

Kwa maelekezo yako hapo juu,je kila afanyae kazi Bandarini ni "Kuli"!?

Kwa "Historia" uliyofundishwa na unayoifahamu wewe,je Rais Karume alizaliwa wapi!?

Ahsanta kwa kunisikiza ndugu yangu.

Shukran.
 
Upo sahihi mkuu, lakini naomba umshauri ndugu yetu Ritz naye atuletee source ya taarifa hii nyeti;

Niwe radhi ndugu yangu maulaga, kwa kuchelewa kukujibu.

Source ya mipini hiyo imetoka kwa Mwalimu wetu wa historia Mohamed Said, pamoja na Masheikh na Wazee wetu ambao wengi wameishatangulia mbele ya haki mmoja wao tumemzika jana Ally Sykes.

Kama utapenda kufyonza Ilm zaidi bado wapo Wazee unaweza kumtafuta Mzee Abbas Sykes, Sheikh Bilal Waikela hawa wameishi zama hizo na Nyerere.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…