Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

historia ya wazee wenu mbona mnaongezeachumvi ya upotoshaji?
mara oo nyerere kafundishwa siasa na wazee wenu, mara kaenda sokoni hana hata senti akitaraji kupewa japo thumni yakununulia pilipili hoho sokoni, mara kafundishwa kuvaa na wazee wenu, mara hakujua kiswahili vizuri, ..............
mkuu Ritz umesahau hayo yote mliyasema?
 
Hivi kwako wewe GRADUATE ni nini mpaka mtu atimize vigezo gani? huwezi kusema Ibn Battuta siyo GRADUATE.

Ritz; Baada ya salamu; Kwangu mimi "u-graduate" ni kigezo tuu watu wamebuni ili kuhalalisha matumizi wa tija ya watu katika Nyanja Fulani. Mara nyingi haina uhusiano na Intelligent Quetient (IQ)-kama spelling ni sawa, ambayo haswa ndiyo tunu mtu anapewa na Muumba wake.

Kwa maana hiyo, mtu kuwa graduate (all levels)haina maana ndiye mbora na mwenye IQ kubwa kuwashinda wenzie. Ukipitia kwa mfano wale wagunduzi wa Cordoba-spain na hawa walioanzisha branch kabisa za mathematics (Aljebra) yote ni zawadi ya IQ. Au Wamisri wa kale walianzisha calendar ya siku 365/yr based on appearance ya stars, hii ni zawadi ya IQ. Babu anawapatanisha wajukuu waligombana na kuhasimiana huku wao ni Maprofessa mpaka wanamkubali kuwa babu hapa Kaongea, ni suala la IQ. Hii ndiyo muhimu. Lakini kwa vile ni vigumu kuwapima kikamilifi watu kwa hili ndio maana madaraja ya elimu yanatumiwa ambayo kimsingi mimi sikubaliani nayo, ila sijui MBADALA.
 

Jasusi,

Nakupa pole sana kwa kutaka kupotosha ukweli. Siku zote marubani wa Air force ni lazima wawe form six na sio form four nao walianzia cheo cha cadet sio private. Kwa zamani kujiunga jeshi ilikuwa hata darasa la saba alikuwa anakubaliwa lakin kwenye taaluma kama Urubani tena wa fighter lazima awe form six . Sasa yeye aliingia kwenye kozi hiyo wenzake wote wakiwa form six yeye form four je hapo napo unaona ni kawaida hiyo?
Canada wamekwenda wengi jeshini ambao wengine ni mafundi wa ndege ambao walikuwa kule Angus Ontario .

Lakin kubwa carleton kuna Kozi nyingi kuanzia certificate, diploma mpaka Ph.D. sasa be specific ni level gani kwani kwenye Degree hakuna jina lake.

Kwa uwadilifu wa Nyerere nilitegemea watoto wake wangepita katika proper channel kama wananchi wengine lakin ndio hivyo tena. Uadilifu wake upo wapi?. Jiulize aliwalipia mwenyewe au alitumia pesa za wananchi wake kusomesha watto wake kwa njia za mkato mkato?

mwisho watoto wangu wapo hapo Silver spring , mary land na insh'Allah Ijumaa mosi nitakuwa hapo likizo ya siku tatu.

Tumia facts katika kuandika kwako na sio hisia. Nimekuuliza vipi niku PM majina ya graduates wote wa Carleton kuanzia 1073 -1990 uona kama unayonena ni sahihi?
 


Sawa MS; Baada ya Salaam, At last utaona jinsi ambavyo inawakera watu kupata impression kuwa ONE family is being amplified juu ya Watanzania wengine. You are a good writer MS. No doubt. Lakini mzee MS umeruhusu sana prejudice in your sights. NINA UHAKIKA KAMA NYERERE wazazi wangeingia in this country kama Mamluki wa kwenda KUUA wahehe na wasambaa kule Lushoto, saa hizi your books zingekuwa zimejaa idadi (estimates) za hao ambao BABU au BABA yake Nyerere aliua huko kwenye ajira yake ya kuwauwa Watanganyika. But you have with caution just said wazazi wa Fulani waliingia kama MAMLUKI. Ukafanya stahiki ya heshima kwa familia husika ukaishia hapo. Lakini unapokuja kwa yule unayemchukia inabidi hata aliye mpa Matango siku Fulani iwe historia ya Kitaifa. Hutumii mizania ya HAKI. One guy whose family started its establishment with the blood of Tanganyikans on its hand (we know what mercenaries DO) is being elevated at the expense ya another person whose fault is to have a different faith other than yours.

No wonder you see reaction ya people like Zumbe, kwa vile THERE IS NO WAY ON EARTH DAR ALONE AS A CITY/TOWN WOULD HAVE WON INDEPENDENCE WITHOUT THE RESOURCES OF THE UP COUNTRY REGIONS, NO WAY. On the other hand ukiwajibu watu simply kuwa NA NYIE ANDIKENI WHILE YOU CHURN OUT MATERIALS WHICH RIDUCULE the very people who brought hope and joy in their distant lands, I find you to be too assuming. In fact you sound RUDE.
 

Intelligence Quotient~IQ.

Tuendelee na mnakasha hujue wa magharibi wanawachukuliwa watu kama Ibn Battuta siyo GRADUATE kutoka na elimu zao ukiangalia mtu kama Ibn Battuta alikuwepo miaka 1304 mpaka 1369 vitu alivyofanya ni vikubwa sana.

Umetaja University of Cordoba ni baadhi ya vyuo vilivyoleta mapinduzi ya elimu duniani wakati huo Ulaya na Marekani bado kuna giza kubwa la ujinga.

Kimsingi Islamic Scholar hawakubariki kwenye nchi za magharibi ingawa wao ndiyo wameleta elimu kubwa huko kwao.
 

Shariff Ritz,

Salaam.

Unajua mimi huwa sipendi malumbano yaso maana,nilishakuambia awali yakuwa hawa jamaa zako unawaweza wewe mwenyewe.

Nimeingia tu hapa ndo nakutana na huu mpini ulompiga nao jamaa wa rohoni!ahaha!! Yaani nimecheka pita kiasi!!

Huyo Mzee wa watu wa Kizaramo ati anakwenda kuvua akiwa na miaka 87!ahaha!! Hili jambo haliingii akilini asilan!

Sisi soote tunajua Wazee wetu khasa wa KiAfrika wanapofikia umri na miaka hiyo wanavyochoka bin taaban...halafu mtu huyohuyo ende akavue na akirejea awe Mufti na wakti huohuo awe ati anajishughulisha na shughuli za kisiasa!?ahaha!!

Halafu baada ya kufariki maskini,ghafula akafufuka na kuanza upya kujishughulisha na shughuli za kisiasa!?ahaha!! Nijuavyo mimi miujiza hiyo walikua wakifanya baadhi ya MaNabii tu!

Unajua mimi juzi pia nilipitia upya baadhi ya vitu hapa,na pia nikachungulia hiyo khabari kiduchu. Nilichofanza nikamwandikia kwa kistaarabu Yericko kumuuliza kama alikusudia Sheikh Hassan Bin Amir,sababu niliona hiyo miaka/umri hai-tally na yale maelezo tulopewa. Lakini nafikiri hakutambua maskini kwanini nilikua namdodosa vile! Matokeo yake akaniletea majibu fulani ya kifedhuli na huku akisisitiza hiyo khabari!?

Jaribu ku-imagine kama hiyo khabari au kosa hilo angelifanza Sheikh Mohammed Said;ungeona jinsi gani Nguruvi3 na ndugu yangu Mag3 shughuli yao ya kebehi na kashfa ingechukua atleast a week minimum Wallahi!

Nipa fursa kuna jamaa inanilazim kumnyooshea maneno japo kiduchu.

Haina neno tuendelee na mnakasha,ndo viroja vya Jamii Forum hivyo.

Ahsanta.

Cc;The Big Show,Nambokola,Sheikh Farid,Mag3,Nguruvi3
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Hakikisha safari hii, unapokuja na hii "khabari yako mpya" unaleta na vielelezo vya kutosha(sources zako,links,vitabu,barua ama chochote cha kusadikika kitaaluma). Maana tumechoka maneno matupu.

Au pia kama utaweza kututajia majina ya hao walokutuma kuleta uchafuzi na ufataani huo hapa jamvini.

Fuatisha mfano wa mwenzio Sheikh Mohammed said,japo mnamfanyia kebehi na tashtit,lakini mwenzenu atleast ana kitabu chake mkononi,kwa hiyo tunajua wapi pa kumuanzia.

Natumai utanifahamu ndugu yangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 

Ritz; Tatizo la ndugu zetu wa magharibi sio kukudhulumu sifa yako kwa sababu wewe sii dini yake. Tatizo lao ni UCHOYO wa KUGAWANA SIFA. Wanapenda KUPATA CREDIT WAO. Aliyempandisha mzungu wa kwanza Mt. Kilimanjaro ni Mchagga, yet utasikia, THE FIRST MAN TO CONQUER KILIMANJARO WAS ..... yule mchagga hatajwi. Mzungu aliyeona chanzo cha mto Nile infact alipelekwa na wenyeji, No name of Africans (utamuharibia credit), Vasco Da Gama aliongozwa pale Pangani kuwa ili afike India inabidi akaondokee Mombasa. Na jinsi ya kufika India akaelekezwa (no names of helpers, I.....discovered). Kuna mahali nilisoma (sikumbuki vizuri, lakini ilkuwa Ufaransa, wakati wa vita Fulani, kulikuwa na battalion ya kiafrika ambayo ilifanya kazi sana dhidi ya maadui (possibly Germans, not sure) hadi maadui ikabidi watimke. Lakini ilipofika sasa kuwa majeshi ya wakombozi yanaingia ule mji waliokuwa wanaupigania na kuufia, ile battalion ya akina MANGI ilipangwa mwisho. Nani ulaya ya wakati huo anataka kusikia credit za kukombolewa na akina Shemahonge???? Ni hulka Ritz, hawa jamaa hata angekuwa ustadh mwenzio, huenda bado ataficha tuu kuwa hiyo paper aliyotoa kwenye mhadhara wewe ulichangia. Waulize watanzania wanaofanya nao UTAFITI wanavyolizwa!!!!!!
 

WICKAMA,
nimekuelewa Mkuu, watoto wasihusishwe na madudu waliyofanya Baba zao uko sawa kabisa! ila kumjadili kiongozi kama Mwalimu kwa mazuri na mabaya yake sidhani kama nikosa! kwani ktk mjadala huo huenda pakapatikana fundisho litakalosaidia kutengeza pale walipoharibu ndio maana Waislamu wa nchi hii wanaitaka Serikali kuunda tume huru kuchunguza madai yao ya dhuluma walizofanyiwa tangu na utawala wa awamu ya kwanza mpaka leo! lakini la kusikitisha madai yao yamekuwa kichekesho mbele ya wa TZ wenzao hasa Wakristo wanaoitaka Serikali isikubali kusikiza madai ya Waislamu na la kushtua zaidi ni Serikali kukubali maoni na matakwa ya Wakristo mifano ipo mingi lakini mfano mmoja;

Baada ya mauaji kufanyika ktk Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998 chini ya Serikali ya Mkapa, Waislamu ktk baraza la Idi waliombwa na Rais Mkapa kuthibitisha madai yao kisayansi na alipopewa, majibu yake ni Serikali yake haiwezi kupuuza maoni ya Wakristo na madai ya Waislamu kuyatupa kapuni!


Kati ya mwaka 1993 na 1994 Padre Lwambano aliiamrisha Serikali ya Mwinyi kuwakamata wahubiri wa Kiislamu kwa kusema Yesu si Mungu na Waziri Lyatonga Mrema alitangaza vita dhidi ya Mashehe kwa kusema atawavua majoho na kuwapiga ngumi! muda mfupi baadae Shehe Kassim Bin Jumaa wa Msikiti wa Mtoro akakamatwa na kuwekwa kizuizini na kuachiwa akiwa kadhoofika na baadae kufariki!

La kusikitisha Mzee Mwinyi alisema dola iwashughulikie Waislamu na wengi baadhi yao waliishia Magerezani!
Sikuambii ni Mashehe wangapi waliwekwa kizuizini enzi za awamu ya kwanza na dhuluma walizofanyiwa hasa kupigwa marufuku jumuiya yao muhimu ya EAWMA! aidha sikuambii nini madhila wanayopata sasa Waislamu chini ya awamu hii ya Rais Kikwete!
Lakini bado ndugu zetu Wakristo wanaona dhuluma hii dhidi ya Waislamu ni uongo wa kutunga au mchezo wa kuigiza! na zaidi pale tunaposhuhudia vyama pinzani hasa Chadema kuungana na Serikali inapokuja issue ya Waislamu! mwenye macho haambiwi tazama! mwenye masikio na asikie!
 



Ritz; Wakati mwingine wanakubali. Soma hii stori

Institute of Arabic and Islamic Studies

Huyu astroner wamempa heshima ya kuita bonde Fulani kwenye uso wa Mwezi JINA LAKE
 
Mohamed Said,
Msiba wa Mzee Ally Sykes umetugusa sote tunaojua mchango wake ktk harakati za kupigania uhuru wa nchi hii! kwaniaba yangu binafsi kwanza nakupa pole wewe binafsi na kutufikishia ktk familia na ndugu wa Marehemu Allah awape subra na Imani! kwani hakika kwake tulitoka na kwake tutarejea!
Shekh MS, umetoa mchango muhimu ktk kufundisha historia ya mashujaa wetu na hasa waasisi wa vyama vilivyopigania uhuru wetu lakini cha kusikitisha kifo cha Mzee Ally Sykes pamoja na viongozi wote waandamizi na wastaafu kuhudhuria msibani, hakuna gazeti hata moja lililoripoti msiba na mazishi ya Mzee Ally Sykes?
 

Sheikh Farid,

Salaam Al Akhiy.

Umefanza jambo jema mno kuurejesha huu mpini hapa jamvini ili watu tujikumbushie japo kiduchu. Najua Sheikh Mohammed aliulezea kwa utuvu kwenye baadhi ya bayana zake za awali.

Kwenye family album ya Mzee wangu hizo pictures za hiyo safari zipo kadhaa. Nafikiri walipofika pale Beirut ndipo walipokutana/walipoungana na Sheikh Yahya Hussein na Bwana Ali Sykes katika harakati na shughuli hizo hizo.

Shukran.

Cc;Ritz,Sheikh Mohammed Said
 
Mkuu Ritz, kwanini tunawagawanya hawa wazee kwenye haya ya "wetu" na "wenu" ? mbona hawa wote walikuwa wazee wa Tanganyika na wao waliheshimiana sana wakapambana na mkoloni "with a common goal"!
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Salaam.

Tatizo lako ndugu yangu una maneno mengi mno,najua mwenyewe unapenda kuziita "hoja".

Inawezekana pia una machungu na stress nyingi mno ambazo umeamua kuja kuzimalizia hapa Jf/jamvini. Mimi binafsi nashukuru kwa sasa huo uhuru wa kusema chochote mtu atakacho hapo Tanzania umekua mwingi mno,tafauti na zile "enzi za Mwalimu".

Kwa sababu naamini mtu kama wewe kama ukiachiwa masaa mengi kuwa mitaani utasababisha madhara makubwa kwa Taifa,khasa kutokana na kauli zako zenye chuki na kuhamasisha maovu. Ndo maana nafarijika kila mara nikuonapo hapa online/jamvini.

Kwa sasa sitanena mengi. Unadai kumwita Sheikh Hassan Bin Amir Mnafiki au Msaliti sio tusi!?

Kuna wakti katika baadhi ya majibizano yenu Sheikh Mohammed Said,alikwambia yakuwa "hilo neno usirudie tena". Wewe ulikereka pita kiasi tena kwa hamaki nyingi mpaka ikanilazim niingilie kati.

Pia ulijaribu kusema yakuwa kwenu Tanga/Makorora hilo ni tusi kubwa mno!? Nilikwambia sio kweli na tukamalizana.

Sasa iweje unarejea tena hapa hapa jamvini,kuhalalisha matusi mengine tena kwa Kiongozi wa kidini,tena huku ukidai na kusisitiza kuwa hilo sio tusi!? Je unajua tafauti ya sifa na kashfa!?

Kwa kifupi kama wewe binafsi umeamua kuendelea kutukana,haina neno. Lakini mtu yeyote mwenye maarifa na akili zake timamu anajua kuwa hilo ni tusi kubwa mno.

Tuendelee na mnakasha ndugu yangu.

Shukran.

Cc;Ritz
 
Shukran kwa tathmini JokaKuu!

Nilivyoelewa mimi ni kuwa namba mbili mpaka nne zinarudi kwenye tatizo uliloliweka namba moja.
Tatizo ni lilelile tu halafu kutokea hapo mtu anaweza kutiririka.

Ninakubali kusahihishwa.
Sideeq,

..je, tumeelewana kwamba Znz ndiyo inainyonya Tgk??

..zaidi, tumekubaliana kwamba kutokana na dhuluma ya muungano dhidi yetu, wa-Tgk ndio tunaopaswa kumlaani Mwalimu Nyerere na siyo nyinyi wa-Zenj??

cc: Nguruvi3, Wickama
 
Last edited by a moderator:
Heee ! wenzangu yamekuwa hayo.

Mimi nimeuliza maswali mbona nashambuliwa kiasi hiki.
Tena imefikia mahali naitwa fataani, nimetumwa n.k. Hivi kwanini watu wanaghadhabu nami.
Yaani hata mahali nisipoingia mtu atatafuta upenyo apitishe jina langu ilimradi tu.

Gombesugu, Mohamed ndiye mwandishi na msomi pekee ninaye mfahamu anayefanya ''self quotation'' au reference.
Huko mimi sipo.

Haya tunayoongea hapa tuna ufahamu nayo. Kama tungekuwa hatujui tusingemvua Mohamed nguo, tukamfunga mikono na miguu kwa nguo hizo na hata kumchapa usoni na mtambara yake.

Wewe ulijua kuwa balozi hakuhutubia Bunge! Tulimuuliza akaingia na tarehe tukamchapa nazo usoni.
Sasa hivi amebaki na Mkoba wa Ibadan! FYI we have strong and wide background! Ninaiangalia dunia kwa mtazamo mpana siyo wa kipata au mfenesini! Gombesugu!

Kama unataka link n.k. tutoa, kwani si unataka link za jinsi gani Rukara alipata passport ya Tz.
Unataka tutaje hata ufuska na majina ya wahusika! ndivyo unataka?
Mimi nasitiri watu na kujisitiri, sipiti nikizungumzia vyumba vya watu na vitoweo hovyo barabarani, nina weledi.

Najua kinachowatia hasira ni sheikh Amir kuitwa Mnafiki na mfitini mkubwa.
Mimi nasema Amir ni mnafiki mkubwa sana nimeeleza sababu kwa kufanya quotation ya maneno ya Mohamed ili muamini zaidi. Nasema Bibi Titi alikuwa na uadilifu kuliko huyu mnafiki mkubwa anayeitwa sheikh.
Mnafiki huyu habri zake za kinafiki zinajulikana.

Nafahamu pia hasira ni kutokana na miba ya muungano, hasa kwa wznz! nawe unajua hilo kwahiyo sitegemei kusikia neno zuri kutoka kwako linalonihusu. Guess what, mimi spade naita spade sisemi ni big spoon!

Kama hakuna majibu ya maswali nitaleta link, subra yavuta heri
 

Muheshimiwa Nguruvi3,

Nakupenda mno ndugu yangu.

Lakini kutokana na hizo kauli zako, hivi sasa nahisi umepandwa na Shamrani. Kwa hiyo nakwacha kiduchu utuame/upumzike,halafu nitaendelea kukubana tena mbavu mpaka ucheue leo.

Leo nafanyia shughuli zangu hapa hapa nyumbani,kwa hiyo nina muda mzuri wa kuchungulia baadhi ya vitu hapa jamvini na huku nikipambana na wewe.

Shukran.
 
Mkuu Nguruvi3 hii habari nikiwahi kuisikia sikia bahati mbaya Mzee wangu wa Gerezani Mohamed Said hakuitia kwenye kitabu chake sijui kwani wakti suala la EAMWS kalizungumzia kwa undani sana ingawa pia kakwepa kuzungumzia sababu za kutimuliwa Kenya.

Mkuu wangu nasubiri darsa,usisahau kunimention nisijepitwa na uhondo.

Nakala Ritz gombesugu JokaKuu Mag3 zumbemkuu kwa taarifa...


 
Last edited by a moderator:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…