Muheshimiwa Nguruvi3,
Salaam.
Tatizo lako ndugu yangu una maneno mengi mno,najua mwenyewe unapenda kuziita "hoja".
Inawezekana pia una machungu na stress nyingi mno ambazo umeamua kuja kuzimalizia hapa Jf/jamvini.
Kwa sababu naamini mtu kama wewe kama ukiachiwa masaa mengi kuwa mitaani utasababisha madhara makubwa kwa Taifa,khasa kutokana na kauli zako zenye chuki na kuhamasisha maovu.
Ndo maana nafarijika kila mara nikuonapo hapa online/jamvini.
Unadai kumwita Sheikh Hassan Bin Amir Mnafiki au Msaliti sio tusi!?
Sasa iweje unarejea tena hapa hapa jamvini,kuhalalisha matusi mengine tena kwa Kiongozi wa kidini,tena huku ukidai na kusisitiza kuwa hilo sio tusi!? Je unajua tafauti ya sifa na kashfa!?
Kwa kifupi kama wewe binafsi umeamua kuendelea kutukana,haina neno. Lakini mtu yeyote mwenye maarifa na akili zake timamu anajua kuwa hilo ni tusi kubwa mno.Tuendelee na mnakasha ndugu yangu.
Shukran. Cc;Ritz
Gombesugu na Sheikh Farid.
Inaonekana neno msaliti na mnafiki kwa Sheikh Amir limewaudhi sana.
Pengine ni kwa kujua kuwa alikuwa kiongozi wa dini na pia siasa kwa waislam basi hapo yapo maudhi.
Msisahau kuwa alikuwa mufti wa Tanganyika pia.
Maneno hayo si matusi na ninazo sababu
1. Msaliti ni mtu aendae kinyume na wenzake au anayewauza wenzake au afanyae mambo nyuma ya migongo ya wenzie.
2. Mnafiki, ni yule anyetenda kinyume au anayelaghai wenzake kwa ghilaba ima kufarahisha au kuwaghilibu
Sheikh Amir ni mwanasiasa na kiongozi wa dini. Alipokuja Tanganyika aliona waislam wakiwa wamedhulumiwa kwa elimu na Wakoloni(ref Ziddy). Jitihada zake zilikuwa kutoa elimu. Katika kufanya hivyo alijikuta katika Political sub committee kama mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika Dar es Salaam(ref Mohamed).
Wajumbe wa sub committee alikuwepo Abdul Sykes ambaye siku moja kabla ya uchaguzi Anatogluo alisema wanampa uongozi mtu wasiyemjua na itakuwa vigumu kumuondoa Nyerere (Mohamed). Kwa mantiki yeye alikuwa miongoni wa walioamua kuhusu uongozi(Mohamed)
Issa Ziddy anaeleza kuwa Amir alikuwa na mchango katika uanzishaji wa Al-dawafia Islamiyya, Jamiya islamiyya fil Tanganyika, EAMWS.Kwa pamoja Mohamed na Ziddy wanamwelezea kama kiongozi wa dini na Mwanasiasa
Baada ya Uhuru Sheikh alipewa fursa na Nyerere ya kuwa katika baraza. Akakataa kuchukua nafasi hiyo.
Badala yake akaendeleza harakati zake za kisiasa misikitini.
Mohamed anasema akitoa darsa na Dawiya, hapo hapo anasema huyu alikuwa katika TAA sub polit comm!!!
Issa Ziddy anaeleza, baada ya kurudi safari ya Egypt iliyohusu chuo kikuu, Sheikh Amir alionywa kubadili mwenendo wa mawaidha yake ya kisiasa sheikh Commorian,ushahidi wa kuwa alikuwa anaendeleza siasa,tofsuti na utetezi wa Mohamed
Maandishi ya Mohamed yamekwepa kuongelea hoja ya Sheikh Amir kupewa fursa na Nyerere na kujikita zaidi ya kutimuliwa kwake tena kwa kusingizia kuundwa kwa EAMWS.
Kuvunjika kwa EAMWS kulianza na ufa Dar es Salaam kabla ya kuhamia Mikoani. Makundi ya Maulid yalikuwa ya Mnazi mmoja na Ilala. Kilichochagiza mtafaruku mikoani ni kutokana na matumizi mabaya ya fedha za EAMWS makao makuu!
Issa Ziddy ameonyesha kuwa kulikuwa na mgogoro wa kisiasa kati ya 'Sheikh Amir na mwanafunzi wake sheh Chaurembo kutokana na masuala ya siasa'. Huu pia ni ushahidi kuwa Amir alikuwa active politically akifanya kazi nyuma ya wanfunzi wake. Ni mgogoro huo pia ulioua jithada za kuanzisha chuo kikuu na wala si fitna ya Nyerere kama asemavyo Mohamed
Makundi yaliyojitenga yalipata nguvu za nje kwasababu tayari Sheikh Amir alikuwa anahubiri siasa na mikutano nje ya chama cha TANU.Makundi hayo yalichukizwa na siasa za chini chini nje ya zile za TANU walizozijua
Sasa kwanini ni msaliti!
Alipaswa kuwa ndani ya system ili kuzuia matatizo(kama yalikuwepo). Alitakiwa awe karibu sana na ''adui'' zake ili afahamu mambo ya kuunusuru uislam kama basi ilidhaniwa hivyo. Hakufanya hivyo na kukidhi maana ya neno msaliti.
Ni mnafiki kwasababu alikataa kufanya siasa huku akiendeleza siasa hizo hizo misikitini kwa kuwatumia watu aliowaita wanafunzi wake.
Kitendo cha kumkatalia Nyerere nafasi alizopewa huku akihubiri siasa kama alivyonywa na Comorian (Ziddy) ni cha kinafiki na kinakidhi maana ya neno hilo.
Kwanini watu wanachukia kusikia msaliti na mnafiki?
Watu wanaochukia kusikia hayo ni wasaliti na wanafiki pia.
Kuna post katika nyuzi hii wametukanwa viongozi wa dini na wazee.
Mathalan,Mufti wa BAKWATA ana elimu gani mbumbu mkubwa, zumbukuku n.k.
Sheikh Hemed bin Jumaa alikuwa Kibaraka wa serikali, Shehe wa Tanga alikuwa Punda wa mapinduzi,
Nyerere laanatulah alikuwa mnafiki, msaliti, habithi na fidhuli.
Wazee hao wakitukanwa ilionekana kama maneno matamu na wala si matusi, vipi leo Sheikh Amir akiambiwa maneno yale yale aliyoambiwa mufti wa BAKWATA, Hemed bin Jumaa, Nyerere ionekane kama ametusiwa?
Hapo hakuna unafiki kweli!!!
Ni mwendo ule ule wa kusema Sheikh Amir alikuwa walii kwahiyo anapaswa kupewa hishma ya darja.
Kama waislam wameamua hivyo haina lalam, kuhoji au kuuliza. Ni kwa mujibu wa imani yao na wanahaki hiyo.
Vipi basi Wakatoliki wakisema Nyerere ni saint wao, waislam hao hao(baadhi) washupalie na kulihusisha na siasa?
Je, ni halali kusema Sheikh Amir aliyekuwa TAA sub pol comm alipewa Uwalii kwasababu ya harakati zake za kisiasa kabla na baada ya uhuru! Endapo sivyo kwanini Nyerere aonekane kupewa u-saint kwasababu ya siasa za kuungamiza Uislam
Nimalizie kwa kusema, haki uliyo nayo mtu ndiyo aliyo nayo mwingine.
Hakuna haki ya kutukana wazee wengine na batwil ya kutukanwa baadhi yao.
Tukishakubaliana hivyo, sasa tuombe radhi sote na kwa wote, la sivyo msaliti na mnafiki si matusi! tunayatumia sote kila siku na hakuna namna ya kuchagua wapi litumike na wapi linawajaza watu upepo.
Pamoja na kashfa na kejeli zako Gombesugu mimi nshakuswamehe maana sisi ni viumbe dhaifu na hatuna utimilifu.
Upanga wangu una makali sehemu mbili, wenzangu makali yenu sehemu moja na hapo ndipo tunapohitilifiana.