Nashukuru kwa majibu mazuri. Nadhani kama walikuwepo wazee wenye dini tofauti, na walipigania uhuru kwa pamoja, vyema ni kusema wapo wazee waliopigania uhuru na wanapaswa kuwekwa katika kumbukumbu za nchi hii. Nadhani kama wameandikwa Wakristo halafu Waislam wakaachwa, hapo kutakuwa na walakini! Vinginevyo wizara husika (Habari na Utamaduni) inapaswa kuratibu zoezi zima la kuweka historia sawa. Kama watu binafsi wakiachwa kuandika wenyewe bila uratibu kutakuwa na bias nyingi sana!
Mwanasharia Iron,
Labda sijakufahamu uzuri naomba kiduchu unijuze upya ndugu yangu;yaani unamaanisha yakuwa pasiwe na ruksa asilan ya
ma-Scholar au
Watafiti wa Historia khasa binafsi kufanza shughuli zao,mpaka wasimamiwe au kupewa vibali na
Serikali au
Wizara husika!?
Jingine nasikia mbona tayari
"Historia" nyingine ilishaandikwa na Chuo cha Kivukoni-
Historia ya Kivukoni.
Nafikiri alichofanya
Mtafiti,MwanaHistoria/Scholar Sheikh Mohammed Said,ni kuleta ile
"second opinion"(niwie radhi hapa nakukopa lugha yako ya Kisharia kiduchu) na kutufaidisha na upande mwingine wa Historia hiyohiyo kwa faida ya soote kama
WaTanzania.
Labda kingine nilichogundua kwa uchechefu wangu,kiletacho rabsha hapa jamvini ni vile
Sheikh Mohammed Said kuwataja hao
Wazee wa Mzizima/Wazee wetu kwa wingi kwenye kitabu chake.
Lakini "kosa" hili la
"jinai",nafikiri hata
Nyerere pia alifanza na ndipo inalazim tumlaumu yeye Nyerere. Kwa mfano bila ya kwenda mbali mno au kurejea nyuma saana ya mnakasha,embu chungulia hiyo hotuba ya huyo
Nyerere mwenyewe hapo anasema nini!?
Naona kawataja Wazee wetu wengi tu,tena baadhi yao kwa majina khasa Wazee wa
D'Salaam,Pwani na Bagamoyo. Nafikiri la muhimu tujiulize,je wakti huo Neyere alikua hakumbuki au hajui baadhi ya sehemu nyingine za Tanganyika au michango ya Wazee wa huko!? Sasa kwanini hakutaka au alishindwa hata kumtaja huyo
Mzee Mbowe,
Chief Marealle au
Marangu na Machame yake!? Mimi binafsi nahisi
Nyerere ndo aloanzisha na kuchochea hii
"vurugu" tulonayo sasa hapa jamvini!?
Kwanini kwenye hiyo hotuba yake ya
"kuaga",hakuona umuhimu wa kutaja hizo sehemu au Mikoa mingine ya
Tanganyika kwa majina kama alivyotilia mkazo na kutaja Wazee wa Mzizima tena wengi wao wakiwa ni
WaIslamu!?
Wallahi,mimi binafsi Nyerere kanistaajabisha,maana hata
Tarime/Mara hakuitaja!? Sasa ndugu yangu,unapohoji kwanini Kaskazini haikutajwa na wale Wazee wa kule pia hawakutajwa,nakusikia kwa kina hicho kilio chako...lakini haya kaanza kufanya Nyerere mwenyewe "
Baba Wa Taifa".
Nafikiri labda,vitu au viswali viduchu kama hivi nijiulizavyo mimi,na pia labda na ukweli mwingine wa
Kitaaluma/Historia ndo ulomfanya au kumshawishi
Sheikh Mohammed Said aanze utafiti wake wa kina na hatimae kuandika hiki kitabu chake. Na sisi leo tupo hapa jamvini,kujaribu kukifanyia minyambulisho ya kina na huku yeye mwenyewe akitusaidia na kutuelekeza pale tunapokwama!?
Pia ni muhimu zaidi,tukumbuke yakuwa
Sheikh Mohammed Said,amejitahidi mno kutaja na kutujulisha maeneo na wanaharakati kutoka takriban kila pembe ya Tanganyika. Wakiwemo Wakristo,Waislamu,wasokua na Dini na wengineo.
Nilitaka kukupa mifano mingi mno ya nchi za nje lakini ni vyema turejee hapo hapo nyumbani.
Hivi leo hii ni watu wangapi hapo
Tanzania wajuao au hata kuthamini mchango wa Mwenyekiti wa
Chadema kule
Mchambawima au Mkanyageni kulinganisha na mchango wa
Padri Dr. Slaa!?...kuna viongozi wangapi wa vijiji au kata wa Chadema huko
Mbozi,Kwa Nkonje,Mandera,Iramba,Mafia,Kibinda na kwingineko,ambao wanajikalif maisha yao na family zao na labda kupata misukosuko kadhaa,je mnazisikia khabari zao kila mara au kwa kina hapo
D'Salaam ukilinganisha na khabari za
Muheshimiwa Mbowe au Padri Dr. Slaa au Viongozi wengine wa level ileile ndogo waliopo hapo
D'Salaam!?
Kwa hiyo nafikiri hao Wazee wa Mzizzima ambao takriban woote walikua ni
WaIslamu, ilichowasaidia pia ni ile
political/Historical connection ya wao kuwepo/kuzaliwa pale D'Salaam. Jambo ambalo ni muhimu mno kihistoria.
Huwezi kufananisha asilan zile harakati na zogo lilikuwapo pale Mzizima wakti huo labda na
Kigombe,Nkasi, Handeni au Hedaru!?
kama kuna zogo au harakati za
Wazee wao huko,ni vyema kuzijua kwa kina hili halina ubishi asilan...lakini itakua ni rare occasions kwa kufafanisha na yalokua yakitokea au kufanyika hapo Mzizizma!?
Sheikh Mohammed na
ZumbeMkuu,washaanza kutoa mifano kadhaa. Nawewe ndugu yangu kumbe una mifano ya fadhila za
kina Mbowe kwa
Nyerere,tafadhali zimwage na tuzichambue kwa pamoja hapa
jamvini.
Labda na wengine wana mifano yao,pia itolewe. Halafu
,Yericko atachambua upi unafaa kuwa ndio harakati za kuchangia Uhuru au la! Maana mifano ya
Wazee wetu sisi ati anaikashifu japo Nyerere mwenyewe ilimkaa mno moyoni mpaka ikamlazim kwenye
"kuaga" aitamke hadhwarani.
Niwie radhi kwa uchechefu wangu.
Nakutakia W'end njema.
Ahsanta.
Cc;Ritz