Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Alhy Habiby gombesugu,

Nasoma bayana zako na miwani ya 3D.

Shariff Ritz,

Kuna Mwanajamvi mwenzetu mstaarabu nafikiri anaitwa Prishaz,basi tangia jana anajaribu kumnasihi Yericko apunguze japo kiduchu yale mambo ya "Ugaidi"!?

Basi nimecheka pita kiasi mchana huu,ati Yericko kama dasturi yake anamjibu kwa kumuuliza kama ashapitia huu mnakasha woote tangia mwanzo,pia vitabu vingapi vya Historia ya Tanganyika ameshavisoma!ahaha!!

Jamaa maskini karejea tena leo kwa ustaarabu na kujieleza upya; yakuwa yeye yupo hapa jamvini kitambo na hayo yalikua ni mawazo yake binafsi/ushauri...basi kajibiwa yakuwa hapo sasa ni vizuri,na haya mambo ya "Ugaidi" bado yanahusika saana kwenye huu mjadala na aendelee tu kuvumilia!?ahahaha!!

Kuna viroja na vitimbi vingine humu ndani hunikumbusha kitambo tulipokua Primary School/Madrassa!ahaha!!

Haina neno Al Akhiy,naona wewe na nduguyo Yericko mshafika mpaka Baghdad kwenye Family ya Al Marhum Saddam Hussein!?ahaha!!

Tuendelee na mnakasha nami nipo hapa nachungulia...

Ahsanta.
 
Nakubaliana nawe kuwa uandishi unapaswa kuwa kazi ya kitaaluma na kila mwenye utafiti ruksa kuandika! Hofu yangu swala hili ni nyeti, linahusu historia ya taifa letu. Hivi watoto wetu hawa wa English medium wanapata wapi rejea sahihi ya historia ya nchi yetu? Fikiri zipo kama rejea tano hivi! Wataelewa historia from loosers view au victors view? Ndio maana naona kuna umuhimu wa kuwa na uratibu maana historia hii si ya mtu binafsi bali taifa zima. Pengine serikali inaweza kuwa na madhaifu yake, basi angalau uratibu wa baraza maalumu la wanataaluma lisilo na shaka katika ueledi wake!

You are absolutely correct. Nadhani UDSM hawakitumii hicho kitabu (nimesikia na kusoma humu JF sina bayana)kwa kuzingatia haya unayosema na kwa kuzingatia aina ya jamii wanayoipa kipaumbele kwa siku za usoni. Asikudanganye mtu humu JF kuwa mbona University za nje wanakisoma. Wanakisoma kwa ajili ya kuja kufanya some research. Lakini sio kweli kuwa ulaya na marekani kila kitabu kinaruhusiwa vyuo vikuu. Vitabu vya Communist propaganda huvikuti Universities za marekani na ulaya. Vitabu vinavyoelekeza jinsi ya kutengeneza mabomu na kuyatega pia hukuti. Kwa hiyo ukimuona mtu anashupaa ni kuwa hajui.

Kitabu kama hiki kinaweza tumiwa sana na seminary za kiislamu kwao ni muhimu kuona na kuandaa mada ya kidini au za kikiristo katika kusoma saikology ya muslim society na kuwafahamu madhaifu yao. Kwa yule ambaye anachembe ya chuki dhidi ya mtu kama Nyerere nadhani nikitabu muafaka.

Shukran kwa maoni yako.
 
Sheikh Farid,

Salaam Al Akhiy. Nami pia nafurahika kukusizika minong'ono yako na pia huzichungulia bayana zako kwa utuvu.

Wajua hizi lugha tumeachiwa na Wazee wetu kwa mahaba makubwa yaso mipaka,basi ni wajibu wetu nasi kuzienzi na kuzitunza kwa unadhifu uso shaka.

Wallahi,leo nalitaka nipumzike japo kiduchu,lakini menijia hamu na shauku la kumsikiza Shariff Ritz kiduchu na huku tukipata darsa la Maalim Al Akhiy Sheikh Mohammed Bin Said.

Nakutakia W'end njema Al Akhiy.

Ahsanta sana.

Gombesugu,
Jana nilialikwa Radio Al Nur Masjid Sahaba Zanzibar nifanye
kumbukumbu ya marehemu Ally Sykes tulikwenda mubashara.

Tulikuwa live.

Jamaa walisisimka sana na zilopoanza simu ndiyo ikawa hekaheka
nguo kuchanika.

Nilifungua na uhusiano wa Ally Sykes na Zanzibar Club 1950 akiwa
na uhusiano na akina Himidi Msoma, Dr. Hassan Kingwaba, Dr.
Ahmed Rashid, Ahmed Rashad Ali, Ali Muhsin, Abdillah Masoud Smuts,
Ali Khamis, Mzee Mwinyi Mpiringo, Wadud na wengine wengi.

Nikamaliza na yaliyotokea baada ya mapinduzi...
 
You are absolutely correct. Nadhani UDSM hawakitumii hicho kitabu (nimesikia na kusoma humu JF sina bayana)kwa kuzingatia haya unayosema na kwa kuzingatia aina ya jamii wanayoipa kipaumbele kwa siku za usoni. Asikudanganye mtu humu JF kuwa mbona University za nje wanakisoma. Wanakisoma kwa ajili ya kuja kufanya some research. Lakini sio kweli kuwa ulaya na marekani kila kitabu kinaruhusiwa vyuo vikuu. Vitabu vya Communist propaganda huvikuti Universities za marekani na ulaya. Vitabu vinavyoelekeza jinsi ya kutengeneza mabomu na kuyatega pia hukuti. Kwa hiyo ukimuona mtu anashupaa ni kuwa hajui.

Kitabu kama hiki kinaweza tumiwa sana na seminary za kiislamu kwao ni muhimu kuona na kuandaa mada ya kidini au za kikiristo katika kusoma saikology ya muslim society na kuwafahamu madhaifu yao. Kwa yule ambaye anachembe ya chuki dhidi ya mtu kama Nyerere nadhani nikitabu muafaka.

Shukran kwa maoni yako.

Tupo pamoja mkuu. Ila hicho kitabu nataka nikisome ili nielewe alikiandika katika nadharia ipi. Nitakitafuta kwa kweli
 
JokaKuu,

Salaam ndugu yangu. Nakusoma na pia kufuatilia bayana zako kwa makini.

Ile khabari ya yule jamaa aliyetunga yale mambo ya "Mwenge wa Uhuru",naona unaiulizia kwa mara ya pili sasa....hivi una maana yako makhusus au unataka tu kujua!?...la kama una mengine tafadhali "funguka" ndugu yangu ili na sisi wengine tupate Ilm.

Nimependa umetumia neno "plots"....haina neno. Lakini alichoandika Sheikh Mohammed Said kiundani ni "Plot" iliyokua kubwa kuliko zoote katika zile harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.

Bila ya shaka labda zilikuwapo hizo "Plots" nyinginezo nyingi na harakati za Wazee wengi huko Mikoani na Vijijini kwingineko...lakini ni mughali kujaribu/kuthubutu kufafanisha na yale yaliokua yakifanzwa na kufanyika pale D'Salaam kupitia kwa Wazee wa Mzizima/Wana Mji. Harakati za pale Mzizima; ndizo zilizokua na nguvu kubwa mno, na ndo ilokua ngome na kitovu kikuu cha zile vuguvugu,chokochoko zoote za kumng'oa mkoloni katika Tanganyika yoote!

Kwa mfano kiduchu hapa;utaona wale jamaa zetu wa Kaskazini walivyoshughulika na ule mgogoro "wao" wa ardhi kule Meru. Inasemekana wao pia walipeleka mwanzo ujumbe huko UN kabla hata ya ule ujumbe wa Wazee wa Tanu uliowakilishwa na Nyerere.

Sasa ukifuatilia kiundani,utagundua vitu vingi mno. Nafikiri ndo maana Nyerere alipowapa hishma ya pekee na kuwataja tu Wazee wa Mzizima na khasa Waislamu peke yao kwenye hiyo hotuba ya "muago",tena huku akiwataja kwa majina na nasaba zao!?

Hii ni mojawapo ya ishara kubwa mno,kwa yeyote mwenye hamu ya kutaka kujua mambo Historia ya Tanganyika kiundani/kitaaluma bila ya kuendekeza udini au ukabila alonao. Kwa sababu huu ni ukweli usopingika. Au kwa lugha nyingine,ni "kigugumizi" kisichofunguka alotuachia Nyerere.

Haya majambo nafikiri hata Nyerere,angelikubaliana na mimi kwa hili. Kwani alijua kiundani ukweli huu na ukarimu, umuhimu wa hao Wazee wa Mzizima.

Ndo maana,kuna maswali nimejaribu kuyaweka japo kwa uchechefu,lakini kipata wasaa jaribu kuyachungulia kwa utuvu kwenye bayana niliomwandikia Iron asubuhi hii.

Niwie radhi kwa uchechefu wangu,na kama nina kosa au unahisi kuna kitu sijafahamu naomba unijuze ndugu yangu.

Ahsanta.

Cc;Ritz
gombesugu,

..sidhani kama kuna mtu anabisha kwamba D'Salaam ilikuwa ndiyo "Central Command" ya harakati za uhuru.

..nadhani "mzozo" uliopo hapa ni kama Mwalimu Nyerere, au mtu mwingine, ndiye aliyekuwa Kamanda Mkuu ktk hiyo "central command."

..je, kati ya Julius Nyerere,Sheikh Hassan Bin Amiri, Mshume Kiyate, Abdu Sykes, etc etc ni nani haswa kiongozi mkuu wa harakati za uhuru wa Tanganyika??

NB:

..simfahamu mtunzi wa maneno " sisi tunataka kuwasha mwenge.." lakini ningependa kumfahamu kwasababu anastahili kuwa-recorgnized kwa mchango wake. Mohamed Said anasema, Prof.Njozi ameripoti ktk kitabu cha mauaji ya mwembechai kwamba Mwalimu aliyatoa maneno hayo ktk maandiko ya zamani ya Wakatoliki.

cc😡Ritz, Jasusi, Mag3, Nguruvi3, SHEIKH FARID, Wickama
 
Last edited by a moderator:

Maneno mazuri kabisa Gombesugu; Umenifungua bwana. Awali nilidhani huyu Nyerere hakuwa hata na fadhila, nimestuka unaposema akiaga alikuwa anataja majina na nasaba ya hao wazee. Hii ni chapter mpya, tuko pamoja mkuu.
 
Tupo pamoja mkuu. Ila hicho kitabu nataka nikisome ili nielewe alikiandika katika nadharia ipi. Nitakitafuta kwa kweli

Iron,

Nadhani umeona kitu nilichokuambia mara ya kwanza kuwa humu kuna pande mbili tu Waislam na Wakisto.

Si umeona mnavyokubaliana kila kitu sababu wote ni Wakirsto ha haa haaa.

Uzuri muandika hicho kitabu Mohamed Said, kasema wazi kuwa alazimishi mtu yeyote kukikubali kila mtu ana hiari yake.

Kitabu cha Mohamed Said ni muhimu kwetu kimewaenzi Wazee wetu hilo ndiyo la msingi hayo mengine Mohamed Said, hawezi kuyazui uzuri wa hicho kitabu kinajisimamia chenyewe.

Kitabu leo kinaenda toleo la tatu, kimewaumiza watu wengi sana na kinaendelea kuwaumiza.
 
Last edited by a moderator:
Yericko Nyerere mimi nafuatilia huu mnakasha toka ulipokuwa na post 35, ila point yangu ilikuwa kwamba huu mnakasha umebase kny uchochezi wa mzee MS juu ya wapigania uhuru,na wachangiaji wengi wamekuwa wakijikita kny kuelimisha juu ya historia ya Tanganyika/ Zanzibar na wapigania uhuru, kwa hivyo binafsi naona kuingiza mambo ya ugaidi kidogo inachanganya mtiririko wa mnakasha,hilo la ugaidi lingejitegemea kwenye uzi wake.Ni maoni yangu

Yericko; nadhani huyu mchangiaji ana wazo zuri. in fact hata mimi nilipata shida ya ku-connect moja kwa moja issues za kina Hunday na Abdulwahid Sykes au John Okello. Kama unacholenga ni kuonyesha kuwa kitabu hiki kinaweza kuleta matatizo kama Iraq na kwingineko, bora kutafuta mifano inayofanana na kusudio moja kwa moja ili sote tuliangukie kuliko muanze kujibizana kama huyu ni chemical au non-chemical Ally.

HUU NDIO UCHEFUCHEFU WANGU JAPO KWA KIDUCHU. HAYA AHSANTA!!!!
 
Last edited by a moderator:
gombesugu,

..sidhani kama kuna mtu anabisha kwamba D'Salaam ilikuwa ndiyo "Central Command" ya harakati za uhuru.

..nadhani "mzozo" uliopo hapa ni kama Mwalimu Nyerere, au mtu mwingine, ndiye aliyekuwa Kamanda Mkuu ktk hiyo "central command."

..je, kati ya Julius Nyerere,Sheikh Hassan Bin Amiri, Mshume Kiyate, Abdu Sykes, etc etc ni nani haswa kiongozi mkuu wa harakati za uhuru wa Tanganyika??

NB:

..simfahamu mtunzi wa maneno " sisi tunataka kuwasha mwenge.." lakini ningependa kumfahamu kwasababu anastahili kuwa-recorgnized kwa mchango wake. Mohamed Said anasema, Prof.Njozi ameripoti ktk kitabu cha mauaji ya mwembechai kwamba Mwalimu aliyatoa maneno hayo ktk maandiko ya zamani ya Wakatoliki.

cc😡Ritz, Jasusi, Mag3, Nguruvi3, SHEIKH FARID, Wickama

Jokakuu; Sijaelewa Professor Njozi kama kweli kasema hivyo, ametoa na kitabu kipi. Nachojua ni kuwa desturi ya Mwenge imeanza hata kabla ya Ukiristo-Olympic torch na mengine. Sielewi kama Wakatoliki walikuwa na desturi ya kuwasha Mienge Milimani, kwa sababu tungeliona wakiendelea nayo popote DUNIANI. Nadhani ni area Nyerere yuko salama dhidi ya waanzilishi wenziwe wa TAA/TANU.
 
Last edited by a moderator:
Salaam ndugu zangu.Kuwepo kwangu jamvini kwa kipindi kirefu kufuatilia mnakasha huu nimejifunza jambo moja muhimu sana,nalo ni kwamba ndugu zetu wa imani tofauti wanapata tabu sana kukubali kwamba uislamu kama dini ilijipambanua wazi wazi kuupinga utawala wa kikoloni.Taasisi nyingi za kiislamu na misikiti ilikuwa ni sehemu za harakati kubwa za kupinga ukoloni.Na ndio maana Mufti ambae ni kiongozi wa juu kabisa wa waislamu sheikh Hassan bin Amir alikuwa akifanya harakati za wazi za kupinga ukoloni na kufikia mpaka kuwavuta watu kuingia TANU kupitia darsa zake misikitini.Haiwezekani sheikh Mohamed aeleze harakati za wazee wa Mzizima bila kuathirika na ushiriki wa dini yao ambao ilitoa msukumo mkubwa kwa wao kudai uhuru. Ahsanteni.
Ndugu Uthman, natoa rai kwako na kwa watu wengine kuwa waangalifu katika kufanya uchambuzi wa masuala mazito kama haya.

Ukiamini kuwa sheikh Chambera alitoa hoja ya kanisa kupinga uhuru kama kanisa, au kuamini kuwa kwavile fulani ni mwislam basi jitihada zake katika uhuru zilichagizwa na Uislam, mwisho wa siku unaweza kujikuta katika maswali usioweza kuyajibu na hivyo hoja zako zikawa teke teke.

Nikukumbushe kwanza ya kuwa siasa na dini kuna wakati zinaingiliana na si kila wakati.
Sheikh Amir, Mufti wa Tanganyika alipingana na wanafunzi wake mmoja wapo akiwa Sheikh Chaurembo juu ya mambo ya kisiasa. Nikuulize, je hilo lilitosha kumuondoa Chaurembo katika Uislam! (Hili la ugomvi wa mwl na mwanafunzi lina hoja naiweka kiporo)

Hili la kusema watu wa imani nyingine ni potofu sana. Si lazima ukubaliane na Mohamed ili uwe mwislam. Na si kila anayekataa habari za Mohamed ni mtu wa imani nyingine. Mbona wapo wa Imani nyingine wanakubaliana na Mohamed?

Sasa kama ukisema watu waliopigania uhuru walichagizwa na Uislam, na nadhani imani inaruhusu kutodhulumiwa, kuna school of thought itakayouliza, hivi znz kituo cha watumwa kuelekea bara Arab kwenye Uislam achilia mbali znz yenyewe kama kitovu cha Uislam East and central Africa, unyama huo ulifanywa kwa Uislam au ulifanywa na watu waliokuwa waislam?

Hebu tuanzie hapo bwana Uthaman
 
Wickama,
Hiyo "tunataka kuwasha mwenge" Nyerere kaitoa katika nukuu moja ya watakatifu wa Kikatoliki.
Msome Njozi "Mwembechai Killings..."Ni moja ya sababu ya kukipiga marufuku kitabu hicho.
Mohamed, pamoja na mnakasha wote huu kukufunulia mambo mengi kuhusu chuki na upotoshaji bado hujifunzi kitu mzee!

Unachowambia wanajamvi ni kuwa maneno hayo Nyerere ameyatumia ili kueneza imani ya kikatoliki.
Kama ilivyokawaida yako ya kutafuta eneo na kuingiza jina la Nyerere na Ukatoliki.

Kwa kundi unalolenga haya maneno yanaweza kuwa ya maana sana.
Kwa kundi la weledi maneno yako yabaki kuwa mshangao mkubwa.

Sidhani kama tungeenda chuo kikuu cha Ibadan hatutakuta watu wakitumia maneno ya filosofia katika kueleza, kukazia au kufafanua hoja.

Hata kama maneno hayo yametoka katika Biblia, kosa ni nini? Je, kosa ni kuwa Nyerere haku-acknowledge source(kama ni kweli) au kosa ni kutumia maneno ya Bibilia?

Mimi huwa nina msemo ninaoutumia kuwa ''elimu itafutwe hadi China''. Maneno haya ni kutoka katika dini ya Kiislam.
Huwa natumia ''Ondoa boriti katika jicho lako ndipo uondoe kibanzi katika jicho la mwenzako'' haya yapo katika Ukristo.
Je, hiyo inatosha kusema nayatumia kueneza imani ABCD!!

Ndivyo ilivyo katika siasa. Kuna wanasiasa maarufu sana wana misemo yao na tunaitumia kila siku bila kuangalia imani zao. Kuna wanasayansi maarufu sana tunatumia filosofi zao kila siku hatuangalii imani zao.

Mtu aliyegundua mambo ya hesabu(algebra kama nipo sahihi) alitoka middle east.
Wazungu na nchi za magharibi zinatumia Social welfare kama model ya zaka kutoka middle east na Uislam kwa ujumla.
Farming irrigation zilianzia middle east n.k

Tofauti na wewe, wazungu wanachukua kile chenye tija na kukifanyia kazi ili kupata mafao tarajiwa, wao siyo myopic wakuangalia nini kimetoka kwa nani na mwenye jina gani.

Unapowazuia watu wasitumie elimu kwa misingi ya dini unawapumbaza huwasaidii.
Leo kuna mtu atasoma meelezo yako na kufikia hatua ya kuamini kuwa hiyo bibilia ndiyo imeleta taabu zote alizonazo kwa kupitia Nyerere! Unampumbaza humsadiii huyu mtu.

Imefika mahali kuna vijana wanasema kuongea kiingereza ni kuonge kikristu. Mwaka jana katika nyuzi nyuzi nyingine ulieleza machungu yako kwanini kiingereza kitumike na si kiarabu alichojiufunza Kimweri na kuendesha kazi zake.
Mwaka huu ukarudia maneno kama bila kuiangalia kwa upana dunia hii ya leo.
Leo waarabu ndio wanaoongoza kwa kujifunza Kiingereza.

Tulikueleza english imekubalika duniani kama lugha ya mawasiliano kama ilivyokubalika Dollar katika exchange.
Unafanya vijana wanaosoma waangalie maneno ya ''tunawasha mwenge'' kama ya Bibilia kwahiyo hawapasi kuyatazama kama nadharia na kuyakosoa au kukubaliana nayo academically kwasababu tayari kuna prejudice ya Ukatoliki na Biblia.

Wewe unapo wa mislead vijana kuhusu misemo ya kifilosofia eti kuisema ni kuunga mkono Ukatoliki, Anglican, Budha au Hindu unawapumbaza vijana. Waache wasome waelewe dunia hii inakwenda wapi Mohamed.
Waache watu wasome wawe intellectuals na si kuwa na elimu ya Narung'ombe, dunia ya leo siyo hiyo!

Kwanini hivi Mohamed!! kwanini mnatafuta simple statement mnaiundia majungu! what do you gain when you fool the society
 
Wanajamvi,
Kitabu kinauzwa Tanzania Publishing House na Ibn Hazim
Media Centre duka hili lipo Msikiti wa Mtoro na Msikiti wa
Manyema.
 
Wanajamvi,
Someni Mwembechai Killings Njozi ameweka kila kitu
kuhusu "kuwasha mwenge" chanzo chake na kasherehesha.

Bahati mbaya niko nje na sina lap top yangu vinginevyo hakika
ningebandika taarifa hii.
 
Iron,
Soma kitabu hicho na nakuhakikishia lazima utaathirika.

Jingine.
Ndugu zangu hawa wanaandika kwa hisia zao.

Mie hawa watu ni wazee wangu.
Nimeishinao na nimepokea mengi kutoka kwao.

Nitakupa dogo tu hapa.

Wote walohusika na mgogoro wa EAMWS walijuta na wengine
walisafiri hadi Zanzibar kwenda kumshika Sheikh Hassan bin
Amir miguu tena mbele ya Sheikh Amir Tajo na Sheikh Issa
Fatawi.

Sheikh aliwasamehe ikapigwa fatha na Sheikh Hassan akatoa ijaza.

Haya yalitokea si zaidi ya miaka kumi baada ya kuundwa BAKWATA
na ukweli wa sakata lote lile kuanza kujulikana ukweli wake.

Habari za akina Geoffrey Sawaya na Rashid Kayugwa, Usalama wa Taifa,
Hamza Aziz kuwa ziko hadhir kwa Waislam.

Nakumbuka kama ishara ya sulhu darsa ya tafsir ya Qur' an Msikiti wa
Mtoro ilokuwa ikisomeshwa kila Ramadhani ilihitimishwa na Sheikh Fatawi
akimwakilisha Sheikh Hassan bin Amir.

Sheikh Fatawi alikuwa mwanafunzi wa Sheikh Hassan na si muda mrefu
Sheikh Hassan akafa.

Mimi nilikuwa mmoja wa wanafunzi walokuwa wakisoma pale na nilijifunza
mengi katika fitna ile ya uhuru kutoka wenyewe wahusika.

Sasa hawa wataweza wapi kushindana na mie katika haya?

Labda nimalize kwa kusema kuwa Sheikh Hassan hakugombana na huyo mwanafunzi
wake ila mwanafunzi aliasi masomo akaondoka kwa Sheikh na hiki ni kisa kirefu iko
siku wakati ukifika nami ni hai In Sha Allan nitakieleza hapa jamvini.

Nimekupa haya kwa kuwa nimekuhisi ni mtu utakae kujifunza ujue ukweli.
 
[SIZE=+0]@Mohamed Said, Nguruvi3,

..huyu hapa Dr.Njozi.

..nadhani hapo nilipomnukuu panatosha kwa ajili ya mjadala wetu.

Dr.Njozi said:
...There was a time when, Tanzania as a nation was also young, beautiful and highly promising. This was a time when Mwalimu Julius K. Nyerere even before Tanganyika’s independence had expressed not his intention but the intention of the people of Tanganyika to light a candle and put it on top of Mount Kilimanjaro, the highest in Africa as a shining symbol and example to the rest of the world of the commitment and grim determination of Tanganyikans to build a just and vibrant society. A society whose testimony by example would shine beyond her borders inspiring ‘hope where there was despair, love where there was hate and dignity where before there was only humiliation.’ The wording of Tanganyika’s lofty declaration of intent echoes, and is patterned after, the following famous prayer of a Roman Catholic saint, Francis of Assisi who prayed: ‘Lord, make me an instrument of Thy peace, Where there is hatred, let me sow love; where there is injury, pardon; where there is doubt, faith; where there is despair, hope; where there is sadness, joy; where there is darkness, light
[/SIZE]
Dr.Njozi said:
[SIZE=+0]The fact that Mwalimu Nyerere modelled Tanganyika’s national ideal after the prayer of a Roman Catholic saint inspired both hope and fear. It enkindled the hope that Nyerere and his team of leaders would be as dedicated as saint Francis was in translating the dream into reality. It also awakened the fear that Nyerere was so profoundly influenced by the teachings of his church that he might consider its doctrines and ideals as necessarily coinciding with those of independent Tanganyika. In the following pages I attempt to show that this fear was not unjustified. At this point I shall give an example or two. In an interview with the Christian Century of March 1, 1972, Mwalimu Nyerere was quoted as saying that his efforts to build African socialism in Tanzania represented his determination to translate in practical terms the teachings contained in The Gospel of Jesus Christ. What is wrong with that? I do not think there is anything wrong with implementing the political and economic teachings of Jesus Christ at a national level, so long as those teachings are consonant with the aspirations of the nation. In this particular case, like in the case of adapting the prayer of St. Francis above, the problem lies in the principle employed not in the details. It is wrong to use the Christian Gospels to guide the political and economic course of an avowedly secular state, even if in many instances the aspirations of the two may coincide. I am not saying it is inherently wrong to use religious books to guide the nation, I am only saying that at present it is constitutionally wrong to do so. We may debate, and I suggest that we should debate the whole concept of secularism, its attractions and its disabilities. We may as a nation reject it. Only then can we use our religious books as guidelines....

[/SIZE]
 
Mmeliona hili bandiko la Lipumba?

LIPUMBA AIBUA JAMBO
ZITO. AKIRI KUMNUSURU KIKWETE UCHAGUZI MKUU MWAKA
2010

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, ameibua suala zito akikihusisha chama chake na "kumnusuru" Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu uliopita. Profesa Lipumba alitoboa siri hiyo katika Msikiti wa Idrissa, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, alikokwenda kuswali swala ya Ijumaa, Huku akisisitiza juu ya umuhimu wa mshikamano wa kiimani, Profesa Lipumba alianza kwa kuzungumzia matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2010, na ushindani mkali wa kisiasa uliokuwapo.

Alisema hawaoni matunda ya jitihada walizofanya kumnusuru Rais Kikwete asishindwe, kwani hata chini ya uongozi wake, Waislamu wameendelea kutothaminiwa. "Ninyi masheikh mnajua vizuri zaidi hali ya kisiasa ilivyokuwa, kwamba ilibidi zifanyike juhudi za makusudi ili kuokoa jahazi.

Lakini pamoja na kuliokoa jahazi, hali halisi inaonyesha mpaka sasa hakuna matunda yoyote yaliyopatikana, na tupo katika mtihani mgumu zaidi," alisema. Katika hali ambayo inasemekana ushindi wa Rais Kikwete ulipatikana kwa mbinu, huku wengine wakiituhumu Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa ilimnusuru mgombea wa CCM, kauli hii ya Profesa Lipumba inadokeza kwamba anajua mkakati zaidi wa kazi ya Tume ya Uchaguzi.

Katika hali isiyo ya kawaida, Profesa Lipumba anaonekana kuhamasisha Waislamu kujipanga akisema "wenzetu wameanza kujipanga" kuelekea 2015.

"Kwahiyo kama Waislamu tunataka kupata haki zetu, kama tunataka kuishi kama raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu, lazima tujipange kuelekea uchaguzi mkuu wa 2015; na sisi tuanze kujipanga kwa sababu wenzetu wameanza kujipanga, vinginevyo tutaendelea kubaki maskini na raia wa daraja la nne katika nchi yetu wenyewe.

"Mwaka 2010 wakati mshindi wa uchaguzi wa rais alipotangazwa, mimi nilikwenda kwenye hafla ya kutangazwa matokeo, na nilikwenda makusudi tu, siyo kwamba uchaguzi ulikuwa huru na wa haki, ila nilikwenda makusudi kwa kujua hali ya kisiasa ilivyokuwa wakati huo. "Huku nilikutana na Sheikh Basaleh.

Nilipokutana naye, alinipongeza; sijui kama yeye anakumbuka, akaniambia ‘umeweka mbele imani yako na umekuwa mwelewa wa mambo.'"

Hata hivyo, licha ya Profesa Lipumba kuwaambia Waislamu wajipange kwa ajili ya uchaguzi mkuu, hakusema wajipange kupitia chama kipi. Lakini alisisitiza kwamba uchaguzi ujao ni zaidi ya siasa au rais yupi anafaa, bali maslahi, hasa ya rasilimali nyeti zinazopatikana katika ukanda wa Pwani ya Mashariki, eneo ambalo alisema linakaliwa zaidi na watu wenye imani ya Kiislamu.

Katika moja ya kauli zake, Profesa Lipumba alisema kwamba kuna chama kimoja kinataka kuchukua madaraka ya nchi, lakini kinasaidiwa na mataifa ya magharibi, yasiyoenzi wala kuthamini imani ya Kiislamu. Kwa muda sasa, zimekuwapo tetesi kwamba CCM imekuwa inafanya siasa za udini dhidi ya vyama vya upinzani, hasa inapoona maslahi yake yapo hatarini.

Mwaka 2010 makada kadhaa wa CCM walitumia mitandao ya simu kuchonga (spoofing) ujumbe wa simu ulioshambulia mgombea mmoja wa upinzani, ukimhusisha na imani yake.

Kauli ya Lipumba imethibitisha pia minong'ono iliyokuwapo muda mrefu kuwa baadhi ya kura za Profesa Lipumba zilipotelea kwa Rais Kikwete.

Katika uchaguzi huo, Lipumba alitangazwa kushika namba ya tatu, nyuma ya Rais Kikwete na Dk. Willibrod Slaa wa CHADEMA.

Alipoulizwa kuhusu ziara yake msikitini na kauli aliyotoa, Profesa Lipumba alikiri kwamba alikwenda kuzungumzia hali ya kisiasa nchini.

Picha Chini Akitoka MSIKITINI kwenye HUO MKUTANO...
576832_502467819806814_85109511_n.jpg
[TABLE="class: cf gz ac3"]
[TR]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD][/TD]
[TD="class: io"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Iron,
Soma kitabu hicho na nakuhakikishia lazima utaathirika.
Jingine.Ndugu zangu hawa wanaandika kwa hisia zao.

Mie hawa watu ni wazee wangu.
Nimeishinao na nimepokea mengi kutoka kwao.

Wote walohusika na mgogoro wa EAMWS walijuta na wengine
walisafiri hadi Zanzibar kwenda kumshika Sheikh Hassan bin
Amir miguu tena mbele ya Sheikh Amir Tajo na Sheikh Issa
Fatawi.

Sheikh aliwasamehe ikapigwa fatha na Sheikh Hassan akatoa ijaza.

Haya yalitokea si zaidi ya miaka kumi baada ya kuundwa BAKWATA
na ukweli wa sakata lote lile kuanza kujulikana ukweli wake.

Habari za akina Geoffrey Sawaya na Rashid Kayugwa, Usalama wa Taifa,
Hamza Aziz kuwa ziko hadhir kwa Waislam.

Mimi nilikuwa mmoja wa wanafunzi walokuwa wakisoma pale na nilijifunza
mengi katika fitna ile ya uhuru kutoka wenyewe wahusika.

Sasa hawa wataweza wapi kushindana na mie katika haya?

Labda nimalize kwa kusema kuwa Sheikh Hassan hakugombana na huyo mwanafunzi
wake ila mwanafunzi aliasi masomo akaondoka kwa Sheikh na hiki ni kisa kirefu iko
siku wakati ukifika nami ni hai In Sha Allan nitakieleza hapa jamvini.
Nimekupa haya kwa kuwa nimekuhisi ni mtu utakae kujifunza ujue ukweli.
Mohamed,
Suala la EAMWS na Sheikh Amir linazidi kuchukua sura mpya.

Kwanza niwaambie wanajamvi kuwa kufuatana na maandishi ya Ziddy, kuna wakati Sheikh Amir alikuwa na ugomvi na Mwanafunzi wake sheikh Chaurembo kutokana na masuala ya KISIASA.

Ni wazi kuwa halikuwa suala la TANU, swali linabaki ni masuala gani ya kisiasa nje ya TANU na kwanini sheikh aliyekuwa mwanachama wa TANU awe na sura nyingine ya kisiasa nje ya TANU?

Pili, Sheikh alikuwa mwanachama wa Al-Jamiyya Islamiyya fil Tanganyika. Na pia alikuwa mwanachama wa Al-Dafiwa fil Islamiyya. Vyama hivi vya kidini vina uhusiano mkubwa sana na familia ya Sykes.
Kuna nyakati Abdul Sykes alikuwa katibu wa Al-Jamiyya Islamiyya fi Tanganyika.

Uhusiano wa Sheikh Amir na familia ya Sykes ndipo ulipozidi kuuma.
Mnakumbuka pia kuhusu AMNUT. Ingawa Mohamed anakanusha kuwa Sheikh Amir hakuwa mwanachama wa AMNUT ningependa pia akanushe kuwa wanafunzi wa Sheikh hawakuwa wanachama na viongozi wa AMNUT.

Kwa mantiki ni kuwa kulikuwa na uhusiano kati ya Sheikh Amir, Familia ya Klesit na AMNUT.
AMNUT walikuwa sympathizers wakubwa wa Abdul na wengi ni wanafunzi wa Amir.
Angalia hiyo triangle vizuri sana.

Kutokana na uhusiano huo chuki ya Abdul Kushindwa na Nyerere katika chaguzi na ukweli kuwa sheikh naye alikuwa katika TAA sub political committee ndiko kuliwaunganisha na kumzuia Sheikh Amir kukataa nafasi alizopewa na Nyerere ili kuendesha siasa za pembeni.

Kukataa nafasi katika serikali kulikuwa ni kosa kubwa sana kisiasa na kidini.
Sheikh aliporejea kutoka Egypt aliahidiwa pauni 55 millions egyptian Pounds.
Kama angekuwa katika serikali hiyo ndiyo ingekuwa fursa nzuri sana ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa chuo kikuu.

Angeabaini mbinu zote chafu au basi kuomba msaada zaidi pale ilipobidi. Hakufanya hivyo kwasababu alikuwa na political agenda nje ya TANU kama alivyobainisha Comorian na mgogoro na mwanafunzi wake Chaurembo juu ya mambo ya kisiasa

Hakukuwa na sababu za yeye kufanya siasa za vichochoroni kama alivyonywa na sheikh Comorian mara baada ya kurejea kwake safarini.

Kwa mujibu wa Ziddy, kulikuwa na migogoro ndani kwa ndani kati ya Sheikh Amir na Sheikh Chaurembo hata kabla ya mradi wa kuanzisha chuo kuanza, na ni migogoro hiyo iliyoua mpango mzima wa kujenga chuko kikuu.

Mohamed Sadi anaposema Nyerere alikuwa na mpango wa kuua mradi wa EAMWS si kweli. Si kweli kwa facts kuwa:

  1. Kulishaanza migogoro ya kisiasa nje ya TANU kati ya Sheikh Amir na Wanafunzi wake iliyohusu siasa nje ya TANU.
  2. Nyerere asingeweza kuruhusu viongozi wa serikali akiwemo Tewa Said Tewa kuambatana na Sheikh ambaye alishajulikana ana siasa za pembeni kwenda kuomba msaada wa kujenga chuo kikuu.Haiingii akilini Nyerere aruhusu viongozi wake ndani ya serikali halafu aje kuzuia chuo.
  3. Mohamed anadai Tewa alipewa ubalozi ili kuua mpango mzima wa ujenzi wa chuo cha EAWMS. Anachosahau ni kuwa Tewa alipewa nafasi ya ubalozi miaka 3 baaada ya ziara ya Egtpt. Endapo mpango huo ungekuwa kama anavyodai basi angemuondoa mapema zaidi.

Limezuka suala la sheikh Amir kuwa Walii. Hilo nasema kwa mujibu wa watu wa imani yake kama limetokea ni sawa. Kinachoshughulisha akili ni kuwa walii ni mtu mwenye sifa zisizo na shaka.

Sheikh Amir alitiliwa shaka sana na watu wa mikoani kuhusu matumizi ya pesa makao makuu alipokuwa kinara.
Hilo ndilo lilianza kumega mikoa ya Tanga, Bukona na Iringa. Linathibitika katika madai ya mikoa hiyo yaliyotakiwa kutimizwa kabla ya kurudi ndani ya EAMWS.

Madai hayo yakieleza wazi kuwa vyanzo na matumizi ya pesa za EAMWS lazima yawekwe wazi. Sasa kwanini Walii atiliwe shaka na je hapo bado hishma yake inabaki katika uwalii akiwa na ''strings attached''

Kuna hoja za Mohamed kuhusu kuzuiliwa na kuonewa. Maswali yanayozuka ni mengi sana ambayo hayana majibu ya maana kwa anayetumia akili

  1. Kwanza, hivi Ansar Sunn ni watu wa imani gani? Mbona wao wana miaradi na hata TV stesheni na wala hawajazuiliwa na kanisa au serikali.
  2. Hawa mashia ni wa imani gani mbona hawajazuiliwa na serikali au kanisa kuwa na miradi yao sehemu zote nchini?
  3. Hawa Ismailia ni wa imani gani, mbona hawajazuliliwa kuwa na miradi nchi nzima
  4. Hivi kwanini mlezi wa EAWMS amerudi na kupewa plot kwa ajili ya chuo kikuu.
  5. Kwanini malalamiko yapo kwa watu nje ya makundi hayo hapo juu.

Na mwisho, labada niulize hivi ilie misaada inayotoka nje kama Saudia na ile inayotolewa na matajiri wa hapa nchini kama ZAKA, imetumika vipi katika investment ya mambo ya social ambayo leo inaweza kuombewa ruzuku serikalini kama za mashirika mengine.

cc.Zumbemkuu, kuna nyuzi uliomba nifunguke!

cc Jokakuu, Shariff Ritz, Almaarufu Gombesugu, Wickama,Jausi, Mag3, Who,gfsowin,Prisharz, Hon Al-khyis'
 
Iron,
Soma kitabu hicho na nakuhakikishia lazima utaathirika.

Nimekupa haya kwa kuwa nimekuhisi ni mtu utakae kujifunza ujue ukweli.
Niasidie mzee wangu, ni kweli kuwa mzee Kreist Mbuyane alikufa maji Ruaha Iringa akiwa katika mapambano na Mkwawa?
 
Ritz,
Mie si wa kujibizana na huyu.

Hana moja alijualo katika hayo ayazungumzayo.

Rashid Kayugwa kabla hajafa aliwaeleza Waislam
mpango mzima ulivyosukwa.

Kayugwa alistaghfiru na akawa anaswali Mtoro hadi
umauti ulipomfika.

Huyu mtu anaejidai anajua sana nakuachieni nyie.
 
Back
Top Bottom