Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Niasidie mzee wangu, ni kweli kuwa mzee Kreist Mbuyane alikufa maji Ruaha Iringa akiwa katika mapambano na Mkwawa?

Maulaga ni kweli Kleist Mbuwane alikufamaji
Mto Ruaha.

Walipofika mtoni walitanguliza ng'ombe kuvuka
kupima kimo cha maji.

Ng'ombe walivuka salama na ndipo walipoingia
majini na yeye Kleist maji yakamsomba.
 
Mohamed,
Suala la EAMWS na Sheikh Amir linazidi kuchukua sura mpya.

Kwanza niwaambie wanajamvi kuwa kufuatana na maandishi ya Ziddy, kuna wakati Sheikh Amir alikuwa na ugomvi na Mwanafunzi wake sheikh Chaurembo kutokana na masuala ya KISIASA.

Ni wazi kuwa halikuwa suala la TANU, swali linabaki ni masuala gani ya kisiasa nje ya TANU na kwanini sheikh aliyekuwa mwanachama wa TANU awe na sura nyingine ya kisiasa nje ya TANU?

Pili, Sheikh alikuwa mwanachama wa Al-Jamiyya Islamiyya fil Tanganyika. Na pia alikuwa mwanachama wa Al-Dafiwa fil Islamiyya. Vyama hivi vya kidini vina uhusiano mkubwa sana na familia ya Sykes.
Kuna nyakati Abdul Sykes alikuwa katibu wa Al-Jamiyya Islamiyya fi Tanganyika.

Uhusiano wa Sheikh Amir na familia ya Sykes ndipo ulipozidi kuuma.
Mnakumbuka pia kuhusu AMNUT. Ingawa Mohamed anakanusha kuwa Sheikh Amir hakuwa mwanachama wa AMNUT ningependa pia akanushe kuwa wanafunzi wa Sheikh hawakuwa wanachama na viongozi wa AMNUT.

Kwa mantiki ni kuwa kulikuwa na uhusiano kati ya Sheikh Amir, Familia ya Klesit na AMNUT.
AMNUT walikuwa sympathizers wakubwa wa Abdul na wengi ni wanafunzi wa Amir.
Angalia hiyo triangle vizuri sana.

Kutokana na uhusiano huo chuki ya Abdul Kushindwa na Nyerere katika chaguzi na ukweli kuwa sheikh naye alikuwa katika TAA sub political committee ndiko kuliwaunganisha na kumzuia Sheikh Amir kukataa nafasi alizopewa na Nyerere ili kuendesha siasa za pembeni.

Kukataa nafasi katika serikali kulikuwa ni kosa kubwa sana kisiasa na kidini.
Sheikh aliporejea kutoka Egypt aliahidiwa pauni 55 millions egyptian Pounds.
Kama angekuwa katika serikali hiyo ndiyo ingekuwa fursa nzuri sana ya kuendeleza mradi wa ujenzi wa chuo kikuu.

Angeabaini mbinu zote chafu au basi kuomba msaada zaidi pale ilipobidi. Hakufanya hivyo kwasababu alikuwa na political agenda nje ya TANU kama alivyobainisha Comorian na mgogoro na mwanafunzi wake Chaurembo juu ya mambo ya kisiasa

Hakukuwa na sababu za yeye kufanya siasa za vichochoroni kama alivyonywa na sheikh Comorian mara baada ya kurejea kwake safarini.

Kwa mujibu wa Ziddy, kulikuwa na migogoro ndani kwa ndani kati ya Sheikh Amir na Sheikh Chaurembo hata kabla ya mradi wa kuanzisha chuo kuanza, na ni migogoro hiyo iliyoua mpango mzima wa kujenga chuko kikuu.

Mohamed Sadi anaposema Nyerere alikuwa na mpango wa kuua mradi wa EAMWS si kweli. Si kweli kwa facts kuwa:

  1. Kulishaanza migogoro ya kisiasa nje ya TANU kati ya Sheikh Amir na Wanafunzi wake iliyohusu siasa nje ya TANU.
  2. Nyerere asingeweza kuruhusu viongozi wa serikali akiwemo Tewa Said Tewa kuambatana na Sheikh ambaye alishajulikana ana siasa za pembeni kwenda kuomba msaada wa kujenga chuo kikuu.Haiingii akilini Nyerere aruhusu viongozi wake ndani ya serikali halafu aje kuzuia chuo.
  3. Mohamed anadai Tewa alipewa ubalozi ili kuua mpango mzima wa ujenzi wa chuo cha EAWMS. Anachosahau ni kuwa Tewa alipewa nafasi ya ubalozi miaka 3 baaada ya ziara ya Egtpt. Endapo mpango huo ungekuwa kama anavyodai basi angemuondoa mapema zaidi.

Limezuka suala la sheikh Amir kuwa Walii. Hilo nasema kwa mujibu wa watu wa imani yake kama limetokea ni sawa. Kinachoshughulisha akili ni kuwa walii ni mtu mwenye sifa zisizo na shaka.

Sheikh Amir alitiliwa shaka sana na watu wa mikoani kuhusu matumizi ya pesa makao makuu alipokuwa kinara.
Hilo ndilo lilianza kumega mikoa ya Tanga, Bukona na Iringa. Linathibitika katika madai ya mikoa hiyo yaliyotakiwa kutimizwa kabla ya kurudi ndani ya EAMWS.

Madai hayo yakieleza wazi kuwa vyanzo na matumizi ya pesa za EAMWS lazima yawekwe wazi. Sasa kwanini Walii atiliwe shaka na je hapo bado hishma yake inabaki katika uwalii akiwa na ‘’strings attached’’

Kuna hoja za Mohamed kuhusu kuzuiliwa na kuonewa. Maswali yanayozuka ni mengi sana ambayo hayana majibu ya maana kwa anayetumia akili

  1. Kwanza, hivi Ansar Sunn ni watu wa imani gani? Mbona wao wana miaradi na hata TV stesheni na wala hawajazuiliwa na kanisa au serikali.
  2. Hawa mashia ni wa imani gani mbona hawajazuiliwa na serikali au kanisa kuwa na miradi yao sehemu zote nchini?
  3. Hawa Ismailia ni wa imani gani, mbona hawajazuliliwa kuwa na miradi nchi nzima
  4. Hivi kwanini mlezi wa EAWMS amerudi na kupewa plot kwa ajili ya chuo kikuu.
  5. Kwanini malalamiko yapo kwa watu nje ya makundi hayo hapo juu.

Na mwisho, labada niulize hivi ilie misaada inayotoka nje kama Saudia na ile inayotolewa na matajiri wa hapa nchini kama ZAKA, imetumika vipi katika investment ya mambo ya social ambayo leo inaweza kuombewa ruzuku serikalini kama za mashirika mengine.

cc.Zumbemkuu, kuna nyuzi uliomba nifunguke!

cc Jokakuu, Shariff Ritz, Almaarufu Gombesugu, Wickama,Jausi, Mag3, Who,gfsowin,Prisharz, Hon Al-khyis'
Nguruvi.
Nimekusoma vizuri na nimekuelewa naomba na mimi niongeze nyama kidogo kwenye haya uliyoandika,kwanza kuhusu Answar sunna kuwa na miradi yao ni kweli wana Radio na Tv station na shule na zahanati kwa taarifa yako tv Imaan walashalipa kila kitu TCRA lakini walipoanza matangazo tuu serikali wakawazuia na huoni kwamba serikali wanajenga hisia mbaya na waislamu na mkuu wa TCRA ni mkristo na hisia za mfumo kristo si ndio zinaanza hapo? pili naingia kwenye OIC hivi Uganda si wanachama wa OIC ni nini kichowakwaza wakristo wa Tanzania kushupalia hilo swala kwamba Tanzania haiwezi kujiunga na OIC! na kama sijakosea Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza kingejengwa chuo kikuu cha kiislamu katika nchi za east Africa lakini Nyerere alikataa halafu Idd Amin alikubali ndio kikaenda kujengwa pale Mbale Uganda na mpaka leo wakristo wa Uganda wanaishi kwa amani na Uganda sio nchi ya kiislamu tofauti na sisi huku kwetu watu wanavyolishwa "matango pori" eti tukijiunga Tanzania itakuwa nchi ya kiislamu. Inasikitisha sanahuku tuendako kwasababu hii nchi kila mtu ana haki ya kula keki ya hii nchi sasa upande fulani unapoona haupati haki ndio maana yanatokea haya tunayoyona. Ahsanta
 
Ingawa Mohamed anakanusha kuwa Sheikh Amir hakuwa mwanachama wa AMNUT ningependa pia akanushe kuwa wanafunzi wa Sheikh hawakuwa wanachama na viongozi wa AMNUT.

Kwa mantiki ni kuwa kulikuwa na uhusiano kati ya Sheikh Amir, Familia ya Klesit na AMNUT.
AMNUT walikuwa sympathizers wakubwa wa Abdul na wengi ni wanafunzi wa Amir.
Angalia hiyo triangle vizuri sana.'
Ninachokulaumu ni kuwa hukujishughulisha kuangalia Uislamu nao unasemaje kuhusu suala la UDUGU KATIKA UISLAMU!

Nina hakika kama ungeangalia usingefikia katika hitimisho hili.

Maadamu AMNUT hawakutoka nje ya Imani ya Kiislamu basi kivyovyote vile aidha Sheikh Amir anakubaliana nao au hakubaliani nao lakini angekuwa na uhusiano nao tu kwa vile bado ni Waislamu na wana haki zao za Kiislamu kwake kama ambavyo pia Sheikh Amir ana haki zake za Kiislamu kwao.

Mfano, sikukubaliana na rai za Bin Laden na Al-qaeda lakini mwisho wa yote kuna haki zake za Kiislamu kwangu ambazo siwezi kumnyima.Vilevile mimi ninahaki zake kwake ambazo hawezi kuninyima...si Waislamu wote walioandamana,kupinga na kukasirishwa na kifo cha Bin Laden wanakubaliana na rai zake! walifanya vile kwa vile Bin Laden alikuwa ni Muislamu mtuhumiwa ambaye hajawahi kupatikanaa na hatia katika mahakama yoyote ile.

...mnakasha unaweza kuendelea sasa.
 
Maulaga ni kweli Kleist Mbuwane alikufamaji
Mto Ruaha.

Walipofika mtoni walitanguliza ng'ombe kuvuka
kupima kimo cha maji.

Ng'ombe walivuka salama na ndipo walipoingia
majini na yeye Kleist maji yakamsomba.
Je? ilikuwa halali kwa muislam Kreist Mbuwane kushirikiana na makafir kwenda kumpiga vita muislam mwenzie Mkwawa? Je Kufa maji kwa Mbuwane ilikuwa adhabu ya Allah dhidi ya dhulma aliyokuwa anafanyiwa Mkwawa na makafir?
 
Ritz,
Mie si wa kujibizana na huyu.

Hana moja alijualo katika hayo ayazungumzayo.

Rashid Kayugwa kabla hajafa aliwaeleza Waislam
mpango mzima ulivyosukwa.

Kayugwa alistaghfiru na akawa anaswali Mtoro hadi
umauti ulipomfika.

Huyu mtu anaejidai anajua sana nakuachieni nyie.
Mohamed Said,

Huyu hana anachokijua zaidi ya hisia zake na kejeli dhidi Sheikh Hassan Bin Amir kaongea uzushi mwingi hili tutaka kutimiza malengo yake lakini bahati mbaya hana ushahidi zaida ya maneno matupu hebu msome hapa chini.
Pili, Sheikh alikuwa mwanachama wa Al-Jamiyya Islamiyya fil Tanganyika. Na pia alikuwa mwanachama wa Al-Dafiwa fil Islamiyya. Vyama hivi vya kidini vina uhusiano mkubwa sana na familia ya Sykes.
Kuna nyakati Abdul Sykes alikuwa katibu wa Al-Jamiyya Islamiyya fi Tanganyika.
Hapa aelewi kuwa Al-Jamiyya Islamiyya fil Tanganyika na Al-Dafiwa fil Islamiyya ndiyo waasisi wa AA. TAA. TANU. kwa kumsaidia mweka hazina wa Al-Jamiyya Islamiyya fil Tanganyika Mzee Iddi Faiz Mafongo na ndiyo mweka hazina wa TANU hawa wazee wote walikuwa wakiishi kama ndugu kwa ushahidi msome Nyerere mwanywe hapa chini.
"Mimi nimeanza siasa na wazee wa Dar es Salaam; na wazee wa Tanzania. Nimeanza nao mapema sana; mapema kweli. Nilirudi kutoka masomoni, Uingereza Oktoba 1952 – miaka 33 nyuma. Wakati huo nikiwa kijana mdogo wa miaka thelathini na kidogo hivi.
Nadhani wanaukumbi mmeona siyo familia ya Sykes peke yake ambao walikuwa karibu na hizi taasisi za dini kwa ushahidi mwingine hebu hapa chini tuangalie kazi zipi zilizokuwa zinafanywa na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir kupitia hizo taasisi.
Al-jamiatul Islamiya (Muslim Association of Tanganyika), andAd-Daawatul Islamiya (Muslim Call) and also the East African Muslims Welfare Society (EAMWS). By using these Societies, Sk, Hassan visited many Countries making Daawa for Muslims and non Muslims. His one student Sk. Ramadhan b. Jaafar told me that Sk. Hassan converted 7 million peoples to Islam. I asked him 7 million or 7 hundred thousand? He told me " Sk. Hassan himself told me that 7 million" (Interview. 2002).
Sheikh Amir alitiliwa shaka sana na watu wa mikoani kuhusu matumizi ya pesa makao makuu alipokuwa kinara.
Hilo ndilo lilianza kumega mikoa ya Tanga, Bukona na Iringa. Linathibitika katika madai ya mikoa hiyo yaliyotakiwa kutimizwa kabla ya kurudi ndani ya EAMWS.

Madai hayo yakieleza wazi kuwa vyanzo na matumizi ya pesa za EAMWS lazima yawekwe wazi. Sasa kwanini Walii atiliwe shaka na je hapo bado hishma yake inabaki katika uwalii akiwa na ''strings attached''
Wanajamvi kwa faida yenu na kwa taifa tunaomba ndugu yetu atupe ushahidi kwa haya maneno yake japo kiduchu atutajie majina ya hao ambao anasema walimtilia shaka Sheikh Hassan Bin Amiri na atufahamishe hizo pesa na mali zililiwa zilkuwa kiasi gani.
Uhusiano wa Sheikh Amir na familia ya Sykes ndipo ulipozidi kuuma.
Mnakumbuka pia kuhusu AMNUT. Ingawa Mohamed anakanusha kuwa Sheikh Amir hakuwa mwanachama wa AMNUT ningependa pia akanushe kuwa wanafunzi wa Sheikh hawakuwa wanachama na viongozi wa AMNUT.
Naona baada ya kuishiwa hoja unalazimisha lete ushahidi kuwa Mufti Hassan Bin Amir alikua AMNUT siyo kuja na maneno matupu hili kukamilisha matakwa yako.
Hapa chini hebu msome Mufti Sheikh Hassan Bin Amir halafu jisome na wewe unavyomuelezea utaona kabisa umejawa nachuki mapoja na husda.
HIS LIFE AND ACHIEVEMENTS
Sk. Hassan b. Ameir (1890-1979) died on October 8,1979, he was undisputedly one among the international scholars, mubalighs, educationists and Muslim writers in East and Central Africa. He is remembered with ever smiling face and pleasant manners among his students and Muslims of this region as a whole. People who wanted to shake his hand or kiss him or discuss about current views of Islamic education surrounded him everywhere he went. His reputation extended beyond the boundaries of East Africa, from Egypt in the north and South Africa in the south, to Burundi, Ruanda and Congo where he conducted darsas now and then when his Headquarter was in Dar es Salaam at the Ngazija/Commorian Mosque before he was deported to Zanzibar (1968) to complete his ten remaining years of life. His name, conduct and Islamic education theory and ideas spread to every corner of Tanganyika and East Africa because of his great work as a Mubaligh in the East African Muslim Welfare Society -EAMWS- (1945-1968). "Perhaps the most popular teacher in terms of numbers of students in Tanzania (at least after 1940, when he moved there from Zanzibar) was Sk. Hassan b. Ameir Al-Shirazi. His popularity stems from his having traveled extensively throughout East Africa to teach. He eventually settled in Dar es Salaam, where he opened his well patronized Madrasat al Shiraziya in the Commorian Mosque." (August H. Nimtz Jr. 1980. 23).
 
Je? ilikuwa halali kwa muislam Kreist Mbuwane kushirikiana na makafir kwenda kumpiga vita muislam mwenzie Mkwawa? Je Kufa maji kwa Mbuwane ilikuwa adhabu ya Allah dhidi ya dhulma aliyokuwa anafanyiwa Mkwawa na makafir?

Kha!
We ndugu maulaga!
Mbona una maswali magumu hivyo?
 
Last edited by a moderator:
Jasusi, hapa siyo Karikoo kaka usimeze mazima kariakoo hakuna miti sijui kama unajua ulipo msikiti wa Iddrisa.
576832_502467819806814_85109511_n.jpg

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba akitoka kuswali Swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, Kinondoni, jana. Picha na Mpigapicha Wetu.

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Nchini, Sheikh Issa Ponda ameiomba Serikali kuunda Tume ya kushughulikia matatizo ya Waislamu. Ponda alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa mawaidha ya Ijumaa katika Msikiti wa Mtambani, wilayani Kinondoni.
Kauli hiyo imekuja siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumhukumu kifungo cha mwaka mmoja nje, baada ya kupatikana na hatia ya kuingia isivyo halali katika eneo la Markazi Chang'ombe.
Alisema kwa muda mrefu Waislamu nchini wamekuwa na madai ambayo Serikali haijaonyesha dhamira ya kuyashughulikia.
"Waislamu wamekuwa wakinyanyasiki katika nchi yao utadhani wakimbizi, tuna madai ya msingi ambayo hayahitaji watu kufungwa au kuundiwa kesi kwa hiyo sasa ni wakati wa Serikali kuunda tume tutakayokwenda kuwaeleza matatizo yetu na vithibitisho vyake," alisema Ponda.
Ponda alisema atahakikisha kuwa anawatetea Waislamu ili wapate haki zao zinazopokwa na baadhi ya watu wasiowapenda waumini wa dini hiyo.
"Wamekuwa wakinitungia njama za kuniondoa kwa misingi ya kuwa mimi siyo Mtanzania, hakuna wa kuniondoa hapa nchini na nitapambana hadi hatua ya mwisho na kuhakikisha kuwa Waislamu wanapata uhuru wao," alinena Sheikh Ponda.
 
Ndugu Uthman, natoa rai kwako na kwa watu wengine kuwa waangalifu katika kufanya uchambuzi wa masuala mazito kama haya.

Ukiamini kuwa sheikh Chambera alitoa hoja ya kanisa kupinga uhuru kama kanisa, au kuamini kuwa kwavile fulani ni mwislam basi jitihada zake katika uhuru zilichagizwa na Uislam, mwisho wa siku unaweza kujikuta katika maswali usioweza kuyajibu na hivyo hoja zako zikawa teke teke.

Nikukumbushe kwanza ya kuwa siasa na dini kuna wakati zinaingiliana na si kila wakati.
Sheikh Amir, Mufti wa Tanganyika alipingana na wanafunzi wake mmoja wapo akiwa Sheikh Chaurembo juu ya mambo ya kisiasa. Nikuulize, je hilo lilitosha kumuondoa Chaurembo katika Uislam! (Hili la ugomvi wa mwl na mwanafunzi lina hoja naiweka kiporo)

Hili la kusema watu wa imani nyingine ni potofu sana. Si lazima ukubaliane na Mohamed ili uwe mwislam. Na si kila anayekataa habari za Mohamed ni mtu wa imani nyingine. Mbona wapo wa Imani nyingine wanakubaliana na Mohamed?

Sasa kama ukisema watu waliopigania uhuru walichagizwa na Uislam, na nadhani imani inaruhusu kutodhulumiwa, kuna school of thought itakayouliza, hivi znz kituo cha watumwa kuelekea bara Arab kwenye Uislam achilia mbali znz yenyewe kama kitovu cha Uislam East and central Africa, unyama huo ulifanywa kwa Uislam au ulifanywa na watu waliokuwa waislam?

Hebu tuanzie hapo bwana Uthaman

Ndugu yangu Nguruvi3,
Kuna sababu za msingi zilizosukuma taasisi za kiislamu na waislamu kwa ujumla kupambana na ukoloni kwa nguvu zote ukilinganisha na dini nyingine.Lazima ufahamu kwamba wakoloni walipokutana Berlin 1884-85 moja katika ajenda zao kubwa kabisa ilikuwa ni kuhakikisha ustawi wa ukristo katika makoloni yao na kufanya jitihada za kuukandamiza uislamu.Infact all participants regarded islam as the most serious enemy of european colonisation in Africa.
Waislamu ndio jamii ilyoathiriwa zaidi na ukoloni hapa Tanganyika,kwa hiyo siajabu kuonekana wao ndio walikuwa mstari wa mbele kupinga ukoloni.

Kwa mchambuzi wa kweli ulichambua jambo kwa ukweli wake badala ya kuficha baadhi ya vitu kwa visingizio vya udini.
Ukweli unabaki kuwa ukristo ilikuwa ni dini iliyosimamiwa na wakoloni na wakristo walipewa upendeleo mkubwa,na ndio maana makanisa mengi hayakujitokezakuupinga ukoloni.Ila wakristo wengi waliupinga ukoloni kama wao bila kupewa msukumo makanisani.

ahsanta.
 
Unaweza ukatupa ushahidi zaidi kuonesha kwamba lengo moja wapo la wakoloni kuja Africa ilikuwa ni kuudhibiti uislam?
Inawezekana walienda pia South East Asia kudhibiti hinduism na Buddhism?
 
[SIZE=+0]@Mohamed Said, Nguruvi3,

..huyu hapa Dr.Njozi.

..nadhani hapo nilipomnukuu panatosha kwa ajili ya mjadala wetu.

Jokakuu; Hii mada ni ngumu sana, at least kwangu. Maana naona mwisho hata professor Njozi imemshinda. Anasema haoni kama ni vibaya taifa kuongozwa na madili ya kidini lakini itakuwa inavunjwa "our secular constitution". Ukishafungua hilo dirisha then inakuja a bigger debate BASI MAADILI YA DINI GANI. Sishangai hakuweza kuijibu. Mbele ya safari huenda maneno kama Mungu kwenye Wimbo wa Taifa, dua bungeni na mashule yataleta matatizo. Ulaya na Marekani sehemu zingine tayari mikasa ya aina hii imewapata.

Yaelekea Nyerere alimhusudu sana huyu St. Francis. Kama Njozi yuko sawa. Lakini pia sio tatizo, wako wanaomhusudu Mama Theresa, Martin Luther, Che-Guevara, Khalid bin Walid, Salahudin. Kila mtu na icon wake.
 
Wanajamvi,
Someni Mwembechai Killings Njozi ameweka kila kitu
kuhusu "kuwasha mwenge" chanzo chake na kasherehesha.

Bahati mbaya niko nje na sina lap top yangu vinginevyo hakika
ningebandika taarifa hii.

Mzee MS; Baada ya salaam. It is unfortunate sielewi kama hiki kitabu kiko on sale nilisoma somewhere kama vile kilizuiliwa sometime, am I right? Kama kinauzwa I could get a copy.
 
Ndugu yangu Nguruvi3,
Kuna sababu za msingi zilizosukuma taasisi za kiislamu na waislamu kwa ujumla kupambana na ukoloni kwa nguvu zote ukilinganisha na dini nyingine.Lazima ufahamu kwamba wakoloni walipokutana Berlin 1884-85 moja katika ajenda zao kubwa kabisa ilikuwa ni kuhakikisha ustawi wa ukristo katika makoloni yao na kufanya jitihada za kuukandamiza uislamu.Infact all participants regarded islam as the most serious enemy of european colonisation in Africa.
Waislamu ndio jamii ilyoathiriwa zaidi na ukoloni hapa Tanganyika,kwa hiyo siajabu kuonekana wao ndio walikuwa mstari wa mbele kupinga ukoloni.

Kwa mchambuzi wa kweli ulichambua jambo kwa ukweli wake badala ya kuficha baadhi ya vitu kwa visingizio vya udini.
Ukweli unabaki kuwa ukristo ilikuwa ni dini iliyosimamiwa na wakoloni na wakristo walipewa upendeleo mkubwa,na ndio maana makanisa mengi hayakujitokezakuupinga ukoloni.Ila wakristo wengi waliupinga ukoloni kama wao bila kupewa msukumo makanisani.

ahsanta.

Uthman; Ukiunda theory inatakiwa ifanye kazi elsewhere. Hayo majibu yako kwa Nguruvi hataeleza kwanini Italy iliivamia Ethiopia kui-colonize huku nayo ni a Christian country. Haitaeleza waingereza kuitawala India, Australia, South Africa, New Zealand. Au Wareno ku-colonise southern America au Wajerumani kuwavamia wenzao huko Europe.

La msingi lazima ujue kila mwanadamu ana uchu wa kuondoa kudhulumiwa. Zimbabwe, Namibia, Angola, kote mapambano yalikuwa ni almost 100% Christians against Christians lakini mmoja ni colonizer. Wasaudia waliwapiga na kuwaondoa waturuki kwa ili hali wote ni moslems 100%.

Please be very objective unapo-analyse such issues.
 
Mzee MS; Baada ya salaam. It is unfortunate sielewi kama hiki kitabu kiko on sale nilisoma somewhere kama vile kilizuiliwa sometime, am I right? Kama kinauzwa I could get a copy.

Unavyomuelezea Prof. Njozi nilidhani umemsoma, ha haa haaa! Kitabu kinauzwa Catholic Bookshop, Mbeya, Iringa, Dar es Salaam, Musoma, utakuwa umesoma vibaya.
 
Unaweza ukatupa ushahidi zaidi kuonesha kwamba lengo moja wapo la wakoloni kuja Africa ilikuwa ni kuudhibiti uislam?
Inawezekana walienda pia South East Asia kudhibiti hinduism na Buddhism?

Nanren,soma katika makubaliano ya Berlin 1884-5 hicho kipengele kipo.tuliposomeshwa historia shuleni kilifichwa makusudi
 
Uthman; Ukiunda theory inatakiwa ifanye kazi elsewhere. Hayo majibu yako kwa Nguruvi hataeleza kwanini Italy iliivamia Ethiopia kui-colonize huku nayo ni a Christian country. Haitaeleza waingereza kuitawala India, Australia, South Africa, New Zealand. Au Wareno ku-colonise southern America au Wajerumani kuwavamia wenzao huko Europe.

La msingi lazima ujue kila mwanadamu ana uchu wa kuondoa kudhulumiwa. Zimbabwe, Namibia, Angola, kote mapambano yalikuwa ni almost 100% Christians against Christians lakini mmoja ni colonizer. Wasaudia waliwapiga na kuwaondoa waturuki kwa ili hali wote ni moslems 100%.

Please be very objective unapo-analyse such issues.

Wickama, Salamu ndugu yangu.Naomba unifahamu kwamba mimi sijatengeneza theory yeyote.Hiyo ni fact ambayo ukifanya research kidogo kwenye hayo makubaliano ya Berlin utaikuta.Vilevile ukidurusu historia wanayosimulia wakoloni wenyewe utakuta wameelezea kwamba walipata resistance kubwa sana kwenye maeneo yenye waislamu wengi.Ideology ya uislamu kufanya dhulma ni dhambi na kukubali kufanyiwa dhulma vilevile ni dhambi,hii dhana wakoloni wamagharibi wakiijua vema.Kumbuka ustaarabu wa kiislamu ulishawahi kutawala sehemu nyingi za ulaya.

Ahsanta.
 
Nanren,soma katika makubaliano ya Berlin 1884-5 hicho kipengele kipo.tuliposomeshwa historia shuleni kilifichwa makusudi

Uthman
Kuwapo kwa resistance katika maeneo yaliyokuwa na waislam wengi haina maana kuwa lengo la ukoloni lilikuwa ni kuudhibiti uislam. Sababu za ukoloni zilikuwa "purely economical"
Ndio maana nikauuliza je walienda Sri lanka na Nepal kudhibiti hinduism? walienda Mynamar, Thailand kudhibiti buddhism?
Na kama mkuu Wickama hapo juu alivyo kueleza, je juhudi za uhuru kwenye nchi kama Botswana, Angola, Zimbababwe, Zambia huoni kama ni juhudi za christians (wazalendo) dhidi ya other christians (wakoloni)?
Au unaona ilikuwa ni waislam (wananchi) dhidi ya wakristo (wakoloni)?
 
Last edited by a moderator:
Ritz,
Mie si wa kujibizana na huyu.

Hana moja alijualo katika hayo ayazungumzayo.

Rashid Kayugwa kabla hajafa aliwaeleza Waislam
mpango mzima ulivyosukwa.

Kayugwa alistaghfiru na akawa anaswali Mtoro hadi
umauti ulipomfika.

Huyu mtu anaejidai anajua sana nakuachieni nyie.

Mzee wetu MS kuliko kusema Nguruvi3 anajidai anajua sana ni vema ungempinga kwa hoja ili sisi wanafunzi tuzidi kufaidika, asante
 
Last edited by a moderator:
Gombesugu,
Jana nilialikwa Radio Al Nur Masjid Sahaba Zanzibar nifanye
kumbukumbu ya marehemu Ally Sykes tulikwenda mubashara.

Tulikuwa live.

Jamaa walisisimka sana na zilopoanza simu ndiyo ikawa hekaheka
nguo kuchanika.

Nilifungua na uhusiano wa Ally Sykes na Zanzibar Club 1950 akiwa
na uhusiano na akina Himidi Msoma, Dr. Hassan Kingwaba, Dr.
Ahmed Rashid, Ahmed Rashad Ali, Ali Muhsin, Abdillah Masoud Smuts,
Ali Khamis, Mzee Mwinyi Mpiringo, Wadud na wengine wengi.

Nikamaliza na yaliyotokea baada ya mapinduzi...

Sheikh Mohammed,

Asalaam alaykum Al Akhiy.

Nipokelea bayana yangu hii adimu kwako.

Nafurahika mno kusikia safari yako hiyo ulofanza kwenda amkuana na nduguzo pale Unguja/Visiwani. Sisi soote ni wamoja tangia dahri nyingi mno.

Ndo maana hata Sheikh Hassan Bin Amir alipoamua kutulizana hapo Mzizima,hakuwa "muhamiaji" asilan. Alikuwapo hapo kwa nduguze wakaribu mno/Wazee wetu. Ndipo ukaona kila nyumba alojaaliwa kupiga hodi,akifunguliwa milango kwa mapana yoote na bashaha yenye tunu.

Pana mengi ya kunena,lakini kwa sasa tuendelee na hii zilzala ilopo hapa jamvini.

Insha Allah,Mola takuongezea faraja na takrima nyingi kwenye hizi jitihada zako za kutufumbua macho nduguzo.

Ahsanta.
 
Gombesugu,
Ahsante ndugu yangu kwa maneno yako mazuri.

Hata sijakaa vyema hii asubuhi simu inaita jamaa
Masjid Sahaba Radio Al Nur wananiomba nende
nikafanye mahojiano na Mkurugenzi wa Radio.

Nimeitika mwito.

Tumefanya kipindi kuhusu Ahmed Rashad Ali na
mchango wake katika harakati za uhuru Afrikawakati akiendesha Radio Afrika Huru kutoka Cairo

miaka ya 1950.

Hii ni radio aloanzisha Gamal Abdel Nasser mwaka
1952 kufanya propaganda kwa niaba ya nchi zile
zilizokuwa ziko chini ya ukoloni.

Hizi ndizo taarifa kutoka Zanzibar.

Back
Top Bottom