Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

I would have been returned again and again if it were not for the transfer, which was my punishment for being with Julius Nyerere among the seventeen founder

Why Nyerere and not OWN brother?????

But we had established our status as a mandate territory in 1950 when Abdulwahid, HamzaMwapachu, Stephen Mhando and Dr. Kyaruzi took over the leadership of TAA.


MS; This is a good story. I did not realize storming into the offices of TAA actually won US mandate as a territory. This Abdul..... was a RAMBO.

Strangely here, these others missed out, they don't remember;

Tanganyika

After the Peace Treaty with Germany signed at Versailles on June 28, 1919, Great Britain undertook, under the mandate of the League of Nations, to administer the former German colony

In 1920, by the Tanganyika Order in Council, 1920, the Office of Governor and Commander-in-Chief of the Territory was constituted. The administration of the Territory continued to be carried out under the terms of the mandate until its transfer to the Trusteeship System under the Charter of the United Nations by the Trusteeship Agreement of December 13, 1946.
In 1946 Tanganyika was approved as a TRUST TERRITORY by the United Nations, in succession of the League of Nations, entrusted to Great Britain. In 1948, a constitutional reform resulted in African and Asian representation in the Legislative Council (established in 1926).
In 1954, JULIUS NYERERE established the TANU (Tanganyika African National Union) which emerged as the dominant political party in the elections of 1958 and 1960. In 1961, independence was proclaimed.


No trace of Rambo here...
 
Code:
Very few people are aware that the speech, which Nyerere delivered before theTrusteeship Council of the United Nations in 1955, was in TAA files since 1950...

No wonder some guys lost the election for TAA in 1953. A Good speech, lying in the TAA files for 5 years!!!! UNUSED. The new leader (Julius) comes in sees value in it, corrects the grammar and off-to New York with it, after some 5 years of cold storage.

Dennis Phombe was right.
 
Gombesugu na Sheikh Farid.
Inaonekana neno msaliti na mnafiki kwa Sheikh Amir limewaudhi sana.
Pengine ni kwa kujua kuwa alikuwa kiongozi wa dini na pia siasa kwa waislam basi hapo yapo maudhi.
Msisahau kuwa alikuwa mufti wa Tanganyika pia.

Maneno hayo si matusi na ninazo sababu
1. Msaliti ni mtu aendae kinyume na wenzake au anayewauza wenzake au afanyae mambo nyuma ya migongo ya wenzie.
2. Mnafiki, ni yule anyetenda kinyume au anayelaghai wenzake kwa ghilaba ima kufarahisha au kuwaghilibu

Sheikh Amir ni mwanasiasa na kiongozi wa dini. Alipokuja Tanganyika aliona waislam wakiwa wamedhulumiwa kwa elimu na Wakoloni(ref Ziddy). Jitihada zake zilikuwa kutoa elimu. Katika kufanya hivyo alijikuta katika Political sub committee kama mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika Dar es Salaam(ref Mohamed).

Wajumbe wa sub committee alikuwepo Abdul Sykes ambaye siku moja kabla ya uchaguzi Anatogluo alisema wanampa uongozi mtu wasiyemjua na itakuwa vigumu kumuondoa Nyerere (Mohamed). Kwa mantiki yeye alikuwa miongoni wa walioamua kuhusu uongozi(Mohamed)

Issa Ziddy anaeleza kuwa Amir alikuwa na mchango katika uanzishaji wa Al-dawafia Islamiyya, Jamiya islamiyya fil Tanganyika, EAMWS.Kwa pamoja Mohamed na Ziddy wanamwelezea kama kiongozi wa dini na Mwanasiasa

Baada ya Uhuru Sheikh alipewa fursa na Nyerere ya kuwa katika baraza. Akakataa kuchukua nafasi hiyo.
Badala yake akaendeleza harakati zake za kisiasa misikitini.

Mohamed anasema akitoa darsa na Dawiya, hapo hapo anasema huyu alikuwa katika TAA sub polit comm!!!
Issa Ziddy anaeleza, baada ya kurudi safari ya Egypt iliyohusu chuo kikuu, Sheikh Amir alionywa kubadili mwenendo wa mawaidha yake ya kisiasa sheikh Commorian,ushahidi wa kuwa alikuwa anaendeleza siasa,tofsuti na utetezi wa Mohamed

Maandishi ya Mohamed yamekwepa kuongelea hoja ya Sheikh Amir kupewa fursa na Nyerere na kujikita zaidi ya kutimuliwa kwake tena kwa kusingizia kuundwa kwa EAMWS.

Kuvunjika kwa EAMWS kulianza na ufa Dar es Salaam kabla ya kuhamia Mikoani. Makundi ya Maulid yalikuwa ya Mnazi mmoja na Ilala. Kilichochagiza mtafaruku mikoani ni kutokana na matumizi mabaya ya fedha za EAMWS makao makuu!

Issa Ziddy ameonyesha kuwa kulikuwa na mgogoro wa kisiasa kati ya 'Sheikh Amir na mwanafunzi wake sheh Chaurembo kutokana na masuala ya siasa'. Huu pia ni ushahidi kuwa Amir alikuwa active politically akifanya kazi nyuma ya wanfunzi wake. Ni mgogoro huo pia ulioua jithada za kuanzisha chuo kikuu na wala si fitna ya Nyerere kama asemavyo Mohamed

Makundi yaliyojitenga yalipata nguvu za nje kwasababu tayari Sheikh Amir alikuwa anahubiri siasa na mikutano nje ya chama cha TANU.Makundi hayo yalichukizwa na siasa za chini chini nje ya zile za TANU walizozijua

Sasa kwanini ni msaliti!
Alipaswa kuwa ndani ya system ili kuzuia matatizo(kama yalikuwepo). Alitakiwa awe karibu sana na ''adui'' zake ili afahamu mambo ya kuunusuru uislam kama basi ilidhaniwa hivyo. Hakufanya hivyo na kukidhi maana ya neno msaliti.

Ni mnafiki kwasababu alikataa kufanya siasa huku akiendeleza siasa hizo hizo misikitini kwa kuwatumia watu aliowaita wanafunzi wake.

Kitendo cha kumkatalia Nyerere nafasi alizopewa huku akihubiri siasa kama alivyonywa na Comorian (Ziddy) ni cha kinafiki na kinakidhi maana ya neno hilo.

Kwanini watu wanachukia kusikia msaliti na mnafiki?

Watu wanaochukia kusikia hayo ni wasaliti na wanafiki pia.
Kuna post katika nyuzi hii wametukanwa viongozi wa dini na wazee.

Mathalan,Mufti wa BAKWATA ana elimu gani mbumbu mkubwa, zumbukuku n.k.
Sheikh Hemed bin Jumaa alikuwa Kibaraka wa serikali, Shehe wa Tanga alikuwa Punda wa mapinduzi,
Nyerere laanatulah alikuwa mnafiki, msaliti, habithi na fidhuli.

Wazee hao wakitukanwa ilionekana kama maneno matamu na wala si matusi, vipi leo Sheikh Amir akiambiwa maneno yale yale aliyoambiwa mufti wa BAKWATA, Hemed bin Jumaa, Nyerere ionekane kama ametusiwa?
Hapo hakuna unafiki kweli!!!

Ni mwendo ule ule wa kusema Sheikh Amir alikuwa walii kwahiyo anapaswa kupewa hishma ya darja.
Kama waislam wameamua hivyo haina lalam, kuhoji au kuuliza. Ni kwa mujibu wa imani yao na wanahaki hiyo.
Vipi basi Wakatoliki wakisema Nyerere ni saint wao, waislam hao hao(baadhi) washupalie na kulihusisha na siasa?

Je, ni halali kusema Sheikh Amir aliyekuwa TAA sub pol comm alipewa Uwalii kwasababu ya harakati zake za kisiasa kabla na baada ya uhuru! Endapo sivyo kwanini Nyerere aonekane kupewa u-saint kwasababu ya siasa za kuungamiza Uislam

Nimalizie kwa kusema, haki uliyo nayo mtu ndiyo aliyo nayo mwingine.
Hakuna haki ya kutukana wazee wengine na batwil ya kutukanwa baadhi yao.

Tukishakubaliana hivyo, sasa tuombe radhi sote na kwa wote, la sivyo msaliti na mnafiki si matusi! tunayatumia sote kila siku na hakuna namna ya kuchagua wapi litumike na wapi linawajaza watu upepo.

Pamoja na kashfa na kejeli zako Gombesugu mimi nshakuswamehe maana sisi ni viumbe dhaifu na hatuna utimilifu.
Upanga wangu una makali sehemu mbili, wenzangu makali yenu sehemu moja na hapo ndipo tunapohitilifiana.
 

Wickama,
Ingelikuwa umekuja na maneno ya kistaarabu tungeliweza kwa
pamoja kufanya majadiliano mazuri na jamvi lingependeza.

Faida kubwa ingepatikana hata kama labda usingekubaliana nami.

Ningependa kukufahamisha kuwa mimi si mtu wa shari wa kutupiana
matusi.

Bahati mbaya umekuja na hamaki, kebehi na kejeli kwa hiyo
kwangu inakuwa tabu kujibu kejeli.
 

Sawa Mzee MS; Wakati mwingine inabidi kutokana na masimulizi ya WAZEE WANGU PIA. HAYA TUPISHE SIKU IPITE. ANOTHER TIME. WITH APOLOGIES.
 
Mzee MS;

Nadhani unanidai maelezo kidogo kwanini nime-treat ile narration yako-Ally na unachoita Kebehi. Nimeisoma kwa makini sana, nikamgundua kuwa alikuwa ana-associate madhila yake tu na Nyerere lakini mema yake ana-associate na Abdulwahid. Yaani kwa mfano mandate ya nchi (this is debatable) Abdul. Taabu ya transfer...... Ghafla anajitokeza na hotuba ya UN ambayo alipaswa kuona aibu kuwa waliiatamia for 5 years.At that point nikakumbuka huyu mzee alikuwa anaongea wewe unamnasa. Yaelekea kwenye editing ulikuwa huru kiasi. Staili ya ku-associate Nyerere na all evils at least tunajua ni your Hallmark, Kwa hiyo kitabu kile NI CHAKO bwana. You just used the guy to pour out more venom. Your ridiculing style of Nyerere in Ally's book is again the same. In life naelewa kwamba statistical chances of two independent authors coming out with similar venom against Julius in much the same style in published books (same style????) are just neglible. Nimepoteza hata appetite ya kukisoma.

If you care for honesty.
 

Nguruvi3,

Hakuna anakasirika wewe kumuita Sheikh Hassan Bin Amir mnafiki, mchochezi, mshenzi, na kejeli na kashfa zingine watu wanakushangaa wewe kuyaandika hayo maneno kutokana na heshima unayopewa humu JF.

Kuna watu wanamtuka Mtume wetu Mohammad matusi ya nguoni sembuse Mufti Hassan Bin Amir.

Lakini unamsoma na anayetukana unamuona MaxShimba, unapuuza au Yesu anatukanwa unamsoma nani Malariasugu unapuuza.

Pomoja kuwa kisu chako kinakata potepote na una haki ya kuandika chochote watu watakusoma vizuri lakini kumbuka huwezi kumtetea Nyerere kwa kurudisha matusi na kejeli na lugha zisizokuwa za kiungwana, kuna watu wakitoa lugha za ivyo hakuna tatizo lakini kama unaona njia unayoitumia ni sahihi kwako hakuna tatizo.

Tusemezane tuendelee na mnakasha...
 
Last edited by a moderator:
Kwa heshima ya Wickama na Yericko, sitakujibu tena. Pole mwenyewe!

Jasusi.

Nami nashukuru kwa hilo kwani bila watu kunisihi ningeweka hapa jamvini majina yote ya waTz waliopitia na ku graduate Carleton University uone uongo wako upo wapi.

Kwani Carleton ni sawa na Muhimbili University si kila mtu anayesoma hapo basi lazima afanye Degree wapo wa certificate na diploma pia japo wote wanatumia majengo hayo hayo.
 


Siku zote ukimuona mtu mwenye akili zake timamu anaanza kuporomosha matusi katika mnakasha jua AMEISHIWA HOJA. waungwana wanamsamehe na kama upo karibu naye akiwa amesimama unatakiwa umwambie akae na mpe maji gjasi moja atulize koo.
 
Siku zote ukimuona mtu mwenye akili zake timamu anaanza kuporomosha matusi katika mnakasha jua AMEISHIWA HOJA. waungwana wanamsamehe na kama upo karibu naye akiwa amesimama unatakiwa umwambie akae na mpe maji gjasi moja atulize koo.

Barubaru,

Hakuna mtu anayeweza kumzuia mtu kutoa kejeli na matusi, kuna vichwa vya kila aina nenda jukwaa la dini kuna vichwa huko kazi yao kutukanana tu mwanzo mwisho cha kushangaza hakuna anayechukia baadhi ya members wakiwa hawapo wanauliziana.

Sasa ndugu yetu Nguruvi3 ni mtu wa aina gani ni mtu ambaye anaandika mengi humu JF mimi binafsi pamoja kuwa tunapinga lakini jukwaa la Great Thinkers tunakuwa pamoja na ninamsoma sana na tunapashana habari, akitoa lugha za ivyo lazima watu tushangae siyo kukasirika kama anavyodhani.
 

Wickama,

Usipende kuwafuatisha mno hao Waingereza na "History yao" waliyotengeneza na kututaka dunia nzima tuijue na kufuata propaganda zao,kama vile walivyo-condense na ku-manipulate mindset za Wananchi wao.

Wewe ni "Msomi wa hali ya juu",jaribu kuwa na uangalifu unaposoma baadhi ya vitu. Au unataka kuwa kama sisi Wanafunzi wa Sheikh Mohammed Said...yaani "unameza tu ngano nzima nzima"!?ahaha!!

Kwa kifupi ndugu yangu hizo topics na khabari za unafiki,urongo na dhuluma za Waingereza ni mwingi mno na wala hatuwezi kumalizia hata kiduchu kwa hapa jamvini.

Kwa mfano miaka hiyo hiyo unayodai wewe yakuwa ati Waingereza ndo walikua "wakikataza" na kuweka "sharia" za kupinga utumwa;sasa si unajua yakuwa huo utumwa pia ulikua ukiendelea kwa kiwango kikubwa ndani ya hiyohiyo Uingereza yenyewe!?

Hapa bado hatujagusia baadhi ya sehemu mbalimbali za West Indies/Carribean ambako,Utumwa ulikuwa ukiendelezwa na ma-Aristocracy wa Kiingereza as early as late 1950's. Hao jamaa walikua na influences/connections kubwa katika Serikali na Upper Class ya pale UK...na unyama/utumwa woote walokua wakifanza,hiyo Serikali ya Uk ilikua ikijua kiundani na kufumbia macho!

Nina hakika unaijua Historia ya Ulimwengu vizuri...embu chungulia ile slavery/child labour walokua wakifanyiwa watoto waduchu/under age maskini na wazazi wao khasa kule Wales na Ireland-North/South yoote. Ninahisi utabubujikwa na machozi japo kiduchu!?

Haya yoote yalikua yakiendelea kwa wingi mno na bila ya kificho mpaka early 1900's...kwa hiyo lazim pia ufahamu yakuwa hao Waingereza, hizo khabari zao za ati kutunga "sharia" ya kitu fulani ndo shughuli zao kila kukicha...tatizo limo kwenye kuhusika kwao. Pia efficiency,implementation,effectiveness ya hizo "sharia zao" walizotunga ina utata mwingi mno! Haya mambo ni mazito ndugu yangu. Waingereza ni wazandik tu mpaka kesho na wao wenyewe wanalijua hili. Wao ndo walochangia na kusababisha kwa kiasi kikubwa hili zogo na vitimbi vyoote vitokeavyo sasa takriban kila pembe ya dunia.

Chungulia pia dhiki,mateso,Utumwa,dhuluma na prostitution ilivyokua imetamalaki katika mji uliokua mchafu na wenye kunuka kuliko yoote katika dunia nzima wakti huo...LONDON!!

Niwie radhi,usijefikiri nimechangia kipande hiki ili kuanzisha malumbano na songombingo nawe,hasha ndugu yangu!

Shukran.

Cc;JokaKuu,Ritz
 
Mkuu gombesugu, hapo kwenye red umeugusa moyo wangu! ni maneno mazuri ya ndugu zetu wahehe!

Maulaga,

Salaam ndugu yangu. Nimefurahi umefarijika japo kiduchu.

Hii yaonyesha yakuwa sisi soote ni wamoja na ni muhimu kushikamana,bila ya kujali mitazamo yetu tafauti ya kidini,makabila,dasturi,koo,tamaduni,itikadi za kisiasa,urangi na mengineyo mengi mno.

Nakujuza yakuwa pia nazungumza na Kihaya kiduchu!ahaha!!

Nakutakia siku njema ndugu yangu.

Ahsanta.
 

Gombesugu; Wala hujaanzisha malumbano. Utumwa ulikuwapo kwenye historia ya WATU, UPO, na HAUTAKWISHA, utabadili rangi, mfumo, na majina. Hayo mbali, Chukulia hivi Kuna Biashara mbili za Watumwa zilipamba Moto kwenye bara hili. Moja ilikuwa kwenye hizi pwani zetu. Nyingine afrika magharibi.

MABWANA WAKUBWA WAMEEITA ILE YA KULEEE!!!! walikoshiriki WAO kamaWEST AFRICAN SLAVE TRADE HII YA HAPA ilyowahusisha kina Al-Maaruf..... IMEITWA EAST AFRICA ARAB SLAVE TRADE Neno Arab ni muhimu katika kuipa hiyo biashara daraja zaidi. Umenipata? Sasa tumeshaelekezwa sera fulani, mwenye kuumizwa tumeshaambiwa humu JF ANDIKA KITABU!!!!! then ukiite WEST AFRICA EUROPEAN SLAVE TRADE; hahahahahah. Zama hizo hakukuwa na JF labda unge-post some materials. Nimekuelewa sana unachosema.

Nakushukuru ndugu yangu, wikiend njema
 

Barubaru; Shukran sana kwa ku-cool down. Infact mnaweza kutoana jasho over a person ambaye for reasons known to those who sent him/her there might have been using a different name (even nationality)for safety or otherwise based on the advice given at that time. Mwaweza kesha mnaumizana while you are all correct. Thanks.
 




Muheshimiwa Nguruvi3,

Shukran nimesoma bayana yako kwa makini. Nimeziona kwa kituo hizo hoja na sababu zako.

Nimekufahamu msimamo wako wa kutaka "fursa" ya kuendeleza matusi na kashfa dhidi ya Al Maaruf Mufti Sheikh Hassan Bin Amir Al Shirazy.

Hili pia haina neno ndugu yangu, kwani "haki yako" na maamuzi ndo muhimu. Nafikiri nilishakufahamisha tangia jana.

Umefanza uzuri pia kuonesha/kutaja yakuwa kuna baadhi ya wengine/wenzio hapa jamvini, nao pia hutukana Viongozi wa Kidini. Nafikiri wakisoma bayana yako watakua washapata salamuzo na kujirekebisha japo kiduchu.

Nguruvi3,pole zako kama umepatwa na dhuluma na madhila kwa bayana zangu. Ama kwa hakika haikuwa makusudio yangu asilan kukukera ndugu yangu. Niwie radhi mno.

Kutokana na mahaba na hishma nilonayo kwako ndo nilichukua ile fursa kukuasa/kukukanya. Labda ile lugha nilotumia ndo haikua nyepesi au yenye kupendeza kwako.

Asilan situmii kashfa wala kejeli dhidi yako. Ni yale mas'khara yetu tu,khasa kati yangu nawe tufanzianayo kila mara hapa jamvini,tena kwa vicheko na furaha ndugu yangu.

Natumai utaridhika na vijielezo vyangu vyenye uchechefu mwingi.

Tuendelee na mnakasha.

Nakushukuru mno,nakutakia siku njema.

Ahsanta.
 
Natamani kuishi katika Tanzania yenye mtazamo kama huu. Basi uzi huu na ulete haya matamanio.
 

Nguruvi; Shukrani sana
Naikumbuka sana hii Paper ya Dr Ziddy. Sehemu ambayo ilinipa HINT kuwa EAMWS kulikuwa na matatizo ni aina ya madai ya ile MIKOA iliyojitoa. Yaani ili warudi nini kifanyike;
1. Kwamba waelewe matumizi na mapato ya EAMWS (Hili sina tatizo nalo, why not????? Lakini inaashiria kulikuwa na aina fulani wao kutojua Mgao wa mkoa fulani ni upi, nani kapewa nini na kwanini na vitu kama hivyo. Hii ni very legitimate advice)
2. Wanataka EAMWS ya TZ (hawa walishachoka kupokea aina fulani ya chain of command toka Mombasa-Hqts) Infact hata matatizo yalipoanza Dr. Ziddy kasema vizuri kuwa Headquarters za EAMWS zilijitahidi lakin zikashindwa. Na hiyo pia could be a problem, kwamba kama mna association, headquarters ziko Namibia, in case of conflict huwa inakuwa tatizo ku-manage kwa haraka. Labda siku hizi za internet na video conferences.
3. Wanataka iongozwe na waafrika. Hii ilimuuma sana Sheikh kwa vile ilikuwa ya kibaguzi (hata mimi siiungi mkono)Inaelekea ilimlenga mhindi aliyekuwa nao kama kiongozi pia. Lakini pia ni enzi tuu baada ya uhuru, kwa hiyo hawa walikuwa na feelings za kiafrika zaidi ya ujumla wa KIDINI
4. Wanataka viongozi wa EAMWS wawe supporters wa TANU (hapa bwana mtu akatae akubali ndipo palikuwa wamegawanyika, meaning kuwa ndani yake kulikuwa na wapinzani wa TANU na Masheikh hawa wa Iringa, Bukoba na Tanga walikuwa na ujasiri wa kutoa political grievances zao).

Na zingine.

Ukimsoma vizuri daktari Ziddy, unaona kuwa siasa za wakatii huo zilimyumbisha sana Sheikh kiasi cha kugombana na wanafunzi wake juu ya SIASA ndiyo maana nimesha-hata mwambia Mzee wangu MS hapa kuwa Sheikh huyu alishauriwa vibaya kugoma mialiko ya kuwa in the cabinet ambapo angewasaidia kina Bibi Titi, kina Tewa, Kina Maswanya and others ku-address madhila ya Waislamu as a MINISTER!!!!!. Bahati nzuri alikuwa mtu very literate. Na no wonder paper imeonyesha kuwa hii political tension among NDIYO ILIYOUA MUSLIM UNIVERSITY dreams. Ndiyo maana hata hiyo maulid tayari wakapa kila mtu kivyake.

Hapa ilikosekana strategy. Silaha zilikuwapo tena tele.

Ama kuhusu Jinsi ya ku-address viongozi, Ni kweli kuwa kiongozi yeyote akiguswa lazima watu wajisikie taabu. Lakini la maana hapa ni kuwa;

1. Haitakuja kutokea dunia hii kuwa na dini moja. Mpaka kiama kinakuja watu watakuwa na madhehebu yao. The best we can do ni kuishi na kusubiri.
2. Kiongozi wa jamii fulani ni stahiki yake kuwa-addressed kwa heshima stahiki, humu wasomaji ni wengi wa dini tofauti
3. Ukianzisha trend ya kushusha heshima ya dhehebu au taratibu za wengine na viongozi wao, usishangae jamaa wakapumua wakaja na mawe juu ya kiongozi na dhehebu lako

Nimemsoma sana Nguruvi in the past. Posts very good stuff. Nadhani hii ni response ya some posts humu kila mara zinashambulia catholic church na ukatoliki (Julius kuwa saint etc) which i also cautioned kuwa hey-guys go slow!!!!
 
"Very few people are aware that the speech, which Nyerere delivered before theTrusteeship Council of the United Nations in 1955, was in TAA files since 1950..."Tangu mwaka 1950 hotuba ileile, maneno yaleyale, hadhira ileile! Hongereni akina Sykes! Mungu azilaze roho zenu mahali pema peponi. Amen.
 
gombesugu,

..wala siwezi kubishana na wewe kwamba MTUME alikataza utumwa.

..dini zote zinakataza na kulaani maovu mbalimbali.

..pamoja na hayo bado kuna vichwa maji miongoni mwa wanadamu ambao hawafuati mafundisho ya dini zao.
 
Last edited by a moderator:
Kadogoo,

..kwa uelewa wangu upande wa Afrika Magharibi vinara ya biashara hiyo walikuwa ni Wazungu.

..huu upande wa Afrika Mashariki Mwarabu ndiye aliyekuwa kinara wa shughuli hizo.

..ushahidi mzito zaidi kwamba Mwarabu amehusika ktk eneo la Afrika Mashariki, na hususan Tanganyika na Zanzibar, ni kitendo cha Sultani wa Zanzibar kulazimika kusaini mikataba[moresby treaty + hamerton treaty]miwili inayozuia biashara ya utumwa.



cc: Mag3, gombesugu, Nguruvi3, Wickama
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…