Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kweli unafikiri wakristu wa Tanzania wamekuwa 'taken care of'? Really?



Ndio maana tunakukatalia; hapa hujaweka alichosema Sivalon; umeweka review ya mtu mwingine kuhusu kitabu cha Sivalon...
 
naam shekhe...!
Wanipa raha sana,mnakasha ukipotea wewe waurudisha kwenye track,,
yan wakisima nchale wakikaa nchalee..!
Yani hoja kwa hoja,bali wengi wao si wenye kuutaka ukweli,ila wewe wape tuh kwa manufaa ya wengi.
Nina hakika wewe hata ukweli ukikuchungulia usoni hutauona wala kuutambua na kwenye mjadala huu naona hata pale ukweli unapokugongea hodi, hata kuufungulia hutaki. Nawapa ushauri mashabiki wa Mohamed Said mkae pembeni mshuhudie simulizi zake za kichochezi na za kuungwaungwa zinavyokosolewa. Msiwe kama mashabiki wanaomsifia mfalme kwa umaridadi huku anatembea mtupu, sana sana mshaurieni achutame.
 

Niliwahi kumuuliza Mohamed, na anikosoe kama siseme kweli, kama yeye anajiona Mtanzania kwanza au Muislamu kwanza.
Alinijibu yeye anajiona Muislamu kwanza. Kwa mantiki hii, leo akinikuta mimi Mtanzania nisiye muislamu nagombana na taleban, yeye atajiunga upande wa taleban kunipiga mimi Mtanzania mwenzake.
 

Nitapatanisha.
Nitaingia upande wa Taliban kama wewe ni dhalim.
 
kaka Yericko Nyerere,bado tunasubiri
majina ya hao waasi waliopewa vyeo na kuwa mabalozi.Ulituahidi kutuletea majina.
Vinginevyo ili tusikuite muongo na mzushi,tutake radhi hapa jamvini kuwa uliongopa
cc
@
Ritz Barubaru kichwakigumu@ THE BIG SHOW
 
Last edited by a moderator:

asante
 

Mag3,

Wakuchutama huwaoni walishachutama siku nyingi.
Wakiiogopa historia ya uhuru wa Tanganyika.

Sisi tunatembea leo kifua mbele.

Mwezi wa Ramadhani.
Nimealikwa kijimsikiti kidogo nikahadhir.

Nimefika pale msikiti umejaa mpaka nje.

Imam ananitambulisha anasema.

Waislam maskini vijijini wanakodi jenereta na inafungwa
katika baiskeli wanakwenda kijiji hadi kijiji wana DVD ya
Mohamed Said wanawaonesha Waislam historia yao.

Nilikuwa nimefuatana na mjomba wangu maneno yale
yamemchoma kanikumbatia analia.

Wakati tunarejea mjini ananambia mjomba mie nalia maana
pale ulipomtaja Abdu Sykes namuona Nyerere anaingia ofisini
kwake pale sokoni 1953/54.

Leo unanambia kasahau cheo chake katika TAA?

Huyu mjomba wangu alikuwa akifanya biashara pale enzi zile.
 

Umekosea kama unadhani hadhi yangu inatokana na kitabu.
Hadhi katika wasomi.

Labda.

Mimi kama hiyo hadhi ninayo basi ni kwa kuwa nafahamika.
Na wazee wangu wanafahamika.

Na Dar es Salaam ndiyo kwetu.

Sikuja Dar es Salaam kutafuta kazi wala kucheza mpira.
 
TEH TEH TEH BABU NAYE YUPO.LAKINI HAPA HATII MGUU WALA PUA.HILI DARSA LA Mohamed Said MAJI YA KINA KIREFU
 
Last edited by a moderator:

Hahahahhhaaaaa.
Me love this.....ok, tuendeleee.
Mi nasoma tu, ila hapa nimefurahi ikanibidi nicheke.
 

Kitu kimoja nisichokikubali kuhusu hizi dini zetu ni kuwa kwa kiasi kikubwa hadithi na maandishi yanaendana na mazingira ya kule ambapo ni chimbuko la didni hiyo, viongozi wengi wa dini wanashindwa kupata tafsiri halisi kwa kuchukilia mambo katika hali ya kimwili zaidi kuliko kiroho. Wengi tunapotea, tujiulize wenzetu wa India, China na kwingineko wao vp? (wao ni makafiri na wapagani?)
 

Kama kawaida yako.

Its like finding a needle in a haystack.

Nitakujibu moja tu.
La Nyerere maana hilo ndilo ulipendalo.

Hakuna awezae kushusha hadhi ya Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hapo hakuna ubishi.

Lakini historia ya uhuru haikuanza na yeye.
Historia ya TANU haiwezi kuanza na Nyerere 1954 kama ilivyogongomewa.

Historia rasmi imewaacha wengi nje na hao wengi ni wazee wangu.
Hawakufurahi na hilo ndiyo maana wakataka nirekebishe historia hiyo.

Hata kama Nyerere atakasirika.

Hapa ndipo paliponifanya ninyanyue kalamu.
Ndiyo maana leo nimo humu jamvini natoa darsa na kipande ninachodarsisha ni 1929 - 1961.
 
Kaka kuna tofauti kubwa kati ya malezi na ustaarabu wa Musoma na Dar es Salaam. Pwani mtu yeyote mwenye umri wa baba yake ni mzee wako.

Tuendelee kusemezana.
Siku za nyuma tulipambana hapa na MS kuhusu Nyerere kama baba wa Taifa. Mashabiki wake walitoa mapovu wakidai kuwa kwa watu wa pwani hasa waislam, "baba" ni yule aliyekuzaa tu. Hakuna kigezo kingine. Bahati mbaya papara zao zikamwabisha mzee MS kwa sababu tulibainisha jinsi anavyoiwaita "baba" wazee wa gerezani. Sasa kuweni makini hata mnapoteteana kwa ushabiki, msiji-contradict.
 
Sidhani kama MS anazungumzia namba. Fulani wa kwanza na yule wa ... Anazungumzia dhulma hadi ya kiuandishi. Anaandikwa mesi tu utadhani alicheza peke yake. Na hili mnalijua, lipo wazi, ila mnalipotezea tu.
 

na hapo ndipo histohisia yake inapochimbuka
 

Huo uwanja wa maulamaa.
Ila hoja hizo zina umri sawa na Uislam wenyewe.

Hoja zimeshindwa Uislam upo hadi leo.
Alhamdulilah.
 
Hahahahhhaaaaa.
Me love this.....ok, tuendeleee.
Mi nasoma tu, ila hapa nimefurahi ikanibidi nicheke.

What a contrast.
My uncle shed tears.

He knew both of them and how close they were to each other.

As we drove back he kept asking me, ''Mohamed what really happened?''
 
Kweli unafikiri wakristu wa Tanzania wamekuwa 'taken care of'? Really?




Ndio maana tunakukatalia; hapa hujaweka alichosema Sivalon; umeweka review ya mtu mwingine kuhusu kitabu cha Sivalon...

Hapana haja ya kuvutana na hiyo.
Achilia mbali iwe ''review'' ambayo siyo.

Tuseme Sivalon kasema uongo.
Hata hiyo mimi sina shida.

Simo humu kushinda ubishi.

Humu kuna watu 13, 000+ wanasikiliza.
Kwa wale waliokuwa hawana taarifa ya rejea hii.

Sasa wamekuwa werevu zaidi kulipo walipoingia...
Watatoka na manufaa katika hii darsa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…