Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Kadogoo,
Sijui kama wana uhusiano.
 

Kadogoo
Huyu Bwana mdogo @Yericko ni mtu wa ajabu sana,
Tena ni kama vile hajielewi,nashangaa tukiwa sote kule kwenye ukamanda wa chadema na pro-chadema wenzetu tunaupinga mwenge na kuimba nyimbo za ufisadi za kuibeza ccm,tukiwa hapa kwenye kuelezea historia za wazee wetu anageuka na kuanza kuutukuza mwenge huo wa uhuru..!
You know yericko anayafanya haya kwa hapa kwa kuwa amejivika chuki za wazi wazi na yupo vitani kweli kweli,
Ameshageuza hapa kama ni uwanja wa crusade vs jihadi,thats why atatumia kila aina ya makombora ili mradi ajihakikishie ushindi,lakin anasahau ya kwamba historia ya kweli haifichiki,na chuki ni ngumu pia kuificha,ni wazi tumeiona chuki yake binafsi na rangi yake halisi...
 
Last edited by a moderator:

Kuwepo kwa faida au kutokuwepo faida ya Mwenge wa Uhuru leo hii ni jambo jingine,

Hapa tunazungumza historia na historia ni katili sana, hata kama kitu utakikana leo lakini historia itabaki huru kwacho!
 
Last edited by a moderator:

Nilipo Underline.

Hakika nimeupenda sana huo usemi kwani nasi tunapata darsa zuri sana la Historia sahihi ya Tanganyika iliyosahaulika kwa nia maalum.
Ahsantum nasi ndio tunakwenda mbio sana kupata darsa.

Ahsantum.

 

Mag3 mbona povu linakutoka naona umeamuwa kuwaorodhesha makamanda hapo juu lakini jinsi ulivyo kuwa na chuki na uislamu mbona kuna kamanda umemsahau THE BIG SHOW au kwasababu hakubaliani na hoja zako? Unaposema mzee MS ni mchochezi hivi unaweza kunionyesha mzee MS wapi aliwaambia watu wakafanye vurugu,hivi dr Slaa alivyo waambia watu mwenyekiti wenu amewekwa ndani hivi makamanda mnakubali watu wakasema hatukubaliiiiiiii!akawaambia watu waende kituo cha polisi ndio yakatokea mauaji nani mchochezi kati ya mzee Mohamed said na Dr Slaa? hilo hulioni wewe na wenzako wanaokupa likes bila hata kutafakari umeandika nini au unataka kuniambia hawa kina NGURUVI3,JOKAKUU,GWALIHENZI,JASUSI,WICKAMA,NGONGO,ZUMBEMKUU,REMOTE,YERICKO na makamanda wengine kama munavyoitana akili zao ni sawa na za "kasuku" kwasababu kasuku kila analolisikia analisema bila ya kulifanyia utafiti na akili ya kasuku iko masikioni!ahsanta tuendelee na mnakasha.
 
Nilipo Underline.

Hakika nimeupenda sana huo usemi kwani nasi tunapata darsa zuri sana la Historia sahihi ya Tanganyika iliyosahaulika kwa nia maalum.
Ahsantum nasi ndio tunakwenda mbio sana kupata darsa.

Ahsantum.


Nikweli kabisa,

Hapa katika uzi huu kuna DARSA na DARASA,

Pia kuna Ilm na Elimu,

Kwahiyo tofautisha hao watu wawili wapatao hivyo vitu,

Kwangu mimi anaefyonza ELIMU katika DARASA hili ni mtu mhimu zaidi!

Lakini anaefyonza Ilm katika Darsa kwangu hana mafaa!
 

Mag3.

Nafikiri una mtazamo finyu katika mada hii. Kama umetazama kiundani sana utaona kuna mashindano makubwa sana ya UDINI na hili wewe angalia LIKES zinazotolewa.

Lakin kwa wasomi siku zote huwa tunaheshimu sana UTAFITI na kama mtu amefanya Utafiti lazim a tukubaliane naye na KAMA TUNATAKA KUPINGA BASI UTAFITI UNAPINGWA NA UTAFITI na sio Bla bla.

Mimi binafsi nimejifunza mengi sana katika huu mnakasha ambazo nilikuwa sijapata kuyasikia na nilipoulizia kwa wazee wakakubali kuwa kweli ni sahihi napenda sana Kumshukuru Al Alkhiy Mohamed Said kutufumbua macho na kuona kile kilichofichwa tena kwa usiri mkubwa. Allah akubarik Sana.

masikitiko angu ni kuwa kuna watu hawatetei ukweli bali wamejawa na USHABIKI wa KIDINI. jambo ambalo ni baa sana kwa mustakabali wa Taifa lenu.

Mag3.
Tanzania mimi ni kwangu kwani ndiko nilikozaliwa na kitovu changu kimezikwa Mwera Znz japo asili yangu ni Oman. Hiyo isikupe khofu. Nimewekeza na nina ndugu wengi huko na ndio maana mara kwa mara nakuja huko na siwezi kuacha kuja huko kwani niliondoka kwa baraka zote za wenyeji wangu na ndio maana natetea haki za wale wanaodhulumiwa huko.



 
Nilipo Underline.

Hakika nimeupenda sana huo usemi kwani nasi tunapata darsa zuri sana la Historia sahihi ya Tanganyika iliyosahaulika kwa nia maalum.
Ahsantum nasi ndio tunakwenda mbio sana kupata darsa.

Ahsantum.


"Najikinga kwa Mwenyezi Mungu nisiwe miongoni wa wajinga" Musa (Mtume wa wana wa Israeli)


Qur'an 2:67
 

Yericko.

Zisikutishe hizo lugha kwani inategemea mtu ametokea wapi.
Mathalan watu kutoka pwani. sokoni wanaita marikiti, Shule tunaita Skuli, Darasa tunaita Darsa, Elimu tunaita Ilmu.etc.

Ni sawa kabisa na watu kutoka kanda ya Ziwa, Ndama anaitwa kimori, Shule wanaita Shure, Kulala wanasema Kurara, safari wanasema safali etc.

Sasa usibague watu kwa mujibu wa lugha zao wewe angalia nini wamekusudia nini katika maandiko yao. Kwani Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu, zenyekubeba maana na zilizokubalika na jamii zitumike ili kuwasiliana.

Pole sana

 
Gombesugu,
Hayo maneno aloweka Shariff Ritz yanatoka katika shairi
la John Drydern.

Hayo ndiyo maneno nilofungulia kitabu changu.
Hakika lulu huipati sharti upige mbizi.
 
Barubaru,
Kila ninapopita humu jamvini ndivyo ninavyozidi kumshukuru Allah.

Maryland Washington...
Nimekaa hapo.

Alhamdulilah.
 
Yericko,
Umetaja mitaa miwili Kipata (sasa ni Mtaa wa Kleist Street) na Mkunguni.

Haya nitakayokueleza yatakuwa na "mafaa" kwako kama upendavyo kusema.
Yako mengi lakini nitanyambua kiduchu.

Tuanze na Kipata.

Kipata na Msimbazi nyumba ya kwanza ilikuwa ya Abdallah Matimbwa.
Huyu ni mmoja wa wanachama wa mwanzo TANU.

Abdallah Matimbwa ni mmoja wa waliochangia ujenzi wa kujenga Chuo Kikuu
Cha Dar es Salaam.

Baada ya uhuru alitoa gari yake kuanzisha ushirika wa CORETCO.

Bado tupo Kipata.
Kipata na Congo.

Nyumba ya kona kwa Abdallah Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association
1929.

Kipata na Nyamwezi.
Nyumba ya Mama Nambaya na mama yake Shabaka.

Nyumba ya mbele no. 32.
Hapa ndipo alipozaliwa Mohamed Said.

Kipata na Sikukukuu nyumba ya Mohamed Clement Mtamila katibu wa TAA wakati
wa Vita Vya Pili ni katika nyumba hii Nyerere aliwasilisha barua kutoka kwa Father
Walsh akishauriwa asomeshe au aache siasa.

Halmashauri Kuu ya TANU Mzee Mtamila akiwa mwenyekiti mmoja wa wajumbe
akiwa Bi Tatu Biti Mzee walikutana ndani ya nyumba hii na uamuzi ukapita Nyerere
ajiuzulu aje Dar es Salaam atakaa kwa Abdu Sykes hadi TANU itakapomtafutia nyumba.

Kipata huku Livingstone huko New Street.
Nyumbani kwa Kleist Sykes na wanae.

Hapa ndipo ulipokuwa umefichwa mtambo wa kuchapa makaratasi ya "uchochezi" na
mchapaji alikuwa Ally Sykes na mkewe Bi. Zainab.

Hapa yapo mengi na Nyerere alikuwa hapungui nyumba hii.
Mkabala na nyumba hii akiishi babu yangu.

Mkunguni na New Street.
Hapo unamkuta Hawa Biti Maftah unaijua nyimbo "Hongera Mwanangu?"

Huyo mwana anaepongezwa ni baba yako Julius Kambarage Nyerere na aliyekuwa akiimbisha
nyimbo hii mikutanoni ni Bi Hawa Biti Maftah.

Hapo hapo mbele ni nyumba ya Idd Tosiri.
Tosiri ndiye aliyempeleka Nyerere Bagamoyo kwenda kumjulisha kwa Sheikh Mohamed Ramia.

Yericko,
Usitudharau wala kujaribu kuwadhalilisha wazee wetu.
Hawa wameacha alama katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Unataka kuidhalilisha mitaa hii alokuwa akikanyaga Baba wa Taifa mitaa ambayo akiitembea
na wazee wetu?

Unataka kuifanya kichekesho Mtaa wa Kipata na Mkunguni ilhali mitaa hii ndiyo iliyomfikisha
Nyerere juu kileleni?

Jitulize na fikiri kabla hujaandika.
Ujuvi haukufai kijana.

Una miaka mingi ya kuishi Allah akipenda.
 
Wickama,
Jiulize kiwango cha "intelligence" yangu kwanza kabla hujaandika.

Sheikh Mohammed Said,

It takes academically enlightened and blessed individual like you Al Akhiy,to fully comprehend what remains blind to the rest of Tanganyikans/Tanzanians.

Thank you again for enlightening our mind,now the main question is what do we do with this knowledge together as Tanzanians.

Now we know why our History,the History of Wazee wetu was kept from us.

When I read these facts,I'm instantly instilled with inspiration,courage and pride in what Wazee wetu accomplished.

Ain't no time like the present. We have had people fighting for truths and our equal rights as citizens of Tanganyika/Tanzania for years,unfortunately,we have had sellouts too!

I think during Nyerere's regime people were bit scared for many valid reasons/atrocities,now they can meet the new Muslim generation.

Insha Allah,you will always remain blessed and truthfully to your Country.

Ahsanta.

Cc;Ritz
 

Shariff Ritz,

Ahsanta sana kwa bayana yako hii adimu iloambatana na huu mpini wa nguvu usobebeka asilan asilin!ahaha!!

Wallahi,mimi ninapoona makhanatha kama haya walotufanzia hao maluuni wa Kizungu(na mpaka leo wanaendelea kutufanzia!),halafu unakuta ati tunashinda hapa jamvini kutwa kucha, kulumbana na kukashifiana baina yetu/Watanzania...ni fedheha na simanzi nyingi mno khasa kwa wale tu wenye kujua undani wa majambo ya dunia!?

Haina neno tuendelee na mnakasha.

Nipenyezea kijisalaamu changu kwa ndugu yangu mpenzi Mag3;mwambie yakuwa leo nimezongwa kiduchu na vijishughuli vya kibaruani, lakini bayana yake naliipata na nimeipenda na kuifurahia mno. Insha Allah tamjibu kwa utuvu japo jioni ya leo au kesho.

Ahsanta.
 

Sheikh Mohammed,

Wallahi,inanilazim nitoe siri yangu...yaani nimeangua kicheko cha nguvu pita kiasi baada ya kusoma hii bayana yako adimu kwa nduguyo Yericko!ahaha!!

Nafikiri vitu au majambo kama haya ndo huwapa taabu nyingi za nyonyo hawa jamaa zetu.

Lakini,kwa mwenye maarifa ni kujiuliza kwani huyo Nyerere alipofika hapo Mzizima,alilala wapi!? Si hiyohiyo Kipata wanayoikashifu leo ndo ilomstiri!?

Au alikwenda kulala nyumbani kwa Governor Twinning!?

Niwie radhi Maalim wangu,leo nina vijishughuli kiduchu vimenitinga...lakini umbea tu umenishika,sishi kuchungulia hapa jamvini!ahaha!!

Ahsanta.

Cc;Al Khalifa The Big Show,Shariff Ritz,Ustadh Boko Ibn Haram
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…