Moja ya mambo ambayo huwa nayasoma na kuninyima raha hapa Jamii Forum ni baadhi ya wasomi kutumia vibaya elimu zao na kutumia nguvu zao zote kupotosha umma.
Katika biashara kuna aina mbili za ujasiriamali..constructive and destructive entrepreneurship Hata yule mama lishe anayeweka hamira kwenye ugali watu washibe kwa ugali kidogo naye ni mjasiriamali (destructive entrepreneurship , japo sio mjasiriamali tunayemtaka kwa maendeleo endelevu.
Kwa vigezo hivyo hivyo, msomi anayetumia usomi wake kuleta takwimu za kuonyesha wingi wa taasisi za kikristo pasipo kutuambia sababu naye ni msomi. Msomi anayetumia muda mwingi na nguvu zake zote kutafuta kila namna ya uhasi, maandiko ambayo hata kwa muktadha wake hayatuhusu watanzania lakini huyasoma na kutuonyesha kwamba ameyasoma, na mwisho kuyaleta kwetu kwa nia ya chuki naye ni msomi, ila ni bahati mbaya sio msomi tunayemtaka.
Niseme machache..Tanzania tunaelekea pabaya. Wasomi elimu zetu tunazitumia vibaya na hivyo tunaongozwa na hisia badala ya uhalisia. Maisha tunayachukulia kama mjadala (debate) tuliyokuwa tunafanya sekondari..upande unaopangwa either proposing or opposing ndio unaoutetea kwa nguvu zote, la muhimu ni upande wako ushinde.
Ebu kila mmoja wetu abadilike na kuwa mtu bora kwa ajili yake na jamii yake. Nchi hii nafasi mbona fursa ziko nyingi tu!
- Hivi mnafurahia nafasi za juu za makampuni makubwa kuchukuliwa na wazungu, wakenya, waganda, waghana, na wanigeria leo hii miaka 51 ya Uhuru?
- Hivi badala ya kujielimisha na kuelimisha jamii yetu kuwa bora kwa ajili ya kulinda tunu za nchi hii jibu limekuwa ni kuwashambuliana hata kwa hoja zilizo wazo na ukweli tunaoweza kutambua kwa usomi wetu?
- Tunapoteza nguvu nyingi kulinda hoja dhaifu hata nafsi zetu zinatusuta!
- Kwa nini huu moto wa udini tusiuanzishe dhidi ya makampuni ya madini yasiyolipa kodi na dhidi ya serikali kugawa rasilimali zetu?
- Hivi umaskini wa nyumbani kwetu kwa sababu ya matatizo ya wazazi kutokujipanga wakati fursa zilikuwepo unasababishwaje na maendeleo ya jirani na watoto wake aliyejipanga?
Siku ujinga huu ukituondoka na kutambua tumefanya makosa itakuwa ni too late! Kupigania kushinda debate na upande wako hata kama si sahihi ni damage kubwa sana kwa ustawi wa jamii ya Tanzania. Kila nisomapo upotoshaji wa kidini huishiwa nguvu ya kufanya chochote maana naona kama wanangu huko mbeleni wataishi kwa kuulizana wewe ni mkristo au muislam? Tujifunze kwa Rwanda juu ya athari ya ubaguzi ndani ya jamii. Kuna rafiki mnyarwanda nilimuuliza kabila lake kama ni mhutu au mtusi akanijibu kwamba baada ya mauaji ya kimbari hairuhusiwi kuuliza swali hilo hadharani. Hii imekuwa kama sheria na kweli hakuniambia mbali na kwamba sote tulikuwa nje ya Rwanda. Wanyarwanda sasa ni wamoja na wanasonga mbele. Najua kwa dini itakuwa ngumu kuficha lakini hii si kitu palipo na upendo.
Niwe wazi baadhi ya michango ya GT humu inanifanya nifikirie vibaya dhidi ya rafiki na ndugu zangu wa kiislamu lakini Mungu ananipa nguvu nazidi kuwapenda zaidi. Ila, mambo haya inabidi yaishe kwani maandiko matakatifu na misaafu yanasema...
mazoea mabaya hujenga tabia mbaya; pia jiweke mbali na dhambi. Haya maneno nimetohoa (paraphrase) kutoka kwenye Biblia na Kuran ili kuleta maana sawa kwa wote. Hivyo tukizoea kuongea kichuki chuki tutaishia kuishi kwa chuki.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake. Rejesha amani iliyopotea, upendo miongoni mwetu kwani sote ni wanao. Siafiki kupeana nafasi kwa kuzingatia udini wala ukabila. Akistahili mwislamu apewe hata kama kwenye idara hiyo waliotangulia wengi ni waislam vivyo hivyo akistahili mkristo apewe hata kama waliotangulia kwenye idara hiyo wengi ni wakristo. AMINA!
Issue hapa inatokana na Dhana ya Serikali kutokuwa na Dini au Serikali ya Kisekula Dhana hiyo ni maarufu Tanzania. Mara nyingi katika masuala yahusuyo dini, viongozi wa serikali husikika wakisema «serikali haina dini, ila wananchi wake wana dini zao ». Hoja ya usekula wa serikali ni ya kihistoria. Ilijengwa kiasi cha miaka miambili iliyopita ikitaka serikali ijiepushe na shughuli za kidini hususan katika masuala ya elimu, mafundisho ya maadili na na ibada.Japokuwa Tanzania imekuwa ikidai kwamba serikali yake ni ya kisekula, hali halisi haioneshi hivyo. Pamoja na madai hayo, serikali ya Tanzania imewahi kuingia katika msuguano na Waislamu na baadhi ya wasiokuwa waislamu pale Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipotaka kuanzisha somo la dini au maadili ya nchi. Kadhia hii ni maarufu kwa jina la "dini mseto". serikali ya kisekula haiwezi ikaja na mipango ya kusomesha dini kwa jina lolote lile liwe la maadili au vyovyote vile.