Nguruvi3,
Asante kwa taarifa hii. Mimi kitabu cha Ghassany kilinishinda kusoma baada ya ukurasa wa kwanza kwa sababu theme yake ni kwamba mapinduzi yalivunja uhuru wa Wazanzibari, hence the headline "kwa heri uhuru."
Jasusi, nakusihi uwe na moyo wa chuma ukisome. Tuhuma zote zimetupwa kwa mtu mmoja.
Utakapokisoma utakutana na maswali mengi yasiyo na majibu kama tulivyoona katika mnakasha.
Ukimsoma Mohamed Said ambaye ni ''co-author' wa kwaheri uhuru ya Ghessany sehemu kubwa ya maudhui yake ni haya haya tunayosoma. Linachoshangaza ni kuwa sehemu kubwa ya wzn wanaona kama ni matusi kwa wanamapinduzi.
Ukiangalia washiriki wa baraza la kwanza la mapinduzi wengi wao walifanya kazi na Mwalim Nyerere.
Hata waliofuata kwa nyakati tofuati bado walifanya naye kazi.
Akina Natepe, A.H. Mwinyi, A.Jumbe, Nassor Moyo, Thabiti Kombo Jecha n.k.
Swali linalofuata ni kuwa je hawa wanakuwa katika kundi gani kwa kuangalia historia ya akina Ghessany!
Ni wanamapinduzi au ni mamluki na vibaraka wa Nyerere walioshirikiana naye katika kuueneza ukristo kwa minajili ya kuuua Uislam?
Sasa ukiangalia mambo yote hayo na jinsi yalivyowekwa utabaki na swali moja muhimu sana.
Hivi Jan 12 kila mwaka ni haki na sahihi kwa wznz kusherehekea mapinduzi yaliyosababishwa na dhana ya kuua Uislam tena kwa kuchukua roho za watu kwa maelfu.