Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Yericko,
Siko hapa kufanya ubishi kuhusu Kipumbwi.

Nimeeleza habari zile kama mtafiti msaidizi wa Dk. Ghassany.
Ukipenda kuamini kuwa Sakura haikuwapo hapana shida.

Ila naamini watazamaji wengi wamenufaika na taarifa hii ambayo
wengi walikuwa hawaijui.
 
Yericko,
Kisa cha Okello ni kifupi sana.

Kama una mahaba na "ubaba wa taifa" katika mapinduzi
ya Zanzibar hebu kwanza kubali kuwa wewe ni "novice"
katika historia.

Ukishakubali ufuate taratibu za kusomeshwa.

Ukitaka kumtafuta mpishi wa mapinduzi anza utafiti wako na
Abdallah Kassim Hanga.

Hanga atakufikisha kwa Oscar Kambona.
Baada ya hapo mambo mteremko.

Zanzibar utabisha hodi nyumbani kwa Wayahudi wawili.
Tanganyika utachungulia sehemu mbili....

Dar es Salaam na Tanga.

Tanga ndipo utamkuta Victor Mkello na Mkwawa ambae kwa uhodari
wake Karume alimpa jina la utani "Tindo."

Namaliza.

Baada ya mapinduzi siku Mkello alipokwenda Zanzibar Hanga akamtambulisha
Mkello kwa Karume.

Karume alisimama na kumkumbatia Mkello.

Je ungependa kujua Karume alisema maneno gani ya kumshukuru Mkello?
 
Mkuu JokaKuu nakubalina nawe kabisa kuhusu dhana ya mapinduzi.
Mkuu Wickama, nakubaliana nawe kuwa historia ya Znz inaandikwa na makundi masilahi ndiyo maana kuna upotoshaji.

Ukisoma kitabu cha Kwaheri uhuru, ni wazi kuwa mapinduzi yalipangwa na kuratibiwa na Nyerere.
Sababu kubwa ilikuwa kueneza Ukristo ndio maana Okello alipelekwa kule.
Walioandika hayo wanatetea kabisa kuwa Sultan alikuwa mwema na ZNZ ilikuwa shwari kabla ya Mapinduzi.

Utetezi huo unafumbia macho migogoro mingi iliyokuwepo kabla ya Tanganyika haijapata uhuru.
Wanasahau kuwa ZNZ ilikuwa ya kwanza kufanya chaguzi katika ukanda huu wa A.Mashariki na kati kwa matatizo.

Kwa upande mwingine kuna kundi ambalo linaonekana kukerwa sana na ukoloni wa Sultan. Hili ndilo umelieleza vema katika suala la ASP.

Sasa ukitaka kufahamu kuhusu ''confusion'' ya mapinduzi ya znz, nimewahi kuuliza hapa.
Kama Mapinduzi yaliratibiwa na Nyerere na kumtuma Okolle na askari wa Kipumbwi
A) Kwanini basi wznz waliokuwa salama wakati wa Sultan wanasherehekea mapinduzi hayo kila siku.
Na hapa uzingatie kuwa mapinduzi yalilenga kuua Uislam kama ilivyosemwa.

B)Ni kwanini kuwepo na wznz wanaosema mapinduzi daima(ambayo yalilenga kuua Uislam) nawengine waseme ni haramu?

c)Je, tukimuuliza Ghessany na Mohamed swali moja, mapinduzi ni halali au ni haram tutapata jibu?

Nakuhakikishia kuwa hakuna aliyewahi kutoa jibu. Hii ni kwasababu historia imeundwa na hivyo uundwaji wake uliolenga watu na matukio unakwama kuwa na connections za maana.

Nijaribu tena kuuliza maswali hayo labda kuna atakayenisadia.
 
Acha kujidanganya.

Tanzania ni muungano wa tanganyika na Zanzibar. Nje ya Muungano wenu hakuna Tanzania bali kuna Zanzibar na Tanganyika.
Unayejidanganya ni wewe na the likes of you. Kikwete anapokuwa Magu au Kirumba ni rais wa Tanganyika. Ndivyo sisi Watanganyika tunavyomuona. Tukishambuliwa na Idi Amin ni rais wa Tanganyika anayeamrisha majeshi yetu kujibu. Siyo rais wa Zanzibar. Kwa hiyo jiulize ni nani anayejidanganya? Kwa nini Wazanzibari wanalalamika?
 

Nguruvi3,
Asante kwa taarifa hii. Mimi kitabu cha Ghassany kilinishinda kusoma baada ya ukurasa wa kwanza kwa sababu theme yake ni kwamba mapinduzi yalivunja uhuru wa Wazanzibari, hence the headline "kwa heri uhuru."
 
Nguruvi3,
Asante kwa taarifa hii. Mimi kitabu cha Ghassany kilinishinda kusoma baada ya ukurasa wa kwanza kwa sababu theme yake ni kwamba mapinduzi yalivunja uhuru wa Wazanzibari, hence the headline "kwa heri uhuru."
Jasusi, nakusihi uwe na moyo wa chuma ukisome. Tuhuma zote zimetupwa kwa mtu mmoja.
Utakapokisoma utakutana na maswali mengi yasiyo na majibu kama tulivyoona katika mnakasha.

Ukimsoma Mohamed Said ambaye ni ''co-author' wa kwaheri uhuru ya Ghessany sehemu kubwa ya maudhui yake ni haya haya tunayosoma. Linachoshangaza ni kuwa sehemu kubwa ya wzn wanaona kama ni matusi kwa wanamapinduzi.

Ukiangalia washiriki wa baraza la kwanza la mapinduzi wengi wao walifanya kazi na Mwalim Nyerere.
Hata waliofuata kwa nyakati tofuati bado walifanya naye kazi.
Akina Natepe, A.H. Mwinyi, A.Jumbe, Nassor Moyo, Thabiti Kombo Jecha n.k.

Swali linalofuata ni kuwa je hawa wanakuwa katika kundi gani kwa kuangalia historia ya akina Ghessany!
Ni wanamapinduzi au ni mamluki na vibaraka wa Nyerere walioshirikiana naye katika kuueneza ukristo kwa minajili ya kuuua Uislam?

Sasa ukiangalia mambo yote hayo na jinsi yalivyowekwa utabaki na swali moja muhimu sana.
Hivi Jan 12 kila mwaka ni haki na sahihi kwa wznz kusherehekea mapinduzi yaliyosababishwa na dhana ya kuua Uislam tena kwa kuchukua roho za watu kwa maelfu.
 
Wickama,
Wakujibu maswali si mie.

Mimi nimeeleza kile kilichokuwa hakifahamiki
kwa wengi.
 

Kweli mzee MS tupo kujua kile kilichofichwa katika historia na tunafaidika na kile unachokiweka, shukran kwa hilo ila kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani lakini hawana uwezo wa kuvunja safari.
 
Jasusi,
Sikuwa mwandishi mwenza na Dk. Ghassany katika kitabu kile
ingawa ningependa heshima hii.

Mimi nilikuwa mtafiti msaidizi tena katika sehemu ndogo ya Dar
es Salaam na Tanga.

Nishapata kukueleza hili huko nyuma.
 
Yericko,
Huko tulishatoka karne nyingi sana.

Mimi nimesema nimemsikia Nyerere mubashara.

Tukakubaliana wanajamvi takriban wote kuwa hapa
iwekwe clip tusikize sauti.

Iweje tena unaturudisha tulikotoka?
Kuna usemi, "Muongo muongoze."
Muongo uliyekubuhu kama wewe huongozeki!
 
Shukrani kwa hii khabari njema kwangu Sheikh Muhammad.

Kweli nilikuwa nikimtakia kheri ya kusilimu Costa, nilikuwa sijui kama amesilimu wala amefariki niliondoka kwenda kupiga box akiwa bado katika Ukristo! Alhamdulillah.
Haya mungeyapeleka kwenye jamvi la dini au misiktini kwenu, hapa mnatuchosha bure wewe na hilo zee lako, eboo!
 
Isalia,
Yako mengi sana katika historia ya Zanzibar ambayo kwa hakika
yanasikitisha.

Kuna mauaji na makaburi ya pamoja (mass graves) na walofanya
unyama ule wanafahamika.

Kuna wakati wa utafiti nilikuwa namuuliza Dk. Ghassany, "Hivi iweje
hawa watu wametenda yale na Allah kawasitiri ni siri yao leo hii wewe
wanakueleza kila kitu kuwa ilikuwa mwaka kadhaa mimi nikafanya kadha
wa kadha na fulani alikuwapo na fulani kisha tukachimba mahali fulani...

Jibu la Dk. lilikuwa, "Kwao wao hii ni therapy ni ponyo katika nafsi zao na
pili wanatubu na kutaka msamaha kwa Allah."

Yako mengi.

Truth and Reconcilliation kama ile ya Afrika Kusini ndiyo itaponya madonda
haya.
 
Jasusi,
Wewe ni mkubwa kwa umri kunipita.

Lakini hutukanwi kwa kisa cha kuwa na umri mkubwa.
Mwanafulani punde kanitusi kwa kusema Costa John
kasilimu kabla hajafa.

Naamini utamkumbuka Costa mlikuwanae Aga Khan.

Hasad kitu kibaya sana chuki ya huyu ndugu imefurtu ada.
 

Mzee MS; Hii inarudi kule kule. Kama Karume alimshukuru Mkello na kumkumbatia na Hanga ndiye mhandisi mtendaji pamoja na hao wayahudi, hii ni involvement ya ASP moja kwa moja. Sasa doubt ya UHALALI wa Mapinduzi haya kwa baadhi yetu unatoka wapi? Lawama kwa Nyerere msingi wake upi? Ndio maana narudia sana swali langu. Hivi ASP walilazimishwa msaada au waliuomba? na kama waliuomba hivi mwenye dhamana ya mapinduzi ni yule aliyekusudia kupindua na kutafuta msaada wa kupindua au yule aliyesikiliza kilio na kutoa msaada?

Tuambiane kama kuna doubt kuhusu uhalali (legality ya ASP kumpindua sultan) wa mapinduzi haya. Nadhani mjadala kuhusu ground operations utafaa baada ya kuvuka hiki kisiki.
 
Wickama,
Wakujibu maswali si mie.

Mimi nimeeleza kile kilichokuwa hakifahamiki
kwa wengi.

Mzee MS; You may wish kujibu. Yericko katuarifu kuwa position yako kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar ni AMBIGIOUS. Awali Nilishamsoma Nguruvi pia Aliongea kuwa wewe ni mwenye huruma na SULTAN

Ama kuhusu yaliyokuwa hayajulikani uko sawa. Ndio shughuli ya historians.
 

Nguruvi; Ndio maana narudia sana swali moja ambalo strangely halijibiwi. ASP walilazimishwa MSAADA au waliuomba? Nani alimfata mwenzake na agenda ya kuipindua serikali ya znz? Haiwezekani jamaa wa zenj na bara wakusanyike kipumbwi out of thin AIR. Nani alimfata mwenzake na kuanzisha agenda?
 
Haya mungeyapeleka kwenye jamvi la dini au misiktini kwenu, hapa mnatuchosha bure wewe na hilo zee lako, eboo!

Muda wowote utakaochukulia mzaa dini ya Watanzania wenzako, basi wewe ndiyo utayechekwa. JF ni huru kwa dini zote.
 

Nguruvi na Jokakuu na Jasusi;
Issue hapa ni kwamba some of us wanakuwa sio wakweli. Is it not tru kuwa ASP waliomba msaada? Is it not true kuwa walikuwa na dhamira ya kupindua serikali ya huko? Justification ya Mapinduzi walikuwa nayo ASP na bado wanayo. Na ninavyojua mimi hawa ASP hawana dini tofauti na wale waliowaondoa madarakani.

Sasa ipo dhana ya kama kwamba bidii ya wazenj kujinasua na utawala wa Sultan ilikuwa kuudhoofisha uislamu. Hapa hakuna anayeeleza kuwa historical abuse dhidi ya Africans and shirazis (ASPs) yalikuwa yanadhalilisha uislamu unaotaka haki na uadilifu.

Then strangely watu wanapokuja na "discoveries" za ground operations za hawa wazenj kujinasua toka kwa sultan all the blames anabeba Kambona na Nyerere? Why him and not Karume?

Nadhani kama yupo wa kulaumiwa ni yule aliyetaka kujikomboa (ASP), sio aliyemsaidia kujikomboa (TANU). Hapa ndipo kwa makusudi panapindishwa.
 
Yericko,
Soma kitabu "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."

Kimeandikwa na Harith Ghassany.
Nashukuru sana ndugu yangu Mohamed Said,

Japokuwa hoja zile mimi ndie nimezileta kwako, na jibu lako kuwa nimsome Daktari Ghassany ni zuri kwangu!

Lakini kumbuka nimeuliza yale kwa mafaa ya watu 200000 wanaofuatilia mnakasha huu, hivyo sio wote wamemsoma au watamsoma Dkt Ghassany

Mimi nimemsoma vema Dkt Ghassany katika andiko lake liitwalo "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru."

Hivyo nimejenga hoja hapo juu kwaajili ya mafaa ya wasomaji wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…