Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Nguruvi vipi mbona hili swali hujalijibu mpaka leo pasha basi hiki kiporo moto !

ASP ililazimishwa kuwatumia Wamakonde wa Kipumbwi?

Viongozi wa Zanzibar waliofanya kazi sambamba na Mwalimu Nyerere na wengine walipo sasa ni wasaliti wa Wazanzibar?
 


Nguruvi3

Crusade war haitakusaidia,na chuki zako dhidi ya uislam hata kama unajaribu kuzificha na kuzionesha tambua ya kwamba pia na hiyo haitakusaidia,

Unapokuja na kuubeza uislam kwa kutoa kauli zako za kuzunguka mbuyu sisi tunakuona umefili hata kabla hiyo mission yako hujaianza,

Na hakuna aliekuambia hapa kwamba Kuondolewa kwa sultan zanzibar basi ni kuanguka kwa uislam,

Labda nikuulize,unauliza hilo kwa dhati ya kutaka kujua au kwa mantiq ya kuuvaa na kuukejeli uislam??

Kipindi sultani anatawala zanzibar kulikuwa kunaendeshwa kama dola ya kiiislam??

Kama ni kweli weka uthibitisho,kama si kweli jipime mwenyewe na uone chuki yako ni ya kiwango gani dhidi ya uislam na waislam??

Inawezekana kabisa ya kwamba walikuwapo waislam ambao walikuwa wanaish zanzibar kipindi hicho cha usultani na walikuwa hawaufurahii uongozi wa kisultani kwa namna moja ama nyingine,unalizungumzaje hilo?

Je unafaham uislam uliingia lin zanzibar??kabla au baada ya usultani???

Tunachokuambia hapa ni kwamba mumeshindwa kuuonesha uchochez wa Moh Said,na mnachokifanya ni kuangaza huku na kule kutafuta kitu ambacho mtaegemea kutafuta uthibitisho lakini bahati mbaya sana mmekosa,

Moh Said hayupo hapa kuweka ligi na mtu au kuweka ubishani,yeye yupo hapa kuweka uhalisia wa historia,

Kama umeshindwa kuiamini na kuikubali ni juu yako,wapo wanayoiamin na ni wengi wenye weledi wao,kama wewe umeshindwa kuafiki kwa kuona Juhudi za ukristo na wakristo hazipewa nafasi kama unavyojaribu kuongelea ni sawa pia,

Lakini uhalisia uko hivyo,na utabakia kuwa hivyo....
 
Last edited by a moderator:
Yericko , Nguruvi3 , Wickama na Mag3.Naona maswali haya yameonekana kuwavutia sana na kila mmoja akiyatoa mnapeana vibwagizo vya ''like''. Dhana inayojaribiwa kujengwa hapa nikuwa ASP ndio walioomba msaada kwa TANU (Nyerere)..hivyo basi Nyerere (TANU) asilaumiwe.Kwa hakika kwa weledi wenu nyie viongozi wangu sikutaraji kuona kama hii nayo pia itakuwa ni hoja. Ni wazi kama mnakubaliana na ukweli kuwa Mapinduzi yale yalikuwa na gharama kubwa na mpaka Serikali ya Tanganyika kuweza kutoa kiasi kile cha fedha kwenda kwa Serikali ya Algeria kwa ajili ya silaha zile (maana sijapata kuona mkikanusha). Kama hivi ndivyo na tujenge dhana kama ASP ndio waliiomba TANU....hivi ilikuwa ni kwa faida ipi ambayo Serikali ya Tamganyika chini ya Mwalimu Nyerere wangeipata kwa kuingia gharama zile kama wao hawakuwa na maslahi kwenye mapinduzi yale?. Kwemwale.
 

Maneno mazito.
 

Kwamba hoja yako nikuwa Serikali ya Tanganyika ingefaidika na nini kwakudhamini mapinduzi ya Zanzibar?

Naomba swali hilo lijibiwe kwa swali hili hapa chini,

Tanzania ilinufaika nini kwa kufadhiri vita vya ukombozi kusini mwa Afrika?

Ukipata jibu, hilo ndio jibu la hoja/swali lako mkuu!
 


Afanaleki..!
Ndiyo jibu hilo??
Hapo umemaliza kila kitu??
Kwa kufadhiri vita vya ukombozi mwa kusini mwa Afrika Tanzania Imenufaika na umaskini huu ulionao sasa,hata wa kufikiri...
So,hilo ndio hasa lilikuwa lengo??
Mnakimbilia hoja za ajabu ajabu zinazojijibu zenyewe huku mkitaraji kuonekana waerevu na wajuvi wa mambo hali ya kuwa ni makanjanja??

Maji ya Moh Said ni Marefu sana,kuyaogelea hamtayaweza...
 

Kweli kabisa Al akhy The Big Show huyu jamaa hana hoja hata kidogo ni mshabiki tuu ngoja nikupe mfano wa huyu jamaa, umeshawahi kuona mtu anapiga ukuta kichwa :frusty: halafu anasikitikia ukuta badala ya kusikitikia kichwa chake waarabu wana msemo unao sema "ASHFIKUU ALAA RAASI LA TUSHFIKUU ALAL JABAAL" onea huruma kichwa chako usionee huruma jabali upo hapo bwana mkubwa.
 
Muongo mkubwa, huna cha kufyonza ilm bali upo kuhamasisha uzushi na uzandiki wa zee lenu lililokubuhu kwa fitna na uzushi.
 


Naam al akhiy Boko haram,

Huyo anadhani sisi tupo hapa kupimana nguvu na yeye,yeye ana nini??

Umaarufu aliodhani angeupata umegeuka kuwa fedheha kwake,shukrani kwake kwa kuwezesha kumwagwa kwa darsa huru hapa na mwalimu wa walimu Moh Said...
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mag3, Mohamed Said alishayaona haya maswali, hana ubavu wa kuyakabili kwani yamemuacha mtupu! huyo Spike Lee kaletwa na ukeleketwa wa imani ya dini yake na kwahiyo hana hoja yoyote ya kisomi zaidi ya hayo makelele yake ya kijinga ya kufyonza ilm na sumu kali ya huyo nabii wao Mohamed Said!
 
Kaka hao watu 200,000 wamekutuma wewe kuwa msemaji wao teh! teh! teh!
Kaa pembeni mzushi wewe, tunataka majibu na sio kufyonza ilm yenye sumu. Kama wewe umezoea kufyonza matakataka ya hao maustaadh wako hiyo ni juu yako!
 
Maneno mazito.
Kwemwale na ndugu yako mfyonza sumu, mnashindwa nini kuelewa jambo dogo kama hili? Ukombozi wa Afrika ilikuwa ni ajenda ya Tanganyika mara tu baada ya kujipatia uhuru wake. Ilishawahi kuwekwa bayana kwamba uhuru wa Tanganyika usingekuwa na maana kama nchi nyingine za kiafrika zingeendelea kuwa mikononi mwa wakoloni. Baada ya hapa Tanganyika na baadae Tanzania ilizisaidia nchi zote zilizohitaji msaada wa ukombozi... nchi zilizonufaika ni pamoja na Namibia, Zimbabwe, Msumbiji...
 
Yukowapi gombesugu
cc suleiman takadir


Hasanalis,

Salaam Al Akhiy.

Nina neno langu takakwambia,si kwa Kizungu bali Kiswahilia. Msiba walinidhamiria wala sijeumia,azma yao ni dhuluma,katu Mola hatakubalia.

Wewe Al Akhiy ndie wa kukutaka radhi wala si mwingine asilan,maana najua madhila yalokusibu kusikia nduguyo janiona.

Wallahi,nipo vyema ni kibarua na safari kiduchu menibana.

Nakuacha na nasaha mbili;mojawapo ni ya kizungu na nyingine ni ya Mzee wetu alokua mashuhuri kwa upande wake.

No one is your friend who demands your silence,or denies your right to speak - A. Walker

Sigida Mpingo hading'oka - Kondo Kipwata.

Nimefurahika kwa kunisikiza.

Tuendelee na hili zogo/"Mnakasha".

Ahsanta.


Cc;Ritz,Barubaru,The Big Show,Boko Haram,JokaKuu
 

Swadakta.Nimekukubali kabisa yakhi..

Ahalan wa sahalan yaa akhiy
 

Kwemwale; Bora wewe unayesema TUJENGE DHANA KAMA ASP NDIO WALIIOMBA TANU. Hicho kitabu unachosema (nimekupa link) na hata CIA report ya wakati huo inaonyesha mafungamano makubwa kati ya ASP na TANU. Hata mzee MS kwenye post yake moja alishawahi kuandika kuwa Nyerere alialikwa na Karume kwenda zenj lakini wenzake wakamhimiza aende mikoa ya kusini kwa vile kulikuwa na kizingiti cha kanisa katika wanachama wa TANU. Hawa walishirikiana. Ukisoma pia utaona hao ASP wakihaha East Africa kutafuta support kuwa jamani sisi tunataka kupindua tukifanikiwa jamni msituangushe "mtutambue haraka".

Kwa hiyo Kwemwale huwezi kumlaani Nyerere kwa Mapinduzi ya Zenj huku ukiwaacha ASP. Huwezi kumlaani eti njama yake ilikuwa ni ujanja wa Kanisa kuua Uislamu kule visiwani bila kujaribu kuonyesha na ASP ni mawakala wa kanisa lipi hapa duniani.

Sasa, waliojenga hisi tuhuma tangu awali wanatumia "Islamic card" bila kujua ASP ni pia waislamu na hata hao waliokuwa wananyanyasa hao watu wa rangi tofauti na yao pia waliswali pamoja.

Uhalali wa Conflict Kwemwale haupimwi na atrocities wala resources spent. Unapimwa na sababu za kuingia kwenye conflict. Kama sababu hazina mashiko, basi hutakubaliwa hoja zako hata kama hukuua mtu wala paka. Wenye sababu za mapinduzi ya zenj SIO TANU. NI ASP. Wao ASP walichofanya ni kutafuta msaada wa kutimiza lengo lao.Hizo kambi za Kipumbwi mwandishi kaonyesha vizuri tuu kuwa wazenj walikuwa wanakuja na wanapewa mafunzo ya kijeshi na kurudi kwao.

Ndio maana TUNAULIZA ILI TWENDE PAMOJA HUU MSAADA WA MAFUNZO,SILAHA NA ASKARI NA WAMAKONDE WA KIPUMBWI NE MENGINEYO, JEE ASP WALIUOMBA AU WALILAZIMISHWA? Kila jibu lina maana yake na ndio ukaona ukimya na wengine kukaa pembeni, sio kuwa hawajui JIBU.

Kwemwale ukiniuliza kama Mugabe alilazimishwa kuleta askari wake wa ZANU-PF kufundishwa mambo ya kivita wakati wanapigania uhuru wao jibu langu ni HAPANA, SAMORA wa Msumbiji pia jibu langu ni Hapana; ANC na kambi zake hadi Morogoro jibu ni Hapana. Na ndio maana wana dhamana na ukombozi wa nchi zao.

TUNASUBIRI JIBU LA ZENJ NA ASP. HATUTAPUNGUKIWA SUBIRA KATIKA HILI

http://kwaheri.files.wordpress.com/2010/05/kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf

ENJOY
 

Oooohoo ndugu yangu kipenzi GombeSugu

Karibu mkuu! Karibu sana!

Pole sana kwa likizo fupi, mshukuru Mungu kwa yalokukuta kwakuwa yeye ndie Muweza wa yote!

Zingatia sheria za jf tunene kwa weledi na mapana kwa mafaa ya taifa letu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…