zomba
JF-Expert Member
- Nov 27, 2007
- 17,240
- 3,930
Zomba; Baada ya salaam; imenibidi nicheke na JIKICHWA!!!!. Mali ya Bonde hiyo mwanangu. Ustadh mimi nimesoma shule ya msingi ya serikali pale moshi mjini. Fani zangu nilisomea SUA (soil sciences). Huyo father unayemsema ndiyo kwanza leo kuona hilo jina.
Ni kwamba Zomba, operation yoyote ya kijeshi ufaulu wake unategemea sana matayarisho na usiri. uliza askari wa jeshi wanajua. La tatu huwa kustukiza (kumtokea adui bila yeye kutarajia). Vyote hivyo vina umuhimu. Askari wanaodurusu hii thread wanajua details.
Tunachokiongelea hapa ni kuwa;
1. wale wamakonde hadi kufika kipumbwi, kulishwa, kufundishwa mbinu za uaskari wakiwa pamoja na wazenj haikuanguka kama mvua. lazima matayarisho yalifanywa, usiri ulitawala na sakura palichaguliwa kwa sababu (umbali toka zenj ni mdogo)
2. sasa kama kambini walikuja wazenj pia kujifunza na kurudi, kuna HUYO aliyewatafuta na kuwaleta toka makwao. Tulichouliza ambacho waheshimiwa wamegoma kujibu ni kimoja; kwamba hivi haya matayarisho, msaada wote huu, ndio kusema ASP walilazimishwa na TANU kuupokea au wao ndio walioanza kuomba msaada kuwa jamani tusaidieni tumngoe sultani? Ushahidi wa reports unaonyesha ASP wakipokea hadi silaha za rashasha toka kwa kina Kambona kwa ajili ya HILO WANALOLIJUA WAO.
Uzito wa hili swali na jibu lake ni kuwa; kama ASP ndio waliowaomba TANU msaada basi ASP ndio wamiliki halali wa mapinduzi na kutokana na umiliki huo, wao ndio waliwajibika na nidhaamu ya askari wao BAADA ya kuiangusha serikali waliyojiandaa siku nyingi waiangushe.
Sasa umeuliza masuala ya Geneva convention yanakuja vipi;
Kuja ni kwa sababu mamlaka inayomiliki askari ikisha twaa madaraka juu ya eneo lilikuwa linagombaniwa (yaani kama baada ya kina Okello kuiangusha serikali), inawajibika MOJAMOJA na usalama wa raia na mali zao. Bila hivyo unakuwa umehalifu na umeweza kufunguliwa mashataka. Kwa kesi za Zenj ilipaswa kuwa hivyo pia. nchi nyingi kwa mfano West Africa, Serikali imepinduliwa, lakini raia na mali zao haraka wanalindwa.
Kukwama kwa JIBU kutoka kwa jirani zangu (na wewe umo)ni kwa sababu kwa muda mrefu waliwekeza katika ghadhabu za matayarisho yanayoonekana(Nyerere hapo)wakamsahau aliyeomba HUO msaada. Kwa sababu OMBI la huu msaada ndio chimbuko la yote haya. Na hili ombi ndilo lilifanyiwa kazi ya kuanzisha kambi, kuleta askari, kuwanunulia silaha nk.
Tanganyika tumefundisha askari wa Msumbiji, Zimbabwe, Angola, nk, lakini nidhamu ya hao askari ndani ya mipaka ya nchi husika ni jukumu la makamanda wa hao askari. Huadhibu nchi walikojifunza.Kwa hiyo kama kuna wa kulaumiwa na kufunguliwa kesi za genocide ni Commander-in-chief aliyekuwa ana mamlaka na jeshi lililoangusha ile serikali na majenerali wake walioshindwa kusimamia nidhamu ya kijeshi.
Geneva Articles zinaongelea tabia zinazotakiwa juu ya jeshi linalokalia ardhi nyingine (iliyotekwa). Ndipo nasema basi natuseme kuwa wale FFU 100 waliofika baadae kitu kama 17/jan ( 5 days later) kuwa ni occupying army, jee wao walivunja hii nidhamu? Kwa sababu hawa 100 kamanda-inchief wao anajulikana (Julius) Ushahidi toka kitabu cha Kwaheri Uhuru.... unaonyesha kufika kwa hawa 100 kuliokoa maisha ya wazenj kibao. Mauaji yalisimama mara moja.
Mshikaji unakijihoma nini? maanake sijakuzoea kuuliza kwa sauti ya STARA. Usiku mwema.
Nakupa hint; google "father Cunningham".
Mengine naona unalalama tu, Jee huo ndio ushahidi wako wa jikichwa la habari? huna zaidi?