Wanajamvi, hapa chini nawakumbusha tu kuhusu serikali aliyoiunda Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofuatia mapinduzi yaliyoutimua utawala wa Kisultani visiwani. Baraza la Mawaziri lililoundwa lilikuwa na wafuatao.
- Mwalimu Julius Nyerere (Christian): President
- Abeid Karume (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Vice President and Minister responsible for Zanzibar affairs.
- Rashidi Kawawa (Muslim): 2[SUP]nd [/SUP]Vice President and Minister of Defence and National Service.
- Nsilo Swai (Christian): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the Presidents Office.
- Abdulrahman Babu (Arab & Muslim): 2[SUP]nd[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the Presidents Office.
- Amir H. Jamal (Indian & Hinduist) 3[SUP]rd[/SUP] Minister of State for Economic Planning in the Presidets Office.
- Aboud Jumbe (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State in the 1[SUP]st[/SUP] Vice Presidents Office.
- Lawi Sijaona (Muslim): 1[SUP]st[/SUP] Minister of State in the 2[SUP]nd[/SUP] Vice Presidents Office.
- Bhoke Munanka (Christian): 2[SUP]nd[/SUP] Minister of State in the 2[SUP]nd[/SUP] Vice Presidents Office.
- Said Maswanya (Muslim): Minister of Agriculture, forests and Animal Husbandry.
- Jeremiah Kasambala (Christian): Minister of Commerce and Cooperatives.
- George Kahama (Christian): Minister of Transport and Buildings.
- Paul Bomani (Christian): Minister of Finance.
- Oscar Kambona (Christian): Minister of Foreign Affairs.
- Job Lusinde (Christian): Minister of Internal Affairs.
- Tewa Said Tewa (Muslim): Minister of Lands, Settlement and Water.
- Kassim Hanga (Muslim): Minister of Industries and Mines.
- Solomon Eliufoo (Christian): Minister of Education.
- Derel Brycesson (British & Christian): Minister of Health.
- Michael Kamaliza (Christian): Minister of Labour.
- Amri Abeid (Muslim) Minister of development and Culture.
- Austin Shaba (Christian): Minister of Housing and Local Government.
- Hasan Moyo (Muslim): Minister of Law.
- Idris Abdulwakil (Muslim) Minister of Information and Tourism.
Wanajamvi wapendwa wakati huo Mwalimu alipendwa kikweli kweli na Watanzania wote bila kujali dini zao, rangi zao wala kabila zao...sura kwenye hili Baraza la Mawaziri mwaka 1964 ni ushahidi tosha kwamba Watanzania hawakubaguliwa wala kubaguana katika misingi yoyote ile. Mapokezi aliyokuwa anayapata Mwalimu kila alipofanya ziara visiwani hayakuwahi kuwa na mfanowe katika historia ya Zanzibar. Kama alikuwepo Mtanzania mwenye dukuduku lolote ni wale Waislaam wachache walioshindwa kuwashawishi Waislaam wenzao kuwaunga mkono hata kabla ya uhuru walipoanzisha chama cha AMNUT mwaka 1958.
Huu uchochezi tunaoushuhudia hivi leo ulikuja kujitokeza muda mfupi baadaye kutokana na chuki za baadhi ya wazee waliokataliwa katika hila zao za kutwaa madaraka kwa kupitia mgongo wa dini. Njama zilianza kufanyika kutaka kuvuruga umoja wa Watanzania kwa kupandikiza mbegu ya chuki ambayo hadi leo mtoto wa mmoja wa wazee hawa anaiendeleza kama tunavyoshuhudia ndani ya mnakasha huu. Swali la kujiuliza ni hili; hivi hawa Waislaam waliokuwa ndani ya hilo Baraza la Mawaziri kuanzia makamu wawili wa Raisi hadi Waziri wa Sheria walikuwa ni wasaliti kwa wananchi wa Zanzibar na Uislaam?
Je Abeid Karume, Abdulrahman Babu, Kassim Hanga, Amri Abed, Aboud Jumbe, Hasssan Moyo na Idris Abduwakil walikuwa ni wasaliti visiwani Zanzibar? Je Wazanzibari wanayathamini mapinduzi yaliyowaweka hawa madarakani? Je, kwa msingi wa madai ya wachochezi kama
Mohamed Said, mapinduzi ya mwaka 1964 yalikuwa haramu? Je Waislam wa bara na visiwani wanawaona hawa kama wasaliti katika Uislaam? Je katika msingi huop huo viongozi wote wa juu wa Jamhuri ya Tanzania ambao wote ni Waislaam, kulingana na uchochezi unaoendelea ni wasaliti katika Uislaam? Je Kikwete, Dr. Bilal, Dr. Shein na Shariff ni wasaliti wa Uislaam?