Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar



Nanren,

Hii forum huru kila moja na mawazo yake jitahidi kuwa mvumilivu ukisoma michango ambayo inakukera.

Sijui kwa nini unapenda kutumia neno wafuasi wa Mohamed Said, sijui wewe mfuasi wa nani?

Hata kama unapingana ki mawazo na msimamo na Mohamed Said, lakini kuna vitu unachota kwako kutoka kwenye historia ya Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:

Si umeona jina la babu yake Salum Abdallah kwenye list ya waasi walioswekwa ndani?
Siri nzima ya chuki ya Moh' Said kwa Nyerere inaanzia hapa. Simulizi za akina Sykes ilikuwa ni uchochoro tu wa kupitishia hasira zake. Na ili apate support among unsuspecting muslims, akaamua ku-concoct conspiracy ya kanisa na Nyerere na mfumo kristo dhidi ya waislam na uislam... Ndio maana tukimuuliza, kama kanisa katoliki lilikuwa na uadui na waislam, na kanisa katoliki tunajua lina mtandao mkubwa, kwanini lifanye hayo mambo hapa TZ tu? kwanini halikuwafanyia waislam wa uganda, Kenya, Mozambique, Malawi? Yeye atakujibu, "hayo sina ujuzi nayo, mimi nasimulia historia ya wazee wangu". Wafuasi wake wanamsaidi kujibu eti " ndio maana Nyerere anafanyiwa mchakato wa kuwa mwenye heri, kwa sababu amelifanyia kanisa mambo mengi". Yote haya ni kutokujua chanzo cha hizi chuki za Moh Said. The guy has grudges!
 
muogope Mungu wako mzee Said;
ukiambiwa uthibitishe unakimbilia kusema wazee wangu walinihadithia

Ithibati gani unataka kuliko haya ninayokueleza?

Ukiwa unataka ithbati ya kimahakama itabidi tufungue
kesi na tulete ushahidi mahakamani na vielelezo vingine.

Mahakama wahoji watu waliotuhumiwa kwa dhulma
na Waislam walete ushahidi.

Ikiwa serikali wanalitaka hilo naamini Waislam tuko tayari.
 

Asante sana mkuu, hayo ni madai upande wa kwanza, je upande wapi (Serikali) wayajua?

Zingatia niliyokupa pale juuuu! Yale ndio madai halisi ya upande wa pili mkuu.
 
Nyerere kwenye moja ya hotuba yake alishawahi kusema kuwa alimwachia aliesema ameiweka tanzania mfukoni baada kuwasiliana na bishop Makarius lakini haikuwahi kutokea majadiliano yenye muafaka kati wa masheikh na nyerere.
 

Sijui kwanini imeku-touch!?! Au...
Mimi mtu wa bara nisamehe. Kiswahili sikijui sana. Labda neno sahihi badala ya neno wafuasi ni mashabiki. Kama ni sahihi, basi, naomba kwenye post zangu huko nyuma uelewe hivyo. Otherwise, samahani kwa yeyote aliyekwazika.
 


wanataka i'lmu gani nyingine zaid ya hiii??

Chukua nukuu hii ndugu yangu,,
"maa aamanat' kablahum' min qariyatin' aha'lakna haaa..!afahum yuu'mi nuun'??
'hawakuamini wengi miongoni mwa ummah zilizoumbwa kabla yao,je wataamin hawa??narudia tena kauli hii,hawawez amini,inawakera na kuwaumiza kuona ukweli huu ukimwaga wazi wazi,hadhwarani pasi na tozo ya aina yoyote ile...!
Basi mungu na akulipe kheri ndugu moh' said kwa maarifa haya unayoyatoa kwa ndugu zako watanzania,kwa kweli wenye kunufaika tunanufaika,na wenye kukaidi wewe zidi tuh kuwashushia nondo,mioyoni mwao yanawaingia haya.
 
Kama babu yangu angekuwa msaliti angepelekwa mahakamani
na kufunguliwa mashtaka.

Hilo halikufanyika si kwake yeye hata kwa wengine.

Walokuwa wahaini walisimamishwa kizimbani na hili
kila mtu analijua na adhabu walizopewa katika hukumu
yao.

Bado mimi nimuugope Mungu?
 
Asante sana mkuu, hayo ni madai upande wa kwanza, je upande wapi (Serikali) wayajua?

Zingatia niliyokupa pale juuuu! Yale ndio madai halisi ya upande wa pili mkuu.

Nimependa sana staili yako ya kujifunza baada ya kukosa hoja umeamua kuja na mbinu mbadala anachosema Mohamed Said, unakigeuza kuwa jibu lako. Hoja ya uchochezi imepotea saizi umejikita kwenye hoja ya uasi.

Bado tunasubiri majibu ya waasi waliopewa msamaha na Nyerere na wengi kupewa vyeo na wengine kuwa mabalozi.
 
Ndiyo maana ndugu yangu vyuo vingi vinanialika
na wanafunzi wengi huja kwangu kwa ushauri.

Hawaendi Chuo Cha Kivukoni.
 

Sijakwazika na chochote unapofanya mjadala wakati umeishachagua upande hata ukitoa hoja zako zinakosa nguvu.
 
ndiyo maana ndugu yangu vyuo vingi vinanialika
na wanafunzi wengi huja kwangu kwa ushauri.

Hawaendi chuo cha kivukoni.

kabisa kabisa,mtu aende chuo cha kivukoni kusoma kitu gani??
Aende kivukoni kuisoma siasa chafu ya ccm?zao la julius lililopotoka?

Abadan asilani mwerevu hawezi kwenda kivukoni,labda kama anaenda kunywa supu ya pweza na samaki wabichi,lakini sio kwenda kuongeza maarifa,pale utaambulia upotofu na mafunzo ya ufisadi tuh yanayoigharam nchi hii kwa sasa.
 

Rudi kwenye sheria za nchi kisha uone rais anamamlaka gani hasa kipengele cha kumuweka mtu kizuizini.

Ni mkosaji yupi hustahili kuwekwa kizuizini na yupi hupelekwa mahakamani,

Mwaka ule wa vuguvugu za uasi wa baba yako na wazee wengine ndipo sheria ile iliridhiwa, yote hiyo nikatika kuwajali na kuwaheshimu tu, mwalimu alikuwa na uwezo wa hata kuwanyonga tena hadharani, lakini busara zake zilizotukuka akaamua kuwaweke kizuizini tu.

Hilo tu linampa sifa ya kipekee ulimwenguni, kwani hakuna kiongozi barani afrika aliyeweza kuwaweka vizuizini waasi wa serikali halali, wengi waliwanyonga tu.
 
Hapana sina chuki na mtu.
Kuacha chuki ikutawale ni sawa na kujitia jela.

Nimeandika historia hii kwa kuwa naijua.

Mke wa Kleist Sykes akiitwa Bi Mluguru biti Mussa.
Mke wa Salum Abdallah akiitwa Bi Zena biti Farijallah.

Majirani hapa Dar es Salaam.
Waume marafiki na wake zao mashoga.

Nimekuwekea taarifa hizi kujivua shutuma yako kuwa
nimepitia kwa akina Sykes kutoa dukuduku langu kuhusu
ugomvi wa babu yangu na Nyerere.

Si hivyo Kleist na babu yangu hao wote ni wazee wangu na
historia zao zimefungamana pamoja na kushikana na historia
ya Tanganyika.
 
Mzee Mohamed Said hongera sana!!! inaonyesha upeo wako ni mkubwa sana, na umejaaliwa uwezo mkubwa wa kutetea na kujibu hoja kwa weledi wa hali ya juu, pamoja na kwamba unashambuliwa na watu wenye upeo tofauti na wenye mtazamo hasi juu yako pamoja na kwamba unawajibu hoja zao kwa ukamilifu lakini kwa sababu tayari wameshakuhukumu kua ni mchochezi na mdini, basi hata ukiwaelewesha kwa ustadi wa namna gani abadan hawatakuelewa wala kukubaliana na wewe, lakini ukweli utabaki pale pale kuwa umetoa somo ambalo hawakulijua hapo kabla na wamefaidika nalo a sio wao tu kila aliyepitia huu uzi kuna kitu amejifunza tofauti na tulivyoaminishwa zamani kutokana na historia ya nchi yetu.mm sikua mchangiji wa hii mada lakini nimekua naifuatilia hii mada tangu mwanzo na sio tu hii mada hua nasoma mada karibu zote hapa jf, na hata wachangiaji wote wa huu uzi wengi wanaokukejeli asilimia kubwa wanajulikana kua wao wako mrengo gani na wameonyesha wazi wazi ni wanaipinga dini fulani, kuazia Yericho nyerere, Jasusi na Jogoo aka Nguruvi hawa jamaa wana ule ubishi wa jadi na wanaile tabia ya kutaka kujifunza kitu kipya kwa njia ya ubishi, kwa kutoa kejeli, jazba na kutoa hoja zisizo kua mashiko kwa sababu tu umegusa sehemu ambayo wao hawapendi iguswe au ipewe shutuma.
 
Nimekueleza historia ya babu yangu.
Babu yangu kapigania uhuru wa nchi hii.

Historia hii ninayoeleza humu ndiyo shahidi.
Hakuwa msaliti.

Kilichompelekea kufungwa jela ni hofu ya Nyerere.
Aliogopa kupambana na yeye siku za baadae katika
uwanja tambarare wa siasa.

Huyu ni mtu aliyeongoza mgomo uliodumu siku 82.
Hiki ndicho kilichomtisha Nyerere.

Ile ati babu yangu alikuwa anaandaa jeshi la kumpindua
Nyerere ni uongo uliokubuhu.

Ndiyo maana alitengeneza orodha yake ya waongo, vibaraka
na wasaliti.

Akifurahi alikuwa akiwataja.

Kuanzia pale alijitoa TANU akajipinda katika kilimo cha tumbaku
Urambo na akafanikiwa sana.

Kafa katuachia nyuma hazina ya kumbukumbu ndiyo hii leo
nami nawarithisheni urithi wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…